MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL APOKEA VIFAA VYA MICHEZO KWA AJILI YA VIJANA WA HARAIKI WA MBIO ZA MWENGE KUTOKA BENKI YA NMB
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea sehemu ya
vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh. Milioni 35, kwa ajili ya vijana
wa Haraiki ya Mbio za Mwenge utakaowashwa Visiwani Pemba Mei 6, mwaka
huu, kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa Benki ya NMB,
Domina Feruzi, wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika Ofisini kwa
Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, jana Mei 2, 2013. Kushoto ni Meneja
wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa benki hiyo, Elieza Msuya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wageni
wake kutoka Benki ya NMB, baada ya makabidhiano ya vifaa vya michezo
vyenye thamani ya Sh. milioni 35 kwa ajili ya vijana wa Haraiki wa mbio
za Mwenge unaotarajia kuwashwa Mei 6, mwaka huu Visiwani Pemba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya
pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa Benki ya NMB, Domina
Feruzi (wa pili kulia) Meneja wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa
benki hiyo, Elieza Msuya (kulia) Ofisa Mahusiano wa benki hiyo, Doris
Kilale (wa pili kushoto) na Huruma Mwaihomba, Ofisa Mahusiano wa benki
hiyo, baada ya makabidhiano hayo.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR
NMB YAENDELEA KUWAHUDUMIA WATEJA WAKE KWA USTADI WA HALI YA JUU.
Afisa wa Benki ya NMB tawi la
Ilala Bw Cuthbert Zimbwe akimuhudumia mmoja wa wateja wa NMB waliofika
katika tawi hilo kwaajili ya Kupata huduma za Kibenki. NMB imeendelea
kuwahudumia Wateja wake
Afisa wa Benki ya NMB tawi la
ilala Cuthbert Zimbwe akiwa na furaha ya kuwahudumia wateja Waliofika na
watakaofika tawini hapo kwaajili ya kujipatia huduma mbalimbali za
kibenki. Sasa mteja wa Benki ya NMB anaweza kupata Huduma za Kibenki
kupitia Simu yake ya Mkononi bila yeye kufika kwenye Matawi ya NMB.
JISEVIE Ni huduma ambayo mteja wa NMB anatakiwa kujiunga na Huduma ya
NMB Mobile kwaajili ya kuweza kupata huduma za kibenki kupitia Simu yake
ya mkononi.
NMB ni Benki ambayo inaongoza kuwa
na mashine zaidi ya 500 za kutolea Pesa Nchini Nzima na Ni benki
inayoongoza Kuwa na Matawi Mengi zaidi ya 150 Nchini Nzima. NMB Benki
yako, Popote ulipo tumekufikia
No comments:
Post a Comment