DROO YA TANO YA PROMOSHENI YA VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO NA SBL, YANGURUMA TENA, MWANZA WAENDELEA KUVUNA ZAWADI
Meneja wa kinywaji cha Serengeti Premium Lager Bw. Allan Chonjo
akizungumza wakati wa kutangaza washindi wa Genereta na Bajaj katika
bahati nasibu ya promosheni ya Vumbua Hazina chini ya Kizibo
iliyofanyika kwenye ofisi za Kampuni hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam
kulia ni Tumainiel Malisa kutoka PWC.
Menejwa mawasiliano wa kampun i ya bia ya Serengeti Imani Lwinga
akizungumza wakati wa kuchezesha bahati nasibu hiyo katikati ni Meneja
wa bia ya bia ya Serengeti Premium Lager na kulia ni Tumainiel Malisa
kutoka PWC
Meneja wa kinywaji cha Serengeti Premium Lager Bw. Allan Chonjo
akizungumza wakati wa kutangaza washindi wa Genereta na Bajaj katika
bahati nasibu ya promosheni ya Vumbua Hazina chini ya Kizibo
iliyofanyika kwenye ofisi za Kampuni hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam
katikati ni Tumainiel Malisa kutoka PWC na kulia ni Abdallah Hemed
kutoka bodi ya mchezo ya kubahatisha.
Zoezi la kukabidhi zawadi kwa washindi
waliojitokeza kushiriki na kushinda zawadi zinazotolewa katika
promosheni ya kipekee ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’ inayoendeshwa na
kampuni ya bia ya Serengeti limeendelea wiki iliyopita katika mikoa ya
Iringa na Mwanza ambapo mshindi wa jenereta na yule
wa bajaj walikabidhiwa zawadi zao katika sherehe zilizohudhuriwa na
umati mkubwa wa watu na kushuhudia SBL ikikabidhi zawadi hizo na kuamsha
hamasa kubwa kwa wapenzi na watumiaji wa biadhaa za SBL.
Asubuhi ya leo droo ya tano ya
promosheni hiyo ‘VUMBUA
HAZINA CHINI YA KIZIBO’ imechezeshwa katika ofisi za kampuni ya bia ya
Serengeti zilizopo maeneo ya Oysterbay jijini na kupata kuhudhuriwa na
waandishi wa habari, wasimamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania,
wadau kutoka ndani na nje ya kampuni hiyo, wakiwemo kampuni ya kuendesha
Bahati Nasibu ya PUSH MOBILE na wahakiki na wakaguzi kutoka PWC-Price
Water House Coopers.
Akiongea
katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa kuchezeshwa kwa droo ya
tano ya promosheni hiyo, Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo bw.
Ephraim Mafuru, amesema “Tumeshakabidhi
jereta nne kwa washindi mbalimbali na zawadi ya pikipiki, bajaj mbili
na gari moja aina ya FORD FIGO ambapo zawadi zote zimeshakabidhiwa kwa
washindi wetu . Hivi karibuni tutasafiri kwenda Mfinga Mkoani Iringa
kukabidhi Bajaj”.
“Naendelea kuwashauri jamii na
watanzania kwa ujumla kwamba promosheni hii ni kwa ajili ya kila
mtanzania mwenye vigezo vya kushiriki kwa hiyo wajitokeze k kwa wingi
kushiriki ili kujaribu bahati kama wenzetu ambao wamejaribu na kupata
zawadi kubwa ambazo hawakutarajia katika maisha yao.” Alisema Mafuru.
Aliongeza kuwa zawadi zinazoshindaniwa
gharama yake ni jumla fedha za kitanzania milioni 780 ikiwemo pesa
taslimu ambazo mshindi anapata papo hapo kupitia matandao wa simu za
mikononi M- pesa. Ikumbukwe kuwa zawadi hizi zinapelekwa hadi pale
mshindi wetu alipo bila yeye kuchangia chochote walakugharamia chochote
ikiwemo usafiri.
Katika droo hii ya tano mshindi ni Isaya
Charles kutoka Igoma mkoani Mwanza ambaye amejishindia Jenereta, wakati
mshindi mwingine Mariam Karumba mwanafunzi wa mwaka wa tatu Chuo Kikuu
cha Saint Agustin pia anatoka mkoani Mwanza amejishindia Bajaj
Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia
bidhaa yake bora kabisa ya Serengeti Premium Lager, Tusker Lager and
Pilsner inaendesha promosheni hii kwa wiki 16 ikiwa na lengo la kuinua
na kuboresha maisha ya wateja wake na watanzania kwa ujumla.
Matukio ya ufunguzi wa mkutano wa AFDB leo jijini Arusha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya
Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB) leo mjini Arusha .
Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Ivory Cost Dr.
Alassane Ouattara (kushoto) akibadilishana mawazo na Rais wa wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dr.Donald Kaberuka(kulia) wakati wa sherehe za
ufunguzi wa mkutano wa 47 wa mwaka wa
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) jana mjini Arusha .
Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)
Dr.Donald Kaberuka akihutubia wakati wa sherehe za ufunguzi wa mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo
ya Afrika (AfDB) jana mjini Arusha .
Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Ivory Cost Dr.
Alassane Ouattara akihutubia wakati wa sherehe za ufunguzi wa mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo
ya Afrika (AfDB) jana mjini Arusha .
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akipongezwa
na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) Dr. Donald Kaberuka (kulia) mara
baada ya kumaliza kutoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo
ya Afrika (AfDB) jana mjini Arusha . Katikati ni Rais wa Serikali ya Jamhuri ya
Ivory Cost Dr. Alassane Ouattara.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa 47 wa mwaka wa
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) wakifuatilia kwa makini hotuba ya
Rais Kikwete wakati wa ufunguzi wa mkutano huo jana mjini Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya
Mrisho Kikwete(kulia) akibadilishana mawazo na Waziri wa Fedha Dr. William
Mgimwa (kushoto) wakati wa sherehe za
ufunguzi wa mkutano wa 47 wa mwaka wa
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) jana mjini Arusha .
Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Arusha
WASAMARIA WEMA TWAOMBWA KUMNUSURU MTOTO HUYU ANAYETAABIKA KWA KUWA NA MATUNDU MATATU KWENYE MOYO
Miguu ya NeemaHali
ya Neema George inazidi kuzorota siku baada ya siku, miguu ikiwa
imevimba, akitaabika katika suala la kula, kuongea na akipata maumivu
makali ya tumbo hasa nyakati za usiku.
Baba
mzazi wa Neema, George Mugunga (kushoto) anasema kuwa mnamo mwaka
2010 mara baada ya hali ya mtoto wake kuzorota alimfikisha katika
hospitali ya Rufaa Bugando kwaajili ya matibabu, lakini mara baada ya
vipimo kufanyika vikaonyesha kuwa moyo wa mtoto wake una matundu
matatu.
Neema
akiwa na mwandishi wa habari hizi Albert G. Sengo aliyefika nyumbani
kwa bibi wa mtoto huyu eneo la Butimba mkoani Mwanza kwaajili ya
kuchukuwa taarifa zaidi.Kutokana
na kiwango kilichotamkwa kuwa kinahitajika kwa ajili ya tiba nje ya
nchi, familia ya mtoto huyu ilikata tamaa kabisa na kukata shauri la
kumpeleka Sengerema kijijini ili akatibiwe na waganga wa kienyeji ndipo
bwana Azizi Bukene (ambaye ni jirani yao) akashauri kuita vyombo vya
habari kwaajili ya kulifikisha kwa umma kwa msaada.
Madaktari
kupitia kliniki aliyokuwa akipata huduma (Bugando) wamesema kuwa
tatizo la neema ni kubwa na haliwezi kupatiwa ufumbuzi hapa nchini bali
linaweza kupata tiba Nchini India kwa makadirio ya gharama ya shilingi
za kitanzania milioni 25.
Pichani mtoto Neema George aliyegundulika kuwa na matundu matatu kwenye moyo.Mtoto Neema George (16) amewaomba wasamaria wema wajitokeze kumchangia fedha ili akapate matibabu ya moyo nchini India.
Familia
ya mtoto huyu inategemea kilimo kama sehemu ya kipato cha kuendesha
maisha ya kila siku, hivyo uwezo wa kufikisha kiwango hicho cha fedha
hata kupata matibabu kwa manufaa ya mtoto huyo kuendelee na masomo ni
ndoto za alinacha.
Nje ya nyumba.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makalla Akabidhi Shilingi Milioni Kumi Kwa Mama wa Marehemu Steven Kanumba Kwa Niaba Ya Serikali, na Kukabidhi Bendera Ya Taifa Kwa Timu ya Taifa ya Mchezo wa Golf
Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makalla
akikabidhi kiasi cha shilingi milioni kumi kwa mama wa marehemu Steven
Kanumba ikiwa ni rambirambi ya Serikali kwa familia.
Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makalla
akikabidhi bendera kwa Timu ya Taifa ya mchezo wa Golf inayotarajiwa
kusafiri kwenda Gaborone Botwsana kwa ajili ya mashindano ya chalenji
ya Afrika kwa upande wa Wanawake.Wapili kushoto ni Mh. Mery Chatanda
(Mbunge).Picha na Benjamin Sawe- Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGA MAFUNZO YA WAKUU WA MIKOA, MAKATIBU TAWALA WA MIKOA NA WAKUU WA WILAYA WA TANZANIA BARA MJINI DODOMA JANA, MEI 30
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
(kulia) akiteta jambo na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati alipofika
katika Ukumbi wa Mtakatifu Gaspar mjini Dodoma jana, kufunga rasmi
Mafunzo ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya
wa Tanzania Bara, yaliyomalizika mjini Dodoma jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisoma hotuba yake wakati akifunga rasmi Mafunzo ya Wakuu wa Mikoa,
Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wa Tanzania Bara,
yaliyomalizika mjini Dodoma jana.
Baadhi
wa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wa
Tanzania Bara, waliohudhuria mafunzo hayo wakimsikiliza kwa makini mgeni
rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya kufunga mafunzo hayo jana.
Baadhi
wa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wa
Tanzania Bara, waliohudhuria mafunzo hayo wakimsikiliza kwa makini mgeni
rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya kufunga mafunzo hayo jana.
Baadhi
wa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wa
Tanzania Bara, waliohudhuria mafunzo hayo wakimsikiliza kwa makini mgeni
rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya kufunga mafunzo hayo jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
(kulia) akiteta jambo na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati akiondoka
katika Ukumbi wa Mtakatifu Gaspar mjini Dodoma jana, baada ya kufunga
rasmi Mafunzo ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa
Wilaya wa Tanzania Bara, yaliyomalizika mjini Dodoma jana.
Wanafunzi Chuo Kikuu wabakwa, walawitiwa
Imeandikwa na Sifa Lubasi, Dodoma
WANACHUO wa Chuo Kikuu cha St John mjini Dodoma, leo wamegoma kuingia
madarasani hadi wawasilishe malalamiko yao kwa Kamanda wa Polisi wa
Mkoa, Zelothe Stephen kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kupigwa
nondo, kuibiwa kadi za benki, kompyuta za mkononi, kulawitiwa na
kubakwa.
Hali hiyo ilisababisha wanafunzi kukusanyika huku wakiwa wamebeba mabango mbalimbali ambayo yalikuwa yakisomeka, ‘Tunaomba ulinzi ili kubaka na kulawitiwa kukomeshwe’, ‘Ulinzi ni haki yetu ya msingi polisi Mko wapi? Tumechoka kuwa wajinga katika jamii yetu na Ulinzi Shirikishi stop crime.’
Baadhi ya wanafunzi hao walilaani vitendo vya wenzao kubakwa na kulawitiwa na kudai kuwa katika siku za hivi karibuni, mwanafunzi wa kiume ambaye anasoma mwaka mwaka wa pili aliibiwa na kisha kulawitiwa hali iliyolazimu alazwe hospitali.
“Kesi kadhaa zimepelekwa polisi lakini hakuna chochote kinachofanyika,” alisikika mwanachuo moja akizungumza kwa jazba.
Walisema kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na wakati mgumu kutokana na kuibiwa vifaa muhimu zikiwemo kompyuta za mkononi hali ambayo hulazimika kuishi kwa hofu.
“Juzi wenzetu wamevamiwa usiku na kuporwa simu tano na laptop tatu sasa tunaona maisha yanakuwa magumu sana kwetu kwani usalama wetu sasa ni mdogo,” alisema mmoja wa wanafunzi hao.
Walisema hali ni mbaya zaidi kwa wanafunzi ambao wanaishi nje ya chuo kwani hata kujisomea nyakati za jioni kumekuwa kwa mashaka kutokana na kuogopa kuvamiwa na vibaka.
Walisema baadhi ya wenzao wanaanza mitihani Juni, hali ambayo inawatia hofu kama wimbi hilo la kuvamiwa na vibaka linaweza hata kupunguza ufaulu mioungoni mwao.
Pia walitaja sababu kadhaa ambazo zinadhaniwa kuwa zinasababisha matukio hayo ni chuo hicho kukosa uzio na hivyo kufanya mwingiliano wa watu na wanachuo kuingia chuoni bila kuwa na utaratibu.
Walisema kundi lisilojulikana limekuwa na kawaida ya kuvamia sehemu ambazo wanachuo wanakaa na baada ya kuiba vitu mbalimbali humalizia kwa kubaka wasichana au kwa kulawiti kama ni mvulana.
Hata hivyo, juhudi za wanafunzi wao kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma hazikufanikiwa baada ya kuelezwa kuwa alikuwa na majukumu mengine ya kikazi, na kutuma mwakilishi wake ambaye ni Mkuu wa Polisi Wilaya, Dominic Mlei na Mkuu Mpya wa Polisi wa Wilaya atakayeanza kazi hivi karibuni, Thadeus Malingumu.
Kwa upande wake, OCD Mlei alisema ulinzi unaanza rasmi leo, kufanya doria maeneo yanayozunguka chuo hicho na maeneo jirani, pia chuo kijenge hosteli za kutosha na kwa kila hosteli za nje na nyumba walizopanga wanafunzi zitakaguliwa kesho na mapungufu ya kiusalama kwenye makazi hayo yataainishwa na wamiliki wataitwa na hosteli zote zitatakiwa kuwa na mageti na ulinzi wa makazi hayo kuboreshwa.
Pia alitaka kuundwa kwa mara moja kwa vikundi vya ulinzi shirikishi.
Hata hivyo, mtumishi wa Chuo hicho, Mzee Muganda alishauri Kituo Kidogo cha Polisi kijengwe Kikuyu na bidii ya doria iongezwe

Source: Habari Leo Mtandaoni
USAFIRI WAANZA KUWA WASHIDA MARA BAADA YA WANAFUNZI UDOM KUPEWA BOOM
Pichani ni Wanafunzi wakigombania Kuwahi nafasi za kukaa katika daladala mapema leo kutokana na Usafiri kuwa Wa Shida
Mara
baada ya wanafunzi wengi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) kupewa fedha
zao za kujikimu hatimaye usafiri wa kwenda mjini umeanza kuwa ni wa
taabu na shida ambapo wanafunzi ukaa kituoni takribani dakika ishirini
hadi thelathini wakisubiri daladala wakati wanafunzi hawakupata fedha
zao hizo usafiri ulikua sio wa kusumbua na daladala zilikua zinasubiri
abiria takribani nusu saa nzima ndio ijaze na kuondoka sasa mambo
yamebadilika kutokana na wanafunzi hao kupata fedha na kusababisha
usafiri kuwa wa Shida sio wakati wa kwenda mjini tu bali hata kurudi
chuo
No comments:
Post a Comment