Friday, June 8, 2012

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa UAE Amtembelea Rais Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam



Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Naibu Waziri wa mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu(UAE) Mhe.Khalid Ghaanim Al Ghaith wakati yeye na ujumbe wake walipowasili kwa mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Mhe.Ghaith anashughulikia pia masuala ya uchumi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na ujumbe kutoka Umoja wa Falme za kiarabu(UAE) unaongozwa na Naibu Waziri wa mambo ya nje wa Falme hizo mhe.Khalid Ghaanim Al Ghait (wapili kulia) wakati ujumbe huo ulipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam leo(picha na Freddy Maro)

ZAWADI SBL ZARINDIMA MKOANI KILIMANJARO, WENGI WAKUSANYIKA KUSHUHUDIA WASHINDI WAKIKABIDHIWA ZAWADI ZAO.

Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Bw.Ephraim Mafuru wa pili kutoka kulia akikabidhi zawadi ya jenereta kwa mshindi wa promosheni ya vumbua hazina chini ya kizibo inayoendeshwa na kampuni hiyo hapa nchini, pamoja naye ni wafanyakazi wa kampuni hiyo tawi la Moshi mkoani Kilimanjaro.
Zawadi hizi zilikabidhiwa jana kwa washindi waliopatikana katika kitongoji cha kiboroloni na majengo mkoani Kilimanjaro. Picha ya pili ni Waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda mkoani humo wakimpongeza bodaboda mwenzao Bw.  Rogers kavishe abaye amejishindia jenereta  sambamba na Bw. Vicent  Lymo ambaye naye amejishindia jenereta.
 Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti Ephraim Mafuru akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi zawadi ya jenereta kwa mshindi.
Bw. Deusdedit Tobias Njau 22akifurahia na wenzake mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya Jenereta.


Kampuni ya bia ya Serengeti jana imekabidhi zawadi ya jenereta mbili kwa washindi wa zawadi hizo katika kitongoji cha kiboroloni moshi mkoani Kilimanjaro ni katika promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO na SBL inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti.
Ni wiki ya 6 sasa kati ya wiki 16za promosheni hiyo ambapo katika droo ya sita iliyochezeshwa hivi karibuni washindi wawili walipatikana ambao ni Bw. Deusdedit Tobias Njau 22 kutoka kiboroloni mkoani Kilimanjaro ambaye alijishindia jenereta mpya na Bw. Vicent Lymo 36 kutoka kibosho mkoani Kilimanjaro ambaye amejinyakulia pikipiki mpya kabisa ambayo naye atakabidhiwa zawadi yake siku chache zijazo pindi taratibu za usajili zitakapokamilika.
Makabidhiano hayo yalifanyika jana na kupata kuhudhuriwa na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini huku tukio zima likishuhudiwa na umati mkubwa wa watu ambao walitoa maoni mabalimbali juu ya zoezi zima la promosheni hiyo na kusema SBL inabadilisha maisha ya watanzania wengi hasa vijana jambo ambalo linapaswa kuigwa na makampuni na mashirika mengine hapa nchini.Washindi hao wameishukuru SBL nakuitaka iendelee na moto huohuo.
Akiongea na waandishin wa habari wakati wa kukabidhi zawadi hizo Mkurugenzi wa masoko SBL Bw. Ephraim Mafuru amesema washindi hao walipatikana kihalali na kwamba kila mtanzania mweneye sifa zilizoainishwa katika vigezo na masharti ya promosheni hiyo ana haki na uwezo wa kushiriki na kushinda zawadi mojawapo au zaidi kati ya zawadi zilitajwa katika promosheni hiyo “leo tunawakabidhi hawa zawadi zao lakini siku chache zijazo tutakuwa hapa tena kwaajili ya kumkabidhi mshindi mwingine pikipiki mpya” alisema Mafuru na kuwataka watanzania wote wenye mapenzi mema na kampuni ya bia ya Serengeti waendelee kushiriki kwani batahi ya mtu haiwezi kwenda kwa mwingine.
Hii ni droo ya sita wiki ya sita mfululizo ambapo bado takriban wiki 16 sasa ili kuisha kwa promosheni hiyo ya pekee na aya kwanza kutokea hapa nchini ambapo zaidi ya milioni 780 za kitanzania zinashindaniwa kote nchini

RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA MAJAJI WAWILI NA KAMISHNA WA MAHAKAMA LEO.

Rais Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Mh. Semistocles Kaijage (kulia) kuwa jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kabla ya uteuzi huo Mh. Semistocles Kaijage alikuwa jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam.
ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akifuarahia Jambo na kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mhe. Edward Rutakangwa (wa tatu kutoka kulia)  mara baada ya kumwapisha leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kulia ni Jaji wa mahakama ya Rufani Mussa Kipenka na Jaji  Semistocles Kaijage (wa kwanza kushoto).
Mh. Rufani Mussa Kipenka akipongezwa na baadhi ya ndugu waliohudhuria hafla fupi ya kuapishwa kwake kuwa jaji wa mahakama ya Rufani Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Mhe. Edward Rutakangwa kuwa kamishna  wa Tume ya Utumishi wa Mahakama katika hafla fupi iliyofanyika leo Ikulu jijini Dares salaam.
Jaji wa mahakama ya Rufaa Mh. Semistocles Kaijage akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine amesema atahakikisha kuwaanatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria,kupunguza mlundikano wa kesi na kuhakikisha kuwa maamuzi yanatolewa kwa haki.
Jaji wamahakama ya Rufani Mh. Mussa Kipenka akisaini hati ya kiapo mara baada ya kuapishwa na Rais  Dkt. Jakaya kikwete leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni jaji mkuu wa Tanzania Mohammed Chande Othman.

MAJINA YA WANAMICHEZO WATAKAOWANIA TUZO ZA (TASWA) YATANGAZWA


Mwenyekiti wa Kamati ya tuzo za Chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA Bw. Masod Saanane akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa City Sports Lounge jijini Dar es salaam leo, kulia ni katibu mkuu wa TASWA Amir Mhando
MAJINA YA WALIOTEULIWA KUWANIA TUZO YA WANAMICHEZO BORA MWAKA 2011/MWANAMICHEZO BORA WA TANZANIA MWAKA 2011, ITAKAYOFANYIKA JUNI 14 MWAKA HUU
KIKAPU:
WANAWAKE
DORITHA  MBUNDA :-JKT QUEENS
EVODIA  KAZINJA:-JKT QUEENS
FARAJA MALAKI:-JESHI STARS
WANAUME
ALPHA KISUSI-Vijana 
FILBERT MWAIPUNGU:-ABC
GILBERT BATUNGI:-ABC
NETIBOLI:
LILIAN SYLIDION
 DORITHA MBUNDA
 GOFU
WANAWAKE:
Madina Iddi (Umri miaka 27)
Hawa Wanyeche (Umri miaka 26)
Ayne Magombe (Umri miaka 24)

WANAUME:
Frank Roman
Nuru Mollel
Issac Anania
GOFU WA KULIPWA:
FADHILI  SAIDI NKYA.
YASINI SALEHE
HASSANI KADIO
OLIMPIKI MAALUM
Ahmada Bakar
Amina Daud Simba-kisahani na tufe
Othman Ally Othman-mkuki, kisahani na tufe.
Cio..
PARALIMPIKI
WANAUME
ZAHARANI MWENEMTI
JOSEPH NZIKU
YOHANA MWILA
WANAWAKE
FAUDHIA CHAFUMBWE
SIWEMA KILYENYI
JANETH MADISE
NGUMI ZA RIDHAA
SULEIMAN SALUM KIDUNDA
VICTOR NJAITI
ABDALAH KASSIM
CIO…
WAOGELEAJI
(WANAWAKE)
MAGDALENA MOSHI
GOURI KOTECHA
MARIAM FOUM

Ecobank launches ‘WIN BIG WITH ECOBANK’ Promotion for individuals and SMEs customers in Tanzania.

Ecobank Tanzania , a subsidiary of the pan-African banking group with presence in 32 African countries, and which opened operations here in Tanzania in 2010, has announced the launch of a promotion tagged “WIN BIG WITH ECOBANK’. 

Ecobank, the leading independent regional banking Group in Africa,  serving wholesale and retail customers, in launching this promotion is not only rewarding existing customers but extending a hand of partnership to Tanzanians, including individual customers whether employed, self employed or students and SMEs. 

 At a press conference held on the 4th of June 2012, the CEO/ Managing Director of Ecobank Tanzania, Mr.  James Koomson-Cantamantu, addressing the media, said 'We have had a rewarding experience, providing excellent banking services to our customers. This promotion gives us another opportunity in a different way to deepen this rewarding experience with our customers and at the same time instilling a culture of saving. “Wealth creation requires the commitment to save and one does not necessarily need large sums of money to start” With Ecobank we do both; give you discipline to save and a chance to realize your dream. 

Being a Pan African bank, we have made similar impact in countries in West, Central and Eastern Africa and would like to do the same here in Tanzania. We don’t just want to advertise ourselves, but also impact the lives of the people we are here to serve in a special way- which is why we are launching this customer engagement promotion. It will give us the opportunity to create a win-win situation for us and our current as well as prospective customers'.
 
                Mr Cantamantu-Koomson added, ‘At the moment we have 5 branches in Dar Es Salaam and plans are well afoot to soon open branches in Arusha and Mwanza. The WIN BIG WITH ECOBANK promotion will increase awareness of the Ecobank brand in the Tanzanian market while also increasing our customer base. Our existing customers will also be delighted since we have not left them out.’
 
The WIN BIG WITH ECOBANK promo is open to existing and new customers. Existing customers automatically earn 50 points while new customers earn 50 points on opening an account with TSH50,000. To qualify for the monthly draws, both existing and new customers need to build up their balances to TSH100,000  which is equivalent to 100 points. A customer who has 100 points qualifies for a monthly draw.
 Ever month 15 winners will emerge from the draws for the next 6 months. Five of these winners will get ipads or laptops depending on their preference, while the remaining 10 will get gift vouchers for clothes, household furniture and electronics or a one night getaway to Zanzibar. At the end of the 6th months, customers who have a balance of TSH500,000 or have increased their monthly balance by TSH100,000 for the period of the promo, are qualified for the final grand price of a brand new Hyundai ix35.

According to Samuel Ayim, Ecobank Tanzania’s Executive Director, Business Development, “The “WIN BIG WITH ECOBANK’ promo is a campaign of a careful and extensive research work focused on creating exciting offers while offering world-class banking services to Tanzanians.

 Our selection of gifts and partners is because we want to truly delight anyone who participates and wins in this promo. Laptops, Ipads, home furnishings and electronics, clothes and short holidays are things people want and need, things people would normally look forward to buying. Ecobank is making it possible in our customers' lives. That is the exciting thing for us”.

Mr. Ayim concluded, 'All you have to do is join the fun, open an account with us. Or increase your deposits with us and you could be a proud winner of any of the items and eventually the car – a Brand New Hyundai Tucson. Hurry open an account and start saving, you just might be one of the lucky winners. Welcome to WIN BIG WITH ECOBANK’.

Airtel yashirikiana na UNESCO kuanzisha Radio za jamii Nchini

Afisa mradi wa habari na mawasiliano UNESCO   Yusuph Al Amin akikabithi radio ya solar kwa mkazi wa kijiji cha Ololosokwan  wakati wa ziara ya kutembelea mradi wa Radio jamii ulioanzishwa chini ya udhamini wa Airtel kwa kushirikia na UNESCO,  Radio zaid ya 200 zilikabithiwa kwa wakazi wa kijiji hapo,  uzinduzi wa  Radio hii utafanyika  mwishoni mwa mwenzi juni,
 Afisa mradi wa habari na mawasiliano UNESCO   Yusuph Al Amin akionyesha jinsi gani radio ya solar inavyofanya kazi mara baada ya kukabithi Radio 200 kwa wakazi wa kijiji cha Ololoskwan wakati wa  ziara ya kutembelea mradi wa Radio jamii ulioanzishwa chini ya udhamini wa Airtel kwa kushirikia na UNESCO, Ololosokwani Radio  inategemea kuzinduliwa mwishoni mwa mwenzi juni, wakishuhudia kushoto ni mwakilishi wa Airtel Ahmed Juma katika ni Yannick Ndoinyo Mkurugenzi mtendaji IrkiRamat Foundation (RAMAT
 wafanyakazi wa Airtel Dua Kazimoto na Mercy Nyange wakiwa katika picha na wanawake wafanyabiashara wa vikundi vidogovidongo wa kijiji cha Ololosokwani wakati wakati walipotembela mradi wa radio unotegemea kuzinduliwa mwishoni mwa mwenzi Juni
wanakijiji cha Ololoskwan na wawakilishi wa UNESCO na Airtel wakiwa katika picha ya pamoja wakati walipotembela mradi wa radio unotegemea kuzinduliwa mwishoni mwa mwenzi Juni
XXXXXXXXX

Airtel yashirikiana na UNESCO kuanzisha Radio za jamii Nchini

*         Mikoa zaidi ya 10 nchini  kufikishiwa Radio za jamii

*         Lengo ni kukuza sekta ya mawasiliano  hususani  maeneo
yaliyo na chagamoto za kijamii.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na UNESCOwamejiunga kuendeleza sekta ya mawasiliano nchini na kuhakikishahuduma za mawasiliano ya radio zinawafikia wananchi wengi hasa walewanaoishi kwenye maeneo ya vijiji  zinavyokumbwa na  changamotonyingi za kijamii pamoja  na kukosekana kwa huduma za radio.

Airtel na UNESCO kwa kutambua umuhimu wa mawasiliano katika karne hiiya 21 na katika kuhakikisha jamii inapata habari za uchumi, siasa naza kijamii ambazo ndizo nyenzo muhimu kwa maendeleo ya jamii yeyoteduniani wameonelea ni vyema kwa kushirikiana na jamii husika kuanzisharadio za jamii (community Radios) ili kutoa nafasi kwa wananchi kupataelimu mbalimbali kwa kupitia Radio hizi zitakazoenea nchini kote.

Lengo kubwa la kuanzisha radio hizo ni kwasababu maeneo mengi yamekosahuduma hizi muhimu za mawasilino na hivyo kujikuta kuwa kwenye mifumoduni  ya kijamii  kama vile ukiketwaji wa wanawake, elimu duni, imani
za kishirikina, Umaskini , unyanyasaji wa kijinsia, kuenea kwa kasikwa ugonjwa wa ukimwi na matatizo mengine mengi.

Akiongea wakati walipotembelea Radio iliyopo Ololosokwani msimamizi wamradi na Afisa uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde alisema, "Airteltunajisikia furaha kuwafikia wananchi na wateja wetu kwa kupitiamtandao wetu uliompana zaidi, tunaamini kwa kupitia radio hizi elimu itatolewa kwa jamii, upatikanaji wa  habari za kiuchumi na biashara kutawezesha kuboresha shughulili za kiuchumi katika maeneo husika na nchi kwa ujumla,  pia radio hizi zitawapa wakazi kufahamu hali ya kisiasa nchini na kupata habari mbalimbali za ndani na nje ya nchi tofauti na ilivyo sasa.

Airtel tunawajali sana na ndio maana ndio mtandao pekee unaopatikanahapa kijijini  Ololosokwani , na leo hii pia bado tumepiga hatuanyingine kwa kushirikiana na wenzetu wa UNESCO kufikisha huduma yaradio pekee ya Tanzania kijinini hapa ambayo masafa yake yatasikikahadi vijiji vya jirani"

Airtel tunaendelea kutimiza dhamira yetu kwa kushirikiana na serikaliya jamuhuri ya muungano chini ya wizara husika kuhakikisha tunachangiakatika kufikisha huduma hii muhimu kwa watanzania na kuleta mabadilikoya kiuchumi na kijamiii katika maeneo yanayoonekana ni duni na ambayohayajafikiwa.

Naye Afisa mradi wa habari na mawasiliano UNESCO   Yusuph Al Aminalisema" mradi wa radio hapa kijiji cha Ololosokwani utawawezeshawakazi wa hapa kupata mawasiliano ya karibu na sehemu mbalimbali zaTanzania, kutawawezesha kujifunza mambo mapya, kutangaza mila nadesturi za kimasai, kuweza kufahama mambo ya utawala bora na kuwezakuhoji viongozi wao, kupata habari mbalimbali, na pia kuelimishawamasai kuendeleza tamaduni zao na maendeleo kwa ujumla.

"Tunawashukuru wenzetu wa Airtel kwa kushirikiana nasi katikakuuanzisha mradi huu kwa kupitia radio hii tutaweza kufikia vijiji 14pindi tutakapoanza kurusha matangazo"alisema Bw, Al AminBw Al-Amin pia aliongeza kwa kusema "Pamoja na mradi wa radio piatumeweza kuanzisha multimedia center itakayowasaidi wakazi wa kijijinihapa na shule ya sekondari iliyopokaribu kuweza kutembelea tovutimbalimbali na kuweza kupata huduma za internet"

Vile vile tumeanzisha mradi wa kuboresha nyumba zakimasai kuondoa moshi na kuongeza mwanga na tutajenga nyumba mbili za mfano hivyo tunategemea wakazi wa hapa watajenga nyumba za makazi zilizo na kiwango kulinganisha na sasa na mradi mwengine ni wa kuboresha maziwa ya ngome na nyama na kuweza kutengeneza viwanda vidogo na kutengeneza jibini na mwisho tunaanzisha mradi wa solar utakao wawezesha wakazi wahapa kupata um eme" aliongeza Al Amin.

Miradi yote hii imeanzishwa baada ya kuanza mradi wa radio na kuona maeneo mengine ambayo tunaweza kuyaboresha na kuleta mabadiliko kwa wakazi wa hapa alimalizia kwa kusema Bw, Al Amin

Akiongea na waandishi wa habari  mkazi wa kijiji cha ololoskwanialiyejitambulisha kwa jina la bi Nekisho Ndoinyo alisema hapa kijijini kwetu hatuna radio ya Tanzania tuaamini kabisa kwa kuanzishwa radio hii kutaleta mafanikio makubwa kwa vikundi vya kina mama na wakazi wa hapa kutangaza biashara zao, tutaweza kupata taarifa mbalimbali , tutaweza kutangaza mila yetu ya kimasai, watoto wetu watapata elimu na kuweza kujua nafasi mbalimbali za shule na kazi, hivyo basi nachukua fulsa hii kuwahamasisha wanakijiji kushiriki katika vipindi vya radio pale itakapoanza kurusha matangazo yake, tumefurahi sana kuweza kupata mawasiliano haya ya radio na tunashukuru sana Airtel na UNESCO kwa jitihada hizi.

Kwa upande wake mkazi wa kijiji cha ololosokwani bi Kootu Tome aliongeza kwa kusema tatizo kubwa la kijiji hicho ni mgogoro wa Ardhi na wawekezaji kuvamia maeneo yao hivyo naamini radio itatoa mwanga kwa jamii na kuweza kutambua haki yao ya kimsingi.

Mradi huu wa Radio za jamiii unaosimamiwa na UNESCO kwa kushirikiana na Airtel  unategemea kufunguliwa rasmi mwishoni mwa mwenzi Juni kwa kuzindua kituo cha Radio kilichopo Ololosokwani  Arusha. Mikoa mingine itakayofikishiwa radio za kujamii ni pamoja na  Kyela Mbeya, Uvinza Kigoma, Pemba na maeneo mengi.

REDDS MISS CHANG'OMBE KUPATIKANA KESHO JUMAMOSI UKUMBI WA QUALITY CENTRE

 Warembo wanaotarajia kuwania taji la Redds Miss Chang'ombe kesho katika ukumbi wa Quality Centre, Dar es Salaam, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano na waandishi wa habari jana kwenye mgahawa mpya wa City Sports & Lounge uliopo mkabala na sanamu ya Askari, katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
 Mwandaaji wa shindano hilo, Tom Chilala (kulia) akizungumza kuhusu maandalizi ya kimbembe hicho. Kutoka kushoto ni Meneja wa kinywaji cha Redds kinachodhamini mashindano hayo, Vick Kimaro na Meneja wa Kampuni ya Nexusw Consulting Agency, Neema David.
        warembo wakiwa kwenye pozi.PICHA NA KAMANDA MWAIKENDA)

No comments:

Post a Comment