MAMIA WAJITOKEZA KUUAGA MWILI WA KAMANDA LIBERATUS BALLOW LEO KATIKA UWANJA WA NYAMAGANA JIJINI MWANZA.
Afande
George Msangi akiongoza ratiba za kumuaga aliyekuwa kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mwanza SACP Liberatus Ballow aliyeuawa usiku wa kuamkia
jumamosi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi katika eneo la Kitangiri
karibu na Hotel ya Tai Five.
Msafara
wa magari ya kuleta mwili wa marehemu Liberatus Ballow yakiingia
katika uwanja wa Nyamagana ili viongozi na wananchi mbalimbali wapate
kuuaga mwili huo.
Magari yakiingia kwa uwanja wa Nyamagana..
Maaskari
walioteuliwa kubeba mwili wa marehemu Liberatus Ballow wakiwa
wamejipanga vyema ili mwili uweze kutolewa ndani ya gari ili uwekwe
sehemu nzuri ambayo kila mtu anaweza kuuaga vizuri.
Hapa wakiushusha kutoka ndani ya gari ili waweze kuubeba.
Safari ya kuelekea sehemu maalum iliyopangwa kwa ajili ya mwili wa marehemu ilianza hiviii..
Maaskari wakiwa sawa kutekeleza jukumu lao..
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza Injinia Everest Ndikillo akienda kuuaga mwili wa
marehemu kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Liberatus Ballow katika uwanja
wa Nyamagana leo.
Viongozi mbalimbali wa Kiserikali wakisimama kwa dakika chache kuupa heshima mwili wa marehemu kamanda Liberatus Ballow.
Baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Polisi wakionekana na huzuni
Afisa Usalama wa Taifa Meja Jacob Mutashi mwenye suti nyeusi kulia akionekana pichani.
Mwili wa Marehemu kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Liberatus Ballow.
Mwandishi Peter Fabian kutoka gazeti la Mtanzania akiweka picha vizuri ya marehemu kamanda Liberatus Ballow.
Saluti kutoka kwa Maafisa wa Polisi walizamu kwa Marehemu Kamanda wa Mkoa wa Mwanza Liberatus Ballow wakitoa heshima za mwisho.
Katibu
wa CCM Mkoa wa Mwanza Joyce Masunga akiweka saini katika daftari la
maombolezo katika msiba wa marehemu kamanda Liberatus Ballow katika
uwanja wa Nyamagana.
Mkurugenzi
wa Makosa ya Jinai Kaminishina Richard Manumba akisalimia na Mkuu wa
Wilaya ya Magu Bi. Jackline Wana huku Katibu tawala wa Mkoa wa Mwanza
Bi. Rosemary Mwanyika akiwa mbele mwenye suti nyeusi.
Ibada
ya ya kumuaga mwili wa marehemu kamanda Liberatus Ballow kama
ilivyoongoza na Watumishi wa Kanisa la Roman Katoliki maana kamanda
alikuwa muumini wa kanisa hilo.
Wakuu
wa wilaya mbalimbali katika Mkoa wa Mwanza na baadhi ya viongozi wa
serikali, vyama vya kisiasa wakionekana katika picha wakiwa na majonzi
makubwa kumpoteza kamanda Liberatus Ballow.
Wananchi
mbalimbali kutoka katika Mkoa wa Mwanza na nje ya Mkoa wa Mwanza
wakionekana katika tukio la kuuaga mwili wa Kamanda Liberatus Ballow.
Wanafamilia
wa marehemu kamanda Liberatus Ballow wakiwa na majonzi makubwa sana
katika uwanja wa Nyamagana wakati wa kuuaga mwili wa mpendwa wao
Liberatus Ballow.
Maafisa
wa Majeshi aina mbalimbali kutoka Tanzania wakionekana katika hafla la
kuuaga mwili wa marehemu kamanda Liberatus Ballow.
Mabanda ambayo watu wamekaa kwa utulivu wakiuaga mwili wa kamanda Liberatus Ballow.
Umati
mkubwa watu wakiwa katika uwanja wa Nyamagana wakati wa kuuaga mwili
wa aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Liberatus Ballow. Picha zote na B Plus Blog
No comments:
Post a Comment