Thursday, July 26, 2012

Watatu wafa katika ajali tofauti tofauti mkoani Dodoma



Na. Luppy Kung’alo, Jeshi la Polisi Dodoma

Watu watatu wamepoteza maisha katika matukio matatu tofauti ya Ajali za Usalama Barabarani jana na kuacha wengine majeruhi katika Mkoa wa Dodoma.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Bw. Edmund Urio alisema tukio la kwanza lilihusisha Mpanda PikiPiki kugonga Mkokoteni ambalo lilitokea siku ya Jumatano tarehe 26/07/2012 majira ya saa sita na dakika tano usiku katika Barabara kuu ya Dodoma /Morogoro eneo la Kibaigwa Wilayani Kongwa

Akizungumzia tukio hili Bw. Edmund Urio alisema kwamba Piki Piki No. T. 202 BDH aina ya FERICON iliyokuwa ikiendeshwa na Joseph Hekela mweye umri wa miaka (27) Mkazi wa kibaigwa iligonga Mkokoteni kwa nyuma uliokuwa ukiendeshwa Barabarani na kusababisha kifo kwa Mpanda pikipiki huyo.

Kamanda Edmund Urio alisema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa mwendesha Pikipiki kwa kutofuata sheria kwani hakupaswa kuwa katika mwendo wa kasi, na kwa mujibu taratibu taa zake zinapaswa kumulika umbali wa mita mia tatu hivyo alipaswa kuuona mkokoteni huo uliokuwa mbele yake.

“Muendesha Mkokoteni naye ana makosa kwani muda wa chombo hicho kutumia Barabara mwisho wake ni saa kumi na mbili jioni, sasa mpaka muda huo wa saa sita usiku kuwepo barabarani ni makosa” Alifafanua Kamanda Urio

Bw. Edmund Urio alisema Muendesha Mkokoteni huo  amekimbia na anatafutwa kwa kosa la kuendesha mkokoteni kwa muda usioruhusiwa na pindi atakapo kamatwa atachukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zinavyotaka.

Katika ajali nyingine iliyohusisha mpanda Pikipiki kuwagonga watembea kwa miguu na kusababisha kifo na majeruhi, Kamanda Edmund Urio Alisema ilitokea mnamo tarehe 25/07/2012 majira ya saa moja na dakika saba jioni (19:07hrs) katika eneo la Ipagara Kata ya Ipagara na Wilaya ya Dodoma kwenye Barabara kuu ya Dodoma/Morogoro.

Akizungumzia ajali hiyo alisema Pikipiki No. T. 662 BKC aina ya LIFAN iliyokuwa ikiendeshwa na mtu asiyefahamika  jina  iliwagonga watembea kwa miguu wawili na kusababisha kifo cha mmoja wao aliyejulikana kwa jina la Theresia Chansi mwenye umri wa miaka (37) mgogo na mkazi wa Ipagara amabaye alifariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.

 “Katika Ajali hiyo kulikuwa na majeruhi wawili ambao ni Mpanda Piki Piki mwenyewe ambaye amepoteza fahamu na amelazwa wodi namba (1) pamoja na Magreth Daniel mwenye umri wa miaka (40) na mkazi wa Ilazo mjini Dodoma ambaye naye amelazwa katika hospitali hiyo ya mkoa wodi namba (10).” alieleza Bw. Edmund Urio.

Kaimu Kamanda huyo wa Mkoa wa Dodoma alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo wa kasi aliokuwa akiendesha mpanda Pikipikki huyo, uliosababisha kushindwa kudhibiti Piki piki yake wakati wakinamama hao walipokuwa wakivuka barabara.

Aidha katika tukio la tatu Kamishna Msaidizi huyo wa Jeshi la Polisi Bw. Edmund Urio alisema gari No. T 668 AYQ aina ya FUSO lilokuwa likiendeshwa na Bw. Philipo Wami mwenye umri wa miaka (30) mkazi wa Msanga liliacha njia na kupinduka kisha kusababisha kifo kwa mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Henry Wami mwenye umri wa miaka (19) na mkazi wa Msanga.

Alisema ajli hiyo lilitokea tarehe 25/07/2012 majira ya saa moja kamilia asubuhi (07:00 hrs) katika maeneo ya Kijiji cha Msanga Wilaya ya Chamwino.

Kamanda Edmund Urio alisema Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kutokana na kushindwa kufanya kazi kwa mfumo wa usukani, uliosababisha gari hiyo kupoteza muelekeo na kupinduka.

Hata hivyo Kamanda Edmund Urio amewaasa watumiaji wote wa barabara kuwa makini na matumizi sahihi ya bararabara ikiwa pamoja na kufuata na kuheshimu sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.

Azania Bank gives 65m/- to supports slam upgrading project

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI MHE. DKT. CHARLES TIZEBA (MB) AFANYA ZIARA KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM JANA


Meneja Msaidizi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bi. Winnie Mulindwa, akitoa taarifa ya namna Bandari ya Dar es Salaam inavyofanya kazi kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba (aliyeshika kichwa), ambaye amefanya ziara ya siku moja katika Bandari ya Dar es salaam. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Omar Chambo, Kulia kwa Katibu Mkuu ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Bw. John Mngodo, Kushoto kwa Meneja Bandari Msaidizi ni Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Uchukuzi,Bi. Tumpe Mwaijande.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kupakua na kupakia makontena Bandarini (TICTS), Bw. Neville Bisett akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba (Mwenye Suti ya Mikono Mifupi),wakati alipofanya ziara ya siku moja kuangalia ufanisi wa Kampuni hiyo katika Bandari ya Dar es Salaam leo.Kulia kwa Naibu Waziri ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,Bw. John Mngodo.

Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba akifafanua jambo kwa uongozi wa Wizara, Bandari na Mkurugenzi Mtendaji wa Kitengo cha Kupakia na kupakua makontena TICTS, kulia kwa Naibu Waziri ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bw. John Mngodo, Kushoto kwa Naibu Waziri ni Meneja Msaidizi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bi Winnie Mulindwa, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo(aliyevaa tai ya blue), Mhandisi Omar Chambo, na Kulia kwa Katibu Mkuu ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kupakua na Kupakia Makontena (TICTS), Bw. Neville Bisett.


Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dkt. Charles Tizeba (Mb),akiongea na baadhi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(hawapo pichani),wakati alipotembelea Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam,Kushoto kwa Naibu Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo, Naibu katibu Mkuu wa Wizara hiyo (wa pili kushoto),Bw. John Mngodo. Na aliyevaa Kizibao ni Meneja Msaidizi wa Bandari ya Dar es Salaam,Bi. Winnie Mulindwa.(Picha Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)



Bajeti ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia yapitishwa kwa mwaka 2012/13

Watu wazidi kujinyakulia zawadi za promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO ya SBL


SERIKALI IMESEMA HAIJADHULUMU MALIPO YA WAHANGA


ZITTO KABWE:NISIHUSISHWE NA MATAMSHI NA MAKANUSHO WA WABUNGE WALIOKUWA KIGOMA


Mafunzo 1st EAC-GIZ Masterclass Photography yaendelea Arusha


MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM LEO


RAIS WA ZANZIBAR DKT SHEIN AMUAPISHA WAZIRI WAZIRI MPYA WA MIUNDOMBINU BAADA YA WA AWALI KUTANGAZA KUJIUZULU JUZI




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Rashid Seif Suleiman, kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano, wakati wa  hafla fupi iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar jana

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Sheikh Daudi Khamis Salim,  kuwa Kadhi wa Rufaa Pemba, wakati wa hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar jana.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, akisalimiana na Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kiapo cha Waziri Mpya wa Miundombinu,Rashid Seif Suleiman, katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar Jana.Picha na Ramadhan Otrhman,Ikulu