Mwanzilishi na Mmiliki wa Mtandao Wa Facebook Mark Zuckerberg WENT FROM SINGLE TO MARRIED
Mark Zuckerberg and Priscilla Chan have married in a surprise ceremony in Palo Alto
The couple have been together for nine years, but did not reveal their engagement
Guests were pictured turning up at the Palo Alto home on Saturday afternoon
Facebook founder and CEO Mark Zuckerberg updated his status to 'married' on Saturday afternoon.
Food was served family-style and included dishes from the couple's
favorite Palo Alto sushi restaurant. The two had been planning the
marriage for months but were waiting until Chan had graduated to hold
the wedding, the guest said.
The timing wasn't tied to the IPO,
since the date the company planned to go public was a "moving target,"
the guest said. Even after the IPO, Zuckerberg remains Facebook's single
largest
shareholder, with 503.6 million shares. And he controls the company with
56 percent of its voting stock. Rather than his trademark hoodie,
Zuckerberg wore a suit for the ceremony, while his bride wore a
traditional wedding dress.
Zuckerberg took his company public in one of the most anticipated stock offerings in Wall Street history Friday. And Chan graduated from medical school at the University of California, San Francisco, on Monday, the same day Zuckerberg turned 28, the person said.
The couple met at Harvard and have been together for more than nine years, the person said.
Zuckerberg designed the ring featuring "a very simple ruby," according to the person.
The ceremony took place in Zuckerberg's backyard before fewer than 100 guests, including Facebook's chief operating officer Sheryl Sandberg.
The guests all thought they were coming to celebrate Chan's graduation but were told after they arrived that the event was in fact a wedding.
The site, which was born in a dorm room eight years ago, has grown into a worldwide network of almost a billion people.
Zuckerberg founded Facebook at Harvard in 2004.He was selected as Time's Person of the Year in 2010, at age 26. Zuckerberg grew up in Dobbs Ferry, N.Y.
Rais Kikwete apata chakula cha jioni na uongozi wa Jumuiya ya Watanzania DMV
Rais Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa kuamkia leo May 20, 2012
alikaribisha kwa chakula cha jioni uongozi wa Jumuiya ya Watanzania
wanaoishi Washington na vitongoji vyake katika hoteli ya Ritz-Carlton
jijini Washington DC. Uongozi huo, kwa niaba ya wanachama wake,
ulimpongeza Rais Kikwete kwa kuwa mmoja wa Marais wanne wa Afrika
walioalikwa kwa mara ya kwanza katika historia kuhudhuria kikao cha nchi
tajiri duniani zijulikanazo kama G-8 katika makazi ya mapumziko ya Rais
wa Marekani ya Camp David, Maryland. Rais wa jumuiya hiyo Bw. Iddy
Sandaly alisema kwamba mualiko wa kuhuduhuria mkutano wa G-8 alioupata
Rais Kikwete umeendelea kudhihirisha kwamba mataifa makubwa yanaheshimu
msimamo wake katika kuendeleza kilimo cha kisasa na kuondoa njaa
duniani, ambavyo ndivyo vilivyokuwa kauli mbiu ya mkutano wa Camp David.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na waziri wa kilimo Injinia
Christopher Chiza pamoja na Waziri wa kilimo wa Zanzibar Mh Suleiman
Othman Nyanga, pamoja na balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh Mwanaidi
Sinare Maajar. (Picha na Ikulu)
WAZEE WA YANGA WAMCHOMOA MWENYEKITI LOYD NCHUNGA MADARAKANI
Mwenyekiti wa Kamati ya Wazee wa Klabu ya Yanga, Ibrahim Akilimali
akitangaza kumfuta Uenyekiti wa timu hiyo, Lyod Nchunga, wakati wa
mkutano wa wanachamauliofanyika kwenye klabu hiyo, Mtaa wa
Jangwani naTwiga jijini Dar es Salaam.
Wanachama wa Yanga wakishangilia tamko la kumg'oa Mwenyekiti wa Klabu hiyo Lyod Nchunga
Mashabiki wa Yanga ambao si wanachama, wakifuatilia mkutano wakiwa mbali
Tofauti na vikao vingine vya Yanga ambavyo hufanyika katika ukumbi wa
jengo la Klabu hiyo, mkutano huu wa leo unafanyika kwenye Uwanja nje ya
jengo.( Picha kwa hisani ya http://bashir-nkoromo.blogspot.com/)
FLAVIANA MATATA KUTOA MSAADA KUMBUKUMBU YA MV BUKOBA
Mwanamitindo
wa kimataifa Flaviana Matata Amekuja nchini akitokea nchini Marekani
ambako ndiko yaliko makazi yake kwa sasa mahsusi kwa ya ajili ya kugawa
msaada wa VIFAA VYA
KUOKOLEA MAISHA MAJINI (life vest) ikiwa ni miaka 16 tangu meli
ya MV BUKOBA izame ambapo mama yake mzazi alifariki kwenye ajali hiyo
anatarajia kugawa msaada wa vifaa hivyo Jumatatu ya 21 May jijini mwanza
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda Apongeza Uhusiona Uliopo Kati Japan na Tanzania,Ahaidi Kuimarisha Uhusiano wa Kibunge
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimshukuru mwenyeji wake Spika
wa Bunge la Japan Mhe. Takahiro Yokomichi na Ujumbe wake wa Wabunge
wanaounda kamati inayoshughulikia Maswala ya Afrika kwa mwaliko
waliompatia yeye na Ujumbe wa wabunge Kutoka Bunge la Tanzania kuja
Japan kubadilishana uzoefu katika maswala ya Kibunge pamoja na
kuimarisha ushirikiano kati ya mabunge haya mawili. Kulia kwa Mhe.
Makinda ni Mhe. Godfrey Zambi na Mhe. James Lembeli walioambatana Na
Mhe. Spika katika Ziara hiyo. Picha na Owen Mwandumbya
--
Na Mwandishi wetu, Tokyo Japan
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda amesema, Tanzania inajivunia uhusiano mzuri
kati yake na Japan. Akizungumza katika majumuisho ya ziara yake nchini
Japan, Mhe. Makinda amesema, Bunge la Tanzania linaishukuru Serikali
ya Japan na Bunge lake kwa kumwalika yeye na Ujumbe wa Wabunge kutoka
Tanzania kuja kujifunza maswala Mabalimbali ya Kibunge ikiwa ni pamoja
na kukuza demokrasia ya kibunge baina ya nchi hizi Mbili.
Amesema,
Pamoja na Japan kupitia katika hali ngumu ya kulipuliwa kwa miji yake
miwili ya Hiroshima na Nagasaki wakati wa Vita kuu ya Pili ya Dunia,
Matetemeko ya mara kwa mara na mafuriko ya Tsunami, lakaini bado uchumi
wake haujayumba kiasi kwamba sasa waJapan wameweza kusima imara
kuijenga nchi yao.
Mhe.
Makinda amesema Demokrasia safi na Siasa imara za Japan ni mfano tosha
na fundisho kwa Tanzania ambapo hivi sasa katika kuimarisha uhusiano
huu wa Kibunge, mabunge haya mawili yatabadilishana uzoefu katika
maeneo mbalimbali kwa lengo la kuimarisha utendaji kazi wa Bunge la
Tanzania.
“
Nchini yenu mmekomaa sana katika Demokrasia, ikiwa ni pamoja na
uendeshaji wa shughuli za Kibunge, sisi kama watanzania tuna mengi
sana tungependa kujifunza kutoka kwenu, leo mmenialika na ujumbe wangu
kutembelea Bunge lenu, lakini napenda kusema huu uwe ndio mwanzo wa
kuimarisha uhusiano wetu, ikiwezekana hata kamati zetu za Bunge zipate
fursa ya kujifunza kutoka kwenu. Ziara za namna hii zitatusaidia
kupanua uelewa wetu katika maswala ya Kibunge“ alisema Mhe. Makinda.
Katika
kuhakikisha kuwa Bunge la Tanzania linaimarisha uhusiano wake na Bunge
la Japan, Spika Makinda ametoa Mwaliko maalum kwa Spika wa Bunge la
Japan Mhe. Takahiro
Yokomichi kuja kutembelea Tanzania ikiwa ni pamoja na kubadilishana
uzoefu na wabunge wengine kutoka Bunge la Tanzania.
Mhe.
Makinda amesema, Bunge la Tanzania linayo kamati ya Bunge
inayoshughulikia maswala ya mambo ya Nje na uhusiano wa Kimataifa, hivyo
ni fursa pekee ya kamati hii na wenzao kutoka Bunge la japan
kushrikiana kwa karibu kuhakikisha ushirikano huu unakuwa imara na
endelevu.
Akimshukuru
Mhe. Makinda kwa kukubali mwaliko wake, Spika wa Bunge la Japan Mhe.
Takahiro Yokomichi, amesema nchi yake iliichagua Tanzania miongoni mwa
nchi za Afrika hususani Africa Mashariki kutembelea Bunge la Japan kwa
kuwa ni nchi yenye demokrasia safi na siasa zake zinaimarika kila kukich
na kuifanya Japan kuvutiwa na maendeleo hayo katika Bunge la Tanzania.
Mhe.
Yokomichi amesema huu ni mwanzo wa ushirikiano muhimu baina ya Mabunge
haya mawili ambapo Bunge la Japan pamoja na kuwa na kamati maalum
inayoshughulikia maswala ya Afrika, bado kuna haja kwa kamati hiyo
kufanya kazi kwa ukaribu na Bunge la Tanzania kwa lengo la kuangalia
maeneo muhimu ambayo Japan itaisaidia Tanzania.
Hata
hivyo Mhe. Yokomichi ameaidi kuishawishi Serikali yake ya Japan ili
iendelee kutenga fungu kubwa zaidi kwa lengo la kusaidia sekta
mbalimbali za maendeleo nchini Tanzania. Tarari Japan ni mchangiaji
Mkubwa katika sekta mbalimbali za maendelo kwa kiasi kikubwa.
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda na Ujumbe wa wabunge 5 kutoka Bunge la
Tanzania upo Japan kwa mwaliko maalum na Bunge la Japan kujadili na
kuimarisha ushirikiano baina ya Mabunge haya mawili, ambapo kabla ya
kuonana na Mwenyeji wake, Ujumbe huo wa Tanzania ulipata fursa ya
kutembelea maeneo mbali mbali ya utalii nchi Japan ikiwa ni pamoja na
eneo la Mji wa Natori lililokumbwa na mafuriko yaliotokea machi mwaka
jana na Mji wa Hiroshima uliosambaratishwa na Bomu la Atomic wakati wa
vita kuu ya dunia mwaka 1945. Spika na Ujumbe wake wanatarajia kurudi
nchini jumanne wiki hii.
MISS EAST AFRICA 2012- UGANDA
PRESS RELEASE
MISS EAST AFRICA 2012
Washiriki watakaoziwakilisha Nchi zao katika fainali
mashindano ya Miss East Africa 2012 wanaendelea kutangazwa katika mchujo
ulioendeshwa na kampuni ya East Africa gazelle
ya Nchino humo.
Mrembo aliyetangazwa mwishoni mwa wiki ni Miss
Ayisha Nagudi (23) kutoka Nchini Uganda atakayeiwakilisha
Nchi hiyo katika fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012.
Miss Ayisha Nagudi ana urefu wa 1.82m ni mwanafunzi wa mwaka pili
katika chuo kikuu cha Makelele jijini Kampala, ambapo anasomea degree ya
Education
Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 ambazo
huandaliwa na kumilikiwa na Kampuni ya Rena
Events Ltd, zitafanjika tarehe 07 mwezi September mwaka huu jijini Dar es
salaam ambapo zitashirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi,
Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion,
Comoros, Seychelles, na Mauritius.
No comments:
Post a Comment