TAARIFA KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII:TAHADHARI YA UGONJWA WA MARBURG
TAHADHARI YA UGONJWA WA MARBURG
Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii, imepokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani
(WHO), tarehe 20 Oktoba, 2012 kuhusu ugonjwa wa Marburg ambao umejitokeza
katika nchi jirani ya Uganda. Maeneo yaliyokumbwa na ugonjwa huo ni
Wilaya ya Kabale, Kanda ya Kusini Magharibi ya nchi, na wilaya hii inapakana
na Rwanda. Mpaka tarehe 24 Oktoba 2012, takriban watu 13 wamepata maambukizo
na 6 wamepoteza maisha..
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa
tahadhari ya Ugonjwa huu kwa wananchi wote, katika mikoa yote ya Tanzania
na hasa wale waliopo katika mikoa ambayo inapakana na na nchi jirani
ya Uganda (Mikoa ya Mara, Mwanza, Kagera na Kigoma).
Marburg ni
ugonjwa wa hatari unaofanana na Ebola na unasababishwa na virusi vijulikanavyo
kwa lugha ya kitaalam “Marburg Virus”. Ugonjwa huu ni miongoni mwa
magonjwa yajulikanayo kwa ujumla kama Homa za Virusi zinazosababisha
kutokwa damu mwilini, (Viral Haemorrhagic Fevers). Chanzo kamili cha
virusi vya ugonjwa huu hakijulikani. Hali inayosababisha mlipuko wake
pia haijulikani. Ugonjwa huu hauna tiba wala chanjo.
Dalili kuu za ugonjwa huu ni pamoja na Homa kali, inayoambatana
na kutokwa damu katika matundu yote ya mwili yaani pua, njia ya haja
kubwa na ndogo, mdomoni, masikioni, machoni, hali inayopelekea kifo
kwa muda mfupi.
Kipindi cha kuonekana kwa dalili za ugonjwa ni kati ya siku 3 hadi 9 baada ya kupata maambukizi.
Ugonjwa huu unaenea kwa urahisi sana na haraka kutoka
mtu mmoja hadi mtu mwingine iwapo mtu atakuwa karibu na mgonjwa na kugusana
na mate, damu, mkojo, machozi, kamasi, maji maji mengine ya mwili, ikiwa
ni pamoja na jasho au kumgusa mtu aliyekufa kwa ugonjwa wa Marburg.Ugonjwa
huu pia unaweza kuenezwa iwapo mtu atagusa nguo au mashuka ya mgonjwa
wa Marburg.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imechukua hatua
zifuatazo katika kukabiliana na tishio la ugonjwa huu:
- Kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kupitia kwa Waganga Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya. Aidha taarifa hii pia imejumuisha namna mgonjwa anavyoweza kutambuliwa (Ainisho la Ugonjwa), “Fact sheet” ya ugonjwa, Mwongozo kwa watumishi wa afya wa namna ya kuchukua sampuli na vipeperushi vinavyoelezea ugonjwa huu.
- Kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa huu kupitia kwa Wataalamu wa Afya katika Mikoa, Wilaya na maeneo ya mipaka. Aidha watalaamu hawa wa Afya pia wanatoa elimu kwa wananchi kuhusu dalili za ugonjwa huu ili endapo ugonjwa huo utatokea uweze kutolewa taarifa mapema.
- Kupeleka vifaa kinga kwa ajili ya watumishi wa afya
Wananchi wanashauriwa kutokuwa
na hofu kwani mpaka sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyeripotiwa nchini.
Wananchi wanashauriwa kutoa taarifa kwenye kituo cha huduma za afya
kilicho karibu mara watakapoona mgonjwa yeyote atakayehisiwa kuwa na dalili za
ugonjwa huu.
Kitengo cha mawasiliano ya Serikali
25/10/201
NAPE,MGEJA NA MAIGE WAFUNGA KAMPENI ZA CCM KATA YA BUGARAMA, KAHAMA
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
akiwa katika mapokezi ya wananchi alipowasili kwenye mkutano wa kufunga
kampeni za CCM za udiwani kata ya Bugarama, Kahama mkoani Shinyanga.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa kufunga kampeni za CCM za
udiwani Kata ya Bugarama, Kahama mkoani Shinyanga, jana Oktoba 27.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige wakiwa na watafiti wa madini kutoka
kampuni ya Majordrilling, katika kijiji cha Kakola wilayani Kahama
mkoani Shinyanga.
Baadhi ya Wazee
wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya
CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipohutubia mkutano wa kufunga
kampeni za udiwani za CCM Kata ya Bugarama, Kahama mkoani Shinyanga.
Kina
mama wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya
Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Kata ya Bugarama , Kahama
mkoani shinyanga.
Mzee
wa miaka 98, Nickson Toma akifuatilia kwa makini mkutano wa kampeni za
udiwani Kata ya Bugarama mkoani Shinyanga uliohutubiwa na Katibu wa
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
akicharaza ngoma kwenye mkutano wa kampeni za udiwani Kata ya Bugarama,
Kahama mkoani Shinyanga.
Wananchi
katika kata ya Bugarama , Kahama mkoani Shinyanga, wakishangilia wakati
wa kufunga kampeni za CCM za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata
hiyo.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
akisalimiana kwa furaha na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Hamis
Mgeja walipokutana katika Kata ya Kakola, kabla ya kwenda kwenye mkutano
wa kufunga kampeni za udiwani za CCM kata ya Bugarama mkoani humo.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Sinyanga Hamis Mgeja wakishiriki kucheza ngoma
ya Baswezi kwenye mkutano wa kampeni za udiwani kata ya Bugarama mkoani
humo.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Sinyanga Hamis Mgeja wakishiriki kucheza ngoma
ya Baswezi kwenye mkutano wa kampeni za udiwani kata ya Bugarama mkoani
humo.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
akimsikiliza kwa makini Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige wakati
akimuombea kura mgombea udiwani wa CCM Kata ya Bugarama, kwenye mkutano
wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika mji mdogo wa Bugarama.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
akimnadi mgombea wa Udiwani kata ya Bugarama, Nixon Igogo kwenye mkutano
wa kufunga kampeni za udiwani za CCM.
MABINGWA WA BALIMI BOAT RACE KAGERA WAPATIKANA
Katibu Tawala wa Manispaa ya Bukoba Clement
Ndiomukama, akimkabidhi kitita cha Tsh.900,000 Nahodha wa timu ya Kabanga
Bushasha, Eliudi Prospa baada ya kuibuka mabingwa kwenye mashindano ya
(Mitumbwi) Balimi Boat Race Wilayani
Bukoba Mkoani Kagera jana ambapo washiriki walishindana kuendesha mitumbwi kwa makasia.
Mabingwa wa mashindano ya Mitumbwi ya Balimi (Balimi
Boat Race) Mkoani Kagera upande wa
wanaume timu ya Kabanga Bushasha wanaume wakishangilia mara baada ya kuwa
mabingwa wa mkoa huo na kukabidhiwa jumla ya shilingi laki tisa (900,000) kama zawadi ya ushindi wa kwanza.
Mabingwa wa mashindano ya Mitumbwi ya Balimi (Balimi
Boat Race) Mkoa wa Kagera upande wa wanawake Timu ya Seleka kutoka Musila,
wakishangilia mara baada ya kuwa mabingwa wa mkoa huo na kukabidhiwa jumla ya
shilingi laki saba (700,000) kama zawadi ya
ushindi wa kwanza.
Katibu tawala wa Manispaa ya Bukoba Clement
Ndiamukama, akifungua mashindano ya Mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race)
yaliyofanyika Wilayani Bukoba Mkoani Kagera ambapo zaaidi ya timu 50 zenye watu
watano kila timu zilishiriki, ambapo walishindana kupiga kasia kwa umbali wa
Kilometa 3 kwenda na kurudi, kushoto ni Meneja wa Mauzo wa Kanda ya Ziwa Endrew
Mbwambo na Afisa wa Sumatra Kapteni Alex Katama.
Meneja wa Bia ya Balimi Edith Bebwa(kulia)
akizungumza na washiriki wa mashindano ya Balimi Boat Race Wilayani Bukoba Mkoani
Kagera mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo ambapo timu tano zitakwenda
kuwakilisha mkoa huo kwenye fainali zitakazofanyika mkoani Mwanza Disemba mwaka
huu.
Waokoaji wakiwakoa wapiga kasia kinamama ambao walipinduka
Mabingwa Wanaumr Wakishangilia Baada Ya Kuwasili
WASHIRIKI wa shindano
la mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) ambayo ni maalum kwa mikoa ya kanda ya
ziwa wametakiwa kutumia pesa wanazozipata kwaajili ya kujiendeleza kwenye
miradi ya maendeleo.
Akizungumza mara
baada ya mashindano hayo Meneja wa Kinywaji hicho Cha Balimi Edith Bebwa,
alisema lengo la mashindano hayo ni kutoa shukrani na kuwawezesha wanywaji wake
hivyo wanapaswa kuzitumia kwenye kujiendeleza kwenye miradi yao.
“Nawaomba mlioshinda
na washiriki wengine ambao pia mmepata pesa hizo mzitumie kwenye miradi
yenu kama ni mvuvi basi ongeza chombo kingine au nyavu ili
mradi uzitumie kwenye uzalishaji” alisema Bebwa.
Awali akifungua
mashindano hayo Katibu Tawala wa Manispaa ya Bukoba Clement Ndiamukama
aliwataka washiriki watakaoshinda kutobweteka na ubingwa badalayake wajipange
kwa mazoezi ili kwenye fainali ya mashindano hayo waupe heshima Mkoa wa Kagera.
“Tunataka mtuletee
heshima kwahiyo wale watakaoshinda watambue wajibu huo wakuletea heshima Mkoa,”
alisema Ndiomukama.
Mashindano hayo
ambayo yalianza Mkoani Kigoma October 27 mwaka huu yanatarajiwa kumalizika
kwenye fainali zitakazofanyika mwezi Disemba mwaka huu Mkoani Mwanza.
No comments:
Post a Comment