BABA wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, mzee Steven Mwaitenda
Baba wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, mzee Steven Mwaitenda akilia na kufarijiwa
Usu Mallya akilia baada ya kushuhudia mzee Steven Mwaitenda akibubujikwa na machozi mbele yao
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Usu Mallya (kushoto) akiwa na Mkuu wa
Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Lilian Liundi walipomtembelea Dk.
Ulimboka kumfariji jana
Mzazi akimlilia mwanaye Dk. Ulimboka kwa uchungu MOI
Baadhi ya wanaharakati anuai wakiwa na maua walipomtembelea Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Ulimboka kumfariji jana
Baadhi ya wanaharakati wakiwa na nyoso za hudhuni baada ya kilio cha baba wa Dk. Ulimboka jana MO
Baba wa Dk.
Ulimboka aangua kilio MOI
Na Joachim Mushi, Thehabari.com
BABA wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, mzee Steven
Mwaitenda amejikuta akiangua kilio kwa uchungu mbele ya wanaharakati ambao
walimtembelea mwanae, Dk. Steven Ulimboka kumpa pole kufuatia tukio la kutekwa
na kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana.
Hali hiyo ilitokea jana jioni katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa
Muhimbili (MOI), ambapo wanaharakati kutoka taasisi na asasi mbalimbali za
utetezi wa haki za binadamu walifika kwa lengo la kumpa pole Dk. Ulimboka
kufuatia kitendo kilichomfika.
Mzee Mwaitenda alijikuta akibubujikwa na machozi na
kushindwa kuendelea kuzungumza alipokuwa akitoa shukrani kwa wanaharakati hao,
kwa niaba ya mwanaye ambaye wanaharakati hao walishindwa kumuona wote kutokana
na hali yake ilivyo sasa.
“Niseme wazi nimefarijika sana kwa ujio wenu kumwona mwanangu dhidi ya
mambo ya kikatili aliyofanyiwa akitetea haki za wengine…,” alisema mzee
Mwaitenda kabla ya kushindwa kuendelea na kuangua kilio mbele ya wanaharakati.
Baada ya tukio hilo
baadhi ya wanaharakati walimshika wakishirikiana na wanafamilia ya mzee Mwaitenda
na kumbebeleza kisha kumtoa mbele ya mkusanyiko huo wa wanaharakati na
kumrudisha wodini huku wakimfariji.
Wakizungumza mara baada ya tukio hilo wanaharakati wameelezea kusikitishwa na
vitendo vinavyoendelea MOI eneo ambalo amelazwa kiongozi huyo wa madaktari
ambavyo vimeendelea kutishia usalama wa Dk. Ulimboka.
Akifafanua zaidi mwakilishi wa wanaharakati hao, Markos Albania alisema
taarifa walizozipata usiku wa juzi kuna wagonjwa ‘feki’ ambao walijitokeza MOI
huku wakitaka kulazwa wodi ya Wagonjwa Mahututi (ICU) alipolazwa Dk. Ulimboka
lakini baadaye waligoma kuingizwa wodini.
“Wapo wagonjwa ambao waliletwa na kutaka kupelekwa ICU moja
kwa moja…kuna watu wanakuja usiku wa manane wakitaka kumtembelea Dk. Ulimboka…matendo
yanayoendelea kutokea ukilinganisha na kauli za Serikali zilizotolewa bungeni
yanatishia usalama na uhai wa mgonjwa,” alisema Albania.
Aidha amesema kitendo cha vyombo vya usalama kuendelea
kumuhoji Dk. Ulimboka akiwa hoi hospitalini si vya kiungwana kwani tayari
muhusika amewataja hadi kwa majina watu ambao anawashuku lakini hadi sasa
hakuna aliyechukuliwa hatua yoyote.
Pamoja na hayo wanaharakati hao wameitaka Serikali kuunda
tume huru mchanganyiko na raia ambayo itachunguza kiundani suala hilo, kwani hawana imani na Jeshi la Polisi ambalo limedai
kuunda timu ambayo inachunguza kwa kina suala hilo.
Dk. Ulimboka ambaye ni kiongozi wa madaktari ambao
wanaendelea na mgomo wan chi nzima kuishinikiza Serikali kutekeleza madai yao alitekwa juzi na watu
wasiojulikana na kupigwa na kuteswa kikatili kabla ya kutelekezwa katika msitu
wa Mabwepande.
*Habari hii imeandaliwa na Mtandao wa Thehabari.com (www.thehabari.com)
MKUTANO WA JUMUIYA YA WASTAAFU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,ZANZIBAR
Miongoni mwa Wastaafu wa Jumuiya ya Muungano wa Tanzania wakimsikiliza Rais wa Zanzibar hayupo pichani wakati alipokutana nao huko Bwawani Mjini Zanzibar. |
Madaktari Bingwa Nao Wagoma
TUKIO
la kutekwa nyara, kupigwa na kujeruhiwa vibaya, kisha kutupwa katika
Msitu wa Pande uliopo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, kiongozi wa
Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka, limechochea kasi ya
mgomo baada ya madaktari bingwa kutangaza kujitosa rasmi kwenye mgogoro
huo.Awali madaktari hao hawakushiriki mgomo huo, lakini jana walieleza
kwa nyakati tofauti kuwa, wameamua kuungana na wenzao kutokana na unyama
aliofanyiwa kiongozi wao akiwa katika harakati za kutetea na kupigania
haki zao.
Madaktari
hao wa hospitali za Muhimbili, Moi, KCMC, Mbeya, Bugando na Ocean Road
ya jijini Dar es Salaam, jana walitangaza rasmi kuwa wameingia kwenye
mgomo huo kushinikiza pamoja na mambo mengine, Serikali kutoa tamko
kuhusu utata wa tukio hilo.
Tukio
hilo la aina yake kutokea nchini, limeathiri upatikanaji wa huduma zote
za matibabu katika hospitali hizo, huku madaktari katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili na Moi, wakielekeza nguvu zao kunusuru maisha ya
mwenzao aliyeumizwa.
Katibu
wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Edwin Chitage, aliwaambia waandishi wa
habari kuwa mgomo huo utaendelea hadi hapo Serikali itakapotekeleza
madai yao.
"Tunaitaka
Serikali kuacha vitisho kwa madaktari nchini, tunaitaka itambue kwamba
mgogoro huu hauwezi kumalizwa kwa njia yoyote vikiwemo vitisho bali ni
kwa kukaa meza ya majadiliano na kukubaliana na madaktari," alisema Dk
Chitega na kuongeza:
"Ninawashukuru
madaktari wote nchi nzima, wauguzi na wafanyakazi wa sekta ya afya kwa
ujumla wao kwa kusitisha huduma baada ya kupigwa mwenzetu. Tunaomba
mshikamano huu uendelee," alisema Dk Chitega.
Gazeti
hili lilishuhudia wagonjwa wakiwa wamekaa katika makundi bila kujua la
kufanya, huku wengine wakiamua kuondoka na kwenda hospitali binafsi.
Waliliambia
Mwananchi kwamba kitendo alichofanyiwa Dk Ulimboka ni cha kinyama na
kuungana na madaktari hao kuitaka Serikali kutatua mgogoro huo haraka.
Wagonjwa
waliofika katika eneo hili pia walielezwa bayana na maofisa wa Moi
kwamba huduma zimesitishwa kutokana na madaktari kugoma.
Ocean Road
Madaktari
bingwa katika Taasisi ya Ocean Road nao waligoma kutoa huduma hatua
iliyozua taharuki kwa wagonjwa waliofika kwa ajili ya matibabu.
Gazeti hili lilishuhudia ofisi za madaktari hao zikiwa zimefungwa na hata zile ambazo zilikuwa wazi, madaktari hawakuwapo.
Mmoja
wa wagonjwa aliyejitambulisha kwa jina la Joyce Dachi, alisema kuwa,
wagonjwa wengi wamekuwa wakiandikishwa mapokezi, lakini wanachukua muda
mrefu kumuona daktari.
Mgomo
huo pia umeendelea katika Hospitali ya Amana wilayani Ilala huku
uongozi wa hospitali hiyo ambao uligoma kuzungumza na vyombo vya habari,
ukihaha kunusuru hali hiyo.
Katika Hospitali za Temeke na Mwananyamala huduma ziliendelea kutolewa kama kawaida.
Mbeya
Katika
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya ,madaktari bingwa ambao awali
hawakugoma jana waliingia kwenye mgomo na kusababisha wagonjwa katika
hospitali hiyo hususan kitengo cha wazazi, kusota bila matibabu.
Habari kutoka katika hospitali hiyo zilieleza kuwa hivi sasa madaktari bingwa wanatoa huduma kwa kujuana.
Mmoja
wa madaktari hao ambaye hakutaka kutajwa gazetini, alisema kitendo
alichofanyiwa Mwenyekiti wa Jumuiya yao kimewakatisha tamaa.
Alisema
kuwa, hali hiyo sasa imehamia hadi katika Kituo cha Wazazi cha Meta na
kufafanua kuwa hali ni mbaya, tayari wajawazito wametakiwa kuhamia
katika Hospitali ya Mkoa ambayo imefurika wagonjwa.
Mkurugenzi
wa Hospitali hiyo ya Rufaa, Dk Eliuter Samky hakuweza kuzungumzia tukio
hilo jana kutokana na kile kilichoelezwa na katibu wake muhtasi kwamba
ana kazi nyingi.
Mwanza
Madaktari
katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC) mkoani Mwanza nao wamegoma,
huku kiongozi wa Kamati Ndogo ya hospitali hiyo inayoshughulikia migomo,
akikataa kuzungumzia hali hiyo.
Akizungumza
na Mwananchi kwa njia ya simu baada ya kutoonekana katika maeneo ya
hospitali, mmoja wa viongozi wa Kamati hiyo, Dk Geogre Adrian, alisema
kwa sasa hawezi kulitolea ufafanuzi suala hilo na kwamba kufanya hivyo,
ni kwenda kinyume na maagizo aliyopewa na Kamati Kuu.
Akizungumzia huduma katika hospitali hiyo alisema kuwa hajui lolote kwa kuwa hawajagusa maeneo ya kazi kwani wapo kwenye mgomo.
Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo alipotafutwa kwa njia ya simu ili kuzungumzia huduma katika hospitali yake, hakupatikana.
Watimuliwa
Jana
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Charles Majinge alitoa tangazo la
kuwataka madaktari waliopo mafunzoni ‘Interns’ katika hospitali hiyo
kurejea kazini na kama watakiuka agizo hilo, watakuwa wamejifukuzisha
wenyewe.
Manyara
Mkoani
Manyara, madaktari kumi katika Hospitali ya Haydom Wilaya ya Mbulu
wamegoma tangu juzi.Idadi ya wagonjwa katika hospitali hiyo
inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),
inaongezeka siku hadi siku.
Wakizungumza
na waandishi wa habari kwa masharti ya kutotaka kutajwa majina yao,
madaktari hao ambao wanafanya mafunzo ya vitendo katika hospitali hiyo,
wamesema kuwa hawatatibu wagonjwa mpaka madai yao yatekelezwe.
Mkuu
wa Wilaya ya Mbulu, Anatory Choya, alithibitisha kutokea kwa mgomo huo
na kufafanua kwamba wanaendelea kufanya mazungumzo ili kupata ufumbuzi.
Choya alisema kuwa madaktari wanaoendelea na kazi, wameelemewa kutokana na wagonjwa kuwa wengi.
Alisema kati ya madaktari 11 wanaosoma kwa vitendo hospitalini hapo, mmoja tu anayesomeshwa na hospitali hiyo, ndiye hajagoma.
KCMC
Hali
katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC mkoani Kilimanjaro imezidi kuwa tete
na kuwafanya ndugu kuwahamishia wagonjwa wao katika hospitali binafsi.
Mwananchi lilitembelea wodi za hospitali hiyo na kukuta vitanda vikiwa wazi.
Wakizungumza
na gazeti hili, baadhi ya madaktari ambao wapo kwenye mgomo kwa sharti
la kutotajwa majina, walisema hawako tayari kurudi kazini kwa kuhofia
usalama wa maisha yao.
Dodoma
Wagonjwa
katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma jana walijikuta wakipata taabu baada
ya madaktari wa hospitali hiyo kusitisha huduma kwa takriban saa sita
kuanzia asubuhi.
Muda wa mchana utoaji huduma katika hospitali hiyo uliendelea ingawa kwa kusuasua.
Tofauti na siku zote, jana chumba cha daktari kilichokuwa wazi ni kimoja tu hali iliyosababisha msongamano mkubwa.
Arusha
Mjini
Arusha, madaktari wameendelea na mgomo katika Hospitali ya Mkoa ya
Mount Meru na kusababisha kudorora huduma huku wagonjwa kadhaa
wakiondolewa hospitalini hapo.
Mgomo
huo, ulianza saa 1 asubuhi hadi saa 6:00 mchana, ambapo madaktari na
wauguzi,waligoma kutoa huduma wakitaka kujua hatima ya Dk Ulimboka.
Walitaka pia kuzungumza na uongozi wa hospitali hiyo na waandishi wa
habari, kuhusu mgogoro wao.
Askari anyimwa huduma
Askari
wa Usalama Barabarani ambaye jina lake halikufahamika mara moja ambaye
alipata ajali jana, alijikuta akishindwa kuhudumiwa katika hospitali ya
Mount Meru na kuondolewa kutokana na mgomo huo.
Askari
huyo, aliyevaa sare, alifikishwa hospitalini hapo saa 5:00 asubuhi
akiwa kwenye teksi, lakini wauguzi waliokuwa zamu walishauri apelekwe
sehemu nyingine.
Hata
hivyo, uongozi wa hospitali ya mkoa, ukiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa,
Dk Omar Chande, jana ulifanya kazi ya ziada ya kuwabembeleza madaktari
hao, kurejea kazini, kusubiri uamuzi wa Serikali.
Mgomo, Dk Ulimboka vyateka Bunge
Mgomo
wa madaktari na kutekwa kisha kupigwa Dk Ulimboka jana vilitawala
mjadala wa Bunge hadi pale Spika Anne Makinda alipotoa mwongozo kwamba
suala hilo lisijadiliwe kwani liko mahakamani.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda alilazimika kutoa ufafanuzi wa hoja yake aliyoitoa
juzi pale alipokuwa akizungumzia mgomo wa madaktari na kuhitimisha
kwamba Serikali ilikuwa inajiandaa kutoa kauli na msimamo wake hivyo
“liwalo na liwe’.
Pinda
alilazimika kutoa maelezo kutokana na swali aliloulizwa na Kiongozi wa
Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe aliyetaka kufahamu maana ya
kauli ya Waziri Mkuu ambayo aliita kuwa ni nzito na iliyozua mjadala
mkali nchini.
Kadhalika,
Mbowe alitaka kufahamu hatua ambazo Serikali imechukua kuhakikisha
kwamba wananchi wanaendelea kupata huduma za tiba kutokana na kuwapo kwa
taarifa kwamba madaktari katika hospitali kadhaa walikuwa wakiendelea
na mgomo.
Kadhalika
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu alimuuliza Pinda
kwamba haoni kwamba ni busara kujiuzulu wadhifa wake kutokana na ahadi
yake kwamba mgomo wa madaktari usingetokea, lakini ahadi hiyo imeshindwa
kutekelezeka.
Akimjibu
Mbowe, Pinda alikiri kutoa kauli hiyo ndani ya Bunge juzi na kusema
alifanya hivyo akiamini kuwa jambo hilo lilikuwa mahakamani na akasema
asingeweza kusema jambo lolote kwa kuwa hana tabia ya kuwa na utovu wa
nidhamu wa kuingilia mambo ya mahakamani.
Hata
hivyo, alijitetea kuwa kabla ya kutoa kauli hiyo bungeni juzi, hakuwa
na taarifa kuhusu tukio la kupigwa kwa Ulimboka na akasema kuwa, kauli
yake haihusiani kabisa na Serikali kuhusika katika jambo hilo kwa namna
yoyote ile.
Waziri
Mkuu alisema tayari amekwishaagiza vyombo husika kufanya uchunguzi wa
kina na kutoa majibu ya haraka ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua
stahiki mara moja.
“Kwanza
namtakia afya njema ndugu Ulimboka, na mimi nataka Watanzania waamini
kuwa tulikuwa katika mazungumzo mazuri na madaktari chini yake Ulimboka
hivyo tukio hilo ambalo limetokea katika mazingira magumu limetushtua
kweli, kama ni Serikali basi ingekuwa ni Serikali ya ajabu
kweli,’’alisema Pinda.
Kuhusu
namna ya kusaidia Watanzania wasiathirike na mgomo huo, alisema tayari
Serikali imeshaagiza madaktari kutoka wizarani kutumika na kuwaomba
waliostaafu kutoa huduma katika kipindi hicho kigumu.
Mkakati
mwingine ni pamoja na kutumia hospitali za Jeshi ikiwamo Lugalo waanze
kutoa huduma hizo wakati Serikali inaendelea kuzungumza kwa utaratibu na
madaktari.
Lissu aliuliza
swali la nyongeza kumtaka Pinda kuachia ngazi hali iliyosababisha
mvutano kwani Waziri Mkuu alikosoa uulizaji wa swali hilo kuwa
halikustahili.
Baada
ya kipindi cha maswali na majibu, Mbunge wa Ubungo (Chadema), John
Mnyika aliomba mwongozo wa Spika kuhusu suala la madaktari akitaka
taarifa ya Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ambayo ilifanyia kazi
suala la mgomo wa madaktari ijadiliwe bungeni.
Hata
hivyo, Spika Makinda alisema ripoti hiyo haiwezi kujadiliwa kwani
tayari Serikali ilishakabidhiwa kwa ajili ya kuifanyia kazi na kwamba
mapendekezo ya Bunge kupitia ripoti hiyo yamefanyiwa kazi kwa kiasi
kikubwa.
Habari
hii imeandaliwa na Neville Meena na Habel Chidawali, Dodoma, Godfrey
Kahango,Mbeya, Joseph Lyimo,Mbulu, Sheilla Sezzy,Mwanza, Rehema Matowo,
Moshi, Masoud Masasi,Dodoma, Fidelis Butahe, Geofrey Nyang'oro Dar,
Mussa Juma, Arusha, Bakari Kiango na Victoria Mhagama.
NMB YAFUNGUA TAWI TEGETA
Wateja wa Benki ya NMB wakipata huduma katika Teller za benki hiyo iliyopo Tegeta Jengo la Kibo Commercial Complex Tegeta Kibaoni |
NMB ni Full Mzuka.
You might also like:
No comments:
Post a Comment