Mwanamuziki muimbaji Rehema
Chalamila maarufu kama RayC amekumbwa na tatizo kubwa la kuathirika na
madawa ya kulevya. Kwa sasa yumo katika hatua za matibabu ya kujaribu
kuondokana na tatizo hilo.
Kwa kadri ya maelezo ya mama yake
dawa ambazo anahitaji kuzitumia ili kuponi ni gharama na pia kama wote
tunavyofahamu pia mgonjwa yoyote anatakiwa kula vizuri, mzigo huu ni
mkubwa kwa huyu mama, kwa hiyo kunahitajika msaada wa kubeba mzigo huo.
Wapenzi wa muziki wa binti huyu na
watu wenye mapenzi mema tunaweza kumsaidia mama huyu kwa kumtumia kiasi
chochote cha fedha kwa kutumia huduma ya tigo pesa kupitia namba
0655999700
Natanguliza shukrani kwa wote watakao weza kutoa msaada wowote kwa ajili ya matibabu ya mwenzetu
Habari hii kwa hisani ya Mzee Kitime-Mwanamuziki Mkongwe hapa nchini.
RAIS KIKWETE AMPA POLE KATIBU WA MUFTI WA ZANZIBAR ALIYEMWAGIWA TINDIKALI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali na kumpa pole Katibu wa
Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhili Soraga ambaye amelazwa katika chumba
cha dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufuatia majeraha ya
usoni na kifuani yaliyotokana na kurushiwa Tindikali na watu
wasiojulikana wakati akifanya mazoezi katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe
mjini Unguja juzi. Rais ambaye amerejea leo Jumanne Novemba 6, 2012
akitokea katika ziara ya kikazi ya takriban juma moja katika mikoa ya
Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida, amemtakia Sheikh Soraga nafuu
ya haraka.PICHA NA IKULU
KUTOKA VIWANJA VYA BUNGENI MJINI DODOMA JANA
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Kibakwe na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, Bungeni Mjini Dodoma Oktoba 6, 2012. |
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda Magalle kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma, Oktoba 6,2012. |
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongea na Mbunge wa Mpedae, Salim Hassan Abdullah Turky kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma,Oktoba 6, 2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) |
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA 8 WA KIMATAIFA WA BIMA JIJINI DAR JANA
Makamu
wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akihutubia wakati akifungua mkutano wa 8 wa Kimataifa wa Bima, ulioanza
leo katika ukumbi wa Blue Peal, jijini Dar es Salaam. Mkutano huo
unatarajia kumalizika Novemba 8 mwaka huu.
Baadhi
ya washiriki wa Mkutano huo wa Kimataiafa wa Bima, kutoka mataifa mbalimbali
wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, wakati akihutubia, katika ukumbi wa Blue Peal, leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akifurahia ngoma ya asili wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa Blue Peal, jijini
Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kufungua mkutano wa 8 wa Kimataifa wa Bima,
ulioanza leo Novemba 6, 2012 ukitarajia kumalizika Novemba 8, mwaka huu.
BODABODA JIJINI MBEYA WAVAMIA KITUOCHA KUUZIA MAFUTA KWAAJILI YA KUHAKIKISHIWA KWELI HAKUNA MAFUTA AU YANAFICHWA
VIJANA WA BODA BODA WAKIWA WAMEVAMIA KITUO CHA ORXY KUTAKA KUJUA KAMA KWELI KUNA MAFUTA AMA LAH.
HAPA KILA MTU ANATAKA KUSHUHUDIA KAMA MAFUTA YAPO AMA LAH
MENEJA
WA KITUO HICHO ALIYE VAA SHATI JEUPE AKIJARIBU KUWATULIZA WATEJA AMBAO
WANA JAZBA KUBWA YA KUTAKA KUJUA KAMA KUNA MAFUTA AU LAH , NA KUWAMBIA
KUWA WANGOJE KWANZA ACHUKUE VIFAA ILI AWAONESHE KUWE KWELI HAKUNA
MAFUTA.
MKUU
WA POLISI WILAYA YA MBEYA NAE ALIKUWEPO ENEO LA TUKIO,KUWATULIZA VIJANA
HAO NA KUWAHAKIKISHIA KUWA WATAONESHWA KUWA KWELI HAKUNA MAFUTA KATIKA
ENEO HILO.
HAPA KATI KATI WANAPO TAZAMA NDIPO KWENYE TANK LA MAFUTA , VIJANA WANANGOJA KUSHUHUDIA.
Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga Amwagiwa Tindikali na Watu Wasiojulikana
Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akitolewa katika Chumba
cha Huduma ya Mwanzo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya kurushiwa
Tindi kali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazowezi huko katika
Kiwanja cha Mwanakwerekwe.
Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akipandishwa kwenye
Gari ya Wagonjwa kwa lengo la kuwahishwa katika Hospitali ya Muhimbili
Dare es Salaam baada ya kurushiwa Tindi kali na watu wasiojulikana
wakati akifanya mazowezi huko katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe.
Wananchi mbalimbali wakishuhudia Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh
Fadhil Soraga akiwahishwa katika Hospitali ya Muhimbili Dare es Salaam
baada ya kurushiwa Tindi kali na watu wasiojulikana wakati akifanya
mazowezi huko katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe.Picha na Yussuf Simai-Maelezo Zanzibar
No comments:
Post a Comment