WASHIRIKI WA REDDS MISS CHANG'OMBE HAO JIANDAE KUJUA NANI ATAIBUKA KIDEDEA
Mashindano
ya kuwania taji la Redds Miss Tanzania 2012 yanazidi kupamba moto kwa
ngazi za vitongoji nchini kote huku vitongoji kadhaa vikiwa tayari
vimesha fanya mashindano yake na vingine vikiendelea na maandalizi.
Wakati
wiki hii Mashindano hayo yakitraji kufanyika katika Vitongoji vya
Kurasini Jijini Dar es Salaam tayari Wanyange wanaowania taji la Redds
Miss Cha'gombe 2012 nao wapo katika mazoezi tayari kwa fainali zao
zitakazo fanyika mapema mwezi ujao.
Pichani
ni warembo wa Chan'gombe wakiwa katika picha ya pamoja iliyopigwa muda
mfupi baada ya kumaliza mazoezi yao Mei 22,2012 katika ukumbi wa TCC
Chan'gombe jijini Dar es Salaam.
Warembo hao 11 wanataraji kupanda jukwaani mapema mwezi ujao kuwania taji hilo na kuwania tiketi ya kushiriki Miss Temeke 2012.
Chanzo: FATHER KIDEVU BLOG
Mkazi wa Arusha ashinda piki piki bahati nasibu ya Simba
Mwandishi wetu
SHABIKI
wa timu ya soka ya Simba mkoani Arusha, Abubakar Hamis ameibuka kidedea
katika droo ya bahati nasibu katika kampeni ya changia simba
inayoendeshwa kwa ushirikiano baina ya Kampuni ya Push Mobile Media na
klabu ya Simba.
Katika
bahati nasibu hiyo Hamis ambaye ni dereva taxi amejinyakulia zawadi ya
pikipiki yenye thamani ya zaidi ya shilingi milion tatu.
Kwa
mujibu wa Meneja Kampeni wa Simba sms, Talib Rashid shabiki huyo ni
miongoni mwa mashabiki zaidi ya 40 wa klabu hiyo kongwe hapa nchini
waliojishindia zawadi mbalimbali ikiwamo pesa taslimu.
"Droo
kubwa itafanyika Julai na mshindi atajinyakulia bajaji," alisema Rashid
na kuongeza mashabiki wanatakiwa kuandika neno Simba na kutuma kwenda
15678 kuingia katika bahati nasibu hii.
Afisa
Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema ushindi wa shabiki huyo ni
uthibitisho tosha kwamba mashabiki wao wanashinda katika bahati nasibu
hiyo.
"Naomba
wanachama na mashabiki wetu wajitokeze kushiriki katika bahati nasibu
hii kwani ni moja ya kuichangia klabu ya Simba iweze kujiendesha na
kufanya vizuri zaidi ndani na nje ya Tanzania," alisema Kamwaga.
Mshindi
atazawadiwa zawadi yake ndani ya wiki mbili kuanzia sasa na kampuni ya
Push Mobile Media itagharimia gharama za usafiri na kulala wakati wa
kuja hapa jijini.
Alisema kuwa kwa sasa wamebakiza piki piki moja na bajaj ambazo drow yao itachezeshwa siku moja
January Makamba Atembelea Vodacom
Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba akilakiwa
na Mkuu wa Mahusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Joseline
Kamuhanda. Makamba alitembelea makao makuu ya Vodacom katika ziara ya
kujifunza shughuli za kampuni hiyo. Katikati ni Meneja wa Mahusiano ya
Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba
akizungumza na watendaji wakuu wa kampuni ya Vodacom (hawapo pichani)
wakati alipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es salaam
katika ziara maalum ya kujifunza shughuli za mawasiliano nchini. Kulia
na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza.
Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi an Teknolojia January Makamba
akikaribishwa makao makuu ya Vodacom Tanzania na Ofisa Mkuu wa
Mahusiano na Mauzo kwa Wateja Wakubwa waVodacom Tanzania Mwamvita
Makamba. Naibu Waziri Makamba alifanya ziara ya utambulisho Vodacom na
kukutana na Uongozi wa kampuni hiyo.
Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba na
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza wakibadilishana
uzoefu kabla ya Naibu Waziri kufanya mazungumzo na watendaji wakuu wa
Vodacom Tanzania alipofanya ziara ya utambulisho makao makuu ya kampuni
hiyo jijini Dar es salaam.
Airtel Sasa Yaja na Viwango Vipya na Nafuu Vya Kupiga Simu Kwa Wateja Wake Wakiwa Zanzibar
Meneja
uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akifafanua jambo
kwawaandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa viwango
vipya nafuu vya mawasliano kwa wateja wa Airtel walioko zanziba (unguja
na Pemba) ofa hiyo itajulikana kama Airtel Nusu shilingi na
itawawezesha wateja wa Airtel kuongea kwa Gharama nafuu kuanzia saa 12
asubuhi hadi saa 4 usiku kwa NUSU shilingi tu kwa sekunde , na kuanzia
saa 4 usiku hadi 11.59 asubuhi ni ROBO shilingi tu kwa sekunde
Airtel-Airtel Pia wateja watafaidika na kupata huduma ya Internet bure
usiku, wapili kushoto ni Meneja Mauzo wa Airtel kanda ya Pwani Bi
Aminata Keita.
Wakwanza
kushoto ni meneja Mauzo wa Airtel Zanzibar Hagai Samson na Meneja
uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando wakifafanua jambo
kwawaandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa viwango
vipya nafuu vya mawasliano kwa wateja wa Airtel walioko zanziba (unguja
na Pemba) ofa hiyo itajulikana kama Airtel Nusu shilingi na
itawawezesha wateja wa Airtel kuongea kwa Gharama nafuu kuanzia saa 12
asubuhi hadi saa 4 usiku kwa NUSU shilingi tu kwa sekunde , na kuanzia
saa 4 usiku hadi 11.59 asubuhi ni ROBO shilingi tu kwa sekunde
Airtel-Airtel Pia wateja watafaidika na kupata huduma ya Internet bure
usiku, wakwanza kushoto ni Meneja Mauzo wa Airtel kanda ya Pwani Bi
Aminata Keita
No comments:
Post a Comment