Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akizungumza
na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi wakati akiwasili
kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam kwa ajili ya
kuzindua rasmi kampeni ya kupambana na Malaria inayoitwa “Malaria Safe
Companys” ambapo Wizara ya afya inashirikiana na pamoja na taasisi za
kimataifa na Makampuni mbalimbali pamoja na Sekta ya michezo, ambapo
wadau mbalimbali wameshiriki katika uzinduzi huo unaofanyika usiku huu
jijini Dar es salaam, kulia ni Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh.
Raymond Mushi.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akizungumza
na Rais Washirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF Bw. Leodger Tenga
wakati alipowasili katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam
kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni ya kupambana na ugonjwa wa Malaria,
kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi.
Wadau
waliohudhuria katika uzinduzi wa kampeni ya kupambana na ugonjwa wa
malaria kutoka kulia ni Mkurugenzi wa michezo katika Wizara ya Habari,
Vijana , Michezo na Utamaduni Bw. Leonald Thadeo, Assah Mwmbene
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Mbunge wa Jimbo la Temeke Mh.
Abbas Mtemvu na Mbunge na Waziri wa zamani Mh. Chrisant Mzindakaya.
Wadau mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo katika Hyatt Regency Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Sahara Media Bw. Samwel Nyala kushoto akiwa na wadau wengine katika uzinduzi huoHyatt Regency Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi huo kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam
Waziri
Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiandika kitu huku Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii Mh. Hussein Mwinyi akipiga makofi katika uzinduzi huo.
Meneja
Mkuu wa Kampuni ya Azam Mzee Salim Mohamed Abeid Bakhressa akitoa
ushuhuda kuhusu malaria ilivytokomezwa katika viwanda vyao.
Rais
wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF Bw, Leodger Tenga
akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo jinsi sekta ya michezo
ilivyosaidia kutokomeza malaria nchini.
Mwimbaji
nguli wa muziki wa Taarab Khadija Kopa pamoja na kundi lake
wakitumbuiza katika hafla hiyo iliyofanyika usiku huu kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam
Meneja
Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena akiwa
katika hafla hiyo, Bodi ya Utalii nchini TTB ni moja ya taasisi
zilizotambuliwa na Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda katkatika hfla hiyo kwa
juhudi zake za kupamana na ugonjwa wa malaria.
IKULU:VIONGOZI WAKUU WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAZINDUA JENGO LA MAKAO MAKUU YA JUMUIYA JIJINI ARUSHA
Mfano wa jengo la Makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiangalia mfano wa jengo jipya la makao
makuu ya Jumuiya hiyo pamoja na maelezo yake baada ya kulifungua rasmi
Novemba 28, 2012 jijini Arusha
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifunua pazia kufungua
rasmi jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya Novemba 28, 2012 jijini
Arusha
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakikata utepe kufungua
rasmi jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya Novemba 28, 2012 jijini
Arusha
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakitembelea sehemu mbali
mbali za jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya baada ya kulifungua
rasmi Novemba 28, 2012 jijini Arusha
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakitembelea sehemu mbali
mbali za jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya baada ya kulifungua
rasmi Novemba 28, 2012 jijini Arusha. Hapa ni katika chumba cha mahakama
ya jumuiya hiyo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie
wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakishuhudia
Mwenyekiti wa Jumuiya Rais Mwai Kibaki wa Kenya akizindua rasmi mfumo wa
kisasa wa kuunganisha shughuli za ushuru wa forodha kwa njia ya mtandao
katika jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya baada ya kulifungua
rasmi Novemba 28, 2012 jijini Arusha
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika chemba ya
mikutano ya Bunge la Jumuiya ya Afrika mashariki katika jengo jipya la
makao makuu ya Jumuiya baada ya kulifungua rasmi Novemba 28, 2012
jijini Arusha
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wakuu wenzie wa nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja
na wadau pamoja na wabunge wa Afrika Mashariki.Picha na IKULU
WADAU WA TAKWIMU NCHINI WAKUTANA KATIKA KONGAMANO LA PILI LA MWAKA JIJINI DAR LEO
Mkurugenzi
wa Takwimu nchini, Morrice Oyuke, akisoma hotuba yake kumwakilisha
Mkurugenzi Mkuu wa TAKWIMU nchini Dkt.. Albina Chuwa, wakati wa
kongamano la pili la mwaka la wadau wa TAKWIMU nchini lililofanyika leo
jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi
kutoka Benki ya Dunia, Thomas Danielewitz, akitoa hotuba yake leo
jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa kongamano la pili la mwaka kwa
Wadau wa Takwimu nchini. Kongamano hilo la siku moja limefunguliwa na
Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Saada M. Salum (hayupo Pichani).
Baadhi
ya washiriki wa kongamano la pili la mwaka unaowashirikisha Wadau wa
Takwimu nchini wakimsikilza Naibu Waziri wa Fedha Dr. Saada M. Salum
(hayupo pichani) katika ufunguzi wa kongamano hilo leo jijini Dar es
Salaam.
Naibu
wa Wizara ya Fedha Dkt. Saada M. Salum akifungua kongamano la pili la
mwaka kwa wadau wa Takwimu nchini leo jijini Dar es Salaam., ambapo
amewasisitiza wadau kutumia takwimu zilizo sahihi. Picha na Mwanakombo
Jumaa- MAELEZO
No comments:
Post a Comment