Wednesday, June 26, 2013

MFALME MSATWI AWASILI LEO JIJINI DAR TAYARI KWA KUHUDHURIA MKUTANO WA SMAT PARTNERSHIP JUNI 28


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Mfalme Mswati wa (ii) wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam leo Juni 26, 2013. Mfalme Mswati wa ii, ametua nchini kwa ajili ya
kuhudhuria Mkutano wa 'Smat Patnership' unaotarajia kuanza Juni 28 mwaka huu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mfalme Mswati ii, baada ya
kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Juni 26, 2013. Mfalme Mswati wa ii, ametua nchini kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 'Smat Patnership' unaotarajia kuanza Juni 28 mwaka huu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Mfalme Mswati ii, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Juni 28, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 'Smat Patnership', unaotarajia kuanza Juni 28. Kushoto ni mke wa Mfalme Mswati. Picha na OMR.

Minister for Foreign Affairs and International Co-operation Bernard Membe Receives copies of Credence from Designate Ambassador of Trinidad and Tobago

 Hon. Bernard K. Membe says goodbye to Designate Ambassador Patrick Edward of Trinidad and Tobago at the end of their discussion. 
 Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation welcomes Designate Ambassador Patrick Edward of Trinidad and Tobago to the United Republic of Tanzania with offices in Kampala, Uganda.
Hon. Bernard K. Membe receives copies of Credence from the Designate Ambassador Edward of Trinidad and Tobago, earlier today  in his office in Dar es Salaam.
 Ambassador Designate Edward explaining gas programs his country has during his discussion with Hon. Membe (not in the photo), earlier today.
 Minister Membe explains something during his discussion with Designate Ambassador Edward of Trinidad and Tobago.
Minister Membe in a discussion with Designate Ambassador Edward of Trinidad and Tobago.  Also in the photo is Ms. Agnes, Foreign Service Officer in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation.All photos by Tagie Daisy Mwakawago -Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation

TIGO KUFANYA TAMASHA KUBWA LA KABANG JUMAPILI HII NDANI YA CCM KIRUMBA MWANZA

 Meneja Chapa wa Tigo Tanzania Bw. William Mpinga akiongea na waandishi wa habari kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litakalofanyika siku ya jumapili hii bure kabisa katika viwanja vya  CCM Kirumba jijini Mwanza, kushoto msanii Diamond Platnumz na kulia msanii Madee ambao watatoa shoo siku hiyo na wasanii wengine.
 Msanii wa bongo flava Diamond Platnumz akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litalofanyika mjini Mwanza siku ya jumapili pembeni yake Meneja Chapa wa Tigo Tanzania Bw. William Mpinga.
 Msanii Madee akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litalofanyika mjini Mwanza siku ya jumapili pembeni yake ni Meneja Chapa wa Tigo Tanzania Bw. William Mpinga na Diamond Platnumz .
  Msanii Richie Mavoko akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litalofanyika mjini Mwanza siku ya jumapili kulia kwake ni Msanii Madee, meneja wa Tigo Bw. William Mpinga na Diamond Platnumz.
Wasanii Diamond Platinumz, Madee wa Tip Top na Richie Mavoko katika picha ya pamoja na Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga. Wasanii wengine watakaokuwepo ni Fid Q,  Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, Recho na Kazi Kwanza.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI        
Tamasha la Tigo Mini Kabaang kufanyika jijini Mwanza
Dar es Salaam, Juni 26, 2013 – Msanii Bora wa mwaka Diamond Platnumz, Fid Q na wasanii wengine sita wanatarijiwa kupagawisha mashabiki zaidi ya elfu sitini katika tamasha la Tigo Mini Kabaang litakayofanyika jijini Mwanza (Rock city) Jumapili hii ya Juni 30.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tamasha hilo, Meneja wa Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga alisema kwamba lengo la tamasha hilo ni kujenga mahusiano ya karibu na wateja wao kwa  kutumia sanaa ya muziki kama njia ya kutangaza huduma za Tigo na bidhaa zake za vifurushi kwa wateja wengi zaidi.
“Tunaamini kwamba tamasha hili litajenga mazingira mazuri yakufanya kampuni na wateja wetu kuelewana zaidi.  Mwisho wa siku tunatarajia wateja wetu kujumuika nasi, kupata burudani yakutosha na kuelimishwa zaidi kuhusu huduma zetu mbali mbali zenye ubora na unafuu kama Mini Kabaang,” alisema Mpinga.
Mini Kabaang inatoa muda wa maongezi wa dakika 20 za bure, 50MB ya kifurushi cha intaneti, pamoja na ujumbe mfupi 100 kwa shilingi 475 tu kwa siku. 
Mkutano huo wa waandishi wa habari pia ulihudhuriwa na wasanii wakubwa kama Madee wa Tip Top, Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, Richi Mavoko, Recho, Kazi Kwanza, Diamond Platnumz na Fid Q, ambao ndio wasanii wa Bongo Fleva watakaopamba siku hiyo ya Jumamosi katika viwanja vya CCM Kirumba kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 12 jioni.
“Mimi pamoja na wasanii wenzangu tunayo furaha kubwa kushiriki katika tamasha la Tigo Mini Kabaang litakalofanyika jijini Mwanza, hakika watu wa Rock city ni washabiki wakubwa wa muziki wetu, na tunatarajia kwenda kuwapa burudani ya kutosha,” alieleza Diamond Platnumz alipoulizwa kuhusu tamasha hilo.
“Binafsi nina furaha yakipekee kufanya tamasha langu la kwanza la wazi jijini Mwanza. Naamini hao mashabiki elfu sitini na zaidi wataonyesha  mapenzi ya dhati kwa muziki wangu. Ninahamu sana ya kufika na kufanya tamasha hii,” aliongeza super staa huyo. 
“Tamasha hili la Tigo Mwanza Mini Kabaang pia litawapa fursa mashabiki kujishindia zawadi mbali mbali kama vile simu, vocha, fulana za nembo ya Tigo na nyingine nyingi. Hakutakuwa na kiingilio siku hiyo, tunapenda kuwakaribisha kila mteja wa Tigo na mshabiki wa bongo fleva kujumuika na kushiriki nasi,” aliongezea Mpinga.
“MINI KABAANG” ni kifurushi cha siku ambacho mteja akijiunga anapata dakika 20 za muda wa maongezi ambazo anaweza kuzitumia kupiga simu kwenda mtandao wowote ule, pia anapata kifurushi cha 50MB ya intaneti na kuweza kutuma ujumbe mfupi 100 kwa mtandao wowote. Kutumia kifurushi hiki mteja anabidi apige namba *148*01#. Huduma hii inapatikana kwa wateja wote wa Tigo kwa gharama nafuu ya shilingi 475 tu kwa siku.
Tamasha za Mini Kabaang ni mfululizo wa maonyesho ya muziki yanayoandaliwa na Tigo, yamekwisha fanyika Morogoro, Moshi na sasa Mwanza. Mikoa mengine itakayofuata ni Mbeya, Dodoma na mikoa mingine.
KUHUSU TIGO:
Tigo ni mtandao wa kwanza wa simu za mkononi nchini Tanzania. Ilianza shughuli mwaka 1994 na inapatikana katika mikoa ishirini na sita (26)
Tanzania bara na visiwani.
Lengo la Tigo ni kuwa mtandao unaoongoza kwa kutoa huduma bora na za ubunifu Tanzania kwa wateja wake wote ambazo zinaendana na mahitaji yao kuanzia huduma za sauti za bei nafuu, vifurushi vya intaneti vyenye kasi kubwa na huduma bora za fedha za simu za mkononi kupitia Tigo Pesa.
Tigo ni sehemu ya kampuni kubwa ya <http://www.millicom.com/> Millicom
International Cellular S.A (MIC) ambayo ni ya unafuu wa huduma na inapatikana kirahisi  kwa zaidi ya wateja milioni 43 katika masoko 13 barani
Afrika na Amerika ya Kusini.
"Tabasamu upo na Tigo"
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Amani Nkurlu – Meneja Mahusiano
+255 658 870 107 au +255 712 223 839

mbaroni kwa tuhuma za kutaka kuua kwa kutumia ushirikina.


 Mtuhumiwa akiwa ndani ya  chumba cha mganga na Mganga wake aitwae Yahaya tayari kwa kufanya mambo ya kishirikina.

Mama mmoja pichani juu ajulilikanae kwa jina la Magreth Simon Nkwera,  amekamatwa kwa Mganga wa kienyeji akijaribu kutekeleza jaribio la kutaka kuwauwa baadhi ya watoto wa mumewe na baadhi ya ndugu zake huko kibaha maili moja mkoani Pwani na hivi sasa yupo katika kituo cha polisi Maili moja akisubiri kupandishwa kizimbani.  
 Mtuhumiwa huyo akiwa ndani ya gari la polisi baada ya kukamatwa akiwa na huyo Mganga wa Kienyeji. 
Mtuhumiwa  ambaye ni mfanyakazi wa shirika la Nyumbu kibaha mkoani Pwani,akiwa anahojiwa na mzee wa ukoo wa Shirima,Afisa polisi jeshi daraja la Kwanza (woii mstaafu) Joseph Shirima mara baada ya kumkamata live kwa sangoma.Habari hii imetolewa na mwenyekiti wa ukoo wa shirima bwana Godilisten Hendrick Shirima.

KUMBUKUMBU ZA SIKU YA 40 YA MSIBA WA BABY SHANGAZI HOTEL MBEYA

FAMILIA YA ZAINABU ABEID ALLY (BABY SHANGAZI HOTELI) YA MBEYA INAPENDA KUCHUKUA FURSA HII KUMKUMBUKA MAMA YAO MPENDWA ALIYEFARIKI USIKU WA TAREHE 5-06-2013 KATIKA HOSPITALI YA RUFAA
JIJINI MBEYA NA KUZIKWA SIKU YA ALHAMISI TAREHE 6.06.2013.

WATOTO WAKO POSTER, MABRUCK, ASHA, HAWA, HUSSEIN, HASIRA NA ABEID WANAUNGANA NA NDUGU NA JAMAA WALIOJITOLEA KWA HALI NA MALI KUHAKIKISHA MAMA YAO MPENDWA ANAPATA KILA AINA YA MSAADA ULIOKUWA UNAHITAJI MPAKA PALE MWENYEZI MUNGU ALIPOCHUKUA ROHO YAKE.

KUMBUKUMBU YA KUTIMIZA SIKU YA 40 BAADA YA KIFO CHA MAMA YETU INATARAJIWA KUFANYIKA NYUMBANI KWAKE MAREHEMU MBEYA SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 6.07.2013 WOTE MNAKARIBISHWA.

MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI.
AHSANTENI SANA

SHUKRANI


MARIETHA NJIMBA (MRS. MZEE MFAUME)

Familia ya MZEE MFAUME na Wazazi Bw & Bibi CLAUDE NJIMBA wa Kinyerezi na Tabata Dar es salaam wanapenda kutoa Shukrani kwa wote walioshiriki  katika msiba wa mpendwa wao MARIETHA NJIMBA (MRS. MFAUME) kilichotokea tarehe 29/05/2013 na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni tarehe 01/06/2013.
Shukrani za pekee tunazipeleka kwa Uongozi na wafanyakazi wote wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dr Kisanga, Dr Mary, wauguzi wa Burhan Hospital, Mapadre na Waumini wa Parokia Katoliki ya Kinyerezi, Kristu Mfalme – Tabata, Majirani, Ndugu,  Jamaa na Marafiki wote kwa jinsi mlivyoshirikiana nasi katika msiba huo. Sio rahisi kuwataja kwa majina wote walioshiriki nasi. Tunaomba mzipokee shukrani zetu kwa waraka huu.
Shukrani za kumaliza msiba huo zitafanyika nyumbani kwake Kinyerezi, siku ya Jumamosi tarehe 06/07/2013 kuanzia 02 asubuhi kwa Ibada ya Misa Takatifu nyumbani kwa Marehemu. Tunawakalibisha wote.
              BWANA  AMETOA  NA BWANA  AMETWAA  JINA  LAKE  LIHIMIDIWE.

MHE. ALI HASSAN MWINYI MGENI RASMI, MASANJA, SHILOLE KUFANYA MAKAMUZI MIAKA 3 YA VIJIMAMBO NA TAMASHA LA UTAMADUNI WA KISWAHILI MAREKANI


Blog ya Vijimambo ikishirikiana na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Washington, DC, Marekani na Jumuiya ya Watanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia wanapanga kusherehekea miaka 3 ya Vijimambo na kukuletea tamasha la kiswahili. Tamasha hili ni kuendeleza lugha na utamaduni wa Kiswahili hapa Marekani ili watoto wanaoishi huku waweze kuendeleza matumizi ya lugha hii na utamaduni wake kizazi hadi kizazi. 

Siku ya July 6, 2013  hapa DMV kwenye Hall la Hampton Conference Center lililopo 
207 w Hampton Pl, 
Capitol Height, MD

Mambo mengi yatakayokuwepo ni Vikundi mbalimbali vya utamaduni, wanamitindo wa mavazi mbalimbali kuwakilisha, vyakula vya Kitanzania, Wasanii kutoka nyumbani ambao ni Shilole na Masanja Mkandamizaji wakishirikiana na wa hapa Marekani yote hayo ni kudumisha utamaduni wetu wa kiswahili

HOTEL KWA WAGENI 
Tumeongeza vyumba 35 Hotel ya Country Inn & Suites 
Na unapopiga simu uliza SWAHILI CULTURE IN USA kusudi upate unafuu wa bei nambari ya simu ni 301 350 8088 na Address ni
8850 Hampton Malls Drive North
Capitol Heights, MD 20843

Hotel za jirani na hapa ni

Hampton Inn

9421 Largo Dr West,

Largo, MD 20774

simu ni 301 499 4600


Extended Stay American

9401 Largo Drive West,

Largo, MD 20774

simu ni 301 3339139

Confort Inn
56 Hampton Park Blvd
Capitol Heghts, MD20743
Simu ni 301 336 8900

Muda wa watoto ni kati ya 10:00 am - 5:00 pm:
Kuanzia 7:00 pm- 3:00 am ni kwa watu wazima tu.

MAVAZI 
10:00 am - 5:00 pm Vazi la Kitanzania
7:00 pm - 3:00 am Vazi lolote lakini uwe umependeza

BURUDANI ZOTE NI KATI YA 10:00 AM - 5:00 PM
USIKU NI CHAKULA NA MUZIKI WA DISKO TU.

Chakula cha mchana Kuanzia kifungua kinywa na vinywaji vitauzwa muda wote iDinner peke yake ndio itakayokua Free.

Tafadhali zingatia muda. Rais Mustahafu Ali Hassan Mwinyi ataingia ukumbini 10:30 am

KARIBU

Rais Kikwete alipowasili mjini Dodoma


Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma juni 25, 2013 kwa ajili ya kuongoza kikao cha kamati Kuu ya CCM na Baraza la Mawaziri.
Rais Jakaya Kikwete akiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma juni 25, 2013 kwa ajili ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM na Baraza la Mawaziri . Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. (Picha na Ofisi ya waziri Mkuu).

Zawose kupiga shoo Bagamoyo

MSANII wa nyimbo za asali za utamaduni wa Kigogo ambaye anatamba ndani na nje ya Tanzania, Msafiri Zawose, anatarajia kupiga shoo ya aina yake maalum ya kuchangia kituo cha AMAP Juni 28, katika mgahawa wa PoaPoa uliopo mjini hapa.

Akizungumza jana Zawose ambaye ni mtoto wa marehemu Hukwe Zawose aliyerithi kipaji cha baba yake kwa kuendeleza utamaduni wa kabila hilo la Wagogo, alisema maandalizi ya shoo hiyo yamekamilika na tayari tiketi zimeanza kuuzwa.

"Wadau wajitokeze kwa wingi  kwenye shoo yetu  maalum ya kusaidia kituo cha AMAP kwa ajiri ya kuwasaidi watoto wasio jiweza kulipa ada zao za shule" alisema Zawose.

Na kuongeza kuwa mbali na burudani ya muziki pia kutakua na maonesho ya bidhaa mbalimbali sambamba na chakula cha tanzania kilichochanganya na usasa.

"Nyimbo ni kama asili yangu, kuna vibao kama Ilima, Mahera na vingine vingi"alimalizia Zawose.

kubainisha kuwa, burudani hiyo itatolewa na yeyey kwa pamoja na bendi yake hiyo ya Sauti Band.

Kwa upande wake Hannah Nelson wa walioandaa shoo hiyo alisema tiketi zinapatikana katika mgahawa huo wa Poa Poa kwa bei tsh 15,000,  huku siku ya tukio Juni 28, mlangoni itakuwa tsh 20,000 ambapo kiingilio hicho kinajumuisha na chakula.
 
"Tiketi zinapatikana Poa Poa Restaurant, karibiuni sana katika shoo hii ambayo ni maalum kuchangia elimu" alisema Annah.

Shoo hiyo inatarajia kuanza majira ya saa 12 jioni hadi saa Sita usiku.
Kituo hicho cha AMAP (Africa  Modern Art Project) kinajishughulisha na shughuli za sanaa mjini hapa na pia kinasomesha watoto wadogo.

Obama should urge promotion of free press in Tanzania

June 25, 2013
His Excellency Barack Obama
President of the United States of America
White House
Via facsimile: +1 202-456-2461


Dear President Obama:

Ahead of your first trip to East Africa, we would like to bring to your attention the deteriorating state of press freedom in Tanzania. In your meetings with Tanzanian President Jakaya Kikwete, we ask that you discuss the critical importance of press freedom to economic development and democracy.
In the past year, CPJ has documented a rise in threats and attacks against journalists in Tanzania. In September 2012, CPJ documented the first work-related journalist killing in the country since we began keeping detailed records in 1992. Police shot at point-blank range Daudi Mwangosi, reporter for TV Channel 10, after the journalist confronted them over the arrest of another reporter. A junior officer was arrested, but several other officers seen as being involved have not been held accountable. Another journalist, Issa Ngumba, was found dead from gunshot wounds in January. CPJ is investigating to determine if the murder was related to his coverage of local farming issues. No one has been arrested.
In addition, several journalists have been attacked in connection with their work. In March, unknown assailants attacked Absalom Kibanda, chairman of Tanzanian Editor's Forum and managing editor of the New Habari media company, leaving the critical columnist with severe injuries. No one has been arrested. Local journalists also said they have often been threatened by officials and high-ranking businessmen via text messages, emails, or intermediaries. Reporters based outside the capital, Dar es Salaam, are often targeted, the sources said.
This new trend of attacks against the press in Tanzania occurs against a backdrop of restrictive anti-press laws. One of them, the 1976 Newspaper Act, which allows the information minister discretionary powers to suspend publications, was used to ban the leading independent weekly Mwanahalisi in July 2012. The constitution includes at least 16 other anti-press laws that have induced journalists to practice self-censorship, our research shows.
Tanzanian authorities said they would present a new press bill this year that would eliminate legislation that censors or restricts the press. But the contents of the bill have been kept from the public, and local and regional media outlets have said they fear renewed anti-press legislation. 
As you know, the Tanzanian government is one of five African nations that signed on to your Open Government Partnership Initiative, a multilateral effort to promote transparency. Tanzania cannot uphold its obligation given the current media climate of threats against the press and existing restrictive legislation. Economic development that benefits Tanzanian citizens can only occur in a system in which officials are held accountable by a free and vibrant press. 
Tanzanian journalists are working in a highly restrictive media environment and are being attacked with impunity. We ask that you urge President Kikwete to promote media freedom in the country, without which vibrant democracy and economic development cannot exist. 
Sincerely,
Joel Simon
Executive Director

CC List:
H.E. Jakaya Kikwete, President of Tanzania
H.E. Mwanaidi S. Maajar, Ambassador of Tanzania to the United States of America
H.E. Alfonso E. Lenhardt, Ambassador of the United States of America to the Republic of Tanzania
Filiberto Ceriani Sebregondi, Head of the Delegation of European Union to the Republic of Tanzania
John Kerry, Secretary of State for the United States of America
Linda Thomas-Greenfield, Assistant Secretary for African Affairs for the United States of America
Dr. Fenella Mukandara, Minister of Information of the Republic of Tanzania
Pansy Tlakula, Special Rapporteur on Freedom of Expression and Access to Information, African Commission on Human and Peoples' Rights
Reginald Mengi, Chairman of the Media Association of Tanzania
Dr. Jeffrey Ashley, USAID / East Africa Mission Director
Kajubi Mukajanga, Executive Secretary of the Media Council of Tanzania
Mohamed Tibanyendera, Chairman of the Media Institute of Southern Africa, Tanzania
Ernest Sungura, Executive Director of the Tanzania Media Fund

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

No comments:

Post a Comment