Tuesday, June 19, 2012

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd Afungua Kambi Rasmi Ya Timu ya Soka ya Mkoa wa Kaskazini Unguja


  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiifunga rasmi Kambi ya Timu ya Soka ya Mkoa wa Kaskazini Unguja hapo katika Jengo la Kituo cha Huduma Rafiki Mahonda. Kulia Ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi na Ameir Katibu wa CCM Wilaya na Kaskazini B. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa ZFA Wilaya ya Kaskazini “A” Khamis Kombo.
  Makamu wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi mchango wa Shilingi 700,000/- kwa Mkuu wa Msafara wa Timu ya Mkoa Kaskazini Unguja ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa ZFA Wilaya ya Kaskazini B Omar Ali Khamis. Mchango huo ni kwa ajili ya ununuzi wa Viatu kwa Timu ya Soka ya Vijana wa Mkoa huo watakaoshiriki Mashindano ya Copa Coca Cola Jijini Dar es salaam yanayptarajiwa kuanza Mwishoni mwa Wiki hii.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Wana soka wa Mkoa wa Kaskazini Unguja chini ya umri wa miaka 17 katika hafla ya kuifunga rasmi kambi yao hapo katika Jengo la kituo cha Huduma rafiki Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja. Timu hiyo inatarajia kuwa miongoni mwa wana michezo watakaoshiriki kwenye mashindano ya Copa Coca Cola yatakayoanza Jijini Dara es salaa Mwishoni mwa Wiki hii

MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA JAJI JOSEPH SINDE WARIOBA KUKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI UKUMBI WA KARIMJEE JUMANNE SAA 3:00 ASUBUHI - 7:00 MCHANA


 Jaji Joseph Sinde Warioba
----

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba kesho, Jumanne, Juni 19, 2012 atakutana na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3:00 asubuhi - 7:00 mchana kwa lengo la kuzungumza nao kuhusu kazi ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya.Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, na Wajumbe wake waliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 6 Aprili na aliwaapisha tarehe 13 Aprili mwaka huu. Tume ilianza kazi rasmi tarehe 1 Mei, 2012.

Katika mikutano hiyo, Mwenyekiti wa Tume atafafanua kazi za Tume, kama zilivyoainishwa katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 na namna Tume
inavyozitekeleza.Mkutano wa aina hiyo pia utafanyika mjini Zanzibar katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani keshokutwa Jumatano, Juni 20, 2012, kuanzia saa 3:00 asubuhi kwa Wahariri waliopo Zanzibar. Pamoja na Mwenyekiti wa Tume, katika mikutano hiyo ya wazi kwa Waandishi wa Habari pia watakuwepo Wajumbe wengine wa Tume.
   


Omega S. Ngole,
Principal Information Officer,
Constitutional Review Commission (Tanzania),
Ohio Street,
PO Box 1681,
Dar es Salaam,
Tel: +255 (0) 22 2133425,
Fax: +255 (0) 22 2133442,
Mobile: +255 (00 757 500800
--

Makamu wa Rais Dk.Gharib Bilal Awasili Salama Nchini Brazil kushiriki Mkutano wa Rio +20

  Makamu wa Rais Dk Gharib Bilal
--
Na Happiness Katabazi, Brazil
MAKAMU wa rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Mohamed Grarib Bilal leo mchana yeye pamoja na msafara wake uliwasili salama jijini Rio de Jeneiro nchini Brazil tayari kwaajili  kwaajili ya kuungana na viongozi wa matiafa mengine ulimwengu kuudhulia mkutano wa mazingira duniani unaotambulika kwa jina la Rio+20.
 
Dk.Bilal ambaye amefuatana Waziri wa ofisi yake anashughulikia mazingira, Tereva Uvisa,Mshauri wa rais Jakaya Kikwete mwandamizi katika masuala ya kidiplomasia, Balozi Liberata Mulamula na maofisa wengine waandamizi wa serikali walipokelewa jana na wenyeji wao ambao ni ubalozi wa Tanzania nchini hapa na serikali ya Brazil.
 
Tayari wakuu wa nchi mbalimbali wameishawasili jijini Rio de Jeneiro kwaajili ya kuudhulia mkutano huo wa kihistoaria mbao utaanza rasmi Juni 20-22 mwaka huu.Miongoni mwa ajenda kuu itakayo jadaliwa ni uharibu wa mazingira hususani wa ukataji ovyo wa misitu ambao mwisho wa siku karibu nchi nyingi hivi sasa zimejikuta zikikabiliwa na matito yatabia ya nchi.

Serikali Ya Tanzania Yapokea Faru Watatu Kutoka Uingereza Kwa Ajili ya Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.

Waziri wa Malisili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akipeana mkono na Balozi wa Uingereza nchini. Bi. Dianne Corner mara baada ya balozi kukabidhi faru watatu walioletwa nchini kutoka Uingereza kwa ajili ya Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.

WAKAWAKA PARTY YA EBSS ILIVYOFANYA NDANI YA UKUMBI WA ROYAL VILLAGE DODOMA

 LINEX JUKWAANI
MSANII KWA JINA DITTO AKIPANDA JUKWAANI KUTUPA BURUDANI
 KWENYE WAKAWAKA PARTY





MSANII AENDAYE KWA JINA LA MWASITI AKITUPA BURUDANI KWENYE JUKWAA LA WAKAWAKA PARTY






MSANII AENDAYE KWA JINA LA WAZIRI AKITUPA BURUDANI KWENYE WAKAWAKA PARTY 







NICHOLAS WA COCA COLA, MWASITI, WILLIAM PINGO WA ZANTEL, DITTO,
 MHE. JANUARY MAKAMBA, AWAICHI MAWALLA WA ZANTEL , 
IBRAHIM ATTAS WA ZANTEL NA LINEX WAKIPATA GROUP PICTURE NA
 MHE. JANUARY MAKAMBA


DITTO, MWASITI NA LINEX WAKIWA CLUB 84.Picha Kwa Hisani ya Dina Ismail Blog

RAIS KIKWETE AAPISHA MWENYEKITI MPYA NA MAKAMISHNA WAPYA WA TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI

 Mwenyekiti wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Bw. Cornel Kananila Mtaki akila kiapo
 Kamishna Mary Cresent Massay akila kiapo
 Kamishna Salma Abdi Chande akila kiapo
 Kamishna Evod Paul Mushi akila kiapo
 Kamishna Sauli Herbert Kinemela akila Kiapo
 Kamishna Yahya Kitambazi Msigwa akila kiapo
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Makamishna wapya wa Tume ya Usuluhishi na

TAARIFA YA MSIBA: WILLIAM FOFO MAPUNDA HATUNAYE TENA

Marehemu William Fofo enzi za uhai wake.

Taarifa ambazo zimetufikia hivi punde Ndugu yetu, Rafiki yetu William Fofo maarufu kwa jina la FOFO amefariki dunia usiku huu akiwa nyumbani kwake Tabata.

Taarifa kamili za sababu ya kifo chake bado hatujazipata, pindi tutakapozipata tutawajulisha, kwa sasa taratibu zote inaendelea nyumbani kwake Tabata na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Amana Ilala Dar es salaam.

TAASISI INAYOJISHUGHULISHA NA MAMBO YA UCHUMI YA DELOITTE YAANDA SEMINA YA BAJETI YA AFRIKA MASHARIKI KWA MWAKA 2012/2013

 Baadhi ya washiriki wa semina ya kujadili bajeti ya nchi za  Afrika Mashariki kwa mwaka 2012/13 wakifatilia semina hiyo iliyoandaliwa na  Taasisi inayojishughulisha na mambo ya uchumi ya Deloitte.
 Meneja Mshauri Taasisi inayojishughulisha na mambo ya uchumi ya Deloitte Bw.Frederick Nsemwa,akiongea wakati wa semina ya kujadili bajeti ya nchi za  Afrika Mashariki kwa mwaka 2012/13 wakifatilia semina hiyo iliyoandaliwa na  Taasisi hiyo.
 Baadhi ya washiriki wa semina ya kujadili bajeti ya nchi za  Afrika Mashariki kwa mwaka 2012/13 wakifatilia semina hiyo iliyoandaliwa na  Taasisi inayojishughulisha na mambo ya uchumi ya Deloitte.
 Baadhi ya washiriki wa semina ya kujadili bajeti ya nchi za  Afrika Mashariki kwa mwaka 2012/13 wakifatilia semina hiyo iliyoandaliwa na  Taasisi inayojishughulisha na mambo ya uchumi ya Deloitte.
 Mkurugenzi wa Asasi zisizo za kiserikali Bw.John Olanga akiongea wakati wa semina ya kujadili bajeti ya nchi za  Afrika Mashariki kwa mwaka 2012/13 wakifatilia semina hiyo iliyoandaliwa na  Taasisi inayojishughulisha na mambo ya uchumi ya Deloitte,katikati ni Mwenyekiti wa shirikisho la viwanda Tanzania Felix Mosha na Mkurugenzi mtendaji wa Samaria Groups Jayesh Shah.
 Mtaalam wa Maswala ya Kodi na nishati ya umeme wa kampuni ya Deloitte Bill Page akichangia mada kuhusiana na bajeti ya nchi za  Afrika Mashariki kwa mwaka 2012/13 wakifatilia semina hiyo iliyoandaliwa na  Taasisi inayojishughulisha na mambo ya uchumi ya Deloitte.
Baadhi ya washiriki wa semina ya kujadili bajeti ya nchi za  Afrika Mashariki kwa mwaka 2012/13 wakibadilishana mawazo baada ya semina hiyo kumalizika iliyoandaliwa

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MWANA WA MFALME NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA SAUDIA, PIA MWENYEKITI WA ARIGATOU INTERNATIONAL, PIA NAIBU WAZIRI MKUU WA KENYA IKULU LEO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana naMwana wa Mfalme na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mhe. Abdulaziz Bin Abullah Bin Abdul Aziz Al Saudi leo Juni 18, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifanya mazungumzo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana akimsinidikisa Mwana wa Mfalme na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mhe. Abdulaziz Bin Abullah Bin Abdul Aziz Al Saudi  leo Juni 18, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifanya mazungumzo
Rais Jakaya Kikwete akimsindikiza Naibu Waziri Mkuu wa Kenya ambaye pia ni Waziri wa Serikali za Mitaa Mhe. Musalia Mudavadi baada ya mnaongezi yao Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mchungaji Keishi Miyamoto, Rais wa Arigatou na Mwenyekiti wa Bodi ya Myochikai na Mlezi-Mwenza wa Kongamano la Mtandao wa Kimataifa wa Dini kwa Watoto
(Global Network of Religions for Children)  leo Juni 18, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifanya mazungumzo

No comments:

Post a Comment