MICHEZO

TASWA FC YACHAPWA MAGOLI 4-0 NA BAGAMOYO VETERANI MJINI BAGAMOYO

Kikosi cha timu ya Chama Cha waandishi wa habari za Mizhezo TASWA FC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa kirafiki kati yake na timu ya Bagamoyo Veteran uliofanyika kwenye uwanja wa Mawanakerenge Mjini Bagamoyo jioni ya leo, ambapo timu ya TASWA FC imechapwa magoli 4-0 na maveterani hao kutoka mjini Bagamoyo,
Timu ya Waandishi wa habari ya TASWA FC imeshiriki katika mchezo huo ikiwa ni moja ya programu ya mkutano wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika kesho kwenye hoteli ya Kiromo View mjini Bagamoyo ambapo utafunguliwa na Ridhiwani Kikwete na Kufungwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ndugu Assah Mwambene
Hiki ndiyo kikosi cha timu ya Bagamoyo Veteran kilichotoa kichapo kwa timu ya TASWA FC mjini Bagamoyo leo.
Baadhi ya waandishi wa habari ambao ni mashabiki wa timu hiyo wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu ya Simba Ibrahim Masoud katikati akizungumza na Mzee Willy Chiwango kutoka gazeti la This Day kulia na Beny Kisaka mkurugenzi mwanadamizi gazeti la Jambo Leo.
Mkuu wa Wilala ya Bagamoyo Ahmed Kipozi wa pili kutoka kulia akizungumza na mwandishi mkongwe kutoka Zanzibar Said Salim huku wanahabari wengine wakifuatilia mazungumzo hayo.
Mchezaji wa timu ya TASWA FC Juma Pinto akimiliki mpira mbele ya beki wa timu ya Bagamoyo Veterani katika mchezo huo uliofanyika kwenyeuwanja wa Mwanakerenge mjini Bagamoyo
Mchezaji wa timu ya TASWA FC Shafii Dauda akimiliki mpirahuku beki wa timu ya Bagamoyo Veterani akiuwania katika mchezo huo, katikati ni mchezji wa timu ya TASWA FC Mohamed Akida.
Mshauri wa timu ya TASWA FC Masoud Sanani akihimiza wachezaji wa TASWA FC kucheza kwa bidii baada ya kuchapwa magoli 4-0 huku wachezaji wa timu hiyo wakishangaa wasijue la kufanya wakati zikiwa zimesalia dakika za majeruhi.PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.


They have the brawn and the talent, and now, they also have the money. These ten athletes are the best of the best in their respective fields and they have translated their success into millions of dollars in earnings and commercial endorsements. They are winners not only in terms of sports glory, but also in financial wealth.

1. Floyd Mayweather, Boxing – $85 million


He responds to the name of Money, and Pretty Boy Floyd has every right to do so. He chooses his opponents carefully, and then methodically cuts them down. He is unbeaten in professional boxing, and has plowed down the likes of Miguel Cotto, Oscar dela Hoya and Shane Mosley, all of who are potential Hall of Fame inductees. Mayweather also knows how to sell his fights, often building an intense antagonism with his opponent to further stoke the public’s interest. And it pays off all the time. The three biggest pay-per-view fights in history outside the heavyweight ranks were all co-headlined by Mayweather. He is considered the best boxer pound-for-pound in the world today, although he can certainly cement that status, as well as earn even more money, if he heeds the public’s clamor for him to fight Manny Pacquiao. It would not hurt if he turns in a good leaf too. Imagine if companies will consider him as an ideal endorser; that would certainly add to his $85 million in pure earnings.

2. Manny Pacquiao, Boxing – $62 million


Once considered the best boxer in the world pound-for-pound with titles in eight weight classes, he has since dropped to second spot. Not that he has stopped fighting, but his victories over Mosley and Antonio Margarito were not as resounding, as he showed mercy to his outclassed opponents and did not go for a knockout. There was also the controversial win over nemesis Juan Manuel Marquez, as well as an equally controversial loss to Timothy Bradley, in which nobody outside of the three judges and Bradley himself thought of the decision as correct. Perhaps, only a fight with Mayweather will wake him up from his recent stupor, though he has been awake enough to maximize his earnings by agreeing to several commercial deals. The man known as Pacman has gobbled up endorsements with Hewlett Packard, Nike and Hennessey.

3. Tiger Woods, Golf – $59.4 million


There was a time when golf enthusiasts wonder if Tiger Woods would ever lose. After a messy divorce, Tiger’s game has dropped and many are now wondering if he will ever win again. Not that he really needs it.  His status as an all-time great has already been confirmed by his 14 victories in major tournaments. And he still raked in nearly $60 million last year, including $4.4 million in endorsements. Those numbers may be peanuts compared to previous years when he was top of the list, but they are still good enough for number three. Besides, he is still only 36 years old, which is not that old in golfing terms. So watch out, as the Tiger is still on the prowl.

4. Lebron James, Basketball – $53 million


Critics have always been waiting for Lebron to make a mistake. They say he disappears during the clutch, passes the ball when he needs to take it strong to the hoop, and gives responsibility to his teammates too much. Lebron made them all shut up last year when he finally got his ring. He can play four positions on the hard court, can defend as well as anyone, and can do pretty much anything with the basketball. He may not be the NBA’s top earner salary-wise, but his prowess has attracted companies like Nike, McDonalds, Sprite and Audemars Piguet. Endorsements alone bring him $40 million.

5. Roger Federer, Tennis – $52.7 million


Years of domination at the top was followed by successful challenges from players like Rafael Nadal and Novak Djokovic, but Roger Federer still knows how to win. And he proved it by winning in Wimbledon again earlier this year, his 17th major and 7th in the most prestigious tournament of all.  Even if he doesn’t win that many tournaments anymore, endorsements with Nike, Rolex and Mercedes Benz will help keep Federer more than afloat.

6. Kobe Bryant, Basketball – $52.3 million


He is the highest-paid player in the NBA. He has five rings, has been the MVP and has two Olympic gold medals. He has lucrative deals with Nike, Vitamin Water and Turkish Airlines. The Black Mamba has got it all.

7. Phil Mickelson, Golf – $47.8 million


Mickelson is right-handed but with a southpaw swing, thus earning himself the nickname Lefty.  And Lefty has delivered, winning four majors along the way. He has struck it huge in the endorsement game as well, with Rolex, Exxon and Callaway all under his wing.

8. David Beckham, Soccer – $46 million


This guy is a winner. He has played for arguably the most glamorous teams in the toughest leagues in the world, namely Manchester United, Real Madrid and AC Milan.  He has won domestic and European championships along the way. He now plays for the LA Galaxy in the US, where he currently resides with his Spice Girl wife, Victoria. And he has a lucrative deal with Adidas, Samsung and H&M.

9. Cristiano Ronaldo, Soccer – $42.5 million


His skills while he was at Sporting Clube de Portugal when he was 18 caught the attention of Manchester United, which promptly signed him up. His all-around play at Old Trafford caught the attention of Real Madrid, which pried him away for more than $130 million. His sublime artistry has caught the attention of Nike and Castrol, which pay him $22 million for his endorsement.  And he has caught the attention of the world, having won various Player of the Year honors the past few years.

10. Peyton Manning, Football – $42.4 million


Sidelined for an extended period because of injuries, Manning took his talent to Denver after 13 years in Indianapolis. He won the Super Bowl with the Colts, and he aims to do the same for the Broncos. And Gatorade and MasterCard couldn’t be any happier; after all, they still have an elite quarterback to promote their brands.

PODOLSKI NA MULLER WALIFELI DHIDI YA URENO: JE REUS NA SCHURRLE WATAANZA DHIDI YA UHOLANZI

Mchezo wao kwanza wa Euro 2012 ulienda kwa mujibu wa Ujerumani walivyotaka - kwa upande wa matokeo, lakini vijana wa Joachim Low hawakuonyesha uwezo mkubwa ambao wengi walikuwa wakiutegemea dhidi ya Ureno. Ushindi wa 1-0 ulikuwa ni bahati kwa timu hiyo kwa kuwa hata Ureno walipoteza sana nafasi kwa kutokuwa na bahati waliyoipata Ujerumani.

Ndio maana haishangazi kuona umma wa Ujerumani ukitegemea kuona mabadiliko kwenye mechi zijazo, kwa kuwa hawakuona timu yao ikicheza kwa kutengeneza nafasi nyingi za magoli dhidi ya kikosi cha Paulo Bento. Low alifanya uamzui mkubwa kwa kumchezesha Mats Hummels na Mario Gomez, lakini mashabiki wanataka kocha wao aongezee ujasiri wakati wa mechi zijazo.

Kuna maswali juu ya nafasi mbili: Thomas Muller na Lukas Podolski wote wanaweza wakaanzia benchi kwenye mechi zijazo. Wote walionyesha kwamba wapo tayari kucheza kwa kujituma bila kuchoka lakini kiukweli hawakucheza vizuri, na sasa Marco Reus na Andre Schurrle wanaweza kuwa wabadili wao dhidi Uholanzi?

Akiwa mmoja ya chipukizi bora wa ligi ya Ujerumani msimu uliopita, kiwango cha Marco Reus akiwa Borussia Monchengladbach kimeonyesha ubora anaoweza kuuleta ndani ya kikosi: akiwa na na rekodi nzuri za ufungaji na ubunifu mzuri kiwanjani. Kwa upande wa Schurrle amekuwa katika form nzuri kwa siku za hivi karibuni katika mechi za kirafiki kuelekea kwenye Euro, pia alikuwa na msimu mzuri na Bayern Leverkusen, na hakuna ubishi kwamba amaelata maswali mengi juu ya nani aanze kati yake na Podolski.

Alifunga magoli kwenye mechi mbili za mwisho za msimu na Leverkusen, na akiwa anatokea benchi dhidi ya Israel aliubadilisha mchezo na kuifanya Ujerumani kuwa tishio tofauti ana alivyokuwepo Podolski kwenye pitch.

"Kiukweli nataka kucheza mara nyingi iwezekanvyo, lakini kuna nafasi moja na watu wengi tunaitaka hivyo mwisho wa siku ni uamuzi wa kocha, japokuwa haijalishi nimecheza au hapana nitaisapoti yangu mwanzo mwisho kiwanjani mpaka nikiwa kwenye benchi." alisema Schurrle muda mfupi kabla ya kuelekea Ukraine.

Wengi wanatabiri kwa tabia ya kocha Low ya kufanya mabadiliko yasiyotegemewa kwenye kikosi, basi ni dhahiri Reus na Schurrle wanwwza wakaanza mbele ya Muller na Podolski

HATIMAYE YANGA YATHIBITISHA MARCIO MAXIMO KUTUA BONGO JUMAPILI HII

Baada ya siku chache zilizopita website hii ilikuwa ya kwanza kuripoti kwamba klabu ya Yanga ipo katika hatua za mwisho za kumsaini Marcio Maximo, leo hii imefahamika kwamba kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa 'Taifa Stars' Mbrazil, Marcio Maximo anatarajia kutua nchini kwa mara nyingine tena toka aondoke nchini mwezi juni mwaka 2010 siku ya jumapili juni 17 saa 9 alasiri.

Maximo anakuja nchini kuchukua mikoba ya Mserbia wa Yanga Kostadin Papic aliyenyimwa mkataba mpya, baada ya ule wa awali wa miezi 6 kuisha wakati ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2011/12 ukielekea mwishoni.


Maximo awali alitarajiwa awasili nchini hapo kesho, na kwa mujibu wa taarifa rasmi na zinasema kocha huyo mwenye msimamo mkali atawasili jumapili na shirika la ndege ya Emirates.


Hii ndiyo ndivyo sivyo ya ubingwa nchi za ulaya

Na Arone Mpanduka(Radio Tumaini)
NDANI ya msimu wa mwaka 2011/2012 tumekuwa tukishuhudia matukio mbalimbali ya kimichezo hasa katika medani ya soka ambayo yamekuwa yakivutia na kusisimua.
Kutokana na kufuatilia kwa karibu zaidi matukio ya soka Barani Ulaya kupitia ligi mbalimbali nimeweza kubaini mambo kadhaa ambayo yamekuwa kinyume na matarajio ya wapenzi wengi wa mchezo wa soka duniani.
Kupitia matukio hayo wengi waliokuwa wanajaribu kutabiri ndivyo, matokeo yake yamekuwa sivyo.Fuatana nami ili tuweze kwenda pamoja hasa kwa kupitia tukio moja hadi lingine kwa kifupi.
BINGWA WA KOMBE LA FA
Hapa wengi walidondosha karata yao ya utabiri kwa timu ya Liverpool hasa kutokana na wachezaji wake kuwa na tabia ya kutokata tamaa katika dakika zote 90 hata kama wakiwa nyuma kwa goli moja ama mawili kitu ambacho wachezaji wa Chelsea wamekikosa.
Licha ya kwamba timu zote zilikuwa na mwenendo mbovu katika msimu wa 2011/2012 lakini Liverpool ilipewa nafasi kubwa zaidi ya kutwaa kombe hili lakini hatimaye mambo yalikuwa kinyume hasa pale ambapo Chelsea ilipofanya maajabu kwa kuinyuka Liver mabao 2-1.
Ramires na Didier Drogba ndiyo waliofanikisha kombe la FA kwenda darajani ambapo kwa mara ya mwisho Chelsea ilitwaa kombe hilo mwaka 2010.
BINGWA WA LIGI KUU YA HISPANIA
Katika ligi hii wengi walikuwa wakiiangalia zaidi Barcelona ambayo ilikuwa ikishiriki ligi kama bingwa mtetezi lakini pia bingwa wa dunia ngazi ya vilabu.
Watu walikuwa na imani na Barcelona hasa kwa uimara iliyonao wa kuweza kumiliki mpira na kupenyezeana pasi za uhakika na hata pia umakini wa washambuliaji wake kama Lionel Messi ambaye ni mgumu kumzuia pindi anaposogelea ‘sebule’ ya timu pinzani.
Hadi ngwe ya mechi za marudiano za ligi kuu ya Hispania inaanza Barcelona ilikuwa kileleni mwa msimamo wa ligi ikifuatiwa na Real Madrid lakini mambo yalibadilika kuelekea mwishoni mwa ligi ambapo Madrid chini ya Jose Mourinho  ikafanikiwa kuitangulia Barcelona kwa tofauti ya pointi 4.
Mambo yalizidi kwenda hivyo hasa kwa timu zote kuhakikisha kwamba hazifanyi makosa kwenye mechi zao na kufanya mashabiki wa soka ulimwenguni kusema kwamba bado Barcelona ana nafasi ya ubingwa hasa katika mechi ambayo wanacheza mwenyewe kwa wenyewe hasa ikizingatiwa kwamba mara zote Madrid ni kibonde wa Barcelona.
Lakini mambo hayakuwa mambo kwani hata walipokutana wenyewe kwa wenyewe Barcelona alikubali kichapo kutoka kwa Real Madrid mara baada ya kupigwa 2-1 na kutengeneza tofauti ya pointi 7 kutoka 4, tofauti ambayoi ilikwenda hadi siku ambayo Real Madrid inatangaza ubingwa.
Hapa ndugu msomaji hadi mwisho wa ligi ubingwa wa Real Madrid ulikuwa kinyume na matarajio ya wengi.
BINGWA WA LIGI KUU YA UINGEREZA
Katika ligi hii inayodhaminiwa na benki kubwa duniani ya Backlays tangu inaanza mwezi Agosti mwaka 2011 mashabiki wengi walikwishaipatia ubingwa timu ya Manchester United hasa baada ya kuanza vizuri msimu kwa kuinyuka Manchester City 3-2 katika mechi ya ngao ya jamii.
Kama hiyo haitoshi Manchester United ilionyesha kwamba ipo vizuri baada ya kutoa vipigo kwa timu kadhaa ikiwemo kipigo cha kihistoria ya mabao 8-1 ilichomnyuka Arsenal na kuweka rekodi ya ushindi wa mabao mengi zaidi katika msimu huo wa ligi kuu.
Kumbe wakati huohuo timu iitwayo Manchester City ilikuwa inakimbiza mwizi kimya kimya hasa baada ya kuonyesha ushindani wa hali ya juu kwa kutoa dozi kwa timu ilizokuwa inakutana nazo.
Hadi kufikia mwezi Januari mwaka 2012 Manchester City walikuwa wanaongoza ligi wakifuatiwa na Manchester United  kitu ambacho kilihamisha mawazo ya wadau wa soka kutoka kwa United hadi City na kusema kwamba City ndiyo bingwa mtarajiwa.
Lakini mwishoni mwa ligi hiyo mambo yalibadilika ambapo wadau wakarejesha utabiri wao kwa Manchester United kuwa ndiye bingwa wa ligi hiyo hasa baada ya timu hizo kuwa na pointi sawa huku City ikiwa kileleni kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa tu.
Utamu ulikuja katika siku ya mwisho ya kumaliza ligi ambapo bingwa alikuwa bado hafahamiki na watu wengi walitabiri kwamba Manchester United atamfunga Sunderland lakini wakiibeza City kwamba isingeweza kuifunga QPR ambayo nayo ilihitaji ushindi ili isishuke daraja.
Hali hiyo ilifanya siku hiyo hata helikopta iliyobeba kombe kuhangaishwa angani ambapo kila dakika ilikuwa inabadili njia zake, mara iende Sunderland mara ibadilike na kwenda Etihad.
Lakini mwisho wa yote Manchester City nayo iliibuka na ushindi wa mshangao wa mabao 3-2 ikitoka nyuma ya mabao 2-1 dhidi ya QPR huku Manchester United ambayo iliiombea City ifungwe ili yenyewe ichukue ubingwa ikajikuta ikipoteza ndoto hiyo licha ya yenyewe kushinda bao 1-0.
Mwisho wa yote Manchester City aliibuka bingwa kiyume na matarajio ya wengi ulimwenguni.
BINGWA WA KLABU BINGWA BARANI ULAYA
Hapa timu za Bayern Munich na Chelsea hazikupewa nafasi kabisa ya kufika hata nusu fainali lakini matokeo yake miamba hiyo ilitinga fainali na kuchuana pale Allianz Arena nchini Ujerumani.
Utabiri ulianza kushika kasi katika hatua ya 16 bora ambao kwa mtazamo wa haraka haraka mashabiki wengi duniani walihisi kwamba fainali itazikutanisha timu za Real Madrid na Barcelona na hapo yoyote kati ya hizo ndiye atakayekuwa bingwa.
Kinyume chake ni kwamba Real Madrid alibwagwa na Bayern Munich katika hatua ya nusu fainali huku Barcelona akibwagwa na kibonde Chelsea katika hatua ya nusu fainali, kitu ambacho kiliwashangaza wengi hasa kwa hali iliyonayo Chelsea kuweza kuiondosha miamba ya dunia Barcelona ambayo ilikuwa na kila sababu ya kufika fainali na kutwaa taji hilo.
Mechi ya fainali kati ya Bayern Munich na Chelsea nayo iliibua watabiri wengi walioegemea upande wa Bayern kwamba ndiyo wangekuwa mabingwa hasa kutokana na sababu nyingi ikiwemo tofauti ya uwezo wa kuuchezea mpira na kasi ya ushambulizi kwa timu hizo ambapo wajerumani waliizidi Chelsea.
Suala lingine ni kitendo cha Bayern kucheza nyumbani , mahali ambapo pana watu wengi wa kuiunga mkono pindi iwapo dimbani.
Matokeo ya mwisho yalikuwa ndivyo sivyo kwani Chelsea iliibuka na ushindi wa penati 4-3 hasa baada ya kutoka sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 za mchezo.



EURO 2012: UHOLANZI VS DENMARK - SAFU BORA YA USHAMBULIAJI DHIDI YA TIMU ISIYOTABIRIKA.

Netherlands-Denmark

VIKOSI VINAVYOWEZA KUANZA
Uholanzi: 1: Stekelenburg 2: Wiel 3: Bouma 4: Heitinga 5: Vlaar 6: De Jong 7: Robben 8: Van Bommel 9: Van Persie 10: Sneijder 11: Afellay

Denmark: 1: Lindergaard 2: Wass 3: Poulsen 4: Kjear 5: Agger 6: Poulsen 7: Rhommedal 8: Kvist 9: Bendtner 10: Erikssen 11: Kron-Dehli

MAMBO MUHIMU KUHUSU MECHI
  • Kumekuwepo na tetesi kwa wiki kadhaa kuelekea Euro 2012 kuhusu kama meneja wa Uholanzi Bert van Marwijk atawachezesha  washambuliaji  wake wawili Klaas-Jan Huntelaar na Robin van Persie, pamoja kupenda kutumia mfumo wa 4-2-3-1 katika kufuzu, van Persie alikuwa akichezeshwa upande wa kulia lakini amekuwa akicheza pekee yake mbele katika mechi za kirafiki za hivi karibuni ikiwemo mechi waliowafunga Ireland mabao 6-0.
  • Ibrahim Afellay pia alicheza vizuri kwenye mechi hiyo, akifunga bao zuri na akiongeza lingine kwa penati. Anaweza kuanza kwenye mchezo wa leo kama kocha ataamua kutumia mfumo wa kushambulia zaidi, akimuacha Van Marwijk akiwa na machaguo mengi kwenye benchi, huku Huntelaar, van der Vaart na Kuyt pia wakiwa na nafasi ya kuanza.
  • Joris Mathijsen pia ana wasiwasi wa kucheza kwenye mchezo wa ufunguzi kwa majeruhi aliyoyapata wiki iliyopita. 
  • Wilfred Bouma anahangaika kuweza kuimudu nafasi ya beki wa kushoto huku vijana Jetro Willems na Stijn Schaars wakiwa wameonyesha viwango vizuri.
  •   Denmark
  • Denmark hawana majeruhi mpya kwenye kikosi, lakini kuna maswali mengi juu ya nani anapaswa kuanza kwenye kikosi.
  • Chistian Poulsen hakuanza katika mechi dhidi ya Australia wiki iliyopita na Niki Zimling anaweza akaanza tena.
  • Pia kumekuwepo na na wasiwasi kuhusu kiwango cha Christian Eriksen, lakini pia kumekuwepo na waiwasi kidogo juu ya nafasi yake ndani ya kikosi lakini uwezo wake na ubunifu ni kitu ambacho Denmark wanahitaji.
  • Wass na Lars Jacobsen wapo kwenye upinzani wa nafasi ya beki wa kulia.

TAKWIMU
Denmark wameshinda mechi zao 4 za mwisho za Euro Cup.

Uholanzi wamekuwa wakifunga mabao atleast mawili katika mechi 6 kati ya saba za mwisho za kombe la Euro.

Denmark  wamekuwa wakifunga mabao atleast mawili katika mechi 4  za mwisho za kombe la Euro.

EURO PREVIEW: UJERUMANI VS URENO: RONALDO KUWAOKOA URENO DHIDI WAJERUMANI?


VIKOSI VINAVOTARAJIWA KUANZA.
Ujerumani: 1: Neur 2: Boateng 3:Lahm 4: Bedstuber 5: Mertesacker 6: Khedira 7:  8: Schwensteiger            9: Klose 10: Ozil 11: Podolski

Ureno: 1: Patricio 2: Pereira 3: Coentrao 4: Alves 5: Pepe 6: Veloso 7: Moutinho 8: Meireles 9: Postiga 10: Ronaldo 11: Nani




 Germany
  • Per Mertesacker amerudi na yupo fiti baada ya kuumia na kukosa nusu ya msimu akiwa na Arsenal. Anatarajiwa kuanza kwenye mechi ya leo akiunda safu ya ulinzi na Badstuber huku Hummels akisubiri kwenye benchi.
  • Bastian Schweinsteiger hajaichezea Ujerumani katika mechi za kirafiki za hivi karibuni lakini amerudi kwenye kikosi na ataanza kwenye mechi ya leo, ingawa yeye, Kroos na Khedira watakuwa wakipigania nafasi mbili za safu ya kiungo cha kati. 
  • Magoli aliyoyafunga kwenye mechi dhidi Switzerland na Israel yanamuweka Andre Schurrle katika nafasi ya kugombania namba ya kuanza kwenye winga ya kushoto, ingawa Podolski ana nafasi kubwa ya kuanza, huku Klose akitegemea kuanza badala ya Gomez.Goals in the games against Switzerland and Israel have put Andre Schurrle right in contention to start on the left flank, though Podolski is likely to be favoured, with Klose also set to get the nod over Gomez up front
  • Nani ana wasiwasi mkubwa wa kucheza kutokana na majeruhi, amekuwa akifanya mazoezi ya pekee yake tofauti na wenzake
  • Manager Bento atahitaji sana winga huyo wa Manchester United awe fiti kwa kuwa washambuliaji wake wa pembeni ndio silaha yake kubwa baada ya washambuliaji wake wa kati wakiongozwa na Postiga kukosa makali. 
  • Rui itabidi aanze kwenye milingoti mitatu mbele ya Eduardo na kinda Beto, huku akiwa chini ya ulinzi wa mabeki wazoefu Bruno Alves na Pepe.

TAKWIMU
Ujerumani wameshinda mechi 10 za mwisho za Euro Cup

Ujerumani wamefunga atleast magoli matatu katika kila mechi nane za mwisho za Euro Cup.

YANGA WAMEFANYA UHUNI KUMSAJILI KELVIN YONDANI ?

Kanuni za ligi kuu ya Vodacom kama zilivyorekebishwa na kupitishwa tarehe 20 julai 2009  na kusainiwa na Rais wa TFF bwana L.C. Tenga na bwana F. Mwakalebela aliyekuwa Katibu Mkuu zinaeleza kinagaubaga jinsi shuguli za usajili na uhamisho wa wachezaji zinavyobidi kufanywa.
Msimu unapokwisha kanuni ya 49 inaeleza kwamba” klabu itawasilisha TFF kwa maandishi, majina ya wachezaji watakaositisha mikataba yao/ kuwa huru katika usajili wa msimu wa ligi katika muda wa uhamisho utakaotangazwa na TFF na kitalazimika kumpa taarifa ya maandishi/ mchezaji au wachezaji husika”. Kanuni hii inaipa mamlaka klabu kwamba ndiyo yenye kuitaarifu TFF juu ya mchezaji yupi yuko huru na ambaye hayupo huru, Simba Sports Club haijawahi kuiandikia TFF juu ya mchezaji Kelvin Yondani kuwa huru na isingeiambia kwamba yupo huru kwa sababu ana mkataba aliousaini tarehe 23/12/2011 ambao kwa mujibu wa kanuni ya 46 mkataba huo unapashwa kuwasilishwa kwa pamoja na mikataba mingine  kwa ajili ya usajili wa msimu wa 2012/2013 kama kifungu hicho kinavyosema “Kilabu zinatakiwa kukamilisha na kuwasilisha kwa pamoja usajili wa timu zote mbili pamoja na majina na mikataba ya makocha wa timu za wakubwa na vijana katika kipindi cha usajili” Kifungu namba 40 kinaeleza kwamba maombi ya usajili wa mchezaji wa kulipwa lazima yawasilishwe pamoja na nakala ya mkataba wa mchezaji, hivyo wakati wa usajili mkataba wa kuendeleza mkataba uliopita kati ya Simba na Kelvin Yondani ndipo unapopashwa kuwasilishwa ingawa Simba imeuwasilisha mapema ili kulionyesha shirikisho hali halisi inayoendelea.
Pamoja na Simba kutoiandikia TFF kwamba Yondani ni mchezaji huru kwani muda haujafika pia kanuni za TFF na zile za FIFA za Regulation on the Status and Transfer of Players katika article 18 na kanuni za TFF katika kanuni ya 44 ambazo zipo “mutatis mutandis” kwa maana kwamba zimenakiliwa herufi kwa herufi lakini zimetofautiana lugha kwani moja ni kiingereza na nyingine ni Kiswahili inaeleza kwamba “kilabu inayotarajia kuingia mkataba na mchezaji wa kulipwa haina budi kuiarifu klabu yake ya sasa kwa maandishi kabla ya kufanya makubaliano na mchezaji wa kulipwa. Mchezaji wa kulipwa atakuwa huru tu kujingia mkataba na klabu nyingine iwapo mkataba wake na kilabu yake ya sasa umekwisha  au utakwisha baada ya miezi sita. Uvunjaji wowote wa sharti hili utastahili vikwazo vinavyofaa.
Hili pia limeelezewa katika kanuni ya 57 (1) kwamba “Kilabu kinachotaka kumsajili mchezaji aliyesajiliwa na kilabu kingine au mwenye mkataba na kilabu kingine, kitalazimika kuafikiana na kilabu chake kabla ya kumsajili mchezaji huyo”. Sababu kubwa ya kuhimiza mawasiliano baina ya klabu mbili ni kwanza kujua kama mchezaji huyo ana mkataba wa nyongeza na timu husika lakini zaidi ya hayo ni kuhakikisha kwamba mchezaji huyo haathiriwi na mazungumzo ya timu nyingine wakati anatekeleza mkataba uliobaki. Yanga walichofanya ni kumrubuni mchezaji kwa kuongea nae bila kibali cha Simba Sc lakini pia wangeomba kibali Simba Sc ingewaeleza kwamba mchezaji huyu ana mkataba mwingine alioisha usaini. Kwa mujibu wa kanuni za TFF na FIFA kitendo cha Yanga kuongea na mchezaji wa Simba SC bila kuiandikia simba chochote ni kosa kubwa sana ambalo Simba inaishitaki Yanga iadhibiwe kwa kufungiwa usajili wake wote wa mwaka huu na mwaka ujao.
Pamoja na hayo timu haiwezi kumsajili mchezaji ata kama amekuwa huru bila kuwasiliana na klabu yake ya zamani kwani idhinisho la usajili lazima litolewe na klabu yake ya zamani  kama kanuni namba 57 (2) inavyoelekeza hivyo hakuna namna yoyote ambayo Yanga inaweza kumsajili Kelvin Yondani bila Simba kupewa taarifa kwanza. Hili limesisitizwa zaidi katika kanuni ya 45 (6) kwamba “mchezaji ambaye ameingia mkataba wa zaidi ya msimu mmoja hatoruhusiwa kujisajili na klabu kingine kabla ya klabu yake mpya kuafikiana na klabu yake ya zamani” mkataba ulioisha wa Kelvin Yondani ulikuwa ni wa miaka miwili na ulioongezwa ni wa miaka miwili pia.
Mabezo haya yanaitia yanga hatiani kwa pande zote kwani maamuzi ya kama Kelvin ni mchezaji huru yanatolewa na Simba SC kama ikiwasilisha barua TFF juu ya wachezaji ambao wanamaliza mikataba au wanasitisha mikataba. Simba SC haijafanya hivyo kwa sababu muda wake bado, kwa mantiki hiyo yoyote anayetaka kujua mustakabari wa Kelvin inabidi awasiliane na Simba SC na jibu atakalopata ni kwamba Kelvin sio mchezaji huru, ana mkataba na Simba ambao kausaini na kuutia dole gumba (dole gumba lina alama za kipekee za mhusika ambazo hawezi kuzikana kama ilivyo kwa DNA).
Yanga wamefanya uhuni wa kumsajili Kelvin Yondani usiku wa tarehe 6/6/2012 kwa ushahidi uliopo, lakini wanasema mkataba umesainiwa ama October  2011 au February 2012, Simba SC itamshitaki wakili yoyote katika Tanganyika Law Society ambaye atashuhudia mkataba huo kwa kuurudisha tarehe za nyuma na kuomba chama hicho cha mawakili kimsimamishe mhusika  uwakili.


GAMBIA YAWASILI KUIKABILI TAIFA STARS





Timu ya Taifa ya Gambia (The Scorpions) imewasili nchini jana (Juni 7 mwaka huu) saa 5.30 usiku kwa ndege ya Kenya Airways tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.




Msafara wa timu hiyo wenye watu 31 wakiwemo wachezaji 22 unaongozwa na


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana na Michezo wan chi hiyo, Malang Jassey.

Viongozi wengine ni Ofisa Utawala wa timu Modou Sowe, Kocha Luciano Machini, makocha wasaidizi Peter Bonu Johnson na Lamin Sambou, Kocha wa makipa Alhagie Marong, mtaalamu wa tiba mbadala (physiotherapist) Pa Matarr Ndow, Mtunza vifaa Sanna Bojang na Daktari wa timu Kalifa Manneh.




Wachezaji ni Musa Camara, Abdou Jammeh, Momodou Futty Danso, Lamin Basmen Samateh, Ousman Koli, Pa Saikou Kujabi, Mustapha Kebba Jarju, Yankuba Mal Ceesay, Demba Savage, Saihou Gassama, Alieu Darboe, Momodou Ceesay, Pa Modou Jagne, Tijan Jaiteh, Bubacarr Sanyang, Christopher Allen, Musa Yaffa, Sulayman Marr, Mamut Saine, Hamsa Barry, Ali Sowe, Omar Colley na Saloum Faal.




Gambia ‘The Scorpions’ itafanya mazoezi yake ya kwanza leo (Juni 8 mwaka huu) saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume wakati kesho muda huo huo itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa.




Kambi ya Taifa Stars iko vizuri ambapo leo jioni timu itafanya mazoezi Uwanja wa Taifa. Pia kesho itafanya mazoezi kwenye uwanja huo huo kuanzia saa 11 jioni baada ya Gambia kuwa wamemaliza.



Jumamosi saa 4 kamili asubuhi kutakuwa na mkutano kati ya makocha wa timu zote mbili; Mdenmark Kim Poulsen wa Taifa Stars na Mtaliano Luciano Machini wa The Scorpions wakiwa na manahodha wao na Waandishi wa Habari utakaofanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Q&A with John Bocco

John Bocco @ SS com




Taifa Stars Striker John Bocco is the hottest property in Tanzanian football.
The 23 year old has been Azam's top scorer since, joining the club in 2007. He managed to score nine goals in his first season (2009/10) in the Tanzania Vodacom Premier League and scored 13 goals in the following term.
Last season he emerged top scorer in the Vodacom Premier League netting 18 times. He is a prolific striker and a top asset for both club and country.

SuperSport.com caught up with the Taifa Stars striker ahead of their world cup qualifier against The Gambia.

SuperSport.com: What was the feeling after finishing the top scorer in the Tanzania Vodacom Premier League?

Bocco: It was the best moment of my career, to become the top scorer in the league. Its a great achievement for a young player like me, who still has a lot of years to play. And I'm aiming to maintain my performances and try to achievement in the future.”

SuperSport.com: How was your trip to Abidjan and the game against Ivory Coast?

Bocco: Our trip was good. The climate in Abidjan is like here in Dar es Salaam. We trained well, we played the game and we lost the game at the end. It was painful to us players, but that's how football is and you have to accept the results as a player.”

SuperSport.com: How was it like to play against World class players like Didier Drogba, Yaya Toure and many others?

Bocco: Its very fortunate for us players who play in local leagues to meet such high rated names face to face. And it gives us courage and comfort, for players like us who want to be like them in the future. It was tough playing against them.

SuperSport.com: How are the training sessions getting through?

Bocco: We have had several training sessions previously, and some in the future - and the players are doing well and responding positively to the coach. And we players have a close relations and united, and really working hard in training focusing on the next game.

SuperSport.com: How do you find your partnership with TP Mazembe striker Mbwana Samatta in the frontline?

Bocco: He is a great player, good lad too. And his contribution in the team is great, its good to have a top performer like him in the team. We are good friends.

SuperSport.com: How do you find Kim Poulsen as the National Team coach?

Bocco: He is a good man, wise too. He has been doing pretty well with us, he teaches well and we players understand him well. I have seen changes in the team since the game against Malawi in terms of what he has been teaching us. There is an improvement in the team. And we keep on working harder and harder.

SuperSport.com: What are your expectations towards the game against Gambia?

Bocco: We expect the game to be tough, but we as players and after losing our first game, we will go out there with full spirit to win the game and turn this round for us.

SuperSport.com: What will be the feeling, when the National team qualifies to the World Cup?

Bocco: It will be a historical moment, it will be unbelievable moment for the players and the country. Because I believe it has never happened for Tanzania. We will work hard, to play in world cup one day.

SuperSport.com: What do you say to the home supporters towards the game against Gambia this weekend?

Bocco: I call on for full support from all Tanzanians, and come cheer us as Supporters not as fans, because when we are out there we represent the whole country, and we do it for the country. Their support will be vital to us, and they will make us fight till the end to get the best results, because football is a game of 90 minutes.


Interviewed by Ricardo Macivic

TETESI HAI: YANGA YAFANYA BALAA LINGINE SIMBA - OKWI KUTUA BONGO KUMALIZANA NAO.

Sekeseke la usajili limeendelea kupamba moto.

Katika kuhakikisha wanaibomoa kabisa safu ya ushambuliaji wa watani wao iliyowafunga kipigo cha aibu cha mabao 5-0 katika mechi ya kufunga msimu uliopita. Klabu ya bingwa ya afrika mashariki na kati, Dar Young Africans inakaribia kumnasa mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda na tegemeo la klabu ya Simba, Emmanuel Okwi.
Taarifa za udaku nilizozipata kutoka ndani ya Yanga ni kwamba timu yao ipo tayari kulipa fedha wanazozitaka Simba ili kuweza kupata huduma za Okwi msimu ujao. Taarifa zinasema kwamba Okwi ambaye kwa sasa yupo nchini Uganda anatarajiwa kutua Tanzania ndani ya kipindi cha masaa 72 kuja kumaliza suala la usajili wake kwenda Yanga ambao inasemekana wamemuhaidi fedha nyngi sana.

EXCLUSIVE: MAXIMO KUTUA JUMANNE KUMALIZANA NA YANGA

Baada ya kufanya vibaya katika msimu uliopita, Yanga wameendelea kuunda timu upya, baada ya juzi kumsainisha Kelvin Yondan, leo hii timu hiyo imehamia kwenye benchi la ufundi.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya zinasema klabu hiyo imemtumia tiketi ya ndege kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Marcio Maximo kwa ajili ya kuja kufanya mazungumzo ya kujiunga na klabu hiyo kwa ajili ya kuliongoza benchi la ufundi la wanajangwani kuanzia msimu ujao.

"Mpaka sasa tumefanya mazungumzo ya awali na Maximo na tumefikia makubaliano ya kimsingi, ambayo tunaweza kuja kuyakamilisha hapa nchini atakapotua siku ya jumanne wiki ijayo." - kilisema chanzo hicho cha kuaminika.

EXCLUSIVE: NSAJIGWA YUPO KENYA ANAFANYA MAZUNGUMZO NA GOR MAHIA

Siku chache baada ya kutemwa na klabu yake ya Yanga, nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania Shedrack Nsajigwa sasa yupo nchini Kenya akifanya mazungumzo ya kujiunga na klabu kongwe ya nchi hiyo Gor Mahia.

Taarifa rasmi nilizozipata kutoka nchini Kenya zinasema kwamba Nsajigwa ametua Kenya jana na leo amekutana na viongozi wa klabu ya Gor Mahia na so far mazungumzo yanaenda vizuri na muda wowote wanaweza kufikia makubaliano na Nsajigwa akajiunga na mtanzania mwenzie ambaye walikuwa wakicheza wote Yanga na timu ya Taifa, Ivo Mapunda.
PREVIEW: URUSI VS CZECH - VITA YA WASHIKA BUNDUKI WA LONDON ROSICKY NA ARSHAVIN


VIKOSI VITAKAVYOANZA
RUSSIA: 1: Akinfeev 2: Anyukov 3: Zhirkov 4: Berezoutski 5: Ignashevitch 6: Denisov 7:Zyryanov     8: Dzagoev 9: Kerzhakov 10 Arshavin 11: Shirokov

CZECH REPUBLIC - 1: Cech 2: Selassie 3: Kadiec 4:Sivok 5: Hubnik 6: Piasil 7: Petrzela 8: Hubschman 9: Baros 10: Rosicky 11: Rezek

MAMBO MUHIMU KUHUSU TIMU
  • Mchezaji wa Sporting Lisbon Marat Izmailov ndio mchezaji pekee aliyekuwa akihofiwa juu ya ufiti wake kuelekea kwenye michuano hii lakini sasa amerudi kwenye hali yake ya kawaida kwenye mazoezi pamoja na Alan Dzagoev, nchini ya nahodha Arshavin.
  • Safu pekee ambayo itakuwa na upinzani ni kwenye goli, Akinfeev atakuwa akipambana na Malafeev.
  • Czech watakuwa na nafuu kwamba mchezeshaji wao Tomas Rosicky amepona kutoka kwenye majeruhi na huku akiwekwa kwenye kikosi kitakachoshiriki kwenye michuano hii na anaweza kucheza nyuma ya mshambuliaji wa kati akama ambavyo katika nusu ya msimu alipokuwa Arsenal.
  • Striker Milan Baros, ambaye japokuwa ana tatizo la misuli na alifanyiwa vipimo juzi jumatano ili kupata uhakika wa ufiti wake, na kama hatokuwa fiti basi Necid na Pekhart watakuwa wanaisubiri nafasi yake.
  • Wachezaji wengine muhimu watawahusisha wachezaji wazoefu kama vile Peter Cech, Kadlec na Plasil.
 TAKWIMU
Russia hawajaruhusu wavu wao kuguswa mara sita kwenye mechi 7 za Euro zilizopita.

Czech Republic wameshinda mechi zao 3 za mwisho kwenye Euro.

Russia hawajafungwa katika mechi zao za mwisho za Euro.

UTABIRI
Russia wataenda kwenye mechi za group ambalo linatajwa kama dhaifu kabisa kwenye michuano kama timu inayopewa nafasi ya zaidi kwenye kundi hilo, ingawa kila mchezo wa kundi hili utakuwa mgumu.

Timu mbili zote zina uzoefu kwenye hatua hii, na makocha wote watakuwa wakiwategemea viungo wao wachezeshaji kusogeza mashambulizi mbele kwenye mechi hii.

UTABIRI:  RUSSIA 2-1 CZECH REPUBLIC

PREVIEW: POLAND VS UGIRIKI - SAFU BORA YA USHAMBULIAJI DHIDI YA UKUTA WA CHUMA


 VIKOSI AMBAVYO VINAWEZA KUANZA LEO
Poland - 1: Szczesny, 2: Boesnisch, 3: Wasilewski/, 4: Perquis,                    5: Murawski/ , 6: Polanski, 7: Piszcek 8:Perquis                       9: Lewandowski 10:Blaszczykowski 11: Rybus
Ugiriki - 1: Chalkias 2: Torosidis 3: Holebas 4: Pepadopoulos                   5: Papastathopoulos 6:Katsourania 7: Maniatis                    8: Karagounis 9: Salpingidis 10:Ninis 11: Samaras


 MAMBO MUHIMU KUHUSU POLAND VS UGIRIKI

  Poland
  • Poland hawana majeruhi kuelekea mchezo huu wa leo wa ufunguzi na wanategemewa kufanya vizuri katika michuano hii mbele ya mashabiki wao.
  • Mshambuliaji wao tegemeo Robert Lewandowski ataongoza mashambulizi, huku akitoa tishio la kufunga magoli baada ya kuwa na msimu mzuri kwenye ligi ya Bundesiliga na Dortmund akisadiana na mshambuliaji mwingine aliyetisha kwenye ligi ya Ufaransa Ludovic Obraniak.
  • Lukasz Piszczek alikuwa ndio beki wa kulia aliyekuwa na takwimu nzuri kwenye ligi kubwa 5 barani ulaya, akifunga mabao 4 na kutoa assists 7 kwenye Bundesliga.
  • Kutakuwa na upinzani mkubwa katika nafasi ya beki wa kati Kyriakos na Avraam. Kyriakos na advantage ya umri mdogo na amekuwa na msimu mzuri na Schalke mwaka huu. Pia alifunga goli la ushindi katika mechi ya kirafiki dhidi ya Armenia.
  • Tatizo kubwa kwa Ugiriki katika wiki kadhaa za nyuma ni kuwa na safu mbovu ya ushambuliaji, katika mechi za kirafiki hivi karibuni walifunga magoli mawili tu, huku magoli yote yakifungwa na mabeki, Hiki ni kitu ambacho inabidi wakirekebishe ikiwa wanataka kuvuka kwenye hatua ya makundi na kuendelea mbele.
  • Pamoja na kuwa na safu mbovu ya ushambuliaji, safu yao ya ulinzi hairuhusu magoli mengi na kwa hakika wapinzani watapata shida kugusa nyavu zao. Wakati waliposhinda kombe hili mwaka 2004, timu yao ilikuwa na ukuta mgumu kuliko na naamini mambo yatakuwa vilievile msimu huu.
  •  
  • FACTS KUHUSU HII MECHI
  • Ugiriki wameshinda mechi 7 kati ya 8 zilizopita kwenye Euro Cup.

    Poland wamepata clean sheet safi kwenye mechi 3 zilizopita dhidi ya Ugiriki  katika mashindano yote.

    Kumekuwepo na wastani wa magoli chini ya 2.5 katika mechi zilizozikutanisha timu hizi.

KULWA NA DOTO MAMA YAO NI MMOJA!





Kikubwa zaidi ninachojaribu kukiangalia ni jinsi ambavyo viongozi wa vilabu vya SIMBA na YANGA wasivyopenda kufuata taratibu na kanuni zilizowekwa, mwenyekiti wa SIMBA ameongelea kwa jazba kubwa sakata la beki wa timu yake Kelvin Yondani kusajiliwa na Yanga, si ajabu kesho tu tukasikia viongozi wa YANGA nao wakilijibu hili kwa mbwembwe.

 

Lakini mwisho wa siku ni lazima tukubali kuwa viongozi wote hawa wa simba na yanga wana mapungufu makubwa sana katika utendaji wao wa Kazi, na namna wanavyoendesha vilabu vyao na mpira wa Tanzania kwa ujumla.

Viongozi hawa wa SIMBA na YANGA Wamekuwa wakifanya mambo mengi sana ya ajabu ajabu. SIMBA na YANGA ni vilabu ambavyo vinatakiwa kuwa mfano wa kuigwa na vilabu vingine vidogo hapa nchini.
Lakini kwa mambo ambayo yamekuwa yakifanyika ndani ya vilabu hivi vikubwa ni ya ajabu sana na ya kusikitisha mno.

Kwa sakata hili la KELVIN YONDANI kumekuwepo na watu ambao wamekuwa wakijaribu kumshutumu mchezaji huyo, lakini mimi binafsi siwezi kumshutumu hata kidogo kwanza, hatujui wakati anasainishwa mkataba na Yanga alikuwa katika mazingira gani labda alitekwa na kulazimishwa,

Pili, labda aliamua tu kusajili huku akisema liwalo na liwe hao Simba wenyewe wamenisainisha mkataba kwa 'mkopo' wakati Yanga wamekuja mezani na mipesa yote hii.
Tatu, kusukumwa na hisia za kukumbuka manyanyaso yasiyoisha ya kushutumiwa kufungisha, mara ugomvi na baadhi ya viongozi Simba.Nne, kutokutambua umuhimu na kuuheshimu mkataba wake na Simba.
Kwa nchi za wenzetu zilizoendelea kitendo cha mchezaji kusaini mkataba ni kitu muhimu mno, lakini huku kwetu umuhimu na thamani ya mkataba hujulikana wakati wa matatizo hasa pale tu mchezaji anapotaka kuondoka na kwenda kujiunga na klabu nyingine.

Mimi nina uhakika wa zaidi ya asilimia mia moja kwamba hakuna mchezaji anayechukua mkataba na kuusoma, kuuelewa vipengele vilivyomo kabla ya kuusaini.


Ninachojua ni kwamba mchezaji huwa anaangalia napata kiasi gani…nazungumza hili kwasababu nina uhakika nalo na lilishawahi kunitokea wakati nacheza mpira, wakishakubaliana anaonyeshwa pakuweka saini na dole gumba kisha anachukua mzigo wake na kusepa.

Ndio maana wenzetu huwa wanawatanguliza wawakilishi, mchezaji anapokwenda kusaini mkataba ni lazima kuwa na meneja/wakala ama mwanasheria wake, lakini hapa kwetu Tanzania ni kinyume kabisa,wachezaji wenyewe hata darasa la saba hawajamaliza halafu anaenda kusaini mkataba tena wa kisheria tena ulioandikwa kwa lugha ya kiingereza, je ana uwezo wa kuelewa? au tunadanganyana tu na kupotezeana muda.

Professionalism inatakiwa kuanzia kwa viongozi wa vilabu kabla ya wachezaji, kwa maana viongozi wanatakiwa kusimamia sheria kama zilivyo, lakini cha kustaajabisha viongozi hao hao wa vilabu ndio wanakuwa vinara kwa kupindisha sheria hizo na kushindwa kwenda nazo sambamba.

Hivyo inapotokea ishu kama hii ya leo pasipo kufuata uweledi ndipo mmoja anaonekana kuonewa au kwenda against na mwenzake lakini kumbe wote wana makosa makubwa.


Ina maana hawa viongozi wanaowasainisha hiyo mikataba ya kisheria hao wachezaji hawajui kama hawana elimu ya kutosha ya kuisoma na kuielewa hiyo mikataba jamani hii lugha ya kiingereza inayotumika kwenye hii mikataba (mimi mwenyewe inaniacha ) ni mchezaji gani wa kitanzania mwenye uwezo wa kuisoma na kuielewa kabla ya kusaini na kuweka dole gumba? kama kweli hawa viongozi wanawatakia mema hawa wachezaji kwanini hiyo mikataba isiwekwe kwenye lugha ya Kiswahili angalau wanaweza kuambulia kitu. ( au kisheria ni lazima mkataba uwe kwenye lugha ya kiingereza ?)
Ishu kama hii ya YONDANI bila kuhangaika sana ebu tuangalie KANUNI ZA USAJILI zinasemaje


Kanuni ya 57
Uhamisho wa mchezaji

(1) Kilabu inaweza kumhamisha mchezaji kutoka kilabu kimoja hadi kingine, kwa madhumuni ya kumsajili, baada ya ligi kumalizika, au katika kipindi cha usajili wa katikati ya msimu. Kilabu inayotaka kumsajili mchezaji aliyesajiliwa na kilabu kingine au mwenye mkataba na kilabu kingine, italazimika kuafikiana na kilabu yake kabla ya kumsajili mchezaji huyo. Hata hivyo kilabu ambayo itaruhusiwa kusajili mchezaji katikati ya msimu ni ile ambayo haijatimiza wachezaji thelathini (30) au ile ambayo imempa mchezaji wake ITC ya kwenda kucheza soka nje ya nchi, au ile ambayo mchezaji wake amehamia kilabu kingine cha ndani kwa mujibu wa kanuni hii.

Kanuni ya 45
Usajili na uhamisho wa wachezaji

(4) Mchezaji ana uhuru wa kujisajili na kilabu kingine katika msimu mmoja iwapo kutakuwa na maelewano kati ya kilabu yake na ile inayotaka kumsajili.
(5) Kilabu inawajibika kuingia mkataba na mchezaji wa kuichezea lakini mkataba huo ni lazima uthibitishwe na TFF. Ada ya kuthibitisha mkataba ni shilingi elfu hamsini (50,000/=).

(6) Mchezaji ambaye ameingia mkataba wa zaidi ya msimu mmoja hatoruhusiwa kujisajili na kilabu kingine kabla ya kilabu yake mpya kuafikiana na kilabu yake ya zamani.

Kanuni ya 56
Katazo

Haitaruhusiwa kwa mchezaji yeyote kutia saini kwenye mikataba wa vilabu viwili tofauti kwa wakati mmoja na inayohusu kipindi kimoja. Mchezaji atakayesaini mikataba ya timu mbili tofauti kwa wakati mmoja, ataadhibiwa kwa mujibu wa kanuni ya 44 (4) ya kanuni hizi.
Kutokana na vipengele hivyo hapo juu hakuna mchezaji ambaye anaweza kuhama timu moja kwenda timu nyingine kihuni huni tu pasipo kufuata kanuni na taratibu.

Sakata la Simba na Azam juu ya usajili wa Ibrahim Jeba.
Lazima tusiwe wanafiki, waswalihi wanasema mkuki kwa nguruwe ila kwa binadamu mchungu, wakati tukiwa tunalijadili sakata hili la Yondani si vibaya pia tukaliwe mezani sakata linalomuhusu mchezaji Ibrahim Jeba aliyesajiliwa na Simba Kutoka Azam pasipo taratibu kufuatwa.


Kanuni ya 44
Masharti ya mikataba kati ya wachezaji na kilabu
(1) Muda wa chini wa mkataba utakuwa kuanzia tarehe ya kuanza kutumika hadi mwisho wa msimu. Muda wa juu wa mkataba utakuwa ni kipindi cha miaka mitano (5). Mikataba ya muda mwingine wowote itakubaliwa kama inafuata Sheria ya Mikataba inavyosema. Mchezaji chini ya umri wa miaka 18 haruhusiwi kuingia kwenye mkataba wa mchezaji wa kulipwa kwa kipindi kinachozidi miaka mitatu (3), sharti lolote linalotaja kipindi kirefu zaidi halitatambuliwa.

(2) Kilabu inayotarajia kuingia mkataba na mchezaji wa kulipwa haina budi kuiarifu kilabu yake ya sasa kwa maandishi kabla ya kufanya makubaliano na mchezaji huyo wa kulipwa. Mchezaji wa kulipwa atakuwa huru tu kuingia mkataba na kilabu nyingine iwapo mkataba wake na kilabu yake ya sasa umekwisha au utakwisha baada ya miezi sita (6). Uvunjaji wowote wa sharti hili utastahili vikwazo vinavyofaa.

Niliposema viongozi wote hasa wa vilabu vya SIMBA na YANGA ndo wenye matatizo makubwa nilikua namaanisha vitendo kama hivi.
Kufanya mazungumzo ya siri na mchezaji pasipo kupata ruhusa ya klabu yake ni kosa kubwa ambalo hata FIFA wanalipiga vita. 

Ina maana Kulwa na Doto hawazijui hizi taratibu na kanuni za kusajili mchezaji ?

Euro 2012: UBAO WA TAKWIMU ZA WACHEZAJI!

Euro 2012 Focus: Player Stats Leaderboards
Euro 2012 Focus: Player Stats Leaderboards
Euro 2012 Focus: Player Stats Leaderboards
Euro 2012 Focus: Player Stats Leaderboards

TETESI : JUMA NYOSO HUYOO YANGA

TAARIFA NILIZOZIPATA HIVI PUNDE BEKI WA SIMBA JUMA NYOSSO MUDA WOWOTE KUANZIA HIVI SASA HUENDA NAYE AKASINI KWA AJILI YA KUJIUNGA NA YANGA.
TAARIFA NILIZOZIPATA KUTOKA KWENYE CHANZO CHA KUAMINIKA KIKOSI KAZI CHA YANGA TAYARI KIPO KWENYE KAMBI YA TIMU YA TAIFA KWA AJILI YA KUMALIZANA NA BEKI HUYO .

EURO 2012: ITALIA NA SAFU YA USHAMBULIAJI YA WENDAWAZIMU CASSANO NA BALOTELLI.

Maneno ya Cesare Prandelli alipomrithi Marcello Lippi kama kocha wa timu ya taifa baada ya kombe la dunia mwaka 2010 ni kwamba ataifanya Azzuri ivutiwa kwa kucheza soka zuri la kushambulia. Kwa hakika amejitahidi sana huku akitambulisha utaratibu wa 'ethical code' (wachezaji wanaokuwa wamesimamishwa kwa makosa ya kinidhamu hawatoitwa timu ya taifa) na kusisitiza katika kuwapa nafasi zaidi viungo wenye ufundi zaidi katika timu yake. Wazo ni kuifanya Italia kucheza kwa staili yake ya mfumo wa tiki-taka, staili inayopendelewa zaidi na Wahispania.

Akiuacha mfumo wa siku nyingi wa kujenga ukuta wa chuma na kucheza kwa mashambulizi ya kushtukiza kwa ajili ya mfumo ambao unatumia na Spain, ambao mpaka sasa umeleta matokeo ya mchanganyiko. italy haikufungwa hata mechi moja kwenye hatua ya kufuzu, lakini wamekuwa wakifungwa kwenye mechi za kirafiki. Skendo ya upangaji wa matokeo ambayo inaliandama soka la nchi hiyo kwa miaka mingi sasa, haitegemewi kuwa na madhara makubwa sasa hivi kuliko ilivyokuwa katika miaka 1982 na 2006, sababu kubwa ni kwa kuwa ni wachezaji wachache wa kikosi cha sasa wameguswa na kashfa hiyo, lakini suala hilo bado linabakia kuwa sio zuri kwa wachezaji.

Droo ya group C haikuwa nzuri kwa Italy, lakini atleast mechi yao dhidi ya Spain itakuwa ya kwanza. Na kupata pointi kutoka kwenye mechi hiyo ni jambo ambalo linawezekana, kwa kuangalia Spain huwa na kawaida ya kuanza vibaya michuano mikubwa, ukiangalia kombe la dunia lilopita walipofungwa na Uswis katika mechi ya kwanza makundi. Baada ya mechi hiyo atleast kidogo mambo yanaweza kuwa mazuri dhidi ya Croatia na Ireland.

WACHEZAJI MUHIMU

Gianluigi Buffon
Nahodha amerudi kwenye kiwango chake baada ya majeruhi yaliyomkumba msimu wa  2010-11. Ukifikiria namna safu ya ulinzi ilivyokuwa dhaifu, Azzuri wanahitaji kuwa na Buffon mwenye kiwango cha juu ili kuepeuka balaa. Ni uchizi sasa kufikiri kwamba safu ya ulinzi ambayo siku zote imekuwa ndio nguzo ya timu ya taifa ya Italia, sasa hivi ndio ulipo udhaifu wao, lakini hapa ndipo tulipo, na sasa tumaini lote lipo kwa Buffon na mikono pamoja na miguu yake kutatua hilo tatizo.


Mario Balotelli
Mario Balotelli alisema hatoshangilia goli mpaka atakapofunga goli la ushindi kwenye world cup au Euro, hivyo hii ndio nafasi pekee kumuona Super Mario akicheza kwa furaha baada ya kutupia kambani. Tuache utani, huu ni muda wake kuweza kuonyesha kwanini makocha wamuamini na kumpa nafasi. Balotelli ana nguvu, ujuzi na kimo kizuri, Anachohitaji ni kutulia na kutumia vizuri nafasi atakazopata huku akijiepusha na suala la nidhamu mbovu. Akifanikiwa kwenye hayo atatisha.


Daniele De Rossi
Katika kiungo ambacho kimejaa wapiga pasi mafundi zaidi, De Rossi ndio kiumbe anayetegemewa kusambaza minguvu yake. Shujaa huyu wa Roma ndio sasa anaelekea kwenye kilele chake, akiwa ameshaji-commit kwenye klabu yake, sasa yupo huru kufikiria timu ya taifa tu. Atakuwa na shughuli ngumu katika kupambana na kuizuia safu ya ulizni wa timu ambayo ni dhaifu kutoguswa

 JE SAFU YA USHAMBULIAJI YA MACHIZI ITAFANYA VIZURI?
Mara tu Giueseppe Rossi alipoumia, mikono ya Prandelli ilikuwa imefungwa. Akawa hana chaguo lingine zaidi ya kuwatumia Balotelli na Antonio Cassano. Hii haihusu suala la uwezo  - -wachezaji wote wawili wana vipaji vikubwa tataizo ni nidhamu: wote wawili wana matukio mengi ambayo yanahusu ukosefu wa nidhamu na tabia nyingine tofauti,ndani na nje ya uwanja. Hivyo hilo ni tatizo ambalo Prandelli inabidi alitafutie suluhisho.

HUU NDO MKATABA WA KELVIN YONDANI NA SIMBA SC.


COPA COCA-COLA TAIFA KUANZA KUTIMUA VUMBI JUNI 24

Michuano ya Copa Coca-Cola ngazi ya Taifa inaanza kutimua vumbi Juni 24 mwaka huu kwenye mikoa ya Dar es Salaam na Pwani huku pambano la ufunguzi likiwa kati ya Kigoma na Lindi litakalofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Upangaji ratiba (draw) umefanyika leo (Juni 7 mwaka huu) kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kushuhudiwa na waandishi wa habari, makocha wa timu za mikoa za Copa Coca-Cola na wadhamini kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola.
Makocha 35 wa timu za Copa Coca-Cola kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani wako kwenye kozi ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) inayoendeshwa na wakufunzi Ulric Mathiot wa FIFA kutoka Seychelles na wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Sunday Kayuni wa Tanzania.
Mikoa 28 ya kimpira ya Tanzania itashiriki katika mashindano hayo na imegawanywa katika makundi manne ya timu saba saba. Baadaye timu zitapambana katika hatua ya robo fainali, nusu fainali na fainali itakayofanyika Julai 15 mwaka huu.
Kundi A lina timu za Arusha, Ilala, Kigoma, Kusini Pemba, Lindi, Rukwa na Ruvuma. Kundi B ni Iringa, Kaskazini Pemba, Manyara, Mjini Magharibi, Morogoro, Mwanza na Tanga. Dodoma, Kaskazini Unguja, Kinondoni, Mara, Mbeya, Mtwara na Temeke ziko kundi C wakati kundi D ni Kagera, Kilimanjaro, Kusini Unguja, Pwani, Shinyanga, Singida na Tabora.
Viwanja vitakavyotumika katika mashindano hayo ambapo mechi zitakuwa zikichezwa asubuhi (saa 2.30) na jioni (saa 10.00) ni Uwanja wa Karume na Tanganyika Packers (Kawe) kwa Dar es Salaam. Viwanja vya Mkoa wa Pwani ni Tamco na Nyumbu. Timu zote katika mashindano hayo zitacheza katika viwanja hivyo.
Mbali ya Kigoma na Lindi, mechi nyingine za ufunguzi Juni 24 mwaka huu ni kundi B Morogoro na Manyara (saa 2.30 asubuhi Uwanja wa Kawe), kundi C ni Temeke na Kinondoni (saa 2.30 asubuhi Uwanja wa Nyumbu) na kundi D ni Kilimanjaro na Kusini Unguja (saa 2.30 asubuhi Uwanja wa Tamco).
Wachezaji wanaotakiwa kushiriki kwenye michuano hiyo ya umri chini ya miaka 17 ni wale waliozaliwa kuanzia Januari 1, 1996.

SAKATA HILI LA YONDANI KWA UPANDE MWINGINE LIMECHANGIWA NA SERA MBOVU YA USAJILI YA SIMBA!

Sakata la usajili wa Kelvin Yondani limetokea kuteka hisia za wengi katika kipindi cha masaa 48. Taarifa ambazo zimetapakaa kwenye vyombo ya habari zinasema kuwa Dar es salaam Young Africans imekamilisha usajili wa Yondani huku nakala ya mkataba wake alioingia na klabu hiyo ukionyesha kuwa amesaini kuichezea Yanga kwa miaka miwili huku akitia kibindoni kiasi cha Milioni 30 huku mshahara wake ukiwa laki nane kwa mwezi.
Upande wa pili wa sinema hii ambao ni klabu anayodaiwa kutoka Yondani ya Simba Sports unadai kuwa Yondani aliongeza mkataba wake wa awali na klabu hiyo kabla hata ya mwisho wa msimu huu uliopita.
Kikubwa kinachonitatiza ni sera ya usajili ya klabu ya Simba ambayo ndio hasa mjadala mkuu kwenye makala haya.
Tukirudi nyuma msimu uliopita Simba ilitangaza kumuacha beki wake wa kati Meshack Abel . Ukiangalia takwimu za michezo ya Simba kwa kipindi cha miaka miwili iliopita utagundua kuwa moja ya matatizo sugu imekuwa safu ya ulinzi, hata hivyo Meshack Abel ni mmoja ya mabeki wa kati shupavu ambao hata kwenye timu ya taifa wamekuwepo kwa kipindi kirefu. Baada ya kumuacha Abel simba iliwasajili Obadia Mungusa na Victor Costa. Hiki ni kipindi ambacho Kevin Yondani alikuwa froze out of the team (inasemekana alikuwa na beef na mmoja wa viongozi).  Smba pia kwa sababu zisizojulikana iliamua pia kumuacha beki wa pembeni kulia Haruna Shamte wakati ambapo alikuwa anachipukia na tayari alikuwa ameanza kuitwa kwenye timu ya taifa  pamoja na kuwa mdogo kiumri.
Mbdala wa Shamte alikuwa beki wa zamani Nasor Masoud Cholo aliyerudishwa toka JKT Oljoro na Shomari Kapombe ambaye awali alisajiliwa kama kiungo ilia ni uwezo wake au versatility yake ambayo imeshuhudia akirudishwa nyuma kucheza wakati mwingine kama beki wa kati na pembeni.
Tetesi ambazo tunazisikia sasa ni kwamba ,Juma Jabu,Obadia Mungusa na Victor Costa wameachwa huku Juma Nyoso naye akiwa mbioni kuachwa na sababu tunayoambiwa ni kwamba amekuwa akiigharimu timu mara kwa mara. Tubaki hapa kwa Nyoso kwanza , huyu ni mmoja wa wachezaji waliotokea kuwa kipenzi cha mashabiki wa Simba kutokana na umahiri kwenye eneo lake na hata ukiangalia kwenye timu ya taifa Nyoso amekuwa akiitwa mara kwa mara hali inayoonyesha kuthaminiwa kwa mchango wake , nyoso pia ni mmoja wa wachezaji ambao wameiwakilisha  Simba kwenye michezo karibu yote kwenye ligi na kimataifa . Nyoso pia ni nahodha wa tatu Simba baada ya Kaseja na Boban. Swali la kijiuliza ni je mchezaji huyu ambaye ametokea kuwa senior player Simba anastahili kutupiwa virago kweli? Eti wanasema kuwa anaigharimu timu kwa kadi nyekundu. ntakurudisha nyuma unakumbuka wakati Fernando Torres anacheza Liverpool,kuna wakati kwenye michezo mitano mfululizo ya United na Liverpool Torres alikuwa anafunga kwa kumpita Nemanja Vidic na zaidi ya hapo Vidic amewahi kuonyeshwa kadi nyekundu katika michezo mitatu mfululizo dhidi ya Liverpool,United ilimfukuza? Jibu ni hapana , kwa hali ya kawaida mwanadamu huwa anapima mema na mabaya au faida na hasara yaani profit vs losses kwa kufanya uwiano , Simba imetwaa ubingwa msimu huu hivyo kwa uwiano halisi tu kadi nyekundu kwa nyoso hata zingekuwa kumi bado sio sababu kwa kuwa Simba imemaliza kwa kutwaa taji.
Turudi kwa mtazamo wa jumla ,kuanzia kwa Meshack Abel,Costa,Jabu,Obadiah,Nyoso ,Haruna na Shamte labda na hili la Yondani,. Kuachwa kwa wote hawa kunamaanisha kuwa Simba inapoteza zaidi ya asilimia 70 ya backline yake baada ya kuwa imetwaa ubingwa na kumaliza nafasi ya pili msimu uliopita tena huku ikiwa sawa na timu iliyotwaa ubingwa ,je hii ni sera nzuri ya usajili ambayo inafanya kazi hapa ???
Tukiachana na hayo huku na kule kuna tetesi kuwa Salum Machaku anapelekwa timu nyingine kwa mkopo. Machaku amesajiliwa msimu uliopita toka Mtibwa. Amecheza Simba msimu mmoja ambao Simba imetwaa ubingwa huku ikifika hatua ya mbali kwenye michuano ya kimataifa . Of course tatizo la machaku limekuwa kushuka na kupanda kwa kiwango pasipo kuwa na muendelezo yaani consistency,lakini tusisahau kuwa huu ni msimu wake wa kwanza , ni vigumu kwa mchezaji ku-settle kwenye msimu wa kwanza ,kwanini amehukumiwa na kuonekana hapaswi kupewa nafasi ya pili ya kujidhatiti kwenye Timu.
Majibu ya maswali yote haya ni rahisi sana, Simba haina sera nzuri ya usajili,maamuzi ya kusajili na kuacha wachezaji yanafanyika kiholela holela sana , hata hili la Yondani ukichunguza kwa ukaribu chanzo ni Simba wenyewe , Yondani alikuwa nje ya timu kwa muda mrefu , taarifa zinasema kuwa klabu ilikuwa haimlipi mshahara , Yanga walionyesha interest ya kumsajili siku nyingi , kilichokuwa kinambana ni mkataba lakini alikuwa frustrated sana na ndio maana akasaini yanga baada ya kuonyeshwa fedha ambazo hakuwa amepewa na Simba . Ukiritimba kama huu ndio unaendelea kulihikumu soka la Tanzania na kwa mtaji huu maendeleo tutayasikia kwa wenzetu kina Mariga, Oliech na Obua.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

   SIMBA SPORTS CLUB           
P.O.BOX 15318 | TEL+255 222183330 |FAX +255 222183330 |MSIMBAZI/MCHIKICHI STREET | DAR ES SALAAM | TANZANIA | EMAIL   simbasportsclub@yahoo.com|WEBSITE www.simba.co.tz| AFFILIATED TO TFF, DRFA and IDFA
                                
Simba Sports club imesikitishwa na kitendo cha Young Africans kuvunja taratibu za usajili kwa kumrubuni mchezaji wake Kelvin Patrick Yondani  kwa kuzungumza naye na baadae kwa ushahidi wa picha kuonekana wakimuandikisha makaratasi ambayo baadae imeripotiwa na vyombo vya Habari kwamba alikuwa akisaini mkataba wa kuichezea timu hiyo ya Young Africans.

Kwamba katika picha hiyo ameonekana mjumbe wa Young aliyejiuzuru bwana Seif Ahmed na hilo lilitoa shaka kama utaratibu huo umefanywa na klabu ya Young, lakini shaka hiyo imeondolewa pale ambapo tovuti ya Young imetangaza kumsajili mchezaji huyo wa Simba SC, lakini zaidi ya hilo picha inaonyesha fedha zikiwa zimewekwa mbele ya mchezaji jambo linaloonyesha mazingira ya kurubuniwa kwani kwa utaratibu wa kifedha, pesa nyingi kiasi hicho malipo yake yanashauriwa/yanapashwa kupitia benki.

Mbali ya hayo picha hiyo inamuonyesha Kelvin akiwa katika jezi ya mazoezi ya timu ya Taifa na yenye logo ya Kilimanjaro na kumbukumbu zinaonyesha mkataba kati ya TBL na TFF tarehe 9/5/2012, kwa haraka haraka tukio hilo limefanyika katika kipindi chini ya mwezi mmoja ingawa taarifa za ushahidi zinaonyesha tukio hilo limetokea jana tarehe 6/6/2012.
Simba Sports Club ilipenda kuamini kwamba tukio hilo haliihusu klabu ya Young kwani bwana Seif Ahmed alishajiuzuru kutoka kwenye kamati ya Young Africans, kwani Young ni klabu kongwe na inayojua taratibu zote za usajili.
Kwamba Simba Sports Club imeshawasiliana na jopo lake la mawakili na inajiandaa kuishtaki klabu ya Young katika chombo husika cha mpira na kudai adhabu ya kutopitisha majina yote ya usajili ya Young kwa mwaka 2012/2013 na miaka mingine miwili ijayo na Simba SC ipo tiyari kufuatilia suala hili hadi katika mahakama ya mpira ya FIFA.
Kelvin Yondani ni mchezaji halali wa Simba Sc aliye na mkataba hadi 31 mei 2014 mkataba ulioongezwa tarehe 23/12/2011 kuundeleza mkataba wa awali uliokuwa unaisha tarehe 31/5/2012. Sheria za FIFA za hadhi na uhamisho wa wachezaji ziko wazi  katika kipengele cha 5 kifungu kidogo cha 2 kinasema kwamba mchezaji atasajiliwa kuichezea timu moja tu kwa wakati mmoja.

Imetolewa leo tarehe 7/6/2012.
MH. ISMAIL ADEN RAGE (MB)
MWENYEKITI
SIMBA SPORTS CLUB

TAARIFA KUTOKA TFF!

WAZIMBABWE KUCHEZESHA TAIFA STARS, GAMBIA
Waamuzi kutoka Zimbabwe ndiyo watakaochezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia hatua ya makundi Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Gambia itakayochezwa Juni 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) mwamuzi wa kati atakuwa Ruzive Ruzive. Waamuzi wasaidizi ni Salani Ncube na Edgar Rumeck wakati mwamuzi wa akiba ni Norman Matemera.
Kamishna wa mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni Fanie Wallace Mabuza kutoka Swaziland wakati mtathmini wa waamuzi (referee assessor) ni Ali Baligeya Waiswa.
Waamuzi hao watawasili nchini kesho (Juni 8 mwaka huu) saa 1.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways wakati Kamishna wa mechi hiyo atawasili siku hiyo hiyo saa 12.50 jioni kwa ndege ya South African Airways. Mtathmini wa waamuzi atatua pia Juni 8 mwaka huu saa 7.55 mchana kwa ndege ya Kenya Airways.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inaendelea na mazoezi leo saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam chini ya Kocha Mkuu Kim Poulsen.
GAMBIA KUWASILI LEO USIKU
Timu ya Taifa ya Gambia (The Scorpions) ambayo awali ilikuwa iwasili nchini leo (Juni 7 mwaka huu) saa 1.40 asubuhi sasa itawasili leo saa 9.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars.
The Scorpions ilipaswa kubadili ndege Dakar, Senegal jana usiku lakini kukawa na ucheleweshaji (delay), hivyo ikashindwa kuwahi Nairobi, Kenya ambapo ingeunganisha kwa ndege ya alfajiri kuja Dar es Salaam.
Kikosi cha timu hiyo chenye wachezaji 22 wakiwemo tisa wanaocheza mpira wa kulipwa nje ya nchi hiyo kitafikia kwenye hoteli Sapphire iliyopo Mtaa wa Lindi na Sikukuu eneo la Kariakoo.
Wachezaji walioko katika msafara huo ni Musa Camara, Abdou Jammeh, Momodou Futty Danso, Lamin Basmen Samateh, Ousman Koli, Pa Saikou Kujabi, Mustapha Kebba Jarju, Yankuba Mal Ceesay na Demba Savage.
Wengine ni Saihou Gassama, Alieu Darboe, Momodou Ceesay, Pa Modou Jagne, Tijan Jaiteh, Bubacarr Sanyang, Christopher Allen, Musa Yaffa, Sulayman Marr, Mamut Saine, Hamsa Barry, Ali Sowe, Omar Colley na Saloum Faal.
PROGRAMU YA MAZOEZI YA GAMBIA
IJUMAA JUNI 8
01.00 asubuhi Mazoezi- Uwanja wa Karume
10.00 jioni   Mazoezi- Uwanja wa Taifa
JUMAMOSI JUNI 9
04.00 asubuhi  Mkutano na Waandishi wa Habari- Ukumbi wa TFF
10.00 jioni  Mazoezi- Uwanja wa Taifa
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

NINGEKUA YONDANI PIA NINGECHUKUA MZIGO !



Well done Kevin Yondani...hata mimi ningefanya hivyo hivyo...unachukua huku m20 kule m30....watapiga kelele weweeeee lakini mwishowe watapatana. watu wenyewe hawako serious tumewazoea. ingekuwa umesaini katika makampuni mawili serious kama Barrick na Vodacom labda...lakini hizi timu za Kariakoo...wala usihofu. wataelewana tu....hakuna jela hapo. kwanza ebu ona noti zenyewe zinatolewa kwa cash badala ya hundi au transactions zinazoeleweka!!! we live just once....

Yanga kiboko
hii jezi ya Kilimanjaro Lager na taifa Stars imetoka May this year, kwa hiyo ule mkataba wa miaka 17 na majina ya kinyumenyume ni zuga tuu.... Mohamed Shaban tuletee picha kama hii ili tujue kuwa mmemsajili kweli vinginevyo imekula kwenu.... Manji kaanza kazi Jangwani

Nina urafiki na wachezaji wengi wa yanga. Siba,azam na klabu nyingne za bongo hata wachezaji wa ndondo,kitu ambacho huwa nasema siku zote ni kwamba wachezaji wa kitanzania wana matatizo makubwa,of course its like the whole soccer family in bongo is fucked up,Yondani amesaini Yanga wakati akiwa na mkataba na Simba ambako alishasaini tunaambiwa sijui 6 months ago,in my opinion a contract has to be r...espected,sheria za mkataba kimataifa ziko hivi,mkataba ukibaki muda mfupi kuisha lazima mazungumzo yafanyike either kurenew au kuuzwa kwa timu nyingine,in between mchezaji hatakiwi hata kuzungumza na timu nyingine bila ridhaa ya timu ambayo tayari ana mkataba nayo ambayo kwa hali ya kawaida lazima itoe ruhusa mazungmzo yaendelee,in this saga Kelvin Yondani is in hot water for signng for two clubs kama ninachokisikia ni sahihi,pia viongozi wa yanga wana kosa kubwa ambalo ni kufanya mazungumzo kinyume cha taratibu na mtu ambaye tayari ana mkataba,viongozi wa simba kwa upande wao wana kosa la kutengeneza situation ya kumfreeze out yondani kwenye timu hali iliomfrustarte na kumfanya asaini timu nyingine,WHY ALWAYS TANZANIA vitu vya kipuuzi kama hivi vinatokea.


kwa uelewa wangu mdogo na hela hizo ni mil. 18



Pesa ya Manji hiyooooooooo
Kweli Manji agombee Yanga..Na Pesa yote hiyo aliyonayo?
Anatafuta nini? Kuna kitu......Ukiona mtu mzima kayavulia nguo ujue kuna jambo....kazi kwenu yanga.......

YANGA YAANZA MAZUNGUMZO NA MAXIMO

Taarifa zisizo rasmi nilizozipata hivi punde klabu ya Yanga ipo kwenye mazungumzo na aliyekua kocha wa Taifa Stars Mbrazil Marcio Maximo.
Kama mazungumzo hayo yatafanikiwa basi Maximo atarejea kwa mara nyingine tena hapa nchini kuja kuifundisha Yanga.

Wednesday, June 6, 2012


UFARANSA: HAIJASHINDA MECHI YOYOTE KWENYE EURO WALA WORLD CUP TANGU 2006: ITAFANYA NINI KWENYE EURO 2012.

Laurent Blanc anaichukua Ufaransa kwenda nayo kwenye Euro 2012 huku akiiongoza timu hiyo kutofungwa katika michezo 20, ambayo inahusisha ushindi dhidi ya Ujerumani, England na Brazil. Lakini kocha huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa bado haipi nafasi kubwa timu. Ufaransa haijashinda mechi yoyote ya mwisho ya michuano mikubwa yenyewe tangu mechi ya nusu fainali ya World Cup 2006 (haikushinda mechi yoyote kwenye Euro 2008 na WOZA 2010), huku wakishika nafasi ya 16, nafasi tisa nyuma ya wapinzani wao England wanaoshika nafasi ya saba kwenye ubora wa viwango wa FIFA.

Blanc bado na maumivu ya kichwa kuhusu upangaji wa kikosi hasa kwenye nafasi ya beki wa kushoto, ambapo Gael Clichy ameonyesha kiwango kizuri kwenye mchi dhidi ya Serbia siku chache baada ya Evra kucheza chini kiwango dhidi ya Iceland. Kiungo mkabaji Yann M'Vila pia ana majeruhi ya enka ambayo yatamfanya asicheze mchezo wa kwanza na Alou Diarra anategemewa kumbadili.

Lakini hiki ni kikosi tofauti sana na kile kilichoenda kwenye kombe la dunia 2010 chini Raymond Domenech nchini South Africa. Golikipa Hugo Lloris sasa ni nahodha, lakini Phillipe Mexes, M'Vila na Karim Benzema ambaye yupo kwenye form sasa hivi, wote waliikosa michuano ya WOZA 2010 hivyo hawakuwemo kwenye aibu iliyopita. Lakini hili haliwezi kusemwa linapojitokeza jina la Frank Ribery, ambaye kwa sasa yupo desparate kuweza kurudisa imani na upendo wa wafaransa. Baada ya miaka 3 bila kufunga bao, Ribery alifunga mara mbili katika mechi 2 za kirafiki zilizopita. Ikiwa ataanza japo kuileta nusu ya uwezo anaonyesha Bayern Munich akiwa kwenye jezi za Blue, then Les Bleus wanaweza kuwashangaza wengi.

WACHEZAJI MUHIMU

Karim Benzema
Tumaini kubwa la soka la Ufaransa lilikuwa na mwanzo mmbaya kwenye career yake ndani ya timu ya taifa ya Ufaransa kwenye michuano ya Euro 2008, pale alipotuhumiwa kwa pamaja na Samir Nasri kwa kutokuwa na heshima kwa wachezaji wakubwa na kwa kutompasia mipra mingi Thierry Henry. Akaachwa kwenye kombe la dunia 2010, lakini amekuwa ndio mfungaji bora wa Ufaransa chini ya Blanc, akifunga mabao matano katika mechi 17, likiwemo goli la ushindi dhidi ya Brazil. Huku akiwa amemaliza msimu wa mafanikio na Real Madrid akifunga mabao 32, huku akitamba kwamba amekuwa mchezaji mzuri zaidichini Jose Mourinho. Na kama hayo maneno yataonekana kwenye vitendo basii Ufaransa itaifadika sana.


Samir Nasri
Mpaka aliposhinda kombe la premier league na Manchester City mwezi uliopita, Nasri alikuwa ameshinda kombe moja tu kwenye maisha yake ya soka la kulipwa: alipofunga goli la ushindi kwenye fainali ya Euro 2004 kwa timu ya vijana wa miaka 17. Nasri ni moja ya sehemu ya kundi 'Kizai cha 87' kinachowahusisha wachezaji waliozaliwa mwaka 1987 na kwa sasa wakiwa ndio wanaelekea kwenye vilele vya viwango vyao wakiwa kwenye timu ya taifa ya wakubwa. Kundi hilo lilikuwa linawahusisha Benzema, Hatem Ben Arfa, Jelemu Menez na Blaise Matuidi - wote walicheza kwenye Euro 2004, na sasa wapo kwenye Euro 2012 ya wakubwa. Kama kiungo mchezeshaji Nasri anayo nafasi ya kuifanya timu ikacheza soka zuri la kushambulia na ahatimaye kuiletea timu ushindi. Ni jukumu ambalo amekuwa alilitumikia siku nyingi, sasa hivi anayo nafasi ya kuonyesha kama kweli anastahili.

Yann M'Vila
Kiungo mkabaji anatarajiwa kuuzwa kwa mapesa mengi mara baada ya michuano hii, na klabu yake. Rennes, inaweza ikataka kuongeza beikama atacheza vizuri kwenye Euro.M'Vila alikuwa na bahati kuikosa world cup, alitoswa na Domenech lakinii chini ya Blanc amejihakikishia nafasi ya kudumu. Akiwa na miaka 21, amekuja kuwa mchezaji muhimu wa Ufaransana kwa jinsi inavyocheza, kuvunja mashambulizi ya wapinzani na kushambulia kutokea kwenye kiungo huku akiwa na uwezo mkubwa wa kupiga pasi. Ameshajulikana kwamba ataikosa mechi yake ya kwanza ya Euro dhidi ya England na anategemewa kurudi dimbani kwenye mechi ya Ukraine.

BIN KLEB ARUDISHA FOMU YAKE NA MANJI JANGWANI


ABDALLAH Ahmad Bin Kleb amerudisha fomu yake ya kugombea Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, lakini inadaiwa alikuwa ana fomu nyingine tatu, ambazo inadaiwa kuwa ni za Yussuf Manji kugombea Uenyekiti, Isaac Chanji, Makamu Mwenyekiti, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakhim Masu. Pichani Bin Kleb akikabidhi fomu hizo.




Anaondoka

TANZANIA YAPANDA VIWANGO VYA FIFA

KIINGILIO MECHI YA TAIFA STARS, GAMBIA 3,000/-
Kiingilio cha chini ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Gambia (The Scorpions) itakayochezwa Jumapili (Juni 10 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 3,000.
Watazamaji watakaolipa kiingilio hicho ni watakaokaa kwenye viti vya rangi ya bluu na kijani ambavyo ni 36,693 kati ya jumla ya viti 57,558 vilivyopo katika uwanja huo wa kisasa. Kiingilio kwa viti vya rangi ya chungwa ni sh. 5,000.
Kwa upande wa VIP C watalipa sh. 10,000 wakati VIP B ni sh. 20,000. Kiingilio kwa jukwaa la VIP A ambalo linachukua watazamaji 748 tu ni sh. 30,000 kwa mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni.
Tiketi zitaanza kuuzwa Jumamosi (Juni 9 mwaka huu) kuanzia saa 2 asubuhi kwenye vituo vya Mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio na Samora, Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Soko Kuu la Kariakoo na Uwanja wa Taifa. Siku ya mechi pia mauzo yatafanyika katika vituo hivyo na baadaye kuhamia Uwanja wa Taifa.
GAMBIA YATARAJIA KUINGIA LEO DAR ES SALAAM
Timu ya Taifa ya Gambia (The Scorpions) inatarajia kuwasili nchini wakati wowote kuanzia leo (Juni 6 mwaka huu) tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars.
Kamati ya Maridhiano inayoendesha Chama cha Soka Gambia (GFA) hadi leo mchana ilikuwa haijatuma taarifa rasmi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) juu ya ujio wake.
Lakini vyombo vya habari vya Gambia vimeripoti kuwa timu hiyo ikiwa na wachezaji 23 na viongozi tisa ilitarajiwa kuondoka huko leo kuja Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na washabiki wengi nchini.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa GFA aliyekaririwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo, Bakary Balder, msafara wa timu hiyo utaongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana na Michezo, Malang Jassey. .
Mbali ya Jassey, viongozi wengine katika msafara huo ni Ofisa Utawala wa timu Modou Sowe, Kocha Luciano Machini, makocha wasaidizi Peter Bonu Johnson na Lamin Sambou, Kocha wa makipa Alhagie Marong, mtaalamu wa tiba mbadala (physiotherapist) Pa Matarr Ndow, Mtunza vifaa Sanna Bojang na Daktari wa timu Kalifa Manneh.
Wachezaji ni Musa Camara, Abdou Jammeh, Momodou Futty Danso, Lamin Basmen Samateh, Ousman Koli, Pa Saikou Kujabi, Mustapha Kebba Jarju, Yankuba Mal Ceesay, Demba Savage, Saihou Gassama, Alieu Darboe, Momodou Ceesay, Pa Modou Jagne, Tijan Jaiteh, Bubacarr Sanyang, Christopher Allen, Musa Yaffa, Sulayman Marr, Mamut Saine, Hamsa Barry, Ali Sowe, Omar Colley na Saloum Faal.
TANZANIA YAPANDA VIWANGO VYA FIFA
Tanzania imepanda kwa nafasi sita kwenye orodha ya viwango ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) iliyotolewa leo (Juni 6 mwaka huu) na shirikisho hilo.
Kwa viwango vya Mei mwaka huu, Tanzania ambayo timu yake ya Taifa (Taifa Stars) inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilikuwa namba 145 hivi sasa imefika nafasi ya 139 ikiwa na pointi 214.
Mei 26 mwaka huu Taifa Stars ilicheza mechi ya kirafiki na Malawi na kutoka suluhu. Malawi yenye pointi 324 imeporomoka kwa nafasi tano kutoka ya 102 hadi 107.
Ivory Coast ambayo katika mechi yake ya mwisho Juni 2 mwaka huu iliifunga Taifa Stars mabao 2-0 imeporomoka kwa nafasi moja kutoka ya 15 hadi 16 ikiwa na pointi 943. Hata hivyo ndiyo inayoongoza kwa upande wan chi za Afrika katika viwango hivyo.
PROGRAMU YA TAIFA STARS KWA MECHI YA GAMBIA
JUMATANO JUNI 6
01.00 asubuhi  Mazoezi- Uwanja wa Karume
10.00 jioni       Mazoezi- Uwanja wa Taifa
ALHAMISI JUNI 7
10.00 jioni   Mazoezi- Uwanja wa Taifa
IJUMAA JUNI 8
10.00 jioni   Mazoezi- Uwanja wa Taifa
JUMAMOSI JUNI 9
04.00 asubuhi  Mkutano na Waandishi wa Habari- Ukumbi wa TFF
11.00 jioni  Mazoezi- Uwanja wa Taifa
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

EXCLUSIVE: ALLY MAYAY ABADILI MAWAZO -ACHUKUA FOMU YA UMAKAMU WA MWENYEKITI

Mchezaji wa zamani na mmoja ya wajumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga ya uongozi uliopita, Ally Mayay amebadili juu ya kutaka kugombea tena ujumbe wa kamati ya utendaji.

Kwaa taarifa nilizonazo kutoka kwake ni kwamba Ally Mayay sasa ameamua kwenda kuchukua fomu za kugombea umakamu uenyekiti wa klabu hiyo aliyoichezea kwa mafanikio miaka kadhaa iliyopita.

Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’- EPISODE 5

*Atua mahakamani, Yanga wamuokoa asipande karandinga
*Akubali kusaini Jangwani bila kuuliza hata mshahara wake

Na Saleh Ally
WIKI ILIYOPITA, Malima alikuwa anawasili katika mahakama ya Kisutu akiwa mshitakiwa wa madawa ya kulevya. Kwa kuwa taarifa kuhusiana na suala hilo zilikuwa zimeripotiwa kwenye vyombo vya habari, watu walikuwa wengi sana, hali iliyomfanya awe mwoga. Nini kitafuatia? Endelea.

TULITEREMKA pale mahakamani huku idadi kubwa ya watu ikiwa inatusubiri, niliwaona baadhi ya watu niliokuwa nawajua wakiwemo mashabiki wa Yanga. Wengi waliniangalia kwa jicho la huruma.
Suala hilo kwa kiasi kikubwa lilinichanganya sana, niliona kama ni mtu ninayeonewa lakini ilikuwa vigumu kuwaeleza watu kilichokuwa kinaendelea ili wanielewe.
Ukichana na hivyo, nisingeweza kupata nafasi ya kuwaeleza namna mambo yangu yalivyokwenda vibaya. Nilichofanya ni kuangalia chini ili kupunguza uchungu kwa kuwa nilihisi huenda ningemwaga machozi.
Baadhi ya watu wa Yanga walikuwa pale wakipiga kelele kunipa moyo kuwa nisijali kwani kila kitu kitaisha. Walinipa moyo kiasi cha kunifanya niamini kweli Yanga ni nyumbani kwangu, hilo ninaliamini hadi leo.
Tuliingia mahakamani na tukaanza kusomewa mashitaka, hatukutakiwa kuzungumza lolote na baada ya hapo tukaombewa dhamana. Lakini tukaelezwa tusingeruhusiwa kupewa dhamana kutokana na uzito wa jambo lenyewe.
Hali hiyo ilinichanganya zaidi, niliona mambo yanazidi kuwa mabaya. Nilikanganyikiwa hasa baada ya kukosa hata nafasi ya kuwaona ndugu zangu. Nikajua ndiyo mwisho wangu.
Yule dada aliendelea kulia, hali hiyo ilinitia huruma sana kwa kuwa niliona kama mimi ndiyo chanzo cha tatizo. Lakini sikuwa na sababu ya kujilaumu maana sikujua lolote kuhusiana na litakalofuatia na wala sikuwa na nia mbaya kwake.
Wakati tukiwa tunajiandaa kupanda karandinga kwenda Segerea, tuliijiwa na kuambiwa dhamana ilikuwa imepatikana. Sikuamini, pia sikujua nani aliyetusaidia kiasi hicho.
Baada ya kutoka, nikagundua walioniwekea dhamana mimi na yule dada ni viongozi wa Yanga ambao tayari walishaanza kushughulikia suala la wanasheria kwa ajili ya kutusaidia kuendesha kesi yetu kitaalam zaidi.
Nilifanikiwa kutoka, ingawa kwa dhamana angalau niliona kama nilikuwa huru kwa kiasi fulani maana siku hiyo ningelala nyumbani. Kikubwa nilitakiwa kukutana na viongozi wa Yanga kujadili kuhusiana na suala hilo.
Hakika sikuwa na ubishi kwa sababu ya mambo mawili makubwa, moja Yanga ipo kwenye damu yangu na hupaswi kuuliza hata chembe. Pili, nilikuwa kwenye matatizo ambayo yananifanya niwe msikivu kupindukia.
Nilipokutana na viongozi wa Yanga, walinieleza namna ninavyoweza kusalimika, kwamba ni kuacha sheria ifuate mkondo wake. Lakini niwe mkweli kwa wanasheria watakaoniwekea.
Wakanipa sharti moja kuwa wao watanipigania hadi mwisho lakini nilitakiwa kufanya kitu kimoja, kuachana kabisa na mambo ya Afrika Kusini, niisahau timu yangu ya Vaal na kusaini Jangwani.
Wakati huo Yanga ilikuwa imefanikiwa kuvuka na kuingia kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo ilihitaji mtu ambaye ni imara kwa ajili ya sehemu ya ulinzi wa kati. Jembe Ulaya likawa chaguo lao.
Sikuwa na sababu ya kubisha, nilikubali haraka sana na nikawaahidi nitafanya mawasiliano na Afrika Kusini na kuwaeleza hali halisi ilivyo ili wasinione ni mbabaishaji.
Unajua wakati ule tumekwenda na Nonda, yeye akasajiliwa na mimi nikakosa kibali, nilikuwa ninawasiliana na mmiliki wa timu hivyo sikupenda kumuangusha maana alifanya juhudi na kunisajili.
Nikakubali kusaini Yanga kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa, kutokana na namna mambo yangu yalivyokuwa mabaya, sikuthubutu kuomba hata senti moja wala kuulizia mshahara wangu utakuwa ni kiasi gani.
Siku ya kusaini, nilizirukia karatasi fasta, nikasaini kwa ajili ya kuichezea Yanga katika michuano hiyo mikubwa huku nikiendelea kupambana na sakata langu ambalo liliendelea kusikika kila sehemu.
Wakati nilipoanza mazoezi Yanga, kila mmoja alitaka kuniona. Mashabiki walijitokeza kwa wingi kutaka kuniona na walikuwa wakinishangaa sana, lakini nilijikausha na kuendelea na shughuli zangu. Nilifanya mazoezi kwa nguvu sana.
Wakati yote yanaendelea, nilijiuliza mara kadhaa ninavyoweza kuzungumza na Wasauz na kuwaeleza kuwa sitarudi kwa kuwa nilishikwa na madawa ya kulevya. Ilinichanganya sana lakini nikaamua kupiga na kuzungumza nao.
MALIMA ameamua kuzungumza na timu yake kuhusiana na kilichomtokea. Je, viongozi wa timu hiyo watamuelewa? Watachukua uamuzi gani wakati yeye tayari ameshasaini kuichezea Yanga huku akiwa na mkataba nao? ITAENDELEA.....

MARADONA; MIMI NI MTU NILIYEKUFA KWA DAKIKA NNE,SASA NAJUA

MAISHA  NI NINI
Umaarufu wake katika soka ulianzia katika timu ya Argentina Juniors  na taratibu baada ya hapo alizichezea timu za Boca Junior,FC BarcelonaNapoli,Sevilla na Newll's Boys .Amewahi kutwaa tuzo mbalimbali katika maisha yake ya soka na mwaka 2000 alipewa tuzo ya mwanasoka bora wa Karne sambamba na Pele wa Brazili heshima waliyopewa na Fifa.Msomaji wa number10 unajua namna Diego Maradona alivyoishi maisha yakr ya utotoni? Vipi kuhusu uwezo wa familia yake? msikilize Diego mwenyewe katika maala hii ya maswali na majibu.
Swali: Ilikuwaje wakati unajifunza soka?
Maradona; Unajua nilijifunza soka nyuma ya nyumba yetu,kuikuwa na uwanja naotumiwa na timu moja ya daraja la nne,niicheza pale kila siku wakati watoto wengine walipokwenda makwao mimi niliendelea kucheza kwa saa mbili zaid giza likiwa tayari limeshaingia.Nilikuwa sioni kitu gizani ,nilikuwa napiga tu mpira nilichokuwa nazingatia ni miti miwili (magoli).Miaka 10 baadae niliposaini mkataba wangu wa kwanza na Argentina Juniors ndipo nilipobaini uamuzi ule wa kucheza gizani ulikuwa sahihi.
Swali: Wewe ulizaliwa Favel Fiorito,eneo linalosifika kwa umasikini katika jiji la Buenos Aires nini hasa ulichokuwa ukifikiria wakati huo,kwa sababu hujasahau watu wa kule na bado unaendelea kuwa nao karibu?
Maradona; Watu masikini hawawezi kamwe kukuahau au kukulaghai,wengi wao ni marafiki zangu na mmoja wao ni kocha wangu,Coppola,huyu alikuwa akiniibia fedha zangu,watu wa Fiorito wapo katika hali ya umasikini.Leo hii kunaweza kuwa na mambo yanayotoa picha ya maendeleo lakini umasikini bado ni ule ule tangu wakati nikiishi pale,lakini wanasiasa na watu walio karibu na serikali wameendelea kuwa matajiri zaidi na zaidi.Niliwahi kuwa na nafasi ya kuwa kama wao lakini nilikataa kwa sababu ningewaibia masikini,kuna wakati nilizungumza na watu wa Argentina waliojiingiza katika maisha ya sisa na niliwaambia kila kitu ambacho hawakutaka kukisikia.
Swali: Katika maisha hayo ya umasikini,unazungumziaje namna baba yako alivyokuwa akiangaikia familia?
Maradona;Nakumbuka hali ilivyokuwa mara ya baba kurudi kutoka kazini,hakuweza kuwa na chakula cha kutulisha watoto wote sisi nane.Watu walioshiba hawawezi kulijua hilo kamwe,hususani wale ambao hawakuwahi kuwa na njaa,dada yangu alilazimika kula chakula pungufu ili tu chakula kibaki kwa ajili yangu wakati wa jioni kwa mazingira kama hayo unalazimika kuwa na huruma na mwenye kujali wasio na chakula.Historia yangu ya utotoni kamwe siwezi kuisahau hivi hivi,Mama yangu alilazimika kudanganya anaumwa tumbo ili tu aweze kupata chakula kwa ajili ya watoto wake na wakati wote alikuwa akiangalia kwenye mabakuli kuhakikisha kama kuna chakula kwa watu wote.Huo ndiyo umasikini,mama yako analazimika kudanganya,mtu unaweza kuuita uongo wa kisayansi,lakini hiyo ndiyo hali halisi ya maisha ilivyokuwa,nakwambia ukweli.
Swali: Huo ni umasikini kama unavyosema lakini kuna watu wanasahau mapema hali hiyo,wewe vipi unaendelea kuwa na fikra za maisha ya utotoni?
Maradona; Nisingeweza kusahau,sisahau umasikini ni wazamani kuliko utajiri,baba yangu alikuwa akifanya kazi Kvantaca ( eneo la sokoni) na wakati wote alikuwa akibeba mifuko mizito hata wakati ambao umri wake ulikuwa mkubwa.Baada ya kurudi nyumbani Mama alikuwa akimuwekea bonge la barafu shingoni ili kupunguza maumivu na sisi watoto wake wakati huo tulikuwa pembeni,huo ulikuwa kama utamaduni ambao hauwezi kuondoka katika fikra zangu
Swali: Tuzungumzie mambo yaliyozoeleka kwa watu masikini nini hasa unachokumbuka zaidi ukiwa mtoto?
Maradona; Heshima,lakini pia hatukuwa na vitu kama sherehe za kuzaliwa,hatukuwa na fedha kwa mambo hayo,marafiki familia na binamu walikuwa wakikubusu na hiyo ilikuwa zawadi kubwa tu.Hali ni tofauti kwa wale ambao ni matajiri,sina shaka kwamba kuna watu wanaofanya makubaliano na wanasiasa na wanasiasa wanatumia pale wanapohitaji kufanya mambo hayo.Kama wewe hukubali katika utaratibu huo unaonekana kichaa,ndiyo mimi kichaa ni bora niwe kichaa kuliko kukubali nitoe kitu ambacho walitakiwa kunihudumia mimi.Unajua mimi ni kama mtu aliyekufa kwa dakika nne na sasa najua maisha ni nini.
Swali: Kuna walijituma kupunguza umasikini mfano ni mwanamuziki,Bono amezunguka dunia nzima kuwashawishi marais wa nchi tajiri kupunguza madeni kwa nchi masikini na ameweza hata kula chakula cha mchana na aliyekuwa Rais wa Marekani,George W Bush
Maradona; Najua jambo moja ambalo sitoweza kulifanya kamwe ni kupata ujasiri wa kula chakula na Bush,sitaona nimefanya jambo jema kwa kula chakula na muuaji wa halaiki.
Swali: Nini hasa unadhani kifanyike kuleta mabadiliko?
Maradona; Nini cha kufanya?Ni vigumu kubadili mambo,lakini muhimu tuyazungumze matatizo kwanza,bahati mbaya Papa (baba mtakatifu) hataki kuzungumzia matatizo na hata anapofanya hivyo anachofikiria ni kitu kimoja,namna ya kuitunza Vatican kama ilivyo kwa Wamarekani.Vatican ni tajiri sana,dola yao ina ngvu.Papa John Paul II hakuwahi kulifahamu kwa undani kuhusu Afrka,hakwenda pale kubusu ardhi na kuwapa chakula watoto masikini na pia hakuwahi kuijua Argentina.Lakin i ni yeye anayechukua dola million 150 inayotokana na matangazo ya kondomu,asasi inatoa fedha hizo kwa ajili ya kampeni ya matangazo ya biahara,lakini yeye Papa hakuwahi kujua lolote kuhusu kondomu,alikuwa anachukua tu fedha.Leo hii hakuna anayezungumza namna Papa alivyoitupa Afrika na watu masikini wameongezeka tangu kuangushwa kwa ukuta wa Berlin.
Swali: Wewe ni rafiki mkubwa wa rais wab Cuba Fidel Castro,mmekutana vipi na mtu huyu?
Maradona; Mwaka 1987 nilipewa tuzo mbili moja na Cuba nyingine na Marekani,niliwaambia Wamarekani wakae na tuzo yao na moja kwa moja nikaenda Cuba.Nilikutana na Fidel na tukazungumza kwa saa tano kuhusu Che Guevara (mwanamapinduzi wa zamani wa Argentina) .Nikweli nilisoma siku nyingi habar za mapinduzi,busara za Che na Fidel na nikajikuta navutiwa na Fidel na kwa mtazamo wangu yeye ni sawa na Simba anayepigania eneo lake,ni mwanasiasa pekee ambaye hana mtazamo wa kuwaibia masikini.
Swali: Umewaji kusema vita kubwa uliyowahi kupamana nayo ni kuachana na matumizi ya madawa?
Maradona; Ndiyo,ni vita kubwa,lakini ilibidi nipambane nayo kwa bidii na niliamini kuwa ilikuwa vita ngumu,ni kama uko katika mechi ambayo umeshindwa na unataka kushinda kwa namna yoyote ile lakini hakuna msaada wa kupata ushindi nje ya kutimiza majukumu yako.
Swali: Wakati ukichezea Napoli mwaka 1991 ulifungiwa kwa kosa la kutumia dawa za kuongeza nguvu,lakini baadaye ulisema kwamba kufungiwa kwako ni kulipiza kisasi baada ya Argentina kuitoa Italia katika kombe la Dunia mwaka 1990.
Maradona; Naamini hivyo,naamini wale Mafia walikuwa na fedha nyingi sana na walikuwa na hasira na mimi.
Swali: Ilikuwaje hadi ukafungiwa kucheza soka?
Maradona; Walikuta Cocaine kidogo na kunifungia kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja kucheza soka.Hiyo yote naamini ilikuwa sababu ya kunitoa nje ya soka kwa maisha yangu ya soka,walidhani wagenimaliza na kuniacha nimekufa mtaani.
Swali: Uliwaambia nini wachezaji wenzako kabla ya mechi yako ya mwisho ukiwa kama mchezaji mwaka 1997,nasikia wengi walilia!!
Maradona; Ndiyo,wote tulilia nilizungumza na mchezaji mmoja mmoja niliwaaga katika soka na nilifahamu kwamba sitovaa tena jezi nikiwa mchezaji.

ALIYENACHO ANAONGEZEWA: MANCHESTER UNITED WASAINI MKATABA MAMILIONI YA PAUNDI WA MIAKA 5 NA KAMPUNI YA GENERAL MOTORS

Manchester United na kampuni ya kutengeneza magari ya kimarekani General Motors(GM) wametangaza wanafunga ndoa ya kibiashara, na engagement party ni leo Alhamisi, May 31, 2012. Kampuni ya GM na Manchester United wametangaza kwamba magari aina ya Chevrolet yatakuwa yakitangazwa kibiashara na dunia nizma na Manchester United, ambayo ina mashabiki wanaokadiriwa kufikia million 659 - jambo litaiongezea na kuifungulia njia brand hiyo sehemu mbalimbali hasa Asia huku Manchester United wakizidi kutunisha akaunti yao ambayo ndio tajiri kuliko vilabu vyote duniani.

GM wataitumia Manchester United.
Kila mtu anajua nia ya General Motors kwenye ubia huu na Manchester United. GM wataitumia Manchester United kufika Asia. Manchester United wanategemea kucheza mechi nyingi nchini China  mwaka huu, na wapo njiani kabisa kumsajili mjapan Shinji Kagawa ambaye anaweza kuja kuwa Icon kwa United na nchi yake. Huoni kama kuna endorsement ya GM kwa Kagawa ikiwa tasajiliwa Manchester United ili kuitangaza brand hiyo nchini Japan na Asia kwa ujumla?

Manchester United watapata fedha nyingi kutoka GM
Naturally, kwenye ndoa hii mahari italipwa kwa Manchester United kutoka kwa GM tena ikiwa ni fedha nyingi sana - mamilioni ya paundi. GM na United wamesaini mkataba wa miaka 5 - jambo litaendelea kutunisha akaunti ya Manchester United na kuzidi kuwapa nguvu ya kung'ang'ania taji la timu tajiri zaidi duniani. Kabla ya udhamini huu wa Chevrolet United walikuwa na mkataba na kampuni ya Ujerumani Audi.
Kwenye dili sasa wachezaji wote wa United na maofisa wa juuwa United watafaidika kwa kupata magari ya kifahari zaidi ya Chevrolet badala ya Audi


JOSE MOURINHO NA GUARDIOLA WAPEWA OFA YA MAMILIONI KUCHAMBUA SOKA LA EURO



Kituo cha Televison cha Televisa wamejaribu kuwaleta pamoja kocha Real Madrid Jose Mourinho na Pep Guardiola.

El Mundo Deportivo limesema Televisa wametoa ofa kwa Mourinho na kocha wa zamani a Barcelona Guardiola ya kiasi cha €1.5 million kwa kila mmoja ili kuweza kushea meza na kufanya uchambuzi wa soka kwenye michuano ya Euro 2012.

Ingawa, Mourinho bado hajatoa majibu kama amekubali au hapana, Guardiola yeye amekataa kabisa, akisistiza anataka kupumzika kabisa kutoka kwenye soka baada ya kuondoka Barca wiki hii.
                       
Wakati wote wakiwa Barcelona Mourinho kama kocha na Guardiola kama mchezaji.
Watu maarufu maarufu ambao wameshawahi kufanya kazi na Televisa ni Luis Figo, Zinedine Zidane na Fernando Morientes.

MANCHESTER CITY, CHELSEA NA VILABU VINGINE EPL HATARINI KUKUMBWA NA ADHABU KALI KWA MATUMIZI MAKUBWA YA FEDHA

Vilabu vya English Premier League vimeonywa kushusha matumizi yao ya pesa, baada ya kutoka kwa ripoti ya matumizi ya fedha ya mwaka kuonyesha kwamba mishahara ya wachezaji ilikuwa imefikia level ya juu sana mpaka kuzidi ukuaji wa mapato ya vilabu hivyo.

Mishahara kwa ujumla imepanda kwa kiasi cha £201 kwenye msimu wa 2010-11, ikipanda kwa asilimia 14 mpaka kufikia takribani £1.6 billion - huku mapato yote ya vilabu yakipanda kwa asilimia 12 mpaka £2.27 billion - kutokana na taarifa za Deloitte.

Huku vilabu 20 vya juu vikitoa mishahara ili kuweza kuwavutia wachezaji wazuri katika harakati za kupata mafanikio, sasa hivi mishahara ya wachezaji inatumia asilimia 70 ya mapato yote yanayopatikana katika vilabu hivyo vya premier league.

Alan Switzer, mkurugenzi wa biashara ya michezo wa Deloitte, amewaonya wamiliki wa vilabu vinavyotumia fedha nyingi kwamba kutumia fedha vizuri kwenye mishahara ni muhimu, tena sasa ikizingatiwa sheria ya matumizi ya fedha ya UEFA ikiwa inakaribia kuanza.

"Ikiwa uwiano wa mishahara na mapato ni asilimia 70 au zaidi, ni vigumu sana kuweza kufanya biashara ya faida," alisema.
"Kwa mtazamo wetu uwiano huo ni wa juu sana huku vilabu na league zikatakiwa kurudi kwenye asilimia 60 kwa mujibu wa sheria ya UEFA."

Upandaji wa mishahara kwenye baadhi ya vilabu vya ligi kumechangiwa na upandaji wa mapato ya kibiashara, klabu hizo zikiwemo Manchester United, Liverpool na Manchester City.

Figures hizi ni  za msimu wa 2010-11 na utakuwa wa mwisho kabla ya sheria ya UEFA haijaanza rasmi kutumika na kutoa adhabu za kulipa faini au kufungiwa kushiriki kwenye mashindano ya shirikisho hilo kwa kosa la kutumia zaidi ya kile klabu inachotengeneza katika kutafuta mafanikio.

Switzer alisema mabingwa Manchester City na mabingwa wa ulaya Chelsea, zinazomilikiwa na Sheikh Mansour na Mrusi Roman Abramovich ndio wanakabiliwa na changamoto kubwa dhidi ya sheria ya FFP (Financia Fair Play).

"Chelsea na Manchester City ndio klabu ambazo zimeweka rekodi ya kupata hasara kubwa zaidi hivyo ndio zinazoweza kuwa kwenye hatari zaidi ya kukumbwa na adhabu kali za FFP," aliongeza.

 

No comments:

Post a Comment