Thursday, May 31, 2012


DROO YA TANO YA PROMOSHENI YA VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO NA SBL, YANGURUMA TENA, MWANZA WAENDELEA KUVUNA ZAWADI

 Meneja wa kinywaji cha Serengeti Premium Lager Bw. Allan Chonjo akizungumza wakati wa kutangaza washindi wa Genereta na Bajaj katika bahati nasibu ya promosheni ya Vumbua Hazina chini ya Kizibo iliyofanyika kwenye ofisi za Kampuni hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam kulia ni Tumainiel Malisa kutoka PWC.
 Menejwa mawasiliano wa kampun i ya bia ya Serengeti Imani Lwinga akizungumza wakati wa kuchezesha bahati nasibu hiyo katikati ni Meneja wa bia ya bia ya Serengeti Premium Lager na kulia ni Tumainiel Malisa kutoka PWC
 Meneja wa kinywaji cha Serengeti Premium Lager Bw. Allan Chonjo akizungumza wakati wa kutangaza washindi wa Genereta na Bajaj katika bahati nasibu ya promosheni ya Vumbua Hazina chini ya Kizibo iliyofanyika kwenye ofisi za Kampuni hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam katikati ni Tumainiel Malisa kutoka PWC na kulia ni Abdallah Hemed kutoka bodi ya mchezo ya kubahatisha.

Zoezi la kukabidhi zawadi kwa washindi waliojitokeza kushiriki na kushinda zawadi zinazotolewa katika promosheni ya kipekee ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’ inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti limeendelea wiki iliyopita katika mikoa ya Iringa na  Mwanza ambapo mshindi wa jenereta na yule wa bajaj walikabidhiwa zawadi zao katika sherehe zilizohudhuriwa na umati mkubwa wa watu na kushuhudia SBL ikikabidhi zawadi hizo na kuamsha hamasa kubwa kwa wapenzi na watumiaji wa biadhaa za SBL.
Asubuhi ya leo droo ya tano ya promosheni hiyo ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’ imechezeshwa katika ofisi za kampuni ya bia ya Serengeti zilizopo maeneo ya Oysterbay jijini na kupata kuhudhuriwa na waandishi wa habari, wasimamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka ndani na nje ya kampuni hiyo, wakiwemo kampuni ya kuendesha Bahati Nasibu ya PUSH MOBILE na wahakiki na wakaguzi kutoka PWC-Price Water House Coopers.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa kuchezeshwa kwa droo ya tano ya promosheni hiyo, Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo bw. Ephraim Mafuru, amesema “Tumeshakabidhi jereta nne kwa washindi mbalimbali na zawadi ya pikipiki, bajaj mbili na gari moja aina ya FORD FIGO ambapo zawadi zote zimeshakabidhiwa kwa washindi wetu .  Hivi karibuni tutasafiri  kwenda Mfinga Mkoani Iringa kukabidhi Bajaj”.
“Naendelea kuwashauri jamii na watanzania kwa ujumla kwamba promosheni hii ni kwa ajili ya kila mtanzania mwenye vigezo vya kushiriki kwa hiyo wajitokeze k kwa wingi kushiriki ili kujaribu bahati kama wenzetu ambao wamejaribu na kupata zawadi kubwa ambazo hawakutarajia katika maisha yao.” Alisema  Mafuru.
Aliongeza kuwa zawadi zinazoshindaniwa gharama yake ni jumla fedha za kitanzania milioni 780 ikiwemo pesa taslimu ambazo mshindi anapata papo hapo kupitia matandao wa simu za mikononi M- pesa. Ikumbukwe kuwa zawadi hizi zinapelekwa hadi pale mshindi wetu alipo bila yeye kuchangia chochote walakugharamia chochote ikiwemo usafiri.
Katika droo hii ya tano mshindi ni Isaya Charles kutoka Igoma mkoani Mwanza ambaye amejishindia Jenereta, wakati mshindi mwingine Mariam Karumba mwanafunzi wa mwaka wa tatu Chuo Kikuu cha Saint Agustin pia anatoka mkoani Mwanza amejishindia Bajaj

Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bidhaa yake bora kabisa ya Serengeti Premium Lager, Tusker Lager and Pilsner inaendesha promosheni hii kwa wiki 16 ikiwa na lengo la kuinua na kuboresha maisha ya wateja wake na watanzania kwa ujumla.

Matukio ya ufunguzi wa mkutano wa AFDB leo jijini Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) leo mjini Arusha .
Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Ivory Cost Dr. Alassane Ouattara (kushoto) akibadilishana mawazo na Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dr.Donald Kaberuka(kulia) wakati wa sherehe za ufunguzi wa  mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) jana mjini Arusha .
Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dr.Donald Kaberuka akihutubia wakati wa sherehe za ufunguzi wa  mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) jana mjini Arusha .
Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Ivory Cost Dr. Alassane Ouattara akihutubia wakati wa sherehe za ufunguzi wa  mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) jana mjini Arusha .
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akipongezwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) Dr. Donald Kaberuka (kulia) mara baada ya kumaliza kutoa hotuba ya ufunguzi wa  mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) jana mjini Arusha . Katikati ni Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Ivory Cost Dr. Alassane Ouattara.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) wakifuatilia kwa makini hotuba ya Rais Kikwete wakati wa ufunguzi wa mkutano huo jana mjini Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete(kulia) akibadilishana mawazo na Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa (kushoto)  wakati wa sherehe za ufunguzi wa  mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) jana mjini Arusha . Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Arusha

WASAMARIA WEMA TWAOMBWA KUMNUSURU MTOTO HUYU ANAYETAABIKA KWA KUWA NA MATUNDU MATATU KWENYE MOYO

 
 Miguu ya NeemaHali ya Neema George inazidi kuzorota siku baada ya siku, miguu ikiwa imevimba, akitaabika katika suala la kula, kuongea na akipata maumivu makali ya tumbo hasa nyakati za usiku.
 Baba mzazi wa Neema, George Mugunga (kushoto) anasema kuwa mnamo mwaka 2010 mara baada ya hali ya mtoto wake kuzorota alimfikisha katika hospitali ya Rufaa Bugando kwaajili ya matibabu, lakini mara baada ya vipimo kufanyika vikaonyesha kuwa moyo wa mtoto wake una matundu matatu.
 Neema akiwa na mwandishi wa habari hizi Albert G. Sengo aliyefika nyumbani kwa bibi wa mtoto huyu eneo la Butimba mkoani Mwanza kwaajili ya kuchukuwa taarifa zaidi.Kutokana na kiwango kilichotamkwa kuwa kinahitajika kwa ajili ya tiba nje ya nchi, familia ya mtoto huyu ilikata tamaa  kabisa na kukata shauri la kumpeleka Sengerema kijijini ili akatibiwe na waganga wa kienyeji ndipo bwana Azizi Bukene (ambaye ni jirani yao) akashauri kuita vyombo vya habari kwaajili ya kulifikisha kwa umma kwa msaada.
Madaktari kupitia kliniki aliyokuwa akipata huduma (Bugando) wamesema kuwa tatizo la neema ni kubwa na haliwezi kupatiwa ufumbuzi hapa nchini bali linaweza kupata tiba Nchini India kwa makadirio ya gharama ya shilingi za kitanzania milioni 25.
 Pichani mtoto Neema George aliyegundulika kuwa na matundu matatu kwenye moyo.Mtoto Neema George (16) amewaomba wasamaria wema wajitokeze kumchangia fedha ili akapate matibabu ya moyo nchini India.
 Familia ya mtoto huyu inategemea kilimo kama sehemu ya kipato cha kuendesha maisha ya kila siku, hivyo uwezo wa kufikisha kiwango hicho cha fedha hata kupata matibabu kwa manufaa ya mtoto huyo kuendelee na masomo ni ndoto za alinacha.
Nje ya nyumba.

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makalla Akabidhi Shilingi Milioni Kumi Kwa Mama wa Marehemu Steven Kanumba Kwa Niaba Ya Serikali, na Kukabidhi Bendera Ya Taifa Kwa Timu ya Taifa ya Mchezo wa Golf

 Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makalla akikabidhi kiasi cha shilingi milioni kumi kwa mama wa marehemu Steven Kanumba ikiwa ni rambirambi ya Serikali kwa familia.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makalla akikabidhi bendera kwa Timu  ya Taifa ya mchezo wa Golf inayotarajiwa kusafiri kwenda  Gaborone Botwsana kwa ajili ya mashindano ya chalenji ya Afrika kwa upande wa Wanawake.Wapili kushoto ni  Mh. Mery Chatanda (Mbunge).Picha na Benjamin Sawe- Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGA MAFUNZO YA WAKUU WA MIKOA, MAKATIBU TAWALA WA MIKOA NA WAKUU WA WILAYA WA TANZANIA BARA MJINI DODOMA JANA, MEI 30

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akiteta jambo na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati alipofika katika Ukumbi wa Mtakatifu Gaspar mjini Dodoma jana, kufunga rasmi Mafunzo ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wa Tanzania Bara, yaliyomalizika mjini Dodoma jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifunga rasmi Mafunzo ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wa Tanzania Bara, yaliyomalizika mjini Dodoma jana.
 Baadhi wa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wa Tanzania Bara, waliohudhuria mafunzo hayo wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya kufunga mafunzo hayo jana.
 Baadhi wa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wa Tanzania Bara, waliohudhuria mafunzo hayo wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya kufunga mafunzo hayo jana.
 Baadhi wa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wa Tanzania Bara, waliohudhuria mafunzo hayo wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya kufunga mafunzo hayo jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akiteta jambo na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati akiondoka  katika Ukumbi wa Mtakatifu Gaspar mjini Dodoma jana, baada ya  kufunga rasmi Mafunzo ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wa Tanzania Bara, yaliyomalizika mjini Dodoma jana.
 

Wanafunzi Chuo Kikuu wabakwa, walawitiwa

Image

Imeandikwa na Sifa Lubasi, Dodoma
 
WANACHUO wa Chuo Kikuu cha St John mjini Dodoma, leo wamegoma kuingia madarasani hadi wawasilishe malalamiko yao kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Zelothe Stephen kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kupigwa nondo, kuibiwa kadi za benki, kompyuta za mkononi, kulawitiwa na kubakwa.

Hali hiyo ilisababisha wanafunzi kukusanyika huku wakiwa wamebeba mabango mbalimbali ambayo yalikuwa yakisomeka, ‘Tunaomba ulinzi ili kubaka na kulawitiwa kukomeshwe’, ‘Ulinzi ni haki yetu ya msingi polisi Mko wapi? Tumechoka kuwa wajinga katika jamii yetu na Ulinzi Shirikishi stop crime.’

Baadhi ya wanafunzi hao walilaani vitendo vya wenzao kubakwa na kulawitiwa na kudai kuwa katika siku za hivi karibuni, mwanafunzi wa kiume ambaye anasoma mwaka mwaka wa pili aliibiwa na kisha kulawitiwa hali iliyolazimu alazwe hospitali.

“Kesi kadhaa zimepelekwa polisi lakini hakuna chochote kinachofanyika,” alisikika mwanachuo moja akizungumza kwa jazba.

Walisema kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na wakati mgumu kutokana na kuibiwa vifaa muhimu zikiwemo kompyuta za mkononi hali ambayo hulazimika kuishi kwa hofu.

“Juzi wenzetu wamevamiwa usiku na kuporwa simu tano na laptop tatu sasa tunaona maisha yanakuwa magumu sana kwetu kwani usalama wetu sasa ni mdogo,” alisema mmoja wa wanafunzi hao.

Walisema hali ni mbaya zaidi kwa wanafunzi ambao wanaishi nje ya chuo kwani hata kujisomea nyakati za jioni kumekuwa kwa mashaka kutokana na kuogopa kuvamiwa na vibaka.

Walisema baadhi ya wenzao wanaanza mitihani Juni, hali ambayo inawatia hofu kama wimbi hilo la kuvamiwa na vibaka linaweza hata kupunguza ufaulu mioungoni mwao.

Pia walitaja sababu kadhaa ambazo zinadhaniwa kuwa zinasababisha matukio hayo ni chuo hicho kukosa uzio na hivyo kufanya mwingiliano wa watu na wanachuo kuingia chuoni bila kuwa na utaratibu.

Walisema kundi lisilojulikana limekuwa na kawaida ya kuvamia sehemu ambazo wanachuo wanakaa na baada ya kuiba vitu mbalimbali humalizia kwa kubaka wasichana au kwa kulawiti kama ni mvulana.

Hata hivyo, juhudi za wanafunzi wao kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma hazikufanikiwa baada ya kuelezwa kuwa alikuwa na majukumu mengine ya kikazi, na kutuma mwakilishi wake ambaye ni Mkuu wa Polisi Wilaya, Dominic Mlei na Mkuu Mpya wa Polisi wa Wilaya atakayeanza kazi hivi karibuni, Thadeus Malingumu.

Kwa upande wake, OCD Mlei alisema ulinzi unaanza rasmi leo, kufanya doria maeneo yanayozunguka chuo hicho na maeneo jirani, pia chuo kijenge hosteli za kutosha na kwa kila hosteli za nje na nyumba walizopanga wanafunzi zitakaguliwa kesho na mapungufu ya kiusalama kwenye makazi hayo yataainishwa na wamiliki wataitwa na hosteli zote zitatakiwa kuwa na mageti na ulinzi wa makazi hayo kuboreshwa.

Pia alitaka kuundwa kwa mara moja kwa vikundi vya ulinzi shirikishi.

Hata hivyo, mtumishi wa Chuo hicho, Mzee Muganda alishauri Kituo Kidogo cha Polisi kijengwe Kikuyu na bidii ya doria iongezwe
Source: Habari Leo Mtandaoni 

USAFIRI WAANZA KUWA WASHIDA MARA BAADA YA WANAFUNZI UDOM KUPEWA BOOM



 Pichani ni Wanafunzi wakigombania Kuwahi nafasi za kukaa katika daladala mapema leo kutokana na Usafiri kuwa Wa Shida
Mara baada ya wanafunzi wengi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) kupewa fedha zao za kujikimu hatimaye usafiri wa kwenda mjini umeanza kuwa ni wa taabu na shida ambapo wanafunzi ukaa kituoni takribani dakika ishirini hadi thelathini wakisubiri daladala wakati wanafunzi hawakupata fedha zao hizo usafiri ulikua sio wa kusumbua na daladala zilikua zinasubiri abiria takribani nusu saa nzima ndio ijaze na kuondoka sasa mambo yamebadilika kutokana na wanafunzi hao kupata fedha na kusababisha usafiri kuwa wa Shida sio wakati wa kwenda mjini tu bali hata kurudi chuo

WANAFUNZI:TUNASOMA MAGAZETI


Wanazuoni wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Wakipitia Magazeti ya leo kutaka kujua kinachoendelea duniani na Tanzania Kwa Ujumla

KILICHOTOKEA MARA BAADA YA BOOM KUINGIA KWENYE ACCOUNT ZA WANAFUNZI UDOM.


RIHANNA AJIACHIA NA PICHA ZAKE ZA JARIDA LA ESQUIRE KWA MARA YA KWANZA KATIKA MTANDAO WA TWITTER


Mwanadada Rihanna ameutumia mtandao wa kijamii aupendao zaidi Twitter, kutoa picha za kwanza alizopiga kwa ajili ya jarida la Esquire. Kama kawaida, Rihanna ametoka bomba kinomanoma! RiRi hakuweka picha peke yake bali aliziongezea maneno ya uchokozi kutoka kwenye wimbo wake ‘Hard’! “They can say whateva, ima do whateva,” Ain’t like me, dat bitch too phony”, na kwenye picha anayoonekana na

Wabunge wa Chadema Waangwa rasmi kwa kuangalia mechi ya kimataifa

Betreff: Wabunge wa Chadema Waangwa rasmi kwa kuangalia mechi ya kimataifa
Baaada ya kazi kubwa ya kuzindua na kuimarisha tawi la chadema Washington Dc Maryland na Virginia,Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Mhe. Peter Msigwa na Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu Dogo janja, Usiku wa Jana Jumatano Mei 30,2011 waagwa rasmi kwa kuangalia mpambano wa kimataifa kati ya US na Brazil ndani ya uwanja wa Fedex, uliopo Landover Maryland Nchini marekani

Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe, Peter Msigwa na Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu Dogo janja, wakiwa na uwongozi wa tawi la Chadema Washington Dc Libe Mwangombe, wanne, Mjomba a.k.a Cosmas, Mzee wa swahilivilla Aboh Shatry wa pili kulia, pamoja na mashabiki wa US, wakiiunga mkono bendera ya taifa. 
Idadi ya wapenzi waliohudhuria katika mpambano huo ni 67,656 wakiwemo Mhe. Nassari Joshua pamoja na Mhe, Peter Msigwa. (Picha maelezo na swahilivilla.blog spot.com)


Wabunge wa chama cha Chadema wakipata flash ya pamoja na warembo wa Kibrazil ndani ya uwanja wa FedexField, uliopo Landover Maryland Nchini marekani. (Picha maelezo na swahilivilla.blog spot.com)


Picha ya pamoja na viongozi wa juu wa Chadema kwenye mpambano wa US na Brazil Usiku wa kuamkia leo Alhamis Mei 31,2012 ndani ya ndani ya uwanja wa Fedex, uliopo Landover Maryland Nchini marekani

Nabendera ya Taifa wakishangilia Bao la kwanza la Brazil lilifungwa kwa Penalti na mchezaji Neymar

Wachezaji wa Brazil wakilinda ngome yao kwa kuwadhibiti timu ya US kwenye mechi hiyo ya kirafiki ambapo timu ya Brazil waliweza kuwabamiza US bao 4-1 nyumbani kwa

US. hoi kwa Brazil baada ya kubamizwa bao nne bao la kwanza lilifungwa na Neymar, na lapili na Thiago mnamo wa dakika ya 11, kipindi cha kwanza. bao la US lilifungwa na Hercules Gomes dakika ya 44 kipindi chakwanza hadi mapumziko Brazil 2 US 1 kwenye mchezo wa kirafiki. (Picha maelezo na swahilivilla.blog spot.com)

WABUNGE PAMOJA NA VIONGOZI WA TAWI LA CHADEMA WASHINGTON DC WATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI




Baada ya kazi pevu ya uzinduzi wa tawi la Chadema jijini Washington Dc wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamtembelea rasmi Balozi wa Tanzania nchini Marekani.



Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar akipata picha ya pamoja na Mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Peter Msigwa ndani ya Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.



Wabunge wa Chadema Mhe. Peter Msigwa wapili kushoto, Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu Dogo Janja, (Watatu kulia), ofisa wa ubalozi Mhe. Peter Msigwa, Kaimu Balozi Mhe Lilian Munanka pamoja na viongozi wa tawi la Chadema Washington Dc wakipata picha ya pamoja na balozi Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar baada ya kumtembelea rasmi siku ya Jumanne Mei 29,2012 Washington Dc Nchini Marekani.

Mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Peter Peter Msigwa akipata picha ya pamoja na waTanzania waishio nchini Marekani, ndani ya Ubalozi wa Tanzania Washington Dc. (Picha na swahilivilla.blogspot.com)

* Media Briefing note for the Global 2013 Smart Partnership Dialogue to be held in DAR ES SALAAM, TANZANIA – 24TH TO 28TH MAY, 2013



Tanzania will host the next Smart Partnership Dialogue that is scheduled to take place from 24th to 28th May, 2013 in Dar es Salaam. President Jakaya Mrisho Kikwete, is expected to officiate the National launch at noon today Tuesday May 29, 2012 at the Karimjee Hall grounds in Dar es salaam. President Kikwete had agreed to host the event during the last dialogue that took place in Putrajaya, Malaysia in June, 2011 - branded the Langkawi International Dialogue.


The Smart Partnership Dialogues are a brainchild of the Commonwealth Partnership for Technology Management. The CPTM which is the social and scientific interlinkage arm of the Commonwealth, has since 1995 undertaken in collaboration with willing national partners to provide a forum that cuts across the east-west, have, have not’s and the developed and developing dichotomy for the discussion of topical subjects in a conducive inclusive, open dialogue. Inspired by the increasing need to ensure a win-win interrelationship between actors, the CPTM, in collaboration with the host country undertake to provide an ambient setting where individuals from all walks of life and professions can meet and hold serious discourse on selected subjects every two years.


To ensure that these dialogues are successful, a two pronged approach is utilized. The first is when the host country convenes a National Dialogue. This involves the gathering together of different sectors of the host community and coming up with a topical issue that is not just locally relevant, but which resonates internationally and merits a grander discourse and focus. The second is when the Host country in collaboration with the CPTM plan for, invite participants and hold an international open dialogue on the selected topic, in essence, host a SMART DIALOGUE. As hosts, the kicking off of the National Dialogue is very crucial.


It is a means for creating National and International awareness of the next host of the Dialogue and avails the opportunity to announce the dialogue venue, topic and dates. The Launch of the National Campaign for the Dialogue in Tanzania will take place on the 29th May, 2012 at the Karimjee Hall Grounds from 10:00 am to 11:00 am. The Host and Patron Advisor for the 2013
Smart Partnership Dialogue, H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania will officially launch preparations for the 2013 Dialogue and introduce the Theme for the Dialogue (Leveraging Technology for Africa’s Socio-Economic Transformation) announce the date for the Dialogue (24th to 28th May, 2013) and the venue (Dar es Salaam) issue a holistic invitation to both the citizens of Tanzania as well as the International Community at large, and share his vision for the Dialogue.




The Dialogue has been branded the GLOBAL 2013 SMART PARTNERSHIP DIALOGUE in anticipation of interest the chosen theme is likely to raise. Technology is a global phenomenon, a global concern, a global topical issue. It is therefore more than likely that a Dialogue on Technology for development shall merit global attention and have a global audience/participation. The Execution of the preparation will be undertaken under the guidance of the Chief Secretary who is the Convener of the Dialogue.




The Chief Secretary will be supported by a National Steering Committee that comprises of Permanent Secretaries from All Ministries as well as Representatives of Keyline Sectors both on Mainland Tanzania and Zanzibar. A Focal Point Team from the Ministry of Foreign Affairs will spearhead the logistical and liaising activities necessary for the successful execution of the Dialogue. The Team will over time incorporate Members from different Links A Resource Group with an Advisory role comprising of key members of the Academia, Business and Corporate Community, Youth, Labour, Culture, Industry and Media has been set up under the leadership of Professor Samuel Wangwe.




Following the National Launch, the next step is scheduled to be contact with different Links within Tanzania who will in turn be linked with counterparts interested in participating in the Dialogue in 2013. A National Dialogue to discuss the theme will follow thereafter. Other African countries that have hosted the Smart Partnership Dialogues include Botswana, Namibia, Zambia, Zimbabwe, Mozambique, Swaziland, Lesotho and Uganda that has hosted it twice. Other countries include Barbados, and Malaysis that has hosted the dialogue nine times.


Issued by
THE FOCAL POINT TEAM, GLOBAL 2013 SMART PARTNERSHIP DIALOGUE, MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION

Uzinduzi rasmi watawi la Chadema Washington Dc na viongozi wa juu wa chadema‏

 Uongozi wa juu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  katika uzinduzi rasmi watawi la Chadema Washington Dc  kwenye meza ya juu wa kwanza kushoto Libe Mwangombe, akifatiwa na Mhe. Peter Msigwa,  Mwenyekiti wa tawi Mhe. Kalley Pandukizi,  Mhe. Zitto Kabwe, na Mhe. Nassari Joshua, Dogo Janja, mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Mirage Hall uliopo University Of Bld, Hysattsville, Maryland Nchini Marekani
 Mhe. Leticia Nyerere
  Mhe. Maryam Msabaha
 Baadhi ya wakereketwa wachukua kadi baada ya uzinduzi wa tawi la chadema Washington




Mhe. Zitto Kabwe akitoa hutba kuelezea mpango mzima wa mambo yanavyoendelea nchini Tanzania