Alhaji Aliu Mahama, the West African country’s Vice
President from 2001 to 2009, died today November 16, at the Cardio Centre of the
Korle Bu Teaching Hospital.
Alhaji Aliu Mahama, the West African country’s Vice President from 2001 to 2009, died today November 16, at the Cardio Centre of the Korle Bu Teaching Hospital.
Hospital sources confirmed news of his death to local media at about 10: 20am.
Rumours about Mahama’s death made the rounds in local media this week only for his family and hospital officials to debunk them, insisting he was doing fine, and that plans were far advanced for him to be flown abroad for treatment.
However, it appeared he could no longer hold on, as he finally passed away on Friday morning, sending waves of sorrow across a country yet to recover from Atta Mills’ death.
Sources say Mahama was on life support for the past few days, due to heart related complications.
Mahama was born on March 3, 1946. He was a Quantity Surveyor by occupation. He became Ghana’s Vice President under the John Agyekum Kufour/NPP administration from January 7 2001 to January 7 2009.
For Source CLICK HERE
RAIS KIKWETE AFUNGA MKUTANO WA MAJAJI ARUSHA LEO
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipokea risala ya Waheshimiwa majaji toka kwa
muwakilishi wao, Jaji Dkt Fauz Twalib, wakati wa kufunga mkutano wa siku
nne wa Majaji uliofanyika katika hoteli ya Snow Crest jijini Arusha leo
Novemba 16, 2012
Rais
Jakaya Kikwete akikufunga mkutano wa siku nne wa Majaji uliofanyika
katika hoteli ya Snow Crest jijini Arusha leo Novemba 16, 2012
Rais
Jakaya Kikwete akikufunga mkutano wa siku nne wa Majaji uliofanyika
katika hoteli ya Snow Crest jijini Arusha leo Novemba 16, 2012.Wengine
kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Nhe. Magesa Mulongo Jaji Mkuu
Mhe. Mohamed Chande Othman, Waziri wa Sheria Mhe Mathias Chikawe, Jaji
Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na Jaji Kiongozi Mhe Fakih
Jundu
Waheshimiwa
majaji wakimsikilia Rais Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani) wakati
wa kufunga mkutano wa siku nne wa Majaji uliofanyika katika hoteli ya
Snow Crest jijini Arusha leo Novemba 16, 2012. PICHA NA IKULU
SERENGETI BOYS KUSHINDA NYUMBANI KWANZA
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Kusaidia timu ya Serengeti Boys ishinde Bw.
Kassim Dewji akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya JB
Belmont jana wakati akielezea mikakati ya kamati hiyo katika kuhamasisha
wadau ili waweze kujitolea na kuhakikisha timu hiyo inashinda mchezo wa
nyumbani kabla ya marudiano ili kujihakikishia kufuzu michuano ya Kombe
la Afrika kwa vijana litakalofanyika nchini Moroco Mwezi Machi mwakani,
Kulia ni mjumbe wa kamati hiyo Bw Salim na katikati ni Katibu Mkuu wa
Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania TFF Bw. Angetile Osiah Jumla ya shilingi milioni 35
zimepatikana ambapo zitasaidia mambo mbalimbali ya maandalizi ya mchezo
wa timu ya Serengeti Boys na Congo Brazaville utakaofanyika siku ya
jumapili Novemba 17.
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania TFF Bw. Angetile
Osiah akizungumza katika mkutano huo kulia ni Henry Tandau katibu mkuu
wa kamati hiyo na katikati ni Kassim Dewji makamu mwenyekiti wa kamati
Katibu Mkuu Mpya wa CCM Abdulrahman Kinana Aripoti Rasmi Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijinbi Dar es Salaam
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimia wafanyakazi wa
Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijinbi Dar es Salaam,
aliporipoti rasmi kazini kwenye ofisi hizo leo asubuhi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungumza na Katibu wa
Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, aliporipoti
leo ofisini, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini
Dar es Salaam.Picha na Bashir Nkromo-Itikadi na Uenezi,-CCM
KATIBU MKUU WA WIZARA YA HABARI AFANYA ZIARA BARAZA LA KISWAHILI LEO
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bwana Seith
Kamuhanda akikagua moja ya majengo ya Baraza la Kiswahili Tanzania
(BAKITA) alipofanya ziara ya ukaguzi wa Ofisi hizo mpya zilizopo
Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.Anaemuelekeza kushoto ni Mtendaji Mkuu
wa Bakita Dkt. Selemani Sewangi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bwana Seith
Kamuhanda akiongea na watumishi wa Baraza la Kiswahili Tanzania (hawapo
pichani) alipofanya ziara ya ukaguzi wa Ofisi hizo mpya zilizopo maeneo
ya Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa BAKITA
Dkt. Seleman Sewangi na kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni
Profesa Hermas Mwansoko.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATOA MHADHARA CHUO KIKUU CHA KILIMO SUA MJINI MOROGORO LEO
Airtel na Unesco kuzindua radio za jamii Arusha vijijini - Ololosokwani
Na Mwandishi wetu
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na shirika la umoja wa mataifa la UNESCO (kesho) jumamosi tarehe 17 Novemba watazindua rasmi radio ya jamii katika kijiji cha Ololosokwani kilichopo tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya ametaarifu kuwa sherehe ya uzinduzi wa radio hiyo ya kijamii inatarajiwa kuhudhuriwa na mgeni wa heshima Waziri wa Mawasiliano nchini Profesa Makame Mbarawa katika kijijini cha Ololosokwani Akiendelea kuelezea alisema "Airtel na Unesco wanatimiza dhamira waliojiweke ya kuwafikia na kusaidia jamii zilizopo pembezoni hasa wakina mama ambao katika jamii hizi wamekuwa wakiachwa nyuma katika mambo mengi na mwisho wake kutotambua nafasi zao"
Singano alisema "Mradi huu utasaidia kupigana na kutokomeza changamoto za mila zilizopitwa na wakati zikiwemo ukiketwaji wa wanawake, elimu duni, imani za kishirikina, umaskini ,unyanyasaji wa kijinsia, kukua kwa kasi kwa ugonjwa wa ukimwi na matatizo mengine maandalizi ya sherehe ya ufunguzi yamekamilika na kubainisha kuwa wananchi wa vijiji vyote jirani na ololosokwani takribani vijiji 14 watafaidika pia kwa kujipatia huduma bora kutoka Airtel ikiwemo ile ya
Airtel Money pesa mkononi wakati wowote kijijini hapo alimaliza kusema Bi, Singano
Akifafanua kuhusu ufungwaji wa Mitambo hiyo ya radio, Afisa mradi wa habari na mawasiliano UNESCO Yusuph Al Amin amesema "mradi wetu wa kijamii umekamilika, tunawashukuru Airtel na wananchi wote kwa ushirikiano wao wa kutuunga mkono kukamilisha lengo, mitambo hii ya mawasiliano utatoa fulsa kwa wakazi wote wa ololosokwani na vjiji jirani kujifunza mambo mapya, pia tunaanzisha multimedia center ambayo utawaweza wakazi wa kijiji hapa kutembelea tovuti mbalimbali, na kuunganishwa na mtandao wa kisasa wa intaneti ya Airtel"
Sehemu nyingine zitakazonufaika na mradi huo wa radio za kijamii ni pamoja na Sengerema Mwanza, Karagwe Kagera, Chake Chake Pemba, Makunduchi Unguja, Pangani Tanga, Kyela Mbeya and Kalama Shinyanga.
RPC KIGOMA AWAPA MAKOTI MAALUMU WAENDESHA BODABODA
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kigoma Frasser Kashai akimvalisha Koti maalumu
(Reflector Jacket) Mwendesha Pikipiki wakati wa Hafla fupi ya
Makabidhiano ya Makoti hayo ambapo waendesha Pikipiki 350 kutoka vijiwe
15 vya Waendesha Pikipiki Katika Wilaya ya Kigoma walikabidhiwa kwaajili
ya kukabiliana na ajali za barabarani .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Frasser Kashaiakimvalisha koti mmoja wa waendesha piki piki(Reflector Jacket)
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kigoma Frasser Kashai akiongea na waendesha Pikipiki
maarufu kama Bodaboda wakati wa Hafla fupi ya Makabidhiano ya Makoti
maalumu ya kuwatambua ambapo waendesha Pikipiki 350 kutoka vijiwe 15 vya
Waendesha bodaboda Katika Wilaya ya Kigoma walikabidhiwa kwaajili ya
kukabiliana na ajali za barabarani .Picha Na Frank Geofray-Jeshi la
Polisi, Kigoma
TAMKO RASMI KUTOKA KWA ASKOFU METHOD KILAINI DHIDI YA GAZETI LA MWANANCHI KUANDIKA KWAMBA AMEIPONDA SAFU YA UONGOZI NA SEKRETARIATI YA CCM
Askofu Method Kilaini Bukoba Catholic Diocese
---
Kwa
masikitiko makubwa nimesoma katika gazeti la Mwananchi kwamba
nimeiponda safu ya uongozi na sekretariati ya CCM. Mimi sijaongea na
gazeti lolote juu ya uongozi wa CCM na wala sina nia au sababu ya
kuuponda uongozi huo. Ni
vibaya kwa gazeti lo lote lile kutumia jina la mtu kwa kueneza maoni
yake. Kama ni waugwana natumaini watasahihisha waliyoyaandika.
Nasikitika sana kwa walikwazwa na hilo. Askofu Kilaini
Askofu Method Kilaini
Bukoba Catholic Diocese
No comments:
Post a Comment