ais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete
akimpongeza Bw. Deo Mwanyika, Makamu wa
Rais wa Kampuni ya Barrick Tanzania baada ya kuibuka mchangiaji mkubwa
kwa kutoa dola za Kimarekani laki 5 kwa ajili ya kuchangia taasisi ya
Mkapa Hiv/Aids Foundation Jumanne Juni 5, 2012 usiku katika hoteli ya
Kilimanjaro jijini Dar es salaam. Kushoto ni Rais Mstaafu wa Awamu ya
Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na kulia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu
Mzee Benjamin William Mkapa aliyeandaa hafla hiyo iliyoweza kukusanya
shilingi bilioni 3.2 na kuvuka malengo ya harambee hiyo kwa asilimia
sita
Rais Jakaya Kikwete,
akimkabidhi picha ya kuchora Ofisa Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya UNDI Consulting Group Limited, Bw Philip Makoka
aliyoinunua kwa shilingi milioni 20 wakati wa Harambee ya kuchangia
fedha programu ya Mkapa Fellows inayoendeshwa naTaasisi ya Mkapa
HIV/AIDS iliyofanyika Dar es Salaam kwenye hoteli ya Kilimanjaro Hyatt
Regency jijini Dar es salaam. Kulia ni mchoraji wa picha hiyo, Bwana
Muzu
Rais Dkt Jakaya Mrisho
Kikwete akisindikizwa na Rais Mstaafu wa Awamu
ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kushoto) na Rais Mstaafu wa Awamu ya
Tatu Mzee Benjamin William Mkapa baada ya kuwa mgeni rasmi katika
harambee ya kuchangia Taasisi ya Mkapa HIV/AIDS foundation na kusaidia
kukusanya shilingi bilioni 3.2 nauvuka malengo ya harambee hiyo kwa
asilimia sita.PICHA NA IKULU
MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AAGANA NA BALOZI WA CANADA ALIYEMALIZA MUDA WAKE NCHINI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na
Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Robert J. Orr, aliyefika Ofisini
kwa Makamu Asubuhi ya leo Juni 06, 2012 kwa ajili ya
kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na
kumkaribisha Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Robert J. Orr, aliyefika
Ofisini kwa Makamu Asubuhi ya leo Juni 06, 2012 kwa ajili ya kumuaga
rasmi baada ya kumaliza muda wake nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na
Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Robert J. Orr, aliyefika Ofisini
kwa Makamu Asubuhi ya leo Juni 06, 2012 kwa ajili ya
kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na
kumkaribisha Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Robert J. Orr, aliyefika
Ofisini kwa Makamu Asubuhi ya leo Juni 06, 2012 kwa ajili ya kumuaga
rasmi baada ya kumaliza muda wake nchini. Picha na Muhidin
Sufiani-OMR
ANOTHER DRAW AND TWO MORE LUCKY TANZANIANS WALK AWAY WITH A GENERATOR AND A MOTORBIKE.
Life
changing winnings, life changing Experiences, this is all happening
with the Under the Crown Campaign.
Today for the sixth week
running the lucky draw for
the campaign “VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO” was held at Serengeti
Breweries’ offices in Oyster bay area.
Speaking at the press
conference, the Director of marketing, Mr.
Ephraim Mafuru said, “We have given away
generators, motorbikes and Bajaj’s,
we still have more for you. Two weeks
ago we gave away a brand new vehicle, Ford
Figo and we still have more cars to give away.
We wish to remind all our consumers
to participate in this promotion as it is designed with them in mind”.
He also reminded Tanzanians that to participate one must be above the
age of 18 years and must be eligible to be part of this exciting
promotion that still has about 12 weeks to go.
The Vumbua Hazina
Chini ya Kizibo promotional campaign draw is highly supervised and in
every draw is done in the highest transparency.
The event every week is graced by the members
of the press, the gaming board of Tanzania and other internal and
external stakeholders including PUSH mobile who have supplied the
mechanics of the game and the reputed PricewaterhouseCoopers who ensures
there is no ambiguity at all and that every Tanzanian has a chance to
win.
The campaign
comprises of prizes worth Tshs 780M in
total that include cash prizes
of over 380M .
The cash prizes come directly to your phone via Mpesa and
other prizes are handed over to the winners at their respective regions
at no extra costs including transport etc.
Today the motorbike went
to Vicent Lymo 36 Years from Kibosh Kilimanjaro
region and Deusdedit Njau 22 Years from Kiboroloni Moshi
Kilimanjaro region has
won a generator. Serengeti Breweries
Limited (SBL) through its high quality
premium drinks, Serengeti Premium
Lager, Tusker Lager and Pilsner Lager has been running
this remarkable campaign that is making huge changes to its customers
and Tanzanians in general.
TAARIFA KUTOKA KWA ZITTO KABWE
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
06.06.2012
YAH: VIPAUMBELE VYA KAMBA YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013
06.06.2012
YAH: VIPAUMBELE VYA KAMBA YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013
Ndg. Waandishi wa Habari
Mwaka 2011/2012 Kambi ya Upinzani Bungeni ilitangaza Vipaumbele vyake katika Bajeti Mbadala ambavyo vilikuwa:
1. Kupunguza misamaha ya kodi mpaka 1% ya pato la Taifa kutoka 3%
2. Kupunguza kodi kwenye bidhaa za mafuta ya petrol na dizeli ili kupunguza mfumuko wa bei
3. Kufuta mfumo wa posho za vikao (Sitting allowances).
4. Kupeleka sehemu ya tozo ya ujuzi (Skills Development levy-SDL) kwenye bodi ya mikopo ya elimu ya juu.
Masuala haya pamoja na mengine yalikuwa sehemu ya Bajeti kivuli iliyowasilishwa Bungeni na Kambi ya Upinzani.
Mapendekezo mawili,
(1) Kodi za mafuta ya Petrol na Diseli na
(2) Tozo ya SDL yalikubaliwa na kutekelezwa. Pendekezo la misamaha ya kodi lilikubaliwa lakini Serikali imeshindwa kulitekeleza na pendekezo la kufutilia mbali posho za vikao halikukubaliwa.
Kambi Rasmi ya Upinzani inataka maelezo ya kina ya kwa nini Serikali imeshindwa kutekeleza ahadi yake iliyoitoa Bungeni kwamba misamaha ya kodi itapungizwa mpaka kufikia 1% ya pato la Taifa. Halikadhalika Kambi ya Upinzani inarejea wito wake wa kufutwa kwa Mfumo wa posho za vikao (sitting allowances).
Serikali imependekeza Bajeti ya Tshs. 15trillioni kutoka Tshs. 13 trillion. Hata hivyo ni dhahiri kwamba Bajeti ya 2011/12 ilikuwa ina changamoto kubwa za utekelezaji. Serikali ieleze itawezaje kutekeleza Bajeti ya 15trillioni?
Katika Bajeti Mbadala ya 2012/2013 Kambi ya Upinzani itajikita katika maeneo yafuatayo na kuishinikiza Serikali kuyatekeleza.
1. Kuendelea kushinikiza kupunguzwa kwa misamaha ya kodi mpaka 1% ya Pato la Taifa. Hivi sasa misamaha ya kodi ni sawa na misaada yote kutoka nchi wahisani, Tshs 1.03 trillioni ni sawa na 3% ya Pato la Taifa.
2. Kuelekeza raslimali fedha kwenye maendeleo vijijini hasa kujenga miundombinu kama barabara za vijijini na umeme vijijini.
3. Kuelekeza fedha za kutosha kukarabati Reli ya Kati na kufufua njia za Reli za Tanga, Moshi na Arusha.
4. Kuongeza wigo wa kutoza tozo la ujuzi (Skills Development Levy) ambapo sasa waajiri wote walipe ikiwemo Serikali na mashirika ya umma. Pia kupunguza tozo hili mpaka 4% ambapo 1/3 itaenda VETA na vyuo vya Ufundi na 2/3 itaenda Bodi ya Mikopo ili kukabili changamoto ya mikopo kwa wanafunzi.
5. Kushusha kima cha chini cha kodi ya mapato (PAYE) mpaka 9% ili kuwezesha wananchi wa hali ya chini kubaki na fedha za kutumia na kukuza uchumi.
6. Kuongeza mapato ya ndani na kupunguza mikopo ya kibiashara kwa kuhakikisha mapato ya ndani yanafikia 20% ya pato la taifa, kuongeza nguvu za kisheria na udhibiti ili TRA ikusanye mapato zaidi kwenye kampuni za simu na kwenye shughuli za uchimbaji wa madini, mafuta na gesi.
7. Kutayarisha Taifa kuwa na uchumi wa Gesi.
8. Kupunguza /kufuta kodi kwenye bidhaaa za vyakula kwa muda maalum ili kushusha mfumuko wa bei.
9. Kuweka mfumo mpya wa elimu kwa kushirikisha sekta binafsi katika kutoa elimu kwa ubora zaidi, ikiwemo kuundwa kwa chombo cha Udhibiti wa Elimu(Regulatory authority)
10. Kutoa vipaumbele na unafuu vya kikodi kwa viwanda vya ndani vinavyotumia malighafi za nchni hasa za kilimo na zenye kuongeza ajira kama Korosho,Pamba na Mkonge.
Kambi ya Upinzani itaendelea kufuatilia kwa karibu sana suala la kukua kwa deni la Taifa amabalo limefikia hadi Tshs 22 trillioni na kutaka ukaguzi maalum kuhusu akaunti ya Deni la Taifa.
Kambi ya Upinzani itawekeza kusimamia kwa karibu suala la matumizi yasiyo na tija ya Serikali hasa kwenye magari na posho mbalimbali na Kwamba fedha nyingi zitumike kwa miradi mikubwa ya maendeleo ili kukuza ajira. Halikadhalika namna ya kupta fedha za kutekeleza mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano
Asanteni sana!
…………………………….
Zuberi Kabwe Zitto(Mb)
Waziri Kivulu-Fedha na Uchumi.
WAJASILIAMALI 11,WAKABIDHIWA RUZUKU ZA SAFARI WEZESHWA JIJINI MBEYA
Meya wa
Manispaa ya Mbeya, Athanas Kapunga(kulia) akimkabidhi Rose Maluila
mashine ya
kutengeneza Crips ya kisasa baada ya kufuzu kupata ruzuku za Safari
Wezeshwa,makabidhiano hayo yalifanyika Viwanja vya CCM Iloma Mjini Mbeya
mwishoni
mwa wiki.Katikati ni Meneja wa
Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo
Meya
wa
Manispaa ya Mbeya, Athanas Kapunga(kulia) akimkabidhi Vumilia Mtweve
Viti,Meza,Krti za Bia na Jiko la Kisasa baada ya kufuzu kupata ruzuku za
Safari
Wezeshwa,makabidhiano hayo yalifanyika Viwanja vya CCM Iloma Mjini Mbeya
mwishoni
mwa wiki.Katikati ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo
Meya
wa
Manispaa ya Mbeya, Athanas Kapunga(kulia) akimkabidhi Bahati Mbata
Cherehani za
kisasa baada ya kufuzu kupata ruzuku za Safari Wezeshwa,makabidhiano
hayo
yalifanyika Viwanja vya CCM Iloma Mjini Mbeya mwishoni mwa wiki.Katikati
ni
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo
Meya
wa Manispaa ya Mbeya, Athanas Kapunga(kulia) akimkabidhi Phares Lyimo
Compresor
ya kutengenezea Ngoma za kisasa na mashine ya Welding baada
ya kufuzu kupata ruzuku za Safari
Wezeshwa,makabidhiano hayo yalifanyika Viwanja vya CCM Iloma Mjini Mbeya
mwishoni
mwa wiki.Katikati ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo
Meneja wa
Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akizungumza na
Wajasiliamali,wageni
waalikwa na wakazi wa Mbeya wakati wa hafla ya kukabidhi ruzuku kwa
wajasiliamali wa Safari Wezeshwa katika Uwanja wa CCM Ilomba Mbeya
mwishoni mwa
wiki.
Meya wa
Manispaa ya Mbeya, Athanas Kapunga(kulia) akimkabidhi Hellen Mwanguku
mashine
ya kuwokea mikate baada ya kufuzu kupata ruzuku za Safari
Wezeshwa,makabidhiano
hayo yalifanyika Viwanja vya CCM Iloma Mjini Mbeya mwishoni mwa
wiki.Kushoto ni
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akutana na viongozi wa Kampuni ya Kilimo ya YARA ikulu jijini Dar es Salaam
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika
mazungumzo na viongozi wa kampuni ya kilimo ya YARA ya nchini Norway
inayoshughulika na
uzalishaji wa mbolea wakati walipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam
leo.Kampuni hiyo ina andaa mipango ya kuzalisha mbolea nchini.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya
pamoja na viongozi wa kampuni ya Kilimo ya YARA ya nchini Norway wakati
alipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam leo.(Picha na Freddy Maro-
IKULU) )
Madiwani Wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya wakabidhiwa Piki piki kwa ajili ya utendaji zaidi wa kazi
Picha ya Pamoja ya Madiwani Muda
mchache Baada ya kukabidhiwa Piki piki Hizo
Mkuu wa wilaya Mbozi akimkabidhi
diwani Piki piki
Hizi ndizo piki piki walizo kabidhiwa
Madiwani
Furaha baada ya kukabidhiwa Piki piki
hizo
Mkuu wa wilaya ya Mbozi wa Tatu
kushoto akiongea Kabla ya kukabidhi piki piki
Picha na Mwandishi wetu aliyepo Mbozi
Picha na Mwandishi wetu aliyepo Mbozi
No comments:
Post a Comment