Nisha wa Bongo Movies Afunguka..Napenda Kuitwa mama au Mke wa Mtu ila.....
Nisha |
MSANII wa filamu Salma Jabu ‘Nisha’ aliyeng’aa kwenye filamu kibao kama vile ‘Kashfa’ na ‘Macho Yangu’, amefunguka juu ya maisha yake, kuwa anapenda kuitwa mama au mke wa mtu lakini anashindwa kufanya hivyo kwa sababu malengo yake hayajatimia na kufikia viwango vya wanawake wengine wenye mafanikio makubwa duniani.
Mtandao wa DarTalk ulifanya mazungumzo na Nisha juu ya mikakati yake ya baadae ya ndoa na familia, ndipo alipofunguka ishu hiyo kwa kusema kuwa haitaji kulelewa na kuwa mwanamke tegemezi kwa mwanaume na ndiyo maana haitaki kuolewa kwa sasa hata kama na mpenzi.
“Wakati wangu wa kuishi ndani ya ndoa bado nasema hivi kwa sababu kila kitu huwa kinaenda na mipangilio siwezi kusema nataka kuwa na watoto wakati sijajiandaa kuwa mama mzuri wa familia,” alisema.
Nisha alitoa ushauri kwa wanawake kuacha tabia ya kutengemea wanaume kwani huo ni utumwa kwa sababu wanakuwa hawana uhuru na maamuzi katikamambo mengi ya msingi.
No comments:
Post a Comment