Monday, December 31, 2012

YAKIWA YAMEBAKI MASAA MACHACHE KUZIMWA KWA MITAMBO YA ANALOJIA HIVI NDIVYO HALI ILIVYO MIDA HII KWENYE OFISI ZA STAR TIMES MWENGE


Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar wakiwa wanasubiria Kuingia ndani ya ofisi ya Star Times Mwenge kutokana na wateja kujaa ndani ya ofisi hiyo kwaajili ya kununua ving'amuzi na kupelekea wateja hao kuingia kwa kusubiriana. Ikumbukwe kuwa  mnamo tarehe 23 februari 2012  Wizara ya Sayansi na Teknolojia kupitia Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA ilitangaza kusitisha urushaji wa matangazo ya televisheni kwa kutumia teknolojia ya analojia kwenda katika mfumo mpya wa digitali kufikia tarehe 31 Disemba 2012 saa sita na dakika moja usiku
Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar wakiwa wamekaa nje ya ofisi ya Star Time Mwenge wakisubiria wateja wengine waliopo ndani wapungue ili na wao waweze kuingia na kununua ving'amuzi vya kampuni hiyo.
 Kijana akitoka kununua king'amuzi cha Kampuni ya Star Times tayari kwa kupokea matangazo ya televisheni kwa njia ya digitali
Mkazi wa Jiji la Dar  akiwa tayari kashajinunulia king'amuzi cha Kampuni ya Star Time tayari kwa kupokea matangazo kwa njia ya digitali ambapo Tanzania inaingia kwenye mfumo mpya wa urushaji wa matangazo ya televisheni kupitia mfumo wa digitali. Kufikia saa sita na dakika moja usiku wa leo Serikali imeagiza wamiliki wote wa vituo vya televisheni kuzima mitambo yao inayotumia teknolojia ya analojia na kuwasha mitambo mipya inayotumia teknolojia ya Digitali.

No comments:

Post a Comment