Watoto watatu ambao hawajatambuliwa majina yao wakiwa wamelala nyuma ya Pickup kwa ajili ya kupelekwa Hospitali baada ya kujeruhiwa na nyaya za umeme.
Watoto watatu ambao walikuwa wakitembea pembezoni mwa barabara
wameangukiwa na nyaya za umeme baada ya gari dogo aina ya Escudo kugonga
nguzo asubuhi maeneo ya Mbagala Zakheem.
Watoto hawa watatu ambao walikuwa wakitembea pembeni wamejeruhiwa
vibaya na kuunguzwa sehemu mbalimbali kwenye miili yao, ambapo wasamalia
wema waliwasaidia na kuwapakia kwenye gari kukimbizwa Hospitali.
Wakazi wa Eneo la Ukonga Majumba Sita
Wilaya ya Ilala jijini Dar es sal;aam wafunga barabara kuu ya Nyerere
katika eneo hilo la majumba sita kushinikiza kuwekwa kwa matuta katika
eneo hilo kufuatia kukuthiri kwa ajali za wakazi wa eneo hilo kugongwa
wavukapo barabara hiyo.
Tukio hilo lilitokea leo majira ya saa
za asubuhi na kudumu hadi saa nane mchana baada ya kijana mmoja
kungongwa katika eneo hilo akijaribu kuvuka barabara hiyo na kufa papo
hapo.
Wakiwa na mabango, mawe na matofali
wakazi hao waname, wanawake, wazee kwa watoto walifurika katika barabara
hiyo na kushinikiza kuja kwa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuwekwa
kwa matuta.
Wananchi wakiwa wamefurika kwa wingi
barabarani na hata Jeshi la polisi lililopfika na kuwasihi waruhusu
magari kupita waligoma na huko mitaani pia walizuia boda boda (pikipiki)
kupita hadi matuta yawekwe.
Magari yakiwa yamezuiwa eneo hilo
karibu na Kambi ya Jeshi Kikosi cha Anga.
Wananchi wakiwa upande wa pili wa
barabara kutaka kujua hatma ya usalama wao.
Watu walikuwa ni wengi. Awali eneo
lingine katikati ya Njia Panda segerea na Minazi Mirefu (Banana)
wanafunzi wa shule ya Msingi Minazi Mirefu waliwahi kuandamana
barabarani hapo kushinikiza kuwekwa kwa matuta baada ya wenzao kadhaa
kugongwa na serikali ikaweka matuta hayo na hivi sasa hali ni shwari
katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment