Thursday, November 29, 2012

WAZIRI KUU MIZENGO PINDA AZINDUA MPANGO WA KUTOKOMEZA MALARIA UNAOITWA “MALARIA SAFE


 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi wakati akiwasili kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam kwa ajili ya kuzindua rasmi kampeni ya kupambana na Malaria inayoitwa “Malaria Safe Companys” ambapo Wizara ya afya inashirikiana na pamoja na taasisi za kimataifa na  Makampuni mbalimbali pamoja na Sekta ya michezo, ambapo wadau mbalimbali wameshiriki katika uzinduzi huo unaofanyika usiku huu jijini Dar es salaam, kulia ni Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Raymond Mushi.
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akizungumza na Rais Washirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF Bw. Leodger Tenga wakati alipowasili katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam  kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni ya kupambana na ugonjwa wa Malaria, kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi.
 
Wadau waliohudhuria katika uzinduzi wa kampeni ya kupambana na ugonjwa wa malaria kutoka kulia ni Mkurugenzi wa michezo katika Wizara ya Habari, Vijana , Michezo na Utamaduni Bw. Leonald Thadeo, Assah Mwmbene Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Mbunge wa Jimbo la Temeke Mh. Abbas Mtemvu na Mbunge na Waziri wa zamani Mh. Chrisant Mzindakaya.
 
Wadau mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo  katika Hyatt Regency Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Sahara Media Bw. Samwel Nyala kushoto akiwa na wadau wengine katika uzinduzi huoHyatt Regency Dar es Salaam.
 
Wadau mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi huo kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam
 
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiandika kitu huku Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh. Hussein Mwinyi akipiga makofi katika uzinduzi huo.
 
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Azam Mzee Salim Mohamed Abeid Bakhressa akitoa ushuhuda kuhusu malaria ilivytokomezwa katika viwanda vyao.
 
Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini  TFF Bw, Leodger Tenga akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo jinsi sekta ya michezo ilivyosaidia kutokomeza malaria nchini.
 
Mwimbaji nguli wa muziki wa Taarab Khadija Kopa pamoja na kundi lake wakitumbuiza katika hafla hiyo iliyofanyika usiku huu kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam
 
Meneja Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena akiwa katika hafla hiyo, Bodi ya Utalii nchini TTB ni moja ya taasisi zilizotambuliwa na Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda katkatika hfla hiyo kwa juhudi zake za kupamana na ugonjwa wa malaria.

IKULU:VIONGOZI WAKUU WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAZINDUA JENGO LA MAKAO MAKUU YA JUMUIYA JIJINI ARUSHA


Mfano wa  jengo la Makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiangalia mfano wa jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya hiyo pamoja na maelezo yake baada ya kulifungua rasmi  Novemba 28, 2012 jijini Arusha
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifunua pazia  kufungua rasmi jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya  Novemba 28, 2012 jijini Arusha
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakikata utepe kufungua rasmi jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya  Novemba 28, 2012 jijini Arusha
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki  wakitembelea sehemu mbali mbali za jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya  baada ya kulifungua rasmi Novemba 28, 2012 jijini Arusha
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki  wakitembelea sehemu mbali mbali za jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya  baada ya kulifungua rasmi Novemba 28, 2012 jijini Arusha. Hapa ni katika chumba cha mahakama ya jumuiya hiyo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki  wakishuhudia Mwenyekiti wa Jumuiya Rais Mwai Kibaki wa Kenya akizindua rasmi mfumo wa kisasa wa kuunganisha shughuli za ushuru wa forodha kwa njia ya mtandao katika  jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya  baada ya kulifungua rasmi Novemba 28, 2012 jijini Arusha
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki  wakiwa katika chemba ya mikutano ya Bunge la Jumuiya ya Afrika mashariki katika jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya  baada ya kulifungua rasmi Novemba 28, 2012 jijini Arusha
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wakuu wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na wadau pamoja na wabunge wa Afrika Mashariki.Picha na IKULU

WADAU WA TAKWIMU NCHINI WAKUTANA KATIKA KONGAMANO LA PILI LA MWAKA JIJINI DAR LEO

 Mkurugenzi wa Takwimu nchini, Morrice Oyuke, akisoma hotuba yake kumwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa  TAKWIMU nchini Dkt.. Albina Chuwa, wakati wa kongamano la pili la mwaka la wadau wa TAKWIMU nchini lililofanyika leo jijini Dar es Salaam. 
 Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia, Thomas Danielewitz, akitoa hotuba yake  leo jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa kongamano la pili la mwaka kwa  Wadau wa Takwimu nchini.  Kongamano hilo la siku moja limefunguliwa na Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Saada M. Salum (hayupo Pichani).
 Baadhi ya washiriki  wa kongamano la pili  la mwaka unaowashirikisha  Wadau wa Takwimu nchini  wakimsikilza Naibu Waziri wa Fedha Dr. Saada M. Salum (hayupo pichani) katika ufunguzi wa kongamano hilo leo jijini Dar es Salaam.
 Naibu wa Wizara ya Fedha Dkt. Saada M. Salum akifungua kongamano la pili la mwaka kwa wadau wa Takwimu nchini leo jijini Dar es Salaam., ambapo amewasisitiza  wadau kutumia takwimu zilizo  sahihi. Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO

WANAFUNZI MACHANGUDOA KATIKA CHUO KIKUU CHA DODOMA ( UDOM ) WAANZA KUSAKWA


RAIS wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOSO), Paul Yunge, amesema kuwa wanafanya uchunguzi wa kina ili kuwanasa wanafunzi wa chuo hicho wanaojihusisha na biashara ya kujiuza kimwili ili wawachukulie hatua.

Yunge alifafanua kuwa, wanafunzi watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo watachukuliwa hatua kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa wengine.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Yunge alisema kazi ya kufanya uchunguzi tayari imeanza na wanategemea wakati wowote watabaini ukweli kuhusiana na jambo hilo.

Alifafanua kuwa, wanafunzi wanaojihusisha na vitendo hivyo wanakidhalilisha na kukishushia heshima chuo hicho ambacho kimsingi kinapaswa kuwa kioo.

“Ni aibu sana kama watu wamekuja UDOM kusoma na badala yake wanageuka na kufanya biashara ya kujiuza ambayo ni ya kudhalilisha utu wao pamoja na chuo kwa ujumla. Jambo hili lazima tulifanyie kazi,” alisema.

Yunge alidai kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya taarifa hiyo kuripotiwa na vyombo vya habari, kitendo ambacho kimeisononesha nchi nzima ukiwemo uongozi wa chuo pamoja na wazazi wa wanafunzi hao.

Hatua ya serikali ya chuo kuanza uchunguzi imekuja baada ya baadhi ya vyombo vya habari wiki iliyopita kuripoti kuwa baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho wanajiuza katika sehemu mbalimbali za mji wa Dodoma.

SAFARI YA MWISHO YA SHARO MILIONEA MCHANA HUU....





 Mwili wa Marehemu Sharo Milionea ukiswaliwa mapema mchana huu kabla ya kupelekwa kwenye nyumba yake ya milele 
 Rafiki mkubwa wa marehemu Sharo Milionea,Mzee Majuto akiwa ameshikwa mkono wakielekea kwenye mazishi mapema mchana huu,Muheza mkoani Tanga.

POLISI AFUKUZWA KAZI BAADA YA KUMBAKA MTUHUMIWA WA KIKE


JESHI la Polisi mkoani Mbeya limemfukuza kazi askari wake Enock Daffa (22) kwa tuhuma za kufanya  mapenzi na mtuhumiwa wa kike mwenye umri wa miaka 25 katika Kituo cha Polisi cha Mji mdogo wa Tunduma, Wilaya ya Momba, mkoani hapa. 


Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani, askari huyo alitenda kosa hilo Novemba 21,2012 na kwamba mtuhumiwa aliyefanya naye mapenzi alikuwa akikabiliwa na kosa la wizi.
Kamanda Athumani alisema kuwa mbali ya kufukuzwa kazi askari huyo tayari amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Aidha alisema kuwa hali kama hiyo haitaweza kuvumiliwa na Jeshi la Polisi na kwamba atakayebainika kufanya tukio kama hilo adhabu yake itakuwa ni kufukuzwa kazi.
Kamanda huyo alitoa wito kwa askari polisi kufanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni za Jeshi la Polisi kama mwongozo unavyowaagiza ili kulinda maadili ya Jeshi la Polisi ambacho ndicho chombo kinachotumika na wananchi katika kuzisimamia sheria.
Akizungumzia tukio hilo, baba mzazi wa askari huyo alisema kuwa kitendo alichofaya mtoto wake si cha kiungwana ambacho pia kimetia fedheha familia yake pia kwa jeshi la Polisi ambalo limepewa dhamana ya kutunza usalama wa raia na mali zake.

WAZIRI WA HABARI AFUNGUA MKUTANO WA MA-RAS JIJINI DAR LEO

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akifungua Mkutano baina ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na wajumbe wa Kamati za Michezo za Mikoa Tanzania Bara “Ma-RAS” (hawapo pichani) Jijini Dar es Salaam.Mkutano huo unalengo la kujadili maendeleo ya Michezo nchini.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akisalimiana na RAS wa Njombe mara baada ya kufungua kufungua Mkutano baina ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na wajumbe wa Kamati za Michezo za Mikoa Tanzania Bara Ma-RAS Jijini Dar es Salaam.Mkutano huo unalengo la kujadili maendeleo ya Michezo nchini. (Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM).

Bendi ya Mashujaa kuzindua Risasi Kidole Leaders leo

BENDI ya Mashujaa leo inazindua albamu yake ya pili ijulikanayo kwa jina la Risasi Kidole pamoja na bendi maarufu ya Congo, Wenge BCBG iliyochini ya mwanamuziki JB Mpiana kwenye  viwanja vya Leaders club.
.................................. 
Uzinduzi huo umepangwa kuanza saa 2.00 usiku na maandalizi yake yamekwisha kamilika kwa mujibu wa meneja wa bendi ya Mashujaa, Martin Sospeter. Sospeter alisema kuwa wamejiandaa vilivyo katika uzinduzi huo na lengo lao kubwa ni kuweka historia katika muziki wa Tanzania.
Alisema kuwa wamekaa kambini muda wa siki mbili na wameandaa vitu vingi vipya kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki wa muziki wa dansi nchini. Alisema kuwa kuna rap ya Ua Mbu na Dume la Simba kutoka kwa marapa wao, Saulo Ferguson na Sauti Radi.
Alifafanua kuwa wanamuziki wake wameadhimia ‘kufunika’ katika uzinduzi huo kwani anahistoria nzuri katika muziki wa Tanzania na kufanya kazi katika bendi nyingi.

“Tunawaomba watanzania waje waone nini tunakifanya mbele ya gwiji la muziki wa dansi Afrika, JB Mpiana, najua wao wamepania, lakini sisi tumepania vilivyo kusafisha nyoyo za mashabiki ambazo kwa sku nyingi hawajapata burudisha la mioyo zao,” alisema.

Kiongozi wa bendi hiyo, Charlz Baba alisema kuwa wamepania kutoa somo kwa wanamuziki wa dansi hapa nchini ambao wamekuwa wakisubiri waone watafanya nini. Alisema kuwa wameandaa nyimbo nyingi nzuri  na wamepatia kutawala soko la muziki hapa nchini.

“Njooni muone nini tunafanya katika muziki wa dansi, kambi yetu imekuwa nzuri na mafanikio makubwa, naomba mashabiki waje kutuunga mkono nasi tutawaunga mkono kwa kutoa burudani safi,”alisema Chalz.

Albamu ya Risasi Kidole ina jumla ya nyimbo sita. Nyimbo hizo ni Umeninyima, Tikisika, Hukumu ya Mnafiki, Ungenieleza, Kwa Mkweo na wimbo uliobebab jina la albamu hiyo, Risasi Kidole.

SERIKALI YAZINDUA BARAZA LA WATAALAM WA KUREKEBISHA UPEO WA MACHO KUONA,PIA YAKABIDHI MAGARI 9 NA PIKIPIKI 107 KUSAIDIA HUDUMA ZA AFYA NCHINI

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wataalam wa Kurekebisha Upeo wa Macho Kuona nchini leo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la wataalam wa kurekebisha upeo wa macho kuona nchini Adam Simbeye (kulia) akiwaeleza wajumbe malengo ya baraza hilo ya kusimamia, kudhibiti na kuratibu utoaji wa huduma bora za macho nchini yanayofanywa na baraza hilo kwa mujibu wa sheria ya Optometria Na.12 ya mwaka 2007. Kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi.
Wajumbe wa Baraza la Wataalam wa Kurekebisha Upeo wa Macho Kuona nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi (Katikati) mara baada ya kuzinduliwa kwa baraza hilo leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dkt. Hussein Mwinyi (kushoto) na mwakilishi wa Shirika la UNFPA nchini Tanzania Bi.Mariam Khan (kulia) kwa pamoja wakisaini nyaraka za kukabidhi magari 9 ya kubebea wagonjwa na pikipiki 107 kwa ajili ya kupelekwa katika maeneo mbalimbali kusaidia huduma za afya.
Mwakilishi wa Shirika la UNFPA nchini Tanzania Bi.Mariam Khan (kulia) akimkabidhi funguo za gari la kubebea wagonjwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi (kushoto) akimkabidhi funguo za gari la kubebea wagonjwa mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Bukombe Dkt.Archard Rwezahura (katikati) leo jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia makabidhiano hayo ni mwakilishi wa Shirika la UNFPA nchini Tanzania Bi.Mariam Khan.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

Saturday, November 24, 2012

KASHFA YA NGONO CHUO KIKUU CHA UDOM (DODOMA) WANAFUNZI WAJIUZA USIKU KWENYE KUMBI ZA STAREHE

SHILOLE ANUSURIKA KUKAMATWA NA POLISI BAADA YA KUHISIWA KUWA ANA MISOKOTO YA BANGI


MSANII wa anayefanya vizuri kwenye muziki na filamu Shilole, amenusurika kumakatwa na polisi baada ya kuhisiwa kuwa na misokoto ya bangi ndani ya gari lake na kusababisha kuhojiwa kwa dakika kadhaa maeneo ya Kinondoni.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana ambapo msanii huyo inadaiwa alikuwa akitokea kwenye ishu zake ndipo maafande hao waliokuwa wakitokea kwenye malindo yao walipomdaka na kumpeleka pembeni kwa lengo la kufanya upekuzi kwenye gari yake.

Inadaiwa kuwa polisi hao hawakukuta kitu chochote zaidi ya sigara za mpenzi wake, ambaye walikuwa wote usiku huo na hata hivyo hawakuwa na dalili zozote za kuwa wamelewa.

Shilole alipozungumza na mwandishi wetu alidai kuwa tukio hilo lilimshangaza sana kwani hakuwa na bangi ndani ya gari lake na hajawahi kutumia kitu hiyo lakini polisi hao walimuhoji kana kwamba anatumia bangi.

Alidai kuwa kuna baadhi ya watu walitaka kumfanyia mchezo mchafu lakini walishindwa kwani alikuwa makini katika kila jambo ambalo alikuwa akilifanya usiku huo, na alipoulizwa kuwa usiku huo alikuwa anatoka wapi alidai kuwa katika harakati zake za hapa na pale.

Mwanamke anayetuhumiwa kumtesa kumlisha kinyesi na kumchoma moto mtoto wa kaka yake kumfungia ndani, amepandishwa kizimbani kwa mara ya pili katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya kujibu shtaka linalomkabili.



Mtuhumiwa Wilvina Mkandala (24)


Hataki kabisa kuonyesha sura yake

Aneth akiwa na wazazi wake mahakamani jana

Akirudishwa tena rumande mpaka tena tarehe 27/11



Baadhi ya akina mama wakiwa nje ya mahamaka wakisubiria kumwona mama huyo mwenye roho mbaya

Akina mama hao wakiwa na hasira kali walisikika wakisema tuachieni kidogo tumfunze adabu