SHILOLE ANUSURIKA KUKAMATWA NA POLISI BAADA YA KUHISIWA KUWA ANA MISOKOTO YA BANGI
MSANII wa anayefanya vizuri kwenye muziki na filamu Shilole, amenusurika kumakatwa na polisi baada ya kuhisiwa kuwa na misokoto ya bangi ndani ya gari lake na kusababisha kuhojiwa kwa dakika kadhaa maeneo ya Kinondoni.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana ambapo msanii huyo inadaiwa alikuwa akitokea kwenye ishu zake ndipo maafande hao waliokuwa wakitokea kwenye malindo yao walipomdaka na kumpeleka pembeni kwa lengo la kufanya upekuzi kwenye gari yake.
Inadaiwa kuwa polisi hao hawakukuta kitu chochote zaidi ya sigara za mpenzi wake, ambaye walikuwa wote usiku huo na hata hivyo hawakuwa na dalili zozote za kuwa wamelewa.
Shilole alipozungumza na mwandishi wetu alidai kuwa tukio hilo lilimshangaza sana kwani hakuwa na bangi ndani ya gari lake na hajawahi kutumia kitu hiyo lakini polisi hao walimuhoji kana kwamba anatumia bangi.
Alidai kuwa kuna baadhi ya watu walitaka kumfanyia mchezo mchafu lakini walishindwa kwani alikuwa makini katika kila jambo ambalo alikuwa akilifanya usiku huo, na alipoulizwa kuwa usiku huo alikuwa anatoka wapi alidai kuwa katika harakati zake za hapa na pale.
Mwanamke anayetuhumiwa kumtesa kumlisha kinyesi na kumchoma moto mtoto wa kaka yake kumfungia ndani, amepandishwa kizimbani kwa mara ya pili katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya kujibu shtaka linalomkabili.
Mtuhumiwa Wilvina Mkandala (24)
Hataki kabisa kuonyesha sura yake
Aneth akiwa na wazazi wake mahakamani jana
Akirudishwa tena rumande mpaka tena tarehe 27/11
Baadhi ya akina mama wakiwa nje ya mahamaka wakisubiria kumwona mama huyo mwenye roho mbaya
Akina mama hao wakiwa na hasira kali walisikika wakisema tuachieni kidogo tumfunze adabu