TAASISI YA WANAFUNZI WANAOSOMA SHAHADA YA KWANZA YA SOSHOLOJIA YA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOMSSO) YAPATA VIONGOZI WAPYA LEO MCHANA
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Kutoka
Mwaka wa 1 alipokua akitoa maelekezo ya nini kifanyike kabla ya Zoezi
la Kupiga kura na Kutangaza washindi
Mgombea wa Nafasi ya Mwenyekiti
katika taasisi ya wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya
Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) Bw Edgar Kelvin ambaye anasomma mwaka
wa 2 alipokua akinadi sera zake kabla zoezi la kupiga alijaanza
Mgombea wa pili wa nafasi ya
Mwenyekiti katika taasisi ya Wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya
Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) Bi Loyce Haule ambaye
anasoma mwaka wa 2 akinadi Sera zake
Mgombea wa Tatu wa Nafasi ya
Mwenyekiti katika taasisi ya Wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya
Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) Bw Mwakindaga Emmanuel
ambaye anasoma mwaka wa 2 akinadi sera zake
Mgombea Wa Nafasi ya Makamu
Mwenyekiti katika taasisi ya Wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya
Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) Bw Mtono Juma ambaye
amepita bila kupingwa kutoka na kuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo na ni
mwanafunzi kutoka mwaka wa kwanza
Mmoja wa Wanafunzi Kutoka Mwaka wa 3
Sophia Mkingiye akiuliza Maswala mara baada ya Wagombea kumaliza kunadi
sera wakati walipokua wakiomba kura kwa wajumbe na wanachama
Mwanafunzi wa Mwaka wa 2 ambaye
anasoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma Bi
Hadija Hassan alipokua akiuliza swali wakati kwa wagombea wa nafasi ya
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma shahada ya Kwanza ya
Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma Wakati Wa Uchaguzi wa Kuwachagua
Viongozi wapya wa Nafasi mbalimbali Katika Taasisi hiyo Mchana wa Leo
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma Shahada
ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma waliohudhuria katika
uchaguzi wa kuchagua viongozi wa taasisi ya Wanafunzi wanaosoma Shahada
ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) katika
uchaguzi uliofanyika ndani ya Chuo Kikuu Cha Dodoma mchana wa leo
Zoezi la Kuesabu kura likiendelea hapo
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Bw
Emmanuel Misungwi Alipokua akitoa Shukrani wa wanachama na wadau wa
taasisi hiyo Kwa Kipindi Chote alichokua madarakani kwa mazuri na mabaya
ambayo taasisi imepitia na kushukuru kwa wanachama kushiriki zoezi la
kupiga kura na kupata viongozi wapya wa Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma
Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO)
Baadhi ya Viongozi wapya wakiwa
katika picha ya pamoja na viongozi waliomaliza muda wao leo mara baada
ya zoezi la kupiga kura kumalizika na hatimaye kuwapata viongozi wa
taasisi ya wanafunzi wanasoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo
Kikuu Cha Dodoma mchana wa leo
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya
Chuo Kikuu Cha Dodoma aliyemaliza muda wake leo Mh Emmanuel Misungwi
(Katikati) Akiwa katika Picha ya Pamoja na Mwenyekiti mpya wa Taasisi
hiyo Mh Edgar Kelvin (Wa kwanza kulia) na Aliyekuwa Mwenyekiti Wa
UChaguzi Wa Kwanza Kushoto
FINA REVOCATUS AIBUKA KIDEDEA NA KUWA REDD'S MISSS IFM 2012
Washiriki walioingia kwenye tano Bora.
Mshindi wa Redd's Miss IFM 2012,Fina Revocatus (katikati) akiwa na Mshindi wa Pili,Jane Augustino (kushoto) na wa Tatu Theresia Issaya muda mfupi baada ya kumalizika kwa shindano lao hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Hoteli ya Blue Peal,Ubungo Jijini Dar.
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva,Diamond akifanya vitu vyake wakati wa onyesho hilo la urembo lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Hoteli ya Blue Peal,Ubungo Jijini Dar.
RAIS KIKWETE KUFUNGUA MKUTANO WA AFDB AMBAO UTAGARIMU BILIONI 12
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano wa (AFDB) Bw. Ngosha
Magonya katikati akiongea na waandishi wa habari mapema leo jijini
Arusha.
Baadhi ya wanakamati wa kamati ya maandalizi ya mkutano wa AFDBwakiwa katika viwanja vya AICC jijini Arusha leo.
NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE-ARUSHA
Benki ya maendeleo ya
Afrika (AFDB)inatarajia kutumia kiasi cha Shilingi bilioni 12 katika mkutano
wake unaoanza Jumatatu jijini Arusha na kufunguliwa na Raisi Jakaya Kikwete huku kiasi cha fedha hizo zikitumika kukarabati
Kumbi mbalimbali za jengo la Kimaitaifa la ukumbi wa AICC kwa kuwa baadhi ya
kumbi za jengo hilo zinaonekana kupitwa na wakati kutokana na utandawazi uliopo
kwa sasa ndani ya nchi zilizoendelea
Akizungumza jijini hapa na waandishi wa habari mwenyekiti wa
kamati ya kitaifa ya mkutano wa benki ya AFDB kwa mwaka 2012 Bw Ngosha Magonya ambapo alisema kuwa mkutano huo utakuwa na
faida kubwa sana
Alifafanua kuwa kupitia mkutano huo ambao utaanza Jumatatu ijayo
utakuwa na faida kubwa sana kwa jiji la Arusha kwa kuwa hata kiwango cha uchumi
kitaaimarika sana kwa kuwa wageni mbalimbali kutoka katika maeneo ya nchi
mbalimbali duniani watabadilishana hata uzoefu
“kwa kipindi hiki ambacho kuna mikutano ndani ya jiji la
Arusha tunatarajia kuwepo na utoafuti wa khali ya juu sana hasa katika mchakato
wa uchumi na kwa hali hii pia tunatarajia hata kufanya maendeleo
mbalimbali ikiwemo kufanya marekebisho
kwa jengo la kimataifa la AICC”alisema bw Magonya
Katika hatua nyingine alifafanua kuwa mbali na kuweza kuimarisha
uchumi wa mkoa wa Arusha pia wanatarajia kutumia fursa mbalimbali za
kuhakikisha kuwa wanakutanisha wafanyabiashara mbalimbali huku malengo yakiwa
ni kuendeleza uchumi kwa walengwa.
Pia alifafanua kuwa mbali na kuweza kuwasaidia
wafanyabiashara hao katika michakato ya kukuza uchumi pia benki hiyo ina
mikakati mbalimbali ya kuendeleza barabara ambazo zitaweza kutumika kama njia
ya mawasiliano hapa Tanzania hali ambayo nayo itachangia kwa kiwango kikubwa
sana hata kuimarisha uchumi wa nchi ya Tanzania
Aliongeza kuwa hapo awali benki hiyo ilikuwa imeshajenga
barabara ya Arusha –Namanga kwa sasa ana mpango wa kujenga barabara ya Arusha –
Holile ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro hali ambayo itachangia sana maendeleo hasa
ya mawasiliano
Alimalizia kwa kusema kuwa wafanyabiashara hasa wa mkoa wa
Arusha wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatumia vema fursa za mkutano huo ili
kuweza kuimarisha biashara zao za kila siku.
TAIFA KATIKA TASWIRA:Marais wastaafu wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi (kulia), Benjamin Mkapa (kushoto), Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume (katikati) sambamba na marais wengine wakiwasili kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini
Marais
wastaafu wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi (kulia), Benjamin Mkapa
(kushoto), Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume (katikati)
sambamba na marais wengine wakiwasili kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha
Witwatersrand, Johannesburg, Afrika Kusini kwa ajili ya kuhudhuria
Mkutano wa kujadili maendeleo ya matumizi ya nishati, Karne ya 21 kwa
nchi za Afrika. (Na Mpigapicha Wetu).
WANAFUNZI WA CHUO CHA SAYANSI YA COMPUTA NA TEKNOLOGIA YA MAWASILIANO WAANZA KAMPENI ZA UCHAGUZI
hizi ndizo barabara za majengo ya hosteli za chuo hicho ambapo makundi
ya watu mbalimbali hupita kwa kuimba nyimbo za harambee huku wakipiga
kampeni
baadhi ya kundi la mgombea wa urahisi akipita huku akiwapunga mkono wa
salamu kwa wanafunzi waliokuwa wakimuangalia na kumshabikia
msafara huu ulipambwa na nyimbo za kishujaa na mchakamchaka kwa mbaaaali
walihakikisha wanapita bweni baada ya bweni wakisaeeema mchague GEORGE kwani anafaa:habari picha na (ZE JOJO)
TAIFA KATIKA TASWIRA:MSHITAKIWA(John Mnyika) na MSHITAKI(Hawa Nghumbi) WAKIBADILISHANA MAWAZO MAHAKAMANI
Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya Chadema, John Mnyika(Kushoto) akiwa na
aliyekuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi Mkuu
2010,Hawa Nghumbi, wakati wakisubiri hukumu, katika Mahakama Kuu Kanda
ya Dar es Salaam, kuhusu kesi ya kupiga matokeo yaliyompa ushindi
Mnyika iliyofunguliwa na Hawa Nghumbi kwenye mahakama hiyo.
Mwanamke Mkazi wa Rufiji Ajeruhiwa Mguu Alipokua Akipambana na Mamba
Mwanamke
Mkazi wa Rufiji, Khadija Boma (40), kifanyiwa tiba na Muuguzi
Geraidina Amani juzi katika wodi 2 ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa
Muhimbili (MOI), Dar es Salaam, baada ya kujeruhiwa mguu alipokuwa
akipambana na Mamba katika Mto Kipoka juzi, Rufiji. Mama huyo ambaye
amekatwa mguu wa kulia aliong'atwa na Mamba, kabla ya kuokolewa na
wananchi, alipambana naye huku akiwa na mtoto mgongoni.Picha na Khamis
Mussa
TANZANIA BEGA KWA BEGA NA UNDP KUJENGA AFRIKA YENYE UHAKIKA WA CHAKULA.
Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa UNDP nchini Tanzania Dk.
Alberic Kacou akizungumza kwa niaba ya UNDP kuhusiana na kuzinduliwa kwa
Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012 ambapo amesema huu sasa ni wakati
kwa nchi za Afrika haswa zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara kujenga
mazingira ya kuelekea mustakabali wenye uhakika wa chakula.
Mshauri
wa Uchumi UNDP Bw.Amarakoon Bandara akifanya 'presentation' ya Ripoti
hiyo. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic
Kacou, Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Mbene na Mkurugenzi wa UNDP
Tanzania Bw. Phillipe Poinsot.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Mbene na Mratibu Mkazi wa Umoja
wa Mataifa Tanzania, Dk. Alberic Kacou (kulia) wakifuatilia maoni ya
Uchambuzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012 kutoka kwa Maprofesa wa
Vyuo vikuu nchini.
Dr.
John Mduma akifanya majumuisho ya nini kifanyike kukabiliana matatizo
ya uhaba wa chakula yanayolikabili bara la Afrika na Afrika Mashariki.
Profesa Joyce Kinabo wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine akieleza uhifadhi wa Chakula kwa ajili ya matumizi ya baadae
Baadhi ya Maofisa wa Umoja wa Mataifa na Wadau wa Serikali wakichangia maoni yao kuhusiana na Ripoti hiyo.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Membe (MB) akisoma hotuba wakati
wa hafla ya Uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012. Kushoto ni
Mkurugenzi wa UNDP Tanzania Bw. Phillipe Poinsot.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Mbene (MB) akikata utepe kuzindua
rasmi Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa
Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou.
"Sasa
imezinduliwa rasmi" Mgeni rasmi Mh. Janet Mbene na Dk. Alberic Kacou
wakionyesha Ripoti hiyo kwa wageni waalikwa na waandishi wa habari.
Baadhi
ya Wageni waalikwa wakipitia Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012
kuelekea kwenye Mustakabali wenye uhakika wa Chakula kwa nchi za Afrika
iliyozinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam
Bara
la Afrika ikiwemo Tanzania limeshakumbwa na matukio kadhaa ya
kukabiliwa na uhaba wa chakula, uliokwenda sambamba na matukio ya watu
wengi kupoteza maisha haswa Kusini mwa jangwa la Sahara na Ukanda wa
Sahel eneo la Afrika Magharibi.
Hali
hiyo imekuwa moja ya changamoto kubwa inazozikabili serikali za mataifa
hayo ambapo yanapambana ili kuitatua ili kila mwananchi barani Afrika
aweze kufurahia kukua kwa uchumi.
Akitoa
hotuba wakati akizindua rasmi Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012 leo
jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Membe (MB) amesema
kwa muda mrefu sura ya eneo la nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa
la Sahara imekuwa ni ya njaa ya kukithiri, ambapo zaidi ya mtu mmoja
katika kila waafrika wane wana tatizo la upungufu wa lishe.
Amesema
Ripoti hiyo inaonyesha kuwa pamoja na ukweli kwamba baadhi ya nchi
zinazokuwa kwa kasi kiuchumi katika kipindi cha miaka kumi ziko Afrika,
lakini bado hali ya maisha ya waafrika ni duni.
Awali
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa UNDP nchini Tanzania
Dk. Alberic Kacou alisema bara la Afrika limejaliwa kuwa na ardhi yenye
rutuba, maji ya kutosha na hali nzuri ya hewa kwa kukuzia mazao, lakini
swali la kujiuliza ni kwanini bado kuna uhaba wa chakula.
Hata
hivyo Dk. Kacou ametoa matumaini kuwa bara la Afrika bado lina uwezo wa
kujijengea mazingira ya kuwa na akiba ya kutosha ya chakula kwa kipindi
kijacho.
Ripoti
hii ya Kwanza ya Maendeleo ya Afrika inasema kwamba ongezeko endelevu
katika uzalishaji kwenye kilimo kunalinda haki ya chakula na uwezo wa
watu kupata chakula.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI CHAKULA CHA JIONI KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MJINI BOTSWANA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mama Asha Bilal, wakiwasili kwenye ukumbi wa tafrija ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Botswana Lt. General Seretse Khama, kwa viongozi wakuu wa Nchi za Afrika waliohudhuria mkutano wa siku mbili kuhusu maendeleo endelevu ya Bara la Afrika Nchini Gaborone Botswana, jana.
RAIS KIKWETE APOKEA UJUMBE MAALUM KUTOKA KWA RAIS ROBERT MUGABE WA ZIMBABWE
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akipokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais
Robert Mugabe wa Zimbabwe uliowasilishwa na Waziri wa nchi ofisi ya Rais
Bwana, Sidney Sekeremayi, Ikulu ndogo mjini Dodoma leo asubuhi.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Bwana Sidney
Sekeremayi, ambaye ni mjumbe maalumu wa Rais Robert Mugabe Ikulu mjini
Dodoma leo asubuhi. Picha na Freddy Maro
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad Akabidhi Bendera Ya Zanzibar Watoto Wanaowawakilisha Watoto Wenzao Mayatima Wakiwa na Viongozi Wao Wanaokwenda nchini Uturuki Kuiwakilisha Zanzibar
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad
akiwakabidhi bendera ya Zanzibar, Watoto wanaowawakilisha Watoto wezao
Mayatima wakiwa na Viongozi wao wanaokwenda nchini Uturuki kuiwakilisha
Zanzibar katika Kongamano la Kimataifa la Kuadhimisha Siku ya Watoto
Yatima litakalofanyika mjini Istambul Uturuki kuanzia tarehe 28/05 hadi
03/06/2012. na kuwajumuisha Watoto wanaotoka Nchi mbalimbali Nduniani
kushiri katika Kongamano hilo.Picha na Salmin Said,-Ofisi ya Makamu wa
Kwanza wa Rais Zanzibar
Waumini wa madhehebu ya Hindu kutoka Tanzania, Kenya, Afrika Kusini, Botswana, India na Uingereza wakiandamana kwenye mitaa mbalimbali ya Jiji la Arusha
Waumini wa
madhehebu ya Hindu kutoka Tanzania, Kenya, Afrika Kusini, Botswana,
India na Uingereza wakiandamana kwenye mitaa mbalimbali ya Jiji la
Arusha kuashiria ufunguzi wa hekalu lao la Swaminarayan Mandir jana.
(Picha na Marc Nkwame).
No comments:
Post a Comment