Friday, June 1, 2012

MWENGE WA UHURU WAKIMBIZWA WILAYA YA NAMTUMBO

Mwenge wa Uhuru ukikimbizwa kuingia katika wilaya ya Namtumbo kuanza kazi ya kuhamasisha shughuli za maendeleo ukitokea wilaya ya Songea.Jumla ya miradi  11 yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 400 imezinduliwa,imewekewa mawe ya msingi na kufunguliwa.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kapteni Honest Mwanossa akichanganya mbolea wakati wa uzinduzi wa shamba la michungwa  kwa kutumia  mbolea vunde kwa kuongeza ubora wa mazao na hifadhi ya mazingira katika kijiji cha Msindo wilaya ya Namtumbo.Shamba hilo lenye ukubwa wa hekari mbili na nusu linamilikiwa na Mzee Venant Haule (mwenye fulana nyekundu).
Mtoto Mezea Seif wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Njalamatata akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru  wakati ulipokuwa katika kijiji hicho wilaya ya Namtumbo kwa kazi ya kuhimiza shughuli za maendeleo  jana.
-Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kapteni Honest Mwanossa akizindua mradi wa kisima cha maji safi ya kunywa kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Utwango wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.Kulia ni Mbunge wa jimbo la Namtumbo Vita Kawawa.
 Raia wa Marekani aliyefahamika kwa jina moja la Penzia akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru wakati uliposimama katika kijiji cha Hanga kutoa ujumbe kwa wananchi kuhusu umuhimu wa wananchi kujiandaa kuhesabiwa ifikiapo Agosti 26,2012.

Na Revocatus A.Kassimba
Afisa Habari
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Ruvuma

No comments:

Post a Comment