Mlipuko mkubwa watokea jijini Nairobi
Mlipuko umetokea katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi na
kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa huku majengo majengo yakiwa yanawaka
moto.
Mlipuko huo umetokea ktika jengo lenye maduka
madogo madogo mengi. Mwandishi wa BBC anasema mlipuko huo umesababisha
bidhaa mbali mbali kama viatu, nguo na vioo vilivyovunjika kusambaa
sehemu yote ya eneo hilo.Picha za Televisheni nchini humo zimeonyesha watu wakikimbia mbali na majengo yaliyo karibu katikati ya mji wa Nairobi.
Kamishna wa Polisi nchini Kenya Mathew Iteere, anasema huenda "hitilafu ya umeme" ndio chanzo cha mlipuko huo, kwa mujibu wa Televisheni ya NTV. Hata hivyo mlipuko huo unaiweka Nairobi katika hali ya wasiwasi.
Kumekuwa na milipuko kadhaa hivi karibuni ndani na nje ya mji huo mkuu huku baadhi ikihusishwa na kundi la wapiganaji wa Al-Shabaab.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia kulikuwa na mlipuko mkubwa na huku vipande vipande vya vioo na vitu vingine vikiwarukia na kujeruhi watu waliokuwa karibu, Gazeti la Nation linaripoti.
Gazeti hilo linaongeza kuwa mlipuko huo umetikisa majengo yaliyo karibu na harakati za kuwahamisha watu zimeanza.

No comments:
Post a Comment