SHIRIKISHO LA NGUMI LA KIMATAIFA (IBF) LAMLILIA MAGOMA SHABAN
Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) pamoja na Kamisheni ya
Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) zinamlilia bingwa wa IBF wa mabara na
bingwa wa dunia wa WBU Magoma Shaban.
Magoma aliyefariki
jana katika hospitali ya Bombo jijini Tanga atakumbukwa kwa umahiri
wake kwenye ngumi za kulipwa.
Safari ya Magoma
Shaban kwenye ngumi za kulipwa ilianzia katika uwanja wa Mkwakwani
jijini Tanga mwaka 1998 wakati Onesmo Ngowi akiwa ndio kwanza
alipoteuliwa na Rais wa zamani wa IBF Robert Lee Sr toka Marekani
kuanzisha shirikisho hilo la IBF katika bara la Afrika.
Katika uwanja huo Magoma Shaban alipigana na Joseph Waweru toka
Kenya na kumshinda kwa KO na kutangazwa kuwa bingwa wa IBF katika bara
la Afrika uzito wa flyweight.
Mwaka 2000 Magoma
chini ya kamouni ya Capital Promoters Limited chuini ya mwandishi wa
bahari mahiri bwana Gabriel Nderumaki alipigana na bondia Totim Lukunim
toka Thailand katika ukumbi wa PTA kugombea mkanda wa IBF wa mabara
katika uzito wa Flyweight na kumshinda kwa KO katika raundi ya 4. Huo
ndio ukawa mwanzo wa magoma Shaban kwenye kwenye matawi ya juu katika
ngumi.
Magoma Shaban alipigania ubingwa wa dunia wa WBU nchini Italy
na kumshinda bondia Ferid Ben Jeddou kwa TKO katika raundi ya 6.
Magoma alikuwa ni bondia aliyeing'arisha Tanzania na bara zima
la Afrika katika medani ya ngumi za kulipwa duniani.
Kwa mantiki hiyo
leo IBF imetangaza rasmi kuuita mkanda wa uzito wa Fly aliokuwa
anachezea Magoma kuwa "Mkanda wa Magoma Shaban" katika
mapambano yote yatakayokuwa yanachezezwa katika uzito huu yatajulikana
kama "Ubingwa wa IBF Africa wa Magoma Shaban".
Tunafanya hivi ili kuwaenzi mabondia wanaoleta mchango mkubwa
katika medani ya ngumi na hivyo majina yao kubakia katika kumbukumbu
zetu milele.
Mola alitoa na
Mola ametwa, jina lake lihidimiwe milele. Amin!
No comments:
Post a Comment