Wednesday, June 13, 2012

Uhaba wa madawati bado ni changamoto shule za msingi Musoma

Wanafunzi wa shule ya Msingi Etaro wakiwa darasani wakimfuatilia mwalimu.wanafunzi wengi katika shule hii wanakaa chini kutokana na uhaba wa madawati.
Wanafunzi wakiendelea na masomo yao huku wengine wakitumia magoti yao kama sehemu za kuandikia huku wakiwa wamekaa chini.
Uhaba wa madawati katika shule za msingi na sekondari umeendelea kuumiza vichwa vya wapenda elimu pamoja na wazazi kwa ujumla nchini.
 
Upungufu wa madawati katika shule za msingi umeendelea kudidimiza kiwango cha elimu nchini huku ukichangia kuongezeka kwa utoro kwa kusababisha wanafunzi wengine kukata tamaa ya kusoma na mazingira ya shule kwa ujumla ambayo si rafiki kwao.

Matokeo ya wanafunzi kukaa chini husababisha wanafunzi kuandika wakiwa wameinama na wengine hata kulala kifudi fudi na wengine kuchuchumaa na hivyo kushindwa kuandika vizuri na pia kuchoka mapema.Hali hii kupelekea matokeo mabaya nyakati za mitihani hasa ya kitaifa.
Hali halisi ndiyo hii wilayani Musoma vijijini
Wanafunzi wengine wakiyageuza madawati mabovu angalau wapate sehemu ya kukaa
Wengine wanatumia viatu vyao kukalia, na wasio na viatu wanakaa kwenye vumbi.Picha Na Haki Elimu

Kaloleni Sekondari: Shule ya kata inayoonesha njia mkoani Arusha

 Ile dhana ya kwamba shule zote za kata ziko katika mazingira magumu na hazifanyi vema katika maendeleo ya elimu siyo inaanza kupingwa kwa vitendo,utafiti uliofanywa na mwandishi kutoka HakiElimu mkoani Arusha umegundua kuwa ingawa shule nyingi za kata hazifanyi vyema na kukabiliwa na changamoto lukuki, kuna baadhi ya shule za sekondari za Kata ambazo zina maendeleo mazuri kitaaluma kushinda hata zile shule Kongwe za Serikali na Shule nyingi za binafsi.

Mfano wa shule za kata zinazofanya vema ni shule ya sekondari ya kata ya Kaloleni iliyoko wilayani Arusha. Shule hii ilianzishwa mwaka 1998 ni moja ya shule zinazofanya vema kielimu ambapo katika mtihani wa kitaifa wa mwaka jana wa kidato cha nne , shule hii ilishika nafasi ya 12 kati ya shule 137 za mkoa wa Arusha zilizofanya mtihani huo na kushika nafasi ya 179 kati ya shule  3108 zilizofanya mtihani huo nchini  .Shule hii ilikuwa na jumla ya watahiniwa 179 waliofanya mtihani huo ambapo watahiniwa 15 walipata daraja la kwanza, 17 wakapata daraja la pili, 47 walipata daraja la tatu, 85 wakapata daraja la nne na 15 walifeli kwa kupata daraja 0.
Vibao mbali mbali kuonesha sehemu na huduma mbalimbali shuleni hapo



Baadhi ya magari ya walimu na wageni yakiwa yameegeshwa shuleni hapo kusubiri wamiliki wao wakiwa kazini

Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya sekondari Kaloleni, Mrs Machange M.J
Tofauti na shule nyingine za kata , shule hii ina maabara kwa ajili ya masomo ya sayansi ambapo mwandishi alifanikiwa kutembelea maabara za somo la Fizikia, Kemia na Bailojia. Pia jambo lingine la utofauti ni mazingira ya shule kuwa mazuri ikiwemo sehemu ya kuegeshea magari ya wafanyakazi na wageni ambapo mwandishi aliduwazwa na neema aliyoiona ya eneo hilo tofauti ya shule nyingine za kata zenye mazingira magumu. Hii huenda ikawa ni kutoka na mazingira ya shule hii kuwa katikati ya jiji la Arusha eneo la Kaloleni.
Maabara kwa shule ya sekondari ya Kaloleni si jambo geni kwani zipo maabara za kila somo la sayansi.hii ni maabara maalumu ya elimu ya viumbe (Baiolojia)
Maabara ya Chemistry
Maabara ya Physics
Pamoja na mafanikio hayo, shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mlundikano wa wanafunzi ambapo kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 967 wa kidato cha kwanza mpaka cha nne, huku kukiwa na idadi ndogo ya walimu na kulazimika kuajiri walimu waliohitimu kidato cha sita kuokoa jahazi. Pia shule hiyo ni moja ya shule zilizopokea wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika katika kidato cha kwanza ambapo jumla ya wanafunzi watatu walikuwa na maksi mbaya sana katika mtihani uliotolewa kwa kupata maksi chini ya tano katika mitihani iliyofanywa ya kuhesabu kusoma na kuandika kufuatia wimbi kubwa la wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika nchini kuchaguliwa kujiunga na masomo ya Sekondari jambo ambalo lilipigiwa kelele na wadau mbalimbali likiwemo shirika la HakiElimu. Habari na picha zote na Abraham Lazaro alieyekuwa Arusha

WAREMBO WA MISS DAR INTERCOLLEGE 2012 WATEMBELEA DUKA LA SHEAR ILLUSIONS MLIMANI CITY, DAR

 Baadhi ya Warembo wa Miss Dar InterCollege wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea duka la Shear Illusions lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Warembo wa Miss Dar InterCollege wakiangalia bidhaa mbali mbali zinazopatikana kwenye duka hilo.
Mmoja ya wafanyakazi wa duka la Shear Illusions la Mlimani City jijini Dar akitoa maelezo kwa warembo wa Miss Dar InterCollege.
 Mrembo wa Miss Dar InterCollege akivalishwa saa.
Warembo wa Miss Dar InterCollege wakigawiwa zawadi na mwalimu wao Marlydia Boniface (wa kwanza kulia) ambazo walipewa mara baada ya kutembelea duka la Shear Illusions ambao ni wadhamini wa shindano hilo.

No comments:

Post a Comment