Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki
Okada kesho anataraji kutia saini makubalino ya msaada wa fedha kiasi cha
shilingi Milioni 380 kwaajili ya miradi miwili ya ujenzi wa bweni La
Wasichana pamoja na Shule ya watoto wenye ulemavu katika mikoa ya Lindi na
Mtwara.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na
Ubalozi huo jijini Dar es Salaam, inasemakuwa miradi hiyo ni upanuzi wa
shule ya wenye ulemavu Dinyecha Wilayani Mtwara utakao gharimu zaidi ya
shilingi Milioni 192 na
ujenzi wa bweni la wasichana sekondari ya Ngapa ya Lindi utakaogharimu
shilingi
Milioni 188.
Miradi hiyo miwili
inasimamiwa na taasisi za Tanzania Life Improvement Association (TALIA) ya Mtwara na Women in
Social Entrepreneurship (WISE) ya mjini Lindi.
Ubalozi wa Japan nchini Tanzania umekuwa
ukichangia fedha katika miradi mbalimbali ya Maendeleo katika sekta ya Afya,
elimu na maji tangu mwaka 1991 ambapo katika kipindi cha miaka 5 iliyopita
mikoa ya Lindi na Mtwara imepatiwa msaada katika miradi 71 iliyogharimu dola za
kimarekani 6,135,418 sawa na shilingi Bilioni 9,614,629485.
Utiaji saini huo utafanyika katika ofisi
za mkuu wa Mkoa wa Lindi na Mtwara kati ya saa 3 asubuhi na saa 5.
WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII ATEMBELEA BANDA LA TANZANIA KATIKA MAONYESHO YA UTALII YA WTM YANAYOFANYIKA JIJINI LONDON UINGEREZA

Waziri Balozi Kagasheki amesifushiriki wa makampuni ya Tanzania katika maonyesho hayo lakini amesisitiza kwamba makampuni hayo yaongeze juhudi za kutangaza utalii wa Tanzania mpaka kufikisha lengo la idadi ya watalii milioni moja kila mwaka, ameongeza kwamba kuna haja ya kuongeza vitanda zaidi nchini Tanzania ili kuongeza idadi ya watalii watakaotembelea katika mbuga zetu na kufanya utalii kuka zaidi, Maonyesho hayo yatazinduliwa rasmi kesho.
Fullshangweblo iko jijini London nchini Uingereza ikikumuvuzishia matukio haya moja kwa moja kutoka katika maeneo ya Excell ambako ndiko maonyesho hayo yanafanyika.












TIMU YA NMB FC YAKUBALI KICHAPO CHA MAGOLI 2 KWA 1 DHIDI YA EXIM FC
Mshambuliaji wa Exim FC, Erick Makule (kushoto) na mchezaji wa NMB F.C Omar Said (kulia) wakipigania mpira, katika mechi ya kirafiki iliyofanyika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam jumapili jioni. Mechi ilimalizika kwa Exim F.C kuifunga NMB F.C 2-1.
Mshambuliaji wa Exim FC, Ammy Ditufu (kulia) na mchezaji wa NMB F.C (kushoto) wakipigania mpira, katika mechi ya kirafiki iliyofanyika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam Jumapili jioni. Mechi ilimalizika kwa Exim F.C kuifunga NMB F.C 2-1.
Na Mwandishi Wetu.
TIMU ya mpira wa miguu ya benki ya Exim ya Tanzania, Exim F.C imeendeleza wimbi la ushindi katika michezo yake ya kirafiki, baada ya kuifunga timu ya NMB magoli 2-1.
Mchezo huo uliochezwa jana katika uwanja wa Karume ulianza kwa kasi hasa kutokana na timu hizo kuwa na upinzani mkubwa pale zinazopokutana.
Jambo hilo lilisababisha timu zote kuanza mchezo kwa kasi huku Exim ikionekana kuwa imara zaidi hasa kutokana na kusheheni wachezaji imara waliokuwa wanapeleka mashambulizi mara kwa mara langoni mwa NMB.
Dakika ya 5, NMB iliweza kupata goli la kwanza baada ya faulo iliyopigwa na Aron Nyanda na kumkuta Nuhu Mkuchu.
Kuingia kwa goli hilo kuliamsha mashambulizi kwa timu ya Exim, ambayo ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Richard Noni na kumuingiza Ami Ditufu.
Mabadiliko hayo yalionekana kuisaidia zaidi Exim, baada ya kuanza kulishambulia lango la NMB kama nyuki na kupelekea kukosa magoli ya wazi katika dakika ya 15, 17 na 20 kupitia kwa wachezaji wake Fadhili Selemani na Norbert Missana.
Kipindi cha pili kilipoanza, NMB walionekana kuzidiwa huku Exim ikindandaza kandanda safi na kuwasaidia kusawazisha goli kupitia kwa Ditufu.
Ditufu alishinda goli hilo, baada ya kupokea pasi safi ya Missana na yeye kupiga shuti lililozaa goli hilo la kwanza kwa Exim.
Kuingia kwa goli hilo, kuliamsha ari ya ushindi kwa Exim ambao walicheza vyema na kufanikiwa kufunga goli la pili kupitia kwa Missana.
Missana alishinda goli hilo katika dakika ya 57 na kuwafanya NMB kuzidi kupoteana na kuipa nafasi zaidi Exim kutawala mchezo huo.
Hadi filimbi ya mwisho Exim ilifanikiwa kutoka uwanjani na ushindi huo wa magoli 2-1.
Akizungumza baada ya mchezo huo, nahodha wa Exim Fadhili Selemani alisema wanafurahi kuifunga NMB ambao ni wapinzani wao wakubwa.
“Hawa ni wapinzani wetu hivyo kuwafunga ni mwanzo tu, kwani tumejiandaa kuwafunga kila mechi hasa kutokana na kuwahi kutufunga michezo miwili”alisema.
Hivyo, alisema ushindi huo ni mwanzo kwa kuwa kila siku wanafanya mazoezi ya nguvu ili kuhakikisha wanashinda michezo yao yote.
RAIS KIKWETE AZINDUA MIRADI YA BARABARA MANYONI-ITIGI-CHAYA na ISSUNA-MANYONI MKOANI SINGIDA LEO
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi barabara ya Issuna-Manyoni akiwa na viongozi wa serikali na wa TANROADS pamoja na wabunge wa mkoa wa Singida.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua ujenzi wa Barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya mkoani Singida leo. Pembeni yake kulia ni Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipozi na viongozi wa serikali na wa kampuni ya ujenzi baada ya kuzindua ujenzi wa Barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya mkoani Singida leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa Barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya mkoani Singida leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua ujenzi wa Barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya mkoani Singida leo.
Sehemu ya barabara mpya karibu na mji wa Manyoni iliyozinduliwa leo na Rais Kikwete.
Sehemu ya barabara mpya iliyozinduliwa na Rais Kikwete karibu na mji wa Katesh mkoani Manyara.
Sehemu ya barabara mpya iliyozinduliwa na Rais Kikwete mkoani Manyara. PICHA NA IKULU
JICHO LA LUKAZA BLOG LIKIANGAZIA MAENEO MBALIMBALI YA TABATA KINYEREZI JIONI HII
Huo unaonekana kwenye picha ni Mbuyu, Mbuyu huo ndio umefanya eneo hilo linaloonekana kwenye picha kuitwa Mbuyuni eneo hilo lipo Tabata Kinyerezi Njia panda ya kuelekea majumba Sita.
Ukiwa unatokea Segerea Kuelekea Kinyerezi lazima upite hapa
UBALOZI WA JAPAN KUTIA SAINI MSAADA WA SHILINGI MILIONI 380 ZA UJENZI WA BWENI LINDI NA SHULE YA WALEMAVU MTWARA
Kijiwe Cha Bodaboda Kilichopo Kinyerezi Mwisho wa daladala
Tamasha la Kuchangia Mtoto wa Kike Nchini Uingereza

Mstahiki Meya akifungua Tamasha.

Mama Balozi akiwaonyesha wageni Rasmi Mameya vitu mbalimbali vitakavyouzwa kwa ajili ya kuchangia mfuko huu.

Mtahiki Meya akiangalia sehemu ya chakula ya Tanzania.

kutoka Kushoto Mh balozi wa Grenada Ruth Elizabeth Rouse, Mtahiki Meya Christopher Buckmaster na Mama Balozi Joyce Kallaghe.

Mama Kiondo akiwa kikazi zaidi kuitangaza Tanzania Pics .

Mama Balozi Akipakwa Hina kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa elimu

Mama Balozi akimkabidhi Mayorese Mrs. Anne Hobson baada ya kununua kitenge katika banda la Tanzania .

Mayorese Mrs. Anne Hobson katika banda la Tanzania.

wateja wakinunua bidhaa kutoka banda la Tanzania.

Sherehe ikiendeleaPics By Frank Eyembe.

Ukumbi wa Royal Borough of Kensington.Pics By Frank Eyembe.
---
Salaam,
Jumuiya
ya Commonwealth Countries League (CCL) inayoshirikisha nchi hamsini na
nne (54) duniani kutoka katika jumuiya ya madola iliandaa tamasha maalum
siku ya jumamosi tarehe 3.11.12 kwa ajili ya kuchangia mfuko wa
kumsaidia na kumwezesha msichana kusoma elimu ya sekondari.
Historia ya
Commonwealth Countries League ilianzishwa rasmi kutoka kwa baadhi ya
wanawake mnamo mwaka 1923 nchini Australia kwa ajili ya kusaidia
kutangaza uelewa wa haki sawa kati ya wanawake na wanaume waliopo nchi
mbalimbali zilizo ndani katika jamuiya ya madola.
Tamasha hili
lilifanyika Royal Borough of Kensington chini ya uongozi kutoka kwa
Mh. Balozi wa Grenada Ruth Elizabeth Rouse ambaye ndio raisi wa jumuiya
hiyo akisaidia na makamu wake mama Balozi Joyce Kallaghe. Wageni Rasmi
walikua Wastahiki Mameya wa Worshipful Royal Borough of Kensington na
Chelsea - Councillor Christopher Buckmaster na Mrs. Anne Hobson Shughuli ya mwaka huu iliandaliwa na wake za
mabalozi kutoka katika jumuiya za Madola hamsini na nne (54) ili
kuchangisha pesa kwa njia ya kuuza vitu mbalimbali vya asili kama
chakula, urembo, maua, vinywaji n.k. Fedha zote zilizopatikana
zilipelekwa kusaidia mfuko huu wa Elimu kwa ajili ya kumsomesha mtoto wa
kike.
Aidha Mama
Balozi Joyce Kallaghe aliongeza kwa kusema ''Elimu ni Ufunguo Wa Maisha
kumsomesha mwanamke ni kuiwezesha jamii nzima hivyo vipaumbele vyote
vimeelekezwa kwa kwa ajili ya kuwasomesha watoto wa kike walio maskini
au wanaoishi katika mazingira magumu ambao wana uwezo wa kuendelea
kusoma elimu ya sekondari katika nchi za jumuiya ya Madola". Tangu
mwaka 2011/2012 mfuko wa Elimu wa CCL ushawawezesha watoto wa kike 364
kutoka nchi 25 ikiwapo Tanzania. Pia aliwasihi wadau kuwa wazalendo kwa
kuchangia mfuko huu kwa kuwasiliana kupitia barua pepe ccl.edfund@googlemail.com
Kiasi cha paundi mia moja hamsini (£150) na Mia nne na hamsini (£450) zinatosha kumsomesha msichana kwa mwaka mzima
Asanteni
Urban Pulse Creative
KHADIJA KOPA ALIVYOFUNIKA MITIKISIKO YA PWANI DAR LIVE
Mzee Yusuf akimchombeza mkewe, Leila Rashid.
Mashabiki waliopanda stejini kumtunza Mzee Yusuf wakijiachia kwa raha zao.
--
MALKIA wa mipasho nchini, Khadija Kopa, juzi (Jumamosi) alifunika
vilivyo katika Tamasha la Mitikisiko ya Pwani lililofanyika ndani ya
ukumbi wa kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar.
Tamasha hilo lilipambwa na makundi mbalimbali ya taarab yakiwemo
Jahazi, Coastal, TOT na mengineyo. Watangazaji mahiri kutoka Times
Radio wakiongozwa na Gardner G Habash na Khadija Shaibu 'Dida'
walinogesha tamasha hilo na kulifanya liwe la kipekee.
No comments:
Post a Comment