Mwenyekiti Mtendaji wa
Makampuni ya IPP Dk. Reginald Mengi akifafanua jambo alipokutana na
Mkurugenzi Mkuu wa Mambo ya Nje wa Ufaransa anayeshughulikia Ukanda wa
Afrika na Bahari ya Hindi, Elisabeth Barbier alipomtembelea Ofisini
kwake kwa mazungumzo jijini Dar es Salaam
Taswira Za Mheshimiwa Godbless Lema Akiung'uruma Kwenye Mkutano Wa Hadhara Wa CHADEMA Manzese Jijini Dar es Salaam
Aliyekua
Mbunge wa Arusha Mjini(CHADEMA)Mheshimiwa Godbles Lema Akiunguruma leo
kwenye mkututano wa hadhara Manzese jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Umoja wa Baraza la Vijana wa CHADEMA John Henche(kushoto)akifwatilia kwa makini mkutano wa Chadema Manzese leo
Mkuu wa Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama ya Chadema WilfredLwakatare(Kulia)akifwatilia kwa makini mkutano wa chadema leo
Sehemu ya Umati Mkubwa wa Wananchi
waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa chadema Manzese jijini Dar es
Salaam Leo.Picha na Kurugenzi Ya Habari-CHADEMA
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad Atembelea Chemchem ya Mtopepo Zanzibar
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Dk. Mustafa Ali Garu,
akimuonesha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif
Hamad namna chemchem inavyotiririka, katika chemchem ya Mtopepo
walipofanya ziara ya kutembelea chemchem hiyo jana tarehe 19/06/2012.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na
uongozi wa ZAWA wakiangalia upungufu wa maji katika eneo la Mtopepo
alipofanya ziara ya kutembelea chemchem ya Mtopepo jana. Kuliani kwake
ni Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Mhe. Ramadhan Abdallah
Shaaban.Picha na Salmin Said-Ofisi Ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
---
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema
serikali italazimika kutumia ukali na kuondoa muhali kwa watu
wanaoendeleza vitendo vya uchafuzi wa mazingira hasa katika vianzio vya
maji.
Amesema ni hatari kuona vitendo hivyo vikiendelea huku taifa
likikabiliwa na uhaba wa maji unaotokana na uharibifu wa mazingira
katika vianzio hivyo.
Akiwa katika ziara ya kutembelea vianzio vya maji katika chemchem ya
Mtopepo, Maalim Seif ametahadharisha kuwa ikiwa vitendo hivyo vitaachiwa
kuendelea, kuna hatari ya taifa kuwa na upungufu mkubwa wa maji katika
miaka michache ijayo.
“Inabidi sasa tuwe wakali ili isije ikafika wakati tukawa hatuna maji katika nchi yetu”, alitahadharisha Maalim Seif.
Amesema katika kudhibiti hali hiyo, serikali itachukua kila aina ya
tahadhari kuhakikisha kuwa vianzio vya maji haviendelei kuharibiwa kwa
maslahi ya vizazi vijavyo na taifa kwa ujumla.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya maji
Zanzibar (ZAWA) Dk. Mustafa Ali Garu amesema changamoto kubwa
wanayokabiliana nayo kwa sasa ni uvamizi wa ujenzi karibu na vianzio vya
maji, hali inayopelekea mfumo wa uzalishaji wa maji kubadilika na
kupunguza kwa kiasi kikubwa kiwango cha maji katika chemchem.
Kwa upande wake Mhandisi wa Mamlaka hiyo injinia Said Saleh amesema
baadhi ya chemchem ndogo ndogo zimeanza kutoweka, na kutaka tahadhari
zaidi zichukuliwe katika kudhibiti uvamizi wa vianzio hivyo.
Amefahamisha kuwa karibu nusu ya kiwango cha maji yamepungua katika
kipindi cha miaka kumi iliyopita kutoka katika chemchem za Mtotopepo na
Mwanyanya, huku chemchem ya Mtopepo ikiwa na upungufu mkubwa zaidi.Ziara
hiyo pia imemshirikisha Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Mhe.
Ramadhan Abdallah Shaaban
Na
Na Hassan Hamad
Ofisi Ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
TCRA yawaasa Watanzania kuhamia Digitali
Naibu Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCR), Fredrick Ntobi.
Waanzania
wametakiwa kujiandaa kuhama katika mfumo wa mabadiliko ya anaelojia
kwenda katika mfumo wa digital ambao hadi ifikapo Desemba 31 mwaka huu
matangazo ya anaelojia yatazimwa rasmi.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa Naibu Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Bw. Frederick Ntobi amesema kuwa kuanzia Januari 2013 wananchi hawataweza tena kutumia mfumo uliopo wa
sasa wa anaelojia.
Amesema kuwa ili kwenda na utandawazi uliopo hadi ifikapo januari 2013 dunia nzima itakuwa imehama katika mfumo wa kutumia anaelojia katika luninga zao hivyo ni vema wananchi wakaanza kujipanga mapema ili kuhakikisha kuwa kila mtu anafikiwa na huduma hiyo.
Amengeza kusema ku wa ili mfumo huoi ukamilike ni vema jamii ikahakikisha kuwa lazima inakuwa na kifaa kiitwacho kingamuzi ambacho ndicho kinatumika katika kubadilisha mfumo ili kuweza kufanikiwa katika ubadilishaji huo.
Bw Ntobi ametaja faidsa ya kutumia mfumo huo kuwa ni pamoja kuwa na matumizi bora ya masafa ,kupata huduma bora za ziada mfano kulipia bili ya umeme,kutuma pesa pamoja na kupata intenet pindi uwapo kwenye luininga zao.
Pia alitaja faida ingine kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa ajira kwa kuwa mfumo utachangia kuongezeka kwa makampuni nmengi ya utangazaji.
MPANGO WA NMB FINANCIAL FITNESS WAENDELEA KATIKA SHULE MBALIMBALI
Dotto Mbwana, mfanyakazi wa NMB Muhimbili akigawa
vijarida vya NMB Financial Fitness kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi
Muhimbili mpango huo ni kwa ajili ya kuwaandaa wanafuzi kupata uelewa wa masuala ya kibenki mashuleni
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mtibwa wakijisomea kijarida
cha NMB Financial Fitness wakati wafanyakazi wa NMB Turiani walipotembelea
shule yao
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Muhimbili wakisoma kijarida
cha NMB Financial Fitness
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Muhimbili wakisoma kijarida
cha NMB Financial Fitness
Meneja wa NMB Muhimbili Janeth Shango akiwasisitizia
wanafunzi juu wa kuweka fedha wakiwa na umri mdogo
No comments:
Post a Comment