Thursday, November 29, 2012

WANAFUNZI MACHANGUDOA KATIKA CHUO KIKUU CHA DODOMA ( UDOM ) WAANZA KUSAKWA


RAIS wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOSO), Paul Yunge, amesema kuwa wanafanya uchunguzi wa kina ili kuwanasa wanafunzi wa chuo hicho wanaojihusisha na biashara ya kujiuza kimwili ili wawachukulie hatua.

Yunge alifafanua kuwa, wanafunzi watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo watachukuliwa hatua kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa wengine.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Yunge alisema kazi ya kufanya uchunguzi tayari imeanza na wanategemea wakati wowote watabaini ukweli kuhusiana na jambo hilo.

Alifafanua kuwa, wanafunzi wanaojihusisha na vitendo hivyo wanakidhalilisha na kukishushia heshima chuo hicho ambacho kimsingi kinapaswa kuwa kioo.

“Ni aibu sana kama watu wamekuja UDOM kusoma na badala yake wanageuka na kufanya biashara ya kujiuza ambayo ni ya kudhalilisha utu wao pamoja na chuo kwa ujumla. Jambo hili lazima tulifanyie kazi,” alisema.

Yunge alidai kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya taarifa hiyo kuripotiwa na vyombo vya habari, kitendo ambacho kimeisononesha nchi nzima ukiwemo uongozi wa chuo pamoja na wazazi wa wanafunzi hao.

Hatua ya serikali ya chuo kuanza uchunguzi imekuja baada ya baadhi ya vyombo vya habari wiki iliyopita kuripoti kuwa baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho wanajiuza katika sehemu mbalimbali za mji wa Dodoma.

SAFARI YA MWISHO YA SHARO MILIONEA MCHANA HUU....





 Mwili wa Marehemu Sharo Milionea ukiswaliwa mapema mchana huu kabla ya kupelekwa kwenye nyumba yake ya milele 
 Rafiki mkubwa wa marehemu Sharo Milionea,Mzee Majuto akiwa ameshikwa mkono wakielekea kwenye mazishi mapema mchana huu,Muheza mkoani Tanga.

POLISI AFUKUZWA KAZI BAADA YA KUMBAKA MTUHUMIWA WA KIKE


JESHI la Polisi mkoani Mbeya limemfukuza kazi askari wake Enock Daffa (22) kwa tuhuma za kufanya  mapenzi na mtuhumiwa wa kike mwenye umri wa miaka 25 katika Kituo cha Polisi cha Mji mdogo wa Tunduma, Wilaya ya Momba, mkoani hapa. 


Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani, askari huyo alitenda kosa hilo Novemba 21,2012 na kwamba mtuhumiwa aliyefanya naye mapenzi alikuwa akikabiliwa na kosa la wizi.
Kamanda Athumani alisema kuwa mbali ya kufukuzwa kazi askari huyo tayari amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Aidha alisema kuwa hali kama hiyo haitaweza kuvumiliwa na Jeshi la Polisi na kwamba atakayebainika kufanya tukio kama hilo adhabu yake itakuwa ni kufukuzwa kazi.
Kamanda huyo alitoa wito kwa askari polisi kufanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni za Jeshi la Polisi kama mwongozo unavyowaagiza ili kulinda maadili ya Jeshi la Polisi ambacho ndicho chombo kinachotumika na wananchi katika kuzisimamia sheria.
Akizungumzia tukio hilo, baba mzazi wa askari huyo alisema kuwa kitendo alichofaya mtoto wake si cha kiungwana ambacho pia kimetia fedheha familia yake pia kwa jeshi la Polisi ambalo limepewa dhamana ya kutunza usalama wa raia na mali zake.

WAZIRI WA HABARI AFUNGUA MKUTANO WA MA-RAS JIJINI DAR LEO

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akifungua Mkutano baina ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na wajumbe wa Kamati za Michezo za Mikoa Tanzania Bara “Ma-RAS” (hawapo pichani) Jijini Dar es Salaam.Mkutano huo unalengo la kujadili maendeleo ya Michezo nchini.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akisalimiana na RAS wa Njombe mara baada ya kufungua kufungua Mkutano baina ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na wajumbe wa Kamati za Michezo za Mikoa Tanzania Bara Ma-RAS Jijini Dar es Salaam.Mkutano huo unalengo la kujadili maendeleo ya Michezo nchini. (Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM).

Bendi ya Mashujaa kuzindua Risasi Kidole Leaders leo

BENDI ya Mashujaa leo inazindua albamu yake ya pili ijulikanayo kwa jina la Risasi Kidole pamoja na bendi maarufu ya Congo, Wenge BCBG iliyochini ya mwanamuziki JB Mpiana kwenye  viwanja vya Leaders club.
.................................. 
Uzinduzi huo umepangwa kuanza saa 2.00 usiku na maandalizi yake yamekwisha kamilika kwa mujibu wa meneja wa bendi ya Mashujaa, Martin Sospeter. Sospeter alisema kuwa wamejiandaa vilivyo katika uzinduzi huo na lengo lao kubwa ni kuweka historia katika muziki wa Tanzania.
Alisema kuwa wamekaa kambini muda wa siki mbili na wameandaa vitu vingi vipya kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki wa muziki wa dansi nchini. Alisema kuwa kuna rap ya Ua Mbu na Dume la Simba kutoka kwa marapa wao, Saulo Ferguson na Sauti Radi.
Alifafanua kuwa wanamuziki wake wameadhimia ‘kufunika’ katika uzinduzi huo kwani anahistoria nzuri katika muziki wa Tanzania na kufanya kazi katika bendi nyingi.

“Tunawaomba watanzania waje waone nini tunakifanya mbele ya gwiji la muziki wa dansi Afrika, JB Mpiana, najua wao wamepania, lakini sisi tumepania vilivyo kusafisha nyoyo za mashabiki ambazo kwa sku nyingi hawajapata burudisha la mioyo zao,” alisema.

Kiongozi wa bendi hiyo, Charlz Baba alisema kuwa wamepania kutoa somo kwa wanamuziki wa dansi hapa nchini ambao wamekuwa wakisubiri waone watafanya nini. Alisema kuwa wameandaa nyimbo nyingi nzuri  na wamepatia kutawala soko la muziki hapa nchini.

“Njooni muone nini tunafanya katika muziki wa dansi, kambi yetu imekuwa nzuri na mafanikio makubwa, naomba mashabiki waje kutuunga mkono nasi tutawaunga mkono kwa kutoa burudani safi,”alisema Chalz.

Albamu ya Risasi Kidole ina jumla ya nyimbo sita. Nyimbo hizo ni Umeninyima, Tikisika, Hukumu ya Mnafiki, Ungenieleza, Kwa Mkweo na wimbo uliobebab jina la albamu hiyo, Risasi Kidole.

SERIKALI YAZINDUA BARAZA LA WATAALAM WA KUREKEBISHA UPEO WA MACHO KUONA,PIA YAKABIDHI MAGARI 9 NA PIKIPIKI 107 KUSAIDIA HUDUMA ZA AFYA NCHINI

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wataalam wa Kurekebisha Upeo wa Macho Kuona nchini leo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la wataalam wa kurekebisha upeo wa macho kuona nchini Adam Simbeye (kulia) akiwaeleza wajumbe malengo ya baraza hilo ya kusimamia, kudhibiti na kuratibu utoaji wa huduma bora za macho nchini yanayofanywa na baraza hilo kwa mujibu wa sheria ya Optometria Na.12 ya mwaka 2007. Kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi.
Wajumbe wa Baraza la Wataalam wa Kurekebisha Upeo wa Macho Kuona nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi (Katikati) mara baada ya kuzinduliwa kwa baraza hilo leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dkt. Hussein Mwinyi (kushoto) na mwakilishi wa Shirika la UNFPA nchini Tanzania Bi.Mariam Khan (kulia) kwa pamoja wakisaini nyaraka za kukabidhi magari 9 ya kubebea wagonjwa na pikipiki 107 kwa ajili ya kupelekwa katika maeneo mbalimbali kusaidia huduma za afya.
Mwakilishi wa Shirika la UNFPA nchini Tanzania Bi.Mariam Khan (kulia) akimkabidhi funguo za gari la kubebea wagonjwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi (kushoto) akimkabidhi funguo za gari la kubebea wagonjwa mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Bukombe Dkt.Archard Rwezahura (katikati) leo jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia makabidhiano hayo ni mwakilishi wa Shirika la UNFPA nchini Tanzania Bi.Mariam Khan.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

No comments:

Post a Comment