Monday, June 18, 2012

DIAMOND KUPAMBA MISS DAR INTERCOLLEGE 2012


Na Mwandishi Wetu
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Nasib Adbdul ‘Diamond’ anatarajiwa kupamba shindano la kumsaka Miss dar Intercollege 2012 linalotarajiwa kufanyika Juni 22 kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa , uliopo mkabala na chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Mratibu wa shindano hilo Dina Ismail alisema jana kwamba mbali na Diamond, onyesho hilo pia litapambwa na burudani kutoka bendi ya Skylight iliyopo chini ya mshiriki wa Tusker Project Fame mwaka juzi, Anneth Kushaba.
Alisema maandalizi ya shindano hilo yanakwenda vema ambapo warembo 14 watakaoshiriki  wanaendelea na mazoezi katika hoteli ya  The Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam
 “Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania ,”alisema Dina.
Warembo watakaoshiriki shindano hilo  wanatoka vyuo vya  Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time,  Ustawi wa Jamii,  Usimamizi wa Fedha (IFM)  na Chuo Kikuu huria (OUT ambapo taji linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM, huku mshindi wa pili wa mwaka jana, Blessing Ngowi alitinga fainali za Miss Tanzania.
Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda  Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
Shindano hilo limedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s,Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band,Lamada Hotel, Screen Masters,Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Shear Illusions,Grand Villa Hotel, Spoti Kizaa zaa, Clouds Fm na blog za Michuzi, Mamapipiro, Bin Zubeiry,Mtaa kwa Mtaa na Fullshangwe.

WAFANYAKAZI BENKI YA UBA WAKIJIANDAA KWENDA KATIKA MAZOEZI KIGAMBONI AMBAKO PIA WALITOA MSAADA KITUO CHA HOPE FAMILY

Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya UBA wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kwenda kwenye mazoezi Kigamboni jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
Kushoto ni Bw. Rock Meneja mkazi wa benki ya UBA nchini na kushoto ni Victor Meneja wa tawi la benki ya UBA Kariakoo wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakijiandaa pamoja na wafanyakazi wengine wa benki hiyo katika tawi la City Centre Branch Posta,  kwenda Kigamboni ambako walikuwa na mazoezi ya viungo  na baadae walitoa misaada mbalimbali ya kibinadamu ikiwa ni vyakula mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni mbili, katika kituo cha watoto yatima cha cha Hope Family kilichopo Kigamboni jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kutoka kulia ni Jack, Marjory, Asha na Natasha wakipozi kwa picha wakati wakijiandaa kwenda kigamboni kwa ajili ya kufanya mazoezi na kutoa msaada katika kituo cha watoto yatima cha Hope Family kilichopo Kigamboni jijini Dar es salaam.

Mmarekani Chris Wilder Ataipa Tanzania Zawadi ya Kusheherekea Miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika Atakapokimbia Kilometa 1 kwa kila Mwaka wa Uhuru wa Tanganyika/Tanzania

Mmarekani Chris Wilder ataipa Tanzania zawadi ya kusheherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika atakapokimbia kilometa 1 kwa kila mwaka wa uhusru wa Tanganyika/Tanzania. Hii ina maana atakimbia kilometa 50 kusheherekea uhuru wa Tanganyika uliotokean mwaka 1961.

Chris wilder ni Physician Assistant kutoka Annapolis, Maryland Marekani na yuko hapa mjini Moshi kukimbia mbio za 22 za Mt. Kilimanjaro Marathon tarehe 24 Juni. Mbio hizi zitaanzia Moshi Klabu mpaka Rau madukani na kurudi mara tatu. Kutakuwa na mbio za kilometa 42, Kilometa 21, Kilometa 10 na Kilometa 5.

Mbio za Mount Kilimanjaro Marathon zilianzishwa na mama Marie Frances anayetoka katika mji wa Bethesda Marekani mwaka 1991 katika mji wa Moshi baada ya kuombwa na balozi wa zamani wa Tanzania nchini Misri kuja kuanzisha mbio za Marathon ili kuitangaza Tanzania. Kila mwaka jumapili ya mwisho ya mwezi wa sita mbio za Mount Kilimanjaro marathon zimekuwa zinafanyika.

Kwa kutambua mchango wake katika kuutangaza mji wa Moshi tangu mwaka 1991, Manispaa ya Moshi ilimzawadia Marie Frances barabara ya zamani ya Bustani Ale na kuiita Marie Frances Boulevard. Aidha Frances alipewa funguo za Manispaa na kufanywa mkazi wa kudumu wa Manispaa ya Moshi katika shereke zilizofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Moshi mwaka 2009.

Mbio za mwaka huu za Mt. Kilimanjaro marathon zitapambwa na mcheza sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz anayewasili mjini Moshi tarehe 21 mwezi huu tayari kushiriki kwenye mbio hizi maarufu. Miss Lorenz ameshiriki kwenye sinema nyingi kama vile Santorini Blue, Perfect Strangers, The Great Fight na nyingine nyingi.

Chris Wilde ni mkimbiaji wa mbio za marathon za Ultra Marathon na mwaka jana alikimbia kilometa 100. Kwa kukimbia kwake kilometa 50 na kuizawadia Tanzania Wilde ataweka historia ya mtu aliyekuja kupanda mlima Kilimanjaro na kukimbia kilometa 50 kama zawadi ya nchi hii tukufu.

------
The American Physician Assistance from Annapolis, Maryland has great passion for running marathons. Chris Wilder 40 years old which is currently climbing Mount Kilimanjaro will give Tanzanian Independence anniversary a special gift by running one kilometer for every year that Tanganyika/Tanzania is celebrating. That will make it 50 kilometer given Tanganyika. Tanzania 50th Anniversary of Independence which is 50 years old.

Chris Wilde and a couple of other USA citizens, Europeans and other runner are taking part on the “50th Anniversary Mount Kilimanjaro Marathon” that is taking place in Moshi this coming Sunday 24th, of June. Wilde took part in the Ultra Marathon and run a perfect 100 meters in June 2012. 

Mount Kilimanjaro Marathon will kick start at the Moshi Country Club to Rau Shopping Centre. Mount Kilimanjaro which is turning 22nd this coming Sunday was founded by Marie Frances from Bethesda, USA in 1991. Frances came to Tanzania on the invitation of former Tanzania ambassador in Egypt after she successfully started Pyramid Marathon and Miss Universe.

In response to her great promotion for Moshi and Tanzania in general Marie Frances was honored by having street renamed on her name. Former Bustani Ale was renamed Marie Frances Boulevard in 2009. She was also given the keys to the Municipal and addition to the permanent residence in Moshi. The unprecedented Mount Kilimanjaro Marathon is to promote Moshi First among equals and take this great region to the next level.  Every year number of runners take part in the Mount Kilimanjaro marathon.

The USA Great Actress Deidre Lorenz who have acted in a number of blockbuster movies and television series will grace this year mount Kilimanjaro marathon. Lorenz’s movies include Santorini Blue, The Great Fight, Perfect Strangers and many more others. 

Chris Wilde will go down in history as the man who came to conquer this highest freestanding mountain in the world and left a great gift for Tanzania as he zooms down to his hundredth meters for his 50 kilometers marathon in June 24t, 2012.

 Taarifa hii imetumwa na:


Grac Soka
Afisa Uhusiano
Mt. Kilimanjaro Marathon

Epiq Bongo Star Search yamaliza kazi mkoani Dodoma

Madam Ritah Paulsen akipokea mtoto kutoka kwa  mshiriki huyu aliyekuja nae katika shindano hilo kabla  kuanza kuimba.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Zantel ambao ni wadhamini wakuu wa EBSS 2012  Awaichi Mawalla akichangia damu 
Na Mwandishi Wetu Dodoma
PAZIA la shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS) kwa mkoa wa Dodoma limefungwa rasmi huku vipaji kibao vikiwa vimejitokeza na kuwavutia majaji.

Kilichovutia zaidi ni washiriki wa miaka 16 ambao walionekana kuimba vema na kuwa kivutio hata kwa washiriki wenzao waliofurika katika ukumbi wa Royal Village.

Akizungumzia shindano hilo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Benchmark Production inayoandaa shindano hilo Ritha Paulsen alisema kuwa amevutiwa na wingi wa washiriki mkoani hapa hasa idadi ya washiriki wasichana pia.

Alisema kuwa ikiwa ni mara ya kwanza kuruhusu washiriki wa miaka 16 kuingia katika usaili wa EBSS 2012 ameshuhudia hazina kubwa ya vipaji  vya washiriki wa umri huo.

Katika usaili huo kulikuwa na washiriki wa aina mbalimbali wakiwamo wanafunzi, wafanyabiashara ndogondogo, vijana wa mitaani na wadau wengineo wa muziki.

Kwa kuthamini umuhimu wa akina mama na watoto mshiriki aliefika kuonesha kipaji chake katika ukumbi huo alipewa nafasi ya kuimba ili aweze kuwahi kuondoka.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Zantel ambao ni wadhamini wakuu wa EBSS 2012  Awaichi Mawalla mbali na kuvutiwa na ushiriki wa vijana waliojitokeza pia alihamasisha upimaji wa damu kwa kuchangia damu kwa kituo cha damu mkoani Dodoma.

“ Kwa kupitia EBSS 2012 tunataka kuwafikia vijana sio tu katika muziki bali pia hata katika kuhamasisha masuala mbalimbali yahusuyo jamii kama vile hili la kuchangia damu na mengineo” alisema Awaichi.

Washindi watakaopatikana watatangazwa baadae katika vyombo vya habari. Baada ya Dodoma kwa sasa inafuata Zanzibar ijumaa ijayo katika eneo la Ngome Kongwe

TAMASHA LA WAJANJA WA VODACOM FUNIKA MBOVU COCO BEACH LEO

 Mmoja wa wakazi wa jijini Dares Salaam aliefika Coco-Beach kushuhudia uzinduzi wa Tamasha la”WAJANJA”Linaloendeshwa na Vodacom Tanzania akipata huduma ya Vodacom Dstv,Tamasha hilo litafanyika  katika mikoa minne hapa nchini likiwa na lengo la kuwaelimisha wananchi kutumia mtandao wa kampuni hiyo kwa kuongea kwa robo shilingi na kutuma ujumbe kwa shilingi ishirini na tano na kutumia facebook na twitter bure.
 Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Joseline Kamuhanda akiongea na waandishi wa habari waliofika kushuhudia uzinduzi wa Tamasha la”WAJANJA”Coco Beach jijini Dares Salaam leo,Tamasha hilo linaloendeshwa na Vodacom Tanzania,Tamasha hilo litafanyika  katika mikoa minne hapa nchini likiwa na lengo la kuwaelimisha wananchi kutumia mtandao wa kampuni hiyo kwa kuongea kwa robo shilingi na kutuma ujumbe kwa shilingi ishirini na tano na kutumia facebook na twitter bure.
 Umati wa wakazi wa Jiji la Dares Salaam waliojitokeza katika uzinduzi wa Tamasha la”WAJANJA”Coco Beach jijini Dares Salaam leo,Tamasha hilo linaloendeshwa na Vodacom Tanzania,Tamasha hilo litafanyika  katika mikoa minne hapa nchini likiwa na lengo la kuwaelimisha wananchi kutumia mtandao wa kampuni hiyo kwa kuongea kwa robo shilingi na kutuma ujumbe kwa shilingi ishirini na tano na kutumia facebook na twitter bure.
 Mtangazaji wa Clouds FM radio ya watu Hamis Mandi( B12)akiwapagawisha kimtindo wapenzi wa hip hop waliofika Coco beach katika tamasha la”WAJANJA”tamasha hilo linaendeshwa na Vodacom Tanzania, limezinduziwa rasmi Leo na litaendelea kufanyika  katika mikoa minne hapa nchini likiwa na lengo la kuwaelimisha wananchi kutumia mtandao wa kampuni hiyo kwa kuongea kwa robo shilingi na kutuma ujumbe kwa shilingi ishirini na tano na kutumia facebook na twitter bure.
 Msanii wa kikundi cha Pah- one akipagawisha wakazi wa jiji la Dares Salaam waliofika katika uzinduzi wa tamasha la”WAJANJA” tamasha hilo linaendeshwa na Vodacom Tanzania, limezinduziwa rasmi Leo na litaendelea kufanyika  katika mikoa minne hapa nchini likiwa na lengo la kuwaelimisha wananchi kutumia mtandao wa kampuni hiyo kwa kuongea kwa robo shilingi na kutuma ujumbe kwa shilingi ishirini na tano na kutumia facebook na twitter bure.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Kevin Twissa (kushoto)akiwa amepozi kwa picha na Mtangazaji wa Clouds FM,Hamis Mandi(B12)

Taifa Stars yatolewa kwa penalti na Mambas Msumbiji

Taifa Stars imetolewa kwenye mechi za mchujo za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kufungwa kwa penalti na wenyeji Msumbiji (The Mambas) katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa ulioko Zimpeto pembeni kidogo ya Jiji la Maputo.
 
Refa Bennett Daniel alipopuliza filimbi ya kumaliza dakika 90 za pambano hilo timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1, hivyo kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo yanayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) mikwaju ya penalti ikatumika kupata mshindi.
 
Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Dar es Salaam, Februari 29 mwaka huu timu hizo
zilitoka sare ya bao 1-1.
 
Msumbiji ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 9 lililofungwa na mshambuliaji Jeremias Sitoe akiungnisha krosi ya Elias Pelembe ambaye mabeki wa Taifa Stars walifikiri ameotea.
 
Stars ilisawazisha bao hilo dakika ya 89 likifungwa kwa kichwa na
Aggrey Morris kutokana na mpira wa kona uliopigwa Amir Maftah.
 
Mikwaju ya penalti tano tano walioifungia Stars walikuwa Amir Maftah, Shabani Nditi na Shomari Kapombe wakati Aggrey Morris na Kevin Yondani.
 
Kwa vile The Mambas nao walikosa mbili ikabidi iongezwe penalti moja moja. Waliofunga kwa upande wa Stars walikuwa John Bocco, Frank Domayo na Mrisho Ngassa wakati Mbwana Samata alikosa.
 
Akizungumzia pambano hilo, Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen aliwapongeza wachezaji wake kwa kupambana hadi dakika ya mwisho.
 
"Tulikuja Maputo tukijua kuwa tunatakiwa kufunga bao, tumeweza kufunga bao ingawa katika dakika za mwisho. Unajua linapokuwa suala la penalti chochote kinaweza kutokea, na ndivyo ilivyokuwa," alisema Kim.
 
Taifa Stars itarejea nyumbani Juni 19 mwaka huu, ambapo itaaondoka hapa saa 4.40 asubuhi kwa kupitia Nairobi, Kenya na kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 1.50 usiku.
 
Kikosi kilipngwa hivi; Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni/John Bocco, Aggrey Morris, Kevin Yondani, Shaabani Nditi, Mrisho Ngasa, Frank Domayo, Thomas Ulimwengu/Haruna Moshi, Mbwana Samata na Mwinyi Kazimoto/Amir Maftah.

MWILI WA MAREHEMU WILLY EDWARD WAHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concerpts Beny Kisaka na Juma Pito wakimfariji mdogo wake na marehemu Willy Edward mara baada ya kuwasili katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ambako mwili wa marehemu umehifadhiwa, Willy Edward alifariki usiku wa kuamkia leo mkoani Morogoro ambako alikuwa akihudhuria semina  ya Sensa kwa matatizo ya Moyo, Mwili wa marehemu Willy Edward utasafirishwa kwenda nyumbani kwao Mugumu Serengeti mkoani Mara kwa mazishi
Mwili wa marehemu Willy Edward ukipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jioni ya leo.
Ndugu jamaa na marafiki wa marehemu wakishusha mwili wa marehemu Willya Edward kwenye gari baada ya kuwasili katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kuhifadhiwa
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda akimfariji Kulwa Karedia mhariri wa magazeti ya Mtanzania ambaye alikuwa mmoja wa marafiki na ndugu waliouleta mwili wa marehemu kutoka mkoani Morogoro.Picha Na Full Shangwe Blogu

MKUU WA MKOA WA MOROGORO AONGOZA USAFIRISHAJI MWILI WA WILLY EDWARD KWENDA DAR ES SALAAM

 Kaka mkubwa wa marehemu aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward Ogunde, George Ongiri Ogunde (wa kwanza kulia) akishirikiana na ndugu, jamaa na waandishi wa habari, kubeba mwili wa  mhariri huyo, aliyefariki dunia ghafla jana  usiku eneo la Forest Hill, mjini Morogoro. Mwili huo ulikuwa unatolewa  chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya mazishi katika Kijiji cha Mugumu kilichopo wilaya ya Serengeti, mkoani, Mara..
 Mbunge wa Jimbo la Morogoro, Azizi Abood, akiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006), Husein Bashe wakisubiri kuuona mwili wa Willy Edward
 Baadhi ya waandishi wa habari akiwemo Mbunge wa Morogoro mjini, Azizi Abood, wakiwa na huzuni walipokuwa wakisubiri kutoa heshima za mwisho katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, muda mfupi kabla ya mwili kusafirishwa Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia) akisikiliza jambo kutoka kwa kaka mkubwa wa marehemu aliyekuwa mhariri mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward Ogunde, George Ongiri Ogunde muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kwenda jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya mazishi katika kijiji cha Mgumo kilichopo wilaya ya Serengeti mkoani Musoma. wa pili kutoka kulia ni Katibu Tawala wilaya ya Morogoro, Alfred Shao na kaka mkubwa upande wa baba, Isack Ugunde.Picha Kwa Hisani Ya Father Kidevu Blog

Matukio ya Msiba wa Marehemu Willy Edward, Mburahati Dar Es Salaam

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Limited, inayochapisha gazeti la Jambo Leo na jarida la Jambo Brand Tanzania, Juma Pinto (kushoto) na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Benny Kisaka (wa pili kushoto) wakiwa kwenye msiba wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa Jambo Leo, marehemu Willy Edward Ogunde ulioopo nyumbani kwa kaka wa marehemu Mburahati, Dar es Salaam leo asubuhi. Wiily amefariki ghafla leo alfajiri mjini Morogoro alikokuwa akihudhuria semina ya siku moja ya masuala ya Sensa. Kutoka kulia ni ndugu zake marehemu; Dennis Ongiri, Joseph Rabach na Julius Rabach.
 Waandishi wa habari wa gazeti la Jambo Leo na Jarida la Jambo Brand Tanzania wakishiriki kwenye msiba wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, marehemu Willy Edward. Mwili wa marehemu Willy unasafirishwa mchana huu kutoka Morogoro kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam. Taratibu za mazishi zinaendelea kuratibiwa kwa ushirikiano wa ndungu na viongozi wa Jambo Concepts, lakini kwa mujibu wa Kaka wa marehemu Rabach ni maazishi yatafanyika nyumbani kwao marehemu, mjini Mugumu Wilaya ya Serengeti, mkoani Mara. Siku ya mazishi itatangazwa baadaye.

   Mjane wa marehemu Willy Edward, Rehema, akiwa kwenye majonzi
 Mjane wa marehemu Willy Edward, Rehema akilia wakati wa msiba huo leo asubuhi
 Waombolezaji wakimfariji mjane wa marehemu Willy Edward, Rehema

Akina mama waombolezaji wakiwa kwenye msiba
 Mtangazaji wa TBC, Grace Kingarame akimfariji  mjane wa marehemu Willy Edward, Rehema.
 Mpiga picha wa TBC, Mary Hondo, akimfariji Rehema.
 Mtoto wa mwisho wa marehemu Willy Edward, Caren (2), akiwa na babake mkubwa, Dennis Rabach
 
Mtoto wa mwisho wa marehemu, Willy Edward, Caren akiwa katika msiba
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Limited, inayochapisha gazeti la Jambo Leo na jarida la Jambo Brand Tanzania, Juma Pinto akihojiwa na Grace Kingarame wa TBC katika msiba huo. (Picha zote na Richard Mwaikenda 'Kamnada wa Matukio')

EXTRA BONGO WAZEE WA KIZIGO WAZIDI KULITIKISA JIJI NDANI YA MEEDA SINZA.

Ally Choki akiwaburudisha washabiki na wapenzi wa Extra Bongo ndani ya Meeda usiku wa kuamkia leo
Choki akicheza show na wanenguaji wake wa Extra bongo ndani ya Meeda Sinza.
Banza Stone Mwana wa Masanja - AKA Jenerale akiimba nyimbo yake ndani ya Meeda Sinza.
Mmiliki wa KAPINGAZ Blog Henry Kapinga alikuwepo ndani ya Meeda Sinza, hapa akishoo luv na kuwapa Big Up Ally Choki na Banza Stone wakati Extra Bongo walipokuwa wanafanya show usiku wa kuamkia leo ndani ya ukumbi huo.
Rapa maarufu namba moja Afrika mashariki wa Extra Bongo Kaba Tano akirap ndani ya Meeda Sinza usiku wa kuamkia leo

No comments:

Post a Comment