Meli hiyo inavyoonekana kwa Nje
Meli hiyo inavyoonekana kwa ndani.
Meli hiyo inavyoonekana kwa Ujumla
---- .
Azam
yaamua kufanya kweli na hivi karibuni meli ya kisasa iko mbioni
kuzinduliwa ambayo ikawezesha watu kwenda na magari yao Zanzibar. Meli
hiyo inauwezo kubeba magari 200, abiria 1500 na Mizigo tani 500.KAMPUNI
ya Usafiri wa baharini ya Azam Marine inatarajia kuzindua meli kubwa
ya kisasa kwaajili ya abiria waendao Dar es Salaam, Pemba na Unguja.
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Hussein Mohamed Said, amesema Julai 15 mwaka
huu meli hiyo yenye urefu wa mita 100 itazinduliwa.
Mohamedi
alisema shida ya usafiri itapungua kwa asilimia kubwa kutokana na meli
hiyo kuwa na uwezo wa kubeba abiria 1500, Mizigo tani 500 na magari
200 ambapo abiria atakae jisikia kwenda na gari lake Zanzibar, Pemba au
Dar es Salaam ataweza kufanya hivyo.
Waziri Mwenye dhamana ya Mawasiliano na Miundombinu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hamadi Masoud, alithibitisha kwamba anataaarifa za ujio wa meli hiyo ambayo alisema kwa kiasi kikubwa itakuwa ni ya kutoa huduma tu na siyakutengeneza faida. Meli hiyo inauwezo wa kwenda kasi ya notkomail 20.
Waziri Mwenye dhamana ya Mawasiliano na Miundombinu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hamadi Masoud, alithibitisha kwamba anataaarifa za ujio wa meli hiyo ambayo alisema kwa kiasi kikubwa itakuwa ni ya kutoa huduma tu na siyakutengeneza faida. Meli hiyo inauwezo wa kwenda kasi ya notkomail 20.
MTOTO WA MBUNGE SITTI MTEMVU AMSAIDIA SH. 500,000 MSICHANA HAPPINESS KAAYA MLEMAVU ANAYEISHI NDANI KWA MIAKA 22
MWANAFUNZI wa Chuo Kukuu cha North Texas cha Marekani, Sitti Mtemvu (kushoto), akitoa msaada wa sh. 500,000 kwa msichana Happines Kaaya (22), aliyezaliwa akiwa mlemavu, katika hafla iliyofanyika Machimbo, Temeke, Dar es Salaam juzi.
Mamake Sitti, Mariam Mtemvu, ambaye ni mke wa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu ampa pole Happiness.
Sitti
ambaye ni mtoto wa kwanza wa Mbunge wa Jimbo la Temeke, akimbusu
Happiness baada ya kutoa msaada huo. Sitti pia ni mmoja wa wakurugenzi
wa Mtemvu Foundation
Mmoja wa wapangaji wa
nyumba anayoishi Happiness na mamake Khadija Msuya akielezea jinsi
wanavyomsaidia msichana huyo mlemavu
Sitti
akitoa msaada mwingine wa sh. 200,000 kwa mtu mwenye ulemavu, Nassoro
Tayari mkazi wa Buza jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kununulia
vipuri vya kutengenezea baiskeli yake.
Na Richard Mwaikenda
MWANAFUNZI wa Chuo Kukuu cha North Texas, Marekani, Sitti Mtemvu, ametoa msaada wa sh. 500,000 kwa msichana Happines Kaaya (22), aliyezaliwa akiwa mlemavu.
Msaada huo alikabidhi kwa mama mzazi wa Happiness, Khadija Msuya katika hafla iliyofanyika kwenye chumba wanachoishi eneo la Machimbo, Temeke, Dar es Salaam juzi.
Siti ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mtemvu Foundation, alisema kuwa ameamua kutoa msaada huo baada ya kuguswa na taarifa za msichana huyo alizozisoma kwenye mafaili ya mfuko huo, zilizopo Temeke, Dar es Salaam.
"Taarifa za msichana huyu, zilinigusa mno kuliko wengine, kiasi cha kuamua kuanza kutoa msaada kwa Happiness aliyezaliwa akiwa mlemavu na analelewa mamake kwa shida,"alisema Siti.
Siti ambaye ni mtoto wa kwanza wa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu, alisema kuwa fedha alizizitoa ni sehemu ya mapato yanayotokana na bajaji zake tatu zinazofanya biashara ya kubeba abiria jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa Bajaji hizo alizinunua kutoka na na fedha alizolipwa baada ya kushiriki kwenye filamu moja nchini Marekani anakosoma.
"Sitoishia kutoa msaada kwa msichana huyo, bali nina imani Mungu akinijalia nitaendelea kutoa msaada kwa yatima na watu wengine wanaoishi kwenye mazingira magumu"alisema Siti.
Mama mzazi wa Happiness, Khadija, alishukuru kupata msaada huo kutoka kwa Sitti, ambao alidai utamsaidia sana kupunguza baadhi ya matatizo yanayomkabili.
Alisema kuwa mtoto huyo ambaye alimzaa akiwa na ulemavu, hana uwezo wa kutembea ambapo hata kula chakula ni vigumu inabidi alishwe na kumsaidia wakati wa kujisaidia.
Alidai kuwa Baba mzazi wa Happiness, Joel Kaaya alimtelekeza yeye na mwanawe ambapo mpaka sasa haijulikani aliko.
Msuya alitoa wito kwa watanzania wengine kujitokeza kusaidia hata ikiwezekana kumnunulia happiness kiti cha magurudumu kitakachorahisisha kumpeleka Hospitali na hata kutoka nje kucheza na wasichana wenzie.
Pia siku hiyo, Siti alitoa msaada mwingine wa sh. 200,000 kwa mtu mwenye ulemavu, Nassoro Tayari mkazi wa Buza jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kununu vipuri vya kutengenezea baiskeli yake.
WAZIRI DR. FENELLA MUKANGARA AFUNGUA MASHINDANO YA UMISETA
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akishuhudia gwaride la maandamano ya wanafunzi wa shule za sekondari wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya shule za Sekondari Tanzania (UMISETA) uliofanyika Kibaha Mkoani Pwani. |
Baadhi ya washiriki wa Mashindano ya shule
za Sekondari Tanzania (UMISETA) wakipita mbele ya mgeni rasmi wakati
wa uzinduzi wa mashindano hayo,uzinduzi huo ulifanyika jana Mkoani Pwani.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt.
Fenella Mukangara akiongea na wachezaji wa Umoja wa Michezo wa shule
za Sekondari Tanzania (UMISETA) (hawapo pichani) wakati alipokwenda
kuzindua mashindano hayo Kibaha mkoani Pwani.Kushoto kwake ni Mkuu wa
Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza na Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Wizara
ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh.Jumanne Sagini.
Baadhi ya washiriki wa Mashindano ya michezo
mbalimbali ya shule za Sekondari Tanzania (UMISETA) wakimsikiliza
kwa makini Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella
Mukangara wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya shule za Sekondari
Tanzania (UMISETA). (Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM)
MWANAMAMA APATA KICHAPO KWA KUDAIWA KUKWAPUA SIMU
Mwanamke ambae jina lake halikuweza kufaamika alijikuta akiambulia
kipigo kutoka kwa wananchi baada ya kutuhumiwa kumchomolea mama mmoja
simu ya kokononi maeneo ya mtaa wa Kongo jijini Dar es salaam.
Hapa akichukua kichapo kutoka kwa wanchi wenye hasira kali
Hapa akikimbia baada ya kichapo kilichomtia adabu.PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE
No comments:
Post a Comment