Monday, January 14, 2013

SILAA WA CCM, AWASHUKIA UVCCM, AWATAKA KUWA JICHO LA CHAMA KISIHUJUMIWE. JERRY SILAA AKIFUNGUA SEMINA YA SIKU MBILI YA VIONGOZI WA UVCCM MKOA WA MBEYA. KUSHOTO  NI AMAN KAJUNA MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA MBEYA
KATIBU WA CCM WILAYA YA MBEYA AKIMWAGA SERA ZA CHAMA CHA MAPINDUZI KWA WAKAZI WA NZOVWE MBEYA 
AMAN KAJUNA MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA MBEYA AKIMKARIBISHA JERRY SILAA AONGEE NA WANANCHI WA NZOVWE MBEYA
JERRY SILAA AKIONGEA NA WANANCHI WA NZOVWE MBEYA
VIJANA WA CCM WAKIWA MAKINI KUMSIKILIZA JERRY SILAA

DOGO AKIMSIKILIZA SILAA

MEYA wa Ilala , Jerry Slaa, amesema kuwa licha ya umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) kuonekana kuwa nguzo ndani ya chama hicho, lakini ndiyo jumuiya inayongoza kwa migawanyiko na makundi ndani ya chama hicho, inayochochewa na watu toka nje.

Slaa ambaye pia, ni mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), kutoka wilaya ya Ilala, amesema kuwa hali hiyo inakiweka rehani chama hicho, hivyo kuwataka vijana hao wabadilike na kuacha kufanya siasa za mtu, bali wafanye siasa za chama, kwani hiyo ndio suluhu itakayoiwezesha chama hicho kurudisha imani kwa jamii.

Alitoa kauli hiyo jana, Jijini hapa, wakati akifungua semina ya siku mbili ya viongozi 60 wa jumuiya hiyo, kutoka wilaya zote za mkoa wa Mbeya, iliyoandaliwa mahususi kwa ajili ya kuwajengea uwezo viongozi kwa lengo la kwenda kukijenga chama baada ya kumalizika uchaguzi wa ndani.

Alisema licha ya kwamba CCM bado inaaminiwa kwa kiasi kikubwa na jamii, lakini bado kuna mambo muhimu ambayo chama hicho na jumuiya zake, kinapaswa kuendelea kuyafanya ili kuendelea kukiimarishaya na kujenga imani zaidi ndani ya jamii.
Hata hivyo , alisema wakati vijana hao wakifurahia kupata nafasi za kushika madaraka mbalimbali, lakini pia wanapaswa kufikiria zaidi wajibu wao kuanzia katuika sehemu wanazotoka hadi kwenye nyadhifa walizoshika, ikiwemo kusimamia ipasavyo utekelezaji wa ilani ya chama hicho.

“Wewe kama kiongozi unapaswa kujiuliza ni kwa kiwango gani umetimiza wajibu wako huko uliko (sehemu wakaoishi), lakini pia ni kiwango gani umezisimamia halmashauri katika kutekeleza ilani ya chama” alisema Slaa.
Alisema kazi kubwa ya jumuiya hiyo na wana CCM kwa ujumula ni kuunganisha nguvu zao kwa pamoja ili kuendelea kukijenga chama ili kiaminiwe na wananchi na hatimaye kuendelea kupewa dhamana ya kuongoza dola.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika ufunguzi huo wa semina elekezi kwa viongozi wa jumuiya hiyo, Mwenyekitti wa jumuiya hiyo Mkoa wa Mbeya, Aman Kajuna, alisema vijana nchini wakiwemo wa CCM wanapaswa kuwa jicho la mabadiliko hapa nchini.

Aliongeza kuwa vijana nchini wanatakiwa kuacha kuendesha mambo na mipango yao kwa mazoea badala yake watekeleze hayo kulingana na mabadiliko ya ulimwengu wa sasa na mahitaji ya jamii.
Baada ya kufungua semina hiyo ya siku mbili, MNEC huyo, alifanikiwa pia kukutana na viongozi mbalimbali wa chama hicho na alitarajiwa kufanya mkutano wa hadhara katika eneo la Nzovwe Jijini hapa.

No comments:

Post a Comment