Waziri wa Fedha,Dk William
Mgimwa kwa niaba ya serikali amepokea sh 7.9 bilioni kutoka benki
ya NMB ikiwa ni gawio la serikali kwa mwaka 2011 kama ilivoidhinishwa
katika mkutano wake mkuu uliofanyika Juni 2, 2012.Gawio hilo lilitokana
na serikali kumiliki asilimia 31.8 ya hisa katika benki ya NMB.
Akizungumza baada ya
kupokea hundi hiyo jijini Dar es Salaam Dk. Mgimwa alisema,
amefurahishwa
na benki ya NMB kwa utendaji wake kwa kuwa mwaka 2010 iliweza kutoa
sh bilioni 5.7
“Benki ya NMB inaonyesha dalili nzuri ya utendaji wake kwa
kuwa ongezeko hili la mwaka 2011 la sh bilioni 7.9 kwa serikali
ni ongezeko zuri na fedha hii iliyotolewa na NMB Imeweza kuichangia
Serikali baada ya kupata faida kwa kuwa ni nyingi sana
na itasaidia kuwalipa wafanyakazi wengi ” alisema Dk.Mgimwa”
Aidha, aliipongez NMB
katika juhudi zake za kuisaidia serikali kupitia shughuli mbalimbali
za kupambana na umasikini na kuboresha maisha ya wananchi wenye
mahitaji. Alisema anathamini mchango wa NMB katika ukusanyaji wa kodi
unaofanywa kupitia matawi yake yaliyosambaa Tanzania nzimai.
Kwa upande wake Afisa
Mtendaji wa NMB, Bw. Mark Wiessing alisema NMB itaendelea
kuleta huduma nafuu za kifedha kwa jamii ya kitanzania katika maeneo
yote ya vijijini na mijini “NMB imeweza kufikia wateja wake nchi
nzima,pia
imeweza kulipa kodi kwa serikali,ndio maana NMB ni benki bora kwa
Tanzania
Tukio hilo muhimu lilishuhudiwa
na manaibu wawili wa wizara ya Fedha na Uchumi, Katibu mkuu wa wizara
ya fedha na manaibu wake watatu, mweka hazina mkuu, wakuu wa wizara
zingine pamoja na wafanyakazi wa NMB.

No comments:
Post a Comment