Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiendesha Kikao cha Muungano, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli
ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar leo, Januari 14, 2013. Wa pili
(kushoto) ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (wa pili (kulia) Ni Makamu wa
pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kushoto) ni Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samiah Suluhu na (kulia) ni
Waziri wa nchi Ofsi ya Makamu wa pili wa Rais zanzibar, Mohamed Aboud.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiteta jambo na Makamu wa pili wa Rais, Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd,
wakati Makamu alipokuwa akiendesha Kikao cha Muungano kilichofanyika
katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar leo.
Katibu
Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula (kulia) Naibu Katibu Mkuu
Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Ngosi Mwihava (katikati) na Mkurugenzi wa
Muungano, Rajab Baraka (kushoto) wakifuatilia vifungu katika machapisho
ya kujadili masuala ya Muungano, wakati wa kikao cha Muungano,
kilichoendeshwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal (hayupo pichani), kilichofanyika leo Januari
14, 2013, katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini
Zanzibar.
Baadhi
ya Mawaziri wakiwa ukumbini humo wakati wakifuatilia kikao hicho cha
Muumgano kilichoendeshwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (hayupo pichani), leo katika
Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar.
Baadhi
ya Mawaziri wakiwa ukumbini humo wakati wakifuatilia kikao hicho cha
Muumgano kilichoendeshwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (hayupo pichani), leo katika
Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Makamu wa pili wa Rais wa
Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais, Samiah Suluhu, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Muungano,
kilichofanyika leo Januari 14, 2013 katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar
Beach Resort, mjini Zanzibar.
WANAFUNZI IFM WAVAMIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI NI BAADA YA KUKOSA ULINZI KWENYE HOSTELI, BAADA YA WENZAO WAKIUME WAWILI KUBAKWA NA MAJAMBAZI NA KULAZWA HOSPITALI. SAKATA LINAENDELEA KIGAMBONI MIDA HII CHINI YA USIMAMIZI WA KAMANDA KOVA
Wanafunzi wa
Chuop Cha Uongozi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) wakiwa mbele
ya geti la Wizara ya Mambo ya ndani walipovamia leo majira ya saa nne na
nusu asubuhi wakiwa na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la polisi
kwenye makazi yao ya Hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa na
majambazi mara kwa mara. Wanafunzi hao walidai siku ya Ijumaa walifanya
kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu siku
waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndio siku waliovamiwa wenzao wawili
wakiume na kubakwa hali iliyosababishwa wanafunzi hao kubakwa.
Majambazi hao wamekua wakidai kupewa Laptop simu na fedha kama
mwanafunzi akikataa humfanyia vitendo vya kulawiti.
|
Ulinzi uliimarishwa nje ya jengo la Wizara ya Mambo ya ndani kufuatia kadhia hiyo ya wanafunzi.
|
Kamanda wa
Polisi wa Kanda maalum ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman
Kova akimsikiliza Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha IFM mara
baada ya kuwasili eneo la ofisi za Wizara ya Mambo ya ndani ambapo
aliwaamuru wanafunzi hao wafuatane waende hadi Kigamboni kwenye Kituo
walichoripoti taarifa zao pamoja na kwenda kwenye Hosteli zao. Kova
aliahidi kushughulikia jambo hilo kwa haraka bila kusita.
|
"Wanafunzi wenzetu wa kiume
wamelawitiwa nyinyi tumewapa taarifa siku ya ijumaa kuwa hatunaulinzi
tunaibiwa hovyo vitu vyetu halafu siku hiyo hiyo unafanyika ubakaji huo"
|
Baadhi ya
wanafunzi wakiwa kwenye mitaa ya Posta jijini humo wakielekea kwenye
kivuko cha Kigamboni ili kwenda kumuonyesha Kamanda wa Polisi wa Kanda
Maalum ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova.
|
Wakianza maandamano kuelekea Feli kwaajili ya kuvuka kwenda Kigamboni.
|
Kova akitoa maelezo kwa waandishi
wa habari juu ya hatua zitakazochukuuliwa baada ya kupata taarifa hizo
ambapo aliwaamuru wanafunzi hao wote kwapamoja kwenda Kigamboni
kufuatilia tukio hilo kwa pamoja.
|
Mitaani Posta.
|
Hadi kieleweke!
|
Tunaimba! Tunavuka bure Tunavuka bure kwenye Pantoni.
|
Kova akishangiliwa wakati wa safari kuelekea Feli.
|
Kwenye Kona ya feli kuwania geti ili waingie bure!
|
Wakajazana kupita kiasdi Kova akazuia kivuko kisiondoke hadi wapungue!
|
Hapa wakigoma kupungua kazi iliyochukua zaidi ya Saa moja hadi kivuko kuendelea na kazi ya kuvusha abiria
|
Pamoja na kutakiwa kupungua hapa
wengine walizidi kuendelea kuingia na kukijaza kivuko hicho. Picha zote
na Raha za Pwani, hii ni sehemu ya kwanza tutawaletea sehemu ya pili ya
tukio hili ambalo hadi hivi sasa filamu inaendelea hapa feli na
ikielekea Kigamboni.Picha Kwa Hisani Ya Mtaa Kwa Mtaa Blog
|
mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya bia ya serengeti steve gannon atembelea mjengoni clouds media group.
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds
Media Group,Joseph Kusaga 'Joe' pichani kushoto akichanganua jambo kwa
Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon mara
baada ya kutembezwa studio mpya na ya kisasa kabisa,iliyofungwa mjengoni
humo,ambayo inatarajia kuanza kutumika hivi karibuni,Steve Gannon
amefanya ziara fupi mwishoni mwa wiki na kutembelea vitengo vyote
kampuni hiyo huku akijionea namna shughuli mbalimbali zinavyofanyika
mjengoni humo.
Steve Gannon akitazama picha za
wasanii mbalimbali wa nje waliowahi kufika nchini Tanzania na kufanya
maonesho yao kadhaa ndani ya ofisi za Prime Time Promotions Ltd.
Mkurugenzi wa mambo ya utafiti na
vipindi vya Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akifafanua jambo
kwa Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon
ambaye nae alikuwa akimsikiliza kwa makini.
Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya
bia ya Serengeti,Steve Gannon akimuuliza jambo mtangazaji wa kipindi cha
Power Breakfast,Gerald Hando kuhusiana na mambo mbalimbali ya
kikazi,alipotembezwa kwenye studio ya ziada.
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds
Media Group,Joseph Kusaga 'Joe' pichani kushoto akifafanua jambo kwa
Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon mara
baada ya kufanya ziara fupi mwishoni mwa wiki na kutembelea vitengo
vyote kampuni hiyo huku akijionea namna shughuli mbalimbali zikifanya
mjengoni humo.
Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon akizungumza jambo na baadhi ya wafanyakazi wa kitengo muhimu cha kampuni hiyo cha Masoko.
Steve Gannon akisalimiana na
Oparesheni Meneja wa Prime Time Promotions Ltd.Balozi Kindamba,mara
alipotembelea ndani ya kampuni hiyo ambayo imekuwa ikijihusisha na
matamasha mbalimbali likiwemo tamasha kubwa la Fiesta ambalo hufanyika
kila mwaka.
Steve Gannon akisalimiana na Gerald Hando
Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya
bia ya Serengeti,Steve Gannon akioneshwa matoleo mbalimbali ya jariba la
burudani la KITANGOMA linachapishwa na kampuni ya Prime Time
Promotions.
Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya
bia ya Serengeti,Steve Gannon akipeana mkono na Mmoja wa wafanyakazi wa
Prime Time Promotions,Godliva Nicholaus mara alipowasili ndani ya ofisi
za kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa mambo ya Masoko na
Mauzo,Shebba Kusaga akifafanua jambo kwa Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni
ya bia ya Serengeti,Steve Gannon.
Chief Editor wa Clouds
TV,Bwa.Kanyopa akitoa maelezo mafupi kuhusiana na ufanyaji wao kazi
ikiwemo na urushaji wa vipi kupitia Tv yao,Pichani kushoto ni Boss Joe
akisikiliza kwa makini.
Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya
bia ya Serengeti,Steve Gannon alitembezwa pia ndani ya chumba maalum cha
kuandalia habari,hapa Mtangazaji wa kipindi cha Michezo Shaffih Dauda
akifafanua jambo kwa Steve Gannon.
Baada ya ziara kutembelea vitengo
mbalimbali vya kampuni hiyo,pia Steve Gannon alipata wasaa wa kukaa meza
moja na uongozi wa juu wa kampuni hiyo na kuzungumza machache,ikiwa ni
sehemu ya mchakato wa ufanisi wa kikazi kwa mwaka mpya wa 2013.
ALAMA YA BARABARANI HAIELEWEKI AU NDIO MAKUSUDI
Malori
yakiwa yameegeshwa ndani ya hifadhi ya barabara ya mandela karibu na
kituo Cha Gereji Huku kibao Cha Alama za Barabarani ambcho kinaonyesha
alama ya kutokurusu Kuegesha Kikiwa Pembeni ya malori hayo. Je hii ni
dharau au mwenye malori hayo yupo Juu ya Sheria au yupo sahihi kwa
kuegesha magari yake hapo?
BALOZI WA NIGERIA NCHINI MAREKANI AMFANYIA DINNER YA KUMUAGA BALOZI WETU MH. MWANAID MAAJAR
Balozi wa Tanzania nchini Marekani
na Mexico Mhe. Mwanaidi Maajar (wapili toka kulia)akiingia nyumbani kwa
Balozi wa Nigeria (hayupo pichani) Potomac, Maryland, huku wakipokelewa
na afisa ubalozi wa Nigeria (wa kwanza kulia) anayesalimia ni mama Lily
Munanka ambaye ni mkuu wa utawala na fedha Ubalozi wa Tanzania nchini
Marekani akifuatiwa na mume wa Balozi, Bwn. Shariff Maajar siku ya
Jumapili January 6, 2013 siku Balozi wa Nigeria alipomfanyia chakula cha
jioni maalum kwa ajili ya kumuaga Balozi wetu ambaye anamaliza muda
wake.
Mhe. Mwanaidi Maajar akilakiwa na
Balozi wa Nigeria nchini Marekani, Mhe.Adebowale Ibidpo Adefuye siku ya
Jumapili January 6, 2013 alipomkaribisha chakula cha jioni maalum kwa
ajili ya kumuaga Balozi wa Tanzania nchini Marekani ambaye anamaliza
muda wake.
Mke wa Balozi wa Nigeria
akisalimiana na kumkaribisha Mhe. Mwanaidi Maajar huku mumewe Bwn.
Shariff Maajar akiwa amesimama kwenye ngazi akiangalia.
Balozi na mumewe Bwn. Shariff
Maajar wakisalimiana na Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Bwn Idd
Sandaly ambaye pia aliongozana na mkewe (wakwanza kushoto) kwenye
chakula cha jioni alichoandaliwa Balozi wetu na Balozi wa Nigeria kwa
ajili ya kumuaga siku ya Jumapili January 6, 2013 nyumbani kwake
Potomac, Maryland.
Kutoka kushoo ni Rais wa Jumuiya
ya Watanzania DMV akiwa pamoja na mkewe, Balozi wa Benin nchini Marekani
Mhe.Cyrille S. Oguin katika picha ya pamoja na Balozi wa Nigeria nchini
Marekani Mhe.Adebowale Ibidpo Adefuye.
Balozi
wa Nigeria nchini Marekani Mhe.Adebowale Ibidpo Adefuye (kulia)
akisalimiana na Mume wa Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico,
Bwn. Shariff Maajar.
Balozi
wa Nigeria nchini Marekani Mhe.Adebowale Ibidpo Adefuye akisalimiana na
kumkaribisha Balozi wa Botswana nchini Marekani Mhe. Tebelelo Seretse nyumbani kwake Potomac, Maryland siku
ya Jumapili January 6, 2013 alipomualika chakula cha jioni maalum kwa
ajili ya kumuaga Balozi wetu ambaye anamaliza muda wake.
Balozi wa Botswana nchini Marekani Mhe. Tebelelo Seretse (kushoto) akiongea jambo na Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Mwanaidi Maajar.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Utawala
na Fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, mama Lily
Munanka, Mke wa Balozi wa Zimbabwe, Balozi wa Zimbabwe nchini Marekani,
Mhe. Dr. Machivenyika Mapuranga na Balozi wa Benin nchini Marekani Mhe.
Cyrille S. Oguin.
Wakati wa chakula.Picha na Vijimambo Blog
No comments:
Post a Comment