Monday, October 22, 2012

viongozi wa jumuiya ya uamsho wafikishwa mahakamani zanzibar leo


Wanafunzi Buguruni Viziwi na Balozi wa Airtel AY-waomba Watanzania kuchangia vifaa vya kufundishia.

Kivuko cha Mto Kilombero

Kivuko cha Mv Kilombero Na. 1 kikivusha wananchi na mali zao juzi Mto Kilombero, mkoani Morogoro kufuatia kivuko cha awali cha Mv Kilombero Na. 2 kuleta hitilafu katika mfumo wa usukani. Picha na  Juma Mtanda

Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad:'CUF itaendelea kuwaunganisha Watanzania.'

MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL AKIHUTUBIA WAKATI WA UFUNGUZI WA MKUTANO WA AKINA MAMA WAJASIRIALIAMALI KUTOKA NCHI ZA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI.

Ukumbi Walipuka kwa Shangwe Baada ya Rais Jakaya Kikwete Kuwasili na Kuhutubia Kwenye Kilele cha mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)Mjini Dodoma

TCRA: TV ZENYE MIGONGO NA MATUMBO MAKUBWA PIA ZITAPOKEA MATANGAZO YA DIGITALI

KATIKA KUSHEHEREKEA MIAKA 67 YA UMOJA WA MATAIFA TANZANIA UN FAMILY DAY YAFANA.

Kikosi cha timu ya Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa katika picha ya pamoja.
Kikosi cha timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Mechi ya Kirafiki kati ya timu ya Umoja wa Mataifa (Blue) na timu ya Wizara ya Mambo ya Nje (Nyeupe) katika UN Family Day ya maadhimisho ya wiki ya Umoja wa mataifa kusheherekea miaka 67 ya Umoja huo zikimenyana kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar.
Austin Makani wa UNHCR (mwenye koti la suti) akiwapa mzuka timu ya Umoja wa Mataifa wakati wa mechi ya kirafiki kusheherekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa ya miaka 67 tangu kuzaliwa kwa shirika hilo.
Hoyce Temu akibadilishana mawazo na baadhi ya wafanyakazi wenzake wakati wa mechi kati ya Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Mataifa katika kusheherekea miaka 67 tangu kuzaliwa kwake.
Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na Wa Wizara ya Mambo na familia zao wakifuatilia mechi hiyo.
Kiongozi wa Benchi la Ufundi la timu ya Umoja wa Mataifa Siraji Ismail akiwa mbinu timu yake wakati wa mapumziko ya kipindi cha kwanza.
Mchezaji wa timu ya UN akiruka sarakasi baada ya kurudisha goli kwa timu ya Wizara ya Mambo ya nje katika kipindi cha pili cha mchezo huo.
Kiungo wa timu ya Umoja wa Mataifa akijaribu kumtoka kiungo wa timu ya Wizara ya mambo ya nje wakati wa mechi ya kirafiki ambapo timu zote mbili zilitoka sare ya Bao 1-1.
Baba na Familia yake.
Jacqueline Namfua wa UNICEF (Kushoto) akifurahi jambo na wafanyakazi wenzake.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou (katikati) akibadilishana mawazo na baadhi ya Wakuu wa vitengo vya Umoja wa Mataifa wakati wa UN Family day kusheherekea miaka 67 tangu kuzaliwa kwa shirika hilo.
Watoto walipata fursa ya kucheza michezo mbalimbali kama inavyoonekana pichani.
Mchezo wa kushindana kuvuta kamba kati ya watoto wa kike na wakiume ambapo watoto wa kike waliwashinda wa kiume.
Wakuu wa Vitengo mbalimbali vya Umoja wa Mataifa wakiongozwa na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou (mwenye kofia) wakishindana kuvuta kamba na Wakuu wa vitengo mbalimbali vya Wizara ya mambo ya Nje ambapo UN iliibuka kidedea katika mchezo huo.
Wizara ya Mambo ya Nje walionekana kuwa wengi na wenye fya na kushindwa katika mchezo.
Pichani juu na chini ni Mchezo wa kushindana kukimbia na magunia kwa wakubwa na wadogo.
Pichani Juu na Chini ni Familia za Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje katika UN Family Day iliyofanyika jijini Dar es Salaam viwanja vya Leaders Club.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa UN Tanzania Sangita Khadka Bista (kushoto) na mfanyakazi mwenzake wakingalia taswira mbalimbali kwenye kamera.
MC wa UN Familya Day Austin Makani wa UNHCR.
Kwaito ilichezeka vilivyo katika kusheherekea miaka 67 ya Umoja wa Mataifa tangu kuzaliwa kwa shirika hilo.
Twende kazi mwendo mdundo.... "Delivering as One".
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa timu ya Wizara ya Mambo ya Nje wakati wa kukabidhi Kombe.
Watoto wakikabidhi Kikombe kwa Kapteni wa timu ya Umoja wa Mataifa Laurean Kiiza kwa niaba ya Dkt. Alberic Kacou.
Kapteni wa timu ya Wizara ya Mambo ya Nje akipokea Kikombe kwa wote baada ya kutoka sare ya Bao 1-1 na timu ya UN.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou akipozi na Timu ya Wizara ya Mambo ya nje.
Dkt. Alberic Kacou na timu ya vijana wa Umoja wa Mataifa.
Makpteni wakipongezana.
Dkt. Alberic Kacou akifurahi jambo na mfanyakazi wa shirika la kazi Tanzania (ILO) Bw. Emmanuel katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akishangaa jambo na wafanyakazi wenzake.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou na Mwakalishi wa UNESCO Tanzania Bi. Vibeke Jensen.
Ulifika wa kati wa msosi na watoto walitangulia na baadae kufuatia wakubwa.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou akifurahi jambo na Familia ya Usia Nkhoma- Ledama.
Familia ya Hoyce Temu.
Dkt. Alberic Kacou (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na UN Cares Team Veronica, Beatrice pamoja na Rosemary wa UNHCR. UN Cares Team walikuwa uwanjani hapo kwa ajili ya kupima Afya, kutoa ushauri nasaha pamoja na elimu ya jinsi ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa familia na Wafanyakazi wa UN na Wizara ya Mambo ya Nje walishiriki katika wiki ya umoja wa mataifa kusheherekea miaka 67 ya kuzaliwa kwa shirika hilo.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou katika picha ya pamoja na Vijana wa YUNA.
Hoyce Temu akizungumza jambo na Vijana wa YUNA.

No comments:

Post a Comment